-->

UKAD lachunguza uendeshaji baiskeli Uingereza

Maafisa shirika la Uingereza la kupambana na matumizi ya dawa za kutitimua misuli, UKAD, wametembelea makao makuu ya uendeshaji baiskeli Uingereza kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za makosa katika mchezo huo. Maafisa wawili wametembelea kituo hicho cha mchezo wa uendeshaji baiskeli Manchester Ijumaa, huku ripoti zikisema wachunguzi 'wamelenga' kituo hicho. Ukad limesema mkutano huo umepangwa kwa ushirikiano kamili wa taasisi hiyo ya uendeshaji baiskeli. Aliyekuwa mwendesha baiskeli wa timu ya Sky Jonathan Tiernan-Locke amesema wiki hii dawa ya kupnguza maumivu ya Tramadol "ilitolewa bure" mnamo 2012. Tiernan-Locke ameiambia BBC kuwa dawa hiyo inayozusha mzozo ilipatikana katika mashindnao ya ubingwa ya Road World Championships miaka minne iliyopita. Taasisi ya kitaifa ya mchezo huo Uingereza imetoa tuhuma hizo dhidiya afisa wa afya aliyekuwepo doctor Richard Freeman, kwa niaba ya BBC. Amekana tuhuma hizo. Image copyright Getty Images

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments