-->

Roberto Di Matteo afutwa kazi Aston Villa

Meneja wa klabu ya Aston Villa ya Uingereza Roberto di Matteo amefutwa kazi siku 124 baada ya kukabidhiwa mikoba katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship. Villa sasa wanatafuta meneja wao wa tano katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja. Walishinda mechi moja pekee kati ya 11 walizocheza ligi ya daraja la pili, ligi ya Championship, chini ya Di Matteo. Di Matteo, 46, ambaye alikuwa mchezaji na meneja wa Chelsea wakati mmoja, aliteuliwa meneja wa Villa baada ya mfanyabiashara Mchina Dkt Tony Xia kununua klabu hiyo mwezi Juni. Villa walizomewa na mashabiki Jumamosi baada ya kulazwa 2-0 ligini Preston. Steve Bruce na Mick McCarthy ni miongoni mwa mameneja wanaopigiwa upatu kumrithi Di Matteo. Katika mechi tano kati ya 11 walizocheza chini ya Di Matteo, walifungwa bao moja kila dakika 85.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments