-->

Europa League: Manchester United walaza Zorya Luhansk

Manchester United wameondoka kwenye mkia kundi lao la ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, baada ya kupata ushindi dhidi ya Zorya Luhansk. Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la pekee dakika ya 69, baada ya kombora la nguvu mpya Wayne Rooney kugonga mlingoti wa goli. Hilo ndilo bao la kwanza la Ibra katika mechi tano, na lilitokana na kombora la kwanza la United lililolenga goli kwenye mechi hiyo. United walitawala pakubwa mchezo huo uliochezewa Old Trafford, ingawa Sergio Romero alihitajika kufanya kazi ya ziada kuzima kombora la Paulinho muda mfupi kabla ya Ibrahimovic kufunga. Mashetani hao Wekundu walitarajiwa kufanya vyema Europa League lakini walianza kampeni yao kwa kulazwa 1-0 na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi mechi yao ya kwanza. United sasa wamo nambari tatu kundini, wakiwa na alama sawa na Feyenoord na moja nyuma ya viongozi Fenerbahce wa uturuki ambao watazuru Old Trafford 20 Oktoba.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments