-->

Rose: Shearer alikuwa sahihi kusema Uingereza inatapatapa

Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya Uingereza Danny Rose amesema Alan Shearer alikuwa sahihi kuita timu hiyo ya taifa kuwa inatapatapa baada ya kujiuzulu kwa meneja Sam Allardyce. Anasema kuwa sio jambo zuri kwa meneja kuondoka muda mfupi akiwa bado hajatimiza mikakati aliyojiwekea na hilo linaathiri pia wachezaji. Rose alikuwa katika kikosi cha Uingereza kilichoifunga Slovakia katika mchezo wa kufuzu kwa kombe la dunia chini ya uongozi wa Allardyce. ''Nilimtumia ujumbe nikimshukuru kwa kunijumuisha katika kikosi chake, na kunifanya kuwa na heshima ningine katika ulingo wa soka la kimataifa, nikamwambia pole sana kwa kupoteza nafasi yake na kumtakia kila la kheri mbeleni'' alisema Rose. Allardyce ameingia katika historia ya kukaa kwa muda mfupi katika timu hiyo kwa siku 67 tu, aliingia baada ya Roy Hodgson kubwaga manyanga alipotolewa mapema katika michuano ya Euro 2016.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments