-->

''Zaidi ya 100 walifariki'' katika maandamano Ethiopia

Daktari mmoja katika hospitali ya mji wa Ethiopia ambapo watu kadhaa waliuawa katika mkanyagano wakati wa maandamano amesema kuwa zaidi ya watu 100 wamefariki ,kulingana na ripoti ya Bloomberg. Serikali ilikuwa imesema kwamba takriban watu 52 walifariki. Bloomberg inasema kuwa watu walizamishwa majini na kufariki ama hata ''kupondwa hadi kufa'' kulingana na Bloomberg. Imesema kuwa vifo hivyo vilitokea wakati watu walipokuwa wakitoroka kutoka kwa magari yaliojihami ambayo yalikuwa yakitumiwa kuwatawanya waandamanaji. Takriban watu 100 walifariki na wengine wanasema kuwa kuna watu wengine waliozikwa chini ya maji ,daktari huyo aliambia Bloomberg kutoka Bishoftu. "Tunasubiri watu zaidi'',anasema kuwa hakuona mtu yeyote aliyefariki kutokana na jeraha la risasi. Ethiopia imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuwaenzi wale waliopoteza maisha yao wakati huohuo Maafisa wa polisi nchini Kenya wamewakamata watu 40 wa jamii ya Oromo kwa kufanya maandamano kinyume na sheria katika mji mkuu wa Nairobi,kulingana na gazeti la Daily Nation. Gazeti hilo limemnukuu afisia mkuu wa polisi wa eneo la Gigiri Vitalis Otieno akisema kuwa maafisa wa polisi waliitwa katika eneo hilo baada ya kundi hilo kuzua ghasia.'Wengine wao wako nchini kinyume na sheria...tunawachunguza na kukagua nakala zao'',aliongezea. Kiongozi wa kundi hilo hatahivyo amesema kuwa waliwaelezea maafisa wa kaunti kuhusu mkutano huo mnamo tarehe 29 mwezi Septemba ,2016 na kulipa fedha zinazohitaji za shilingi 3000 kwa mujibu wa ripoti hiyo. Mkutano huo unafuatia ripoti za watu kutoka kwa jamii ya Oromo ambao inadaiwa kuwa waliuawa katika mkanyagano wakati wa maandamano siku ya Jumapili nchini Ethiopia.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments