-->

ITF yatoa onyo kwa wachezaji baada ya kupunguza adhabu ya Sharapova

Chama cha Tennis duniani ITF kimempunguzia mchezaji nyota wa tennis Maria Sharapova adhabu ya kufungo cha miaka miwili na sasa itakuwa miezi 15. Lakini kimesema kuwa wachezaji wa mchezo huo hawataruhusiwa kukata rufaa kama watahisiwa kuhusika kwa maksudi na matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni. Katika taarifa yake chama hicho kimesema kuwa hakitakuwa tayari kupokea maelezo yoyote ambayo yanaonyesha kuwa mchezaji alitumia dawa hizo kwa maksudi baada ya taarifa zote kutolewa. Sharapova ni mshindi mara tano wa Grand slam na kwa mujibu wa jarida la Forbes ni mwanadada anayelipwa zaidi katika mchezo huo kwa miaka 11 mfululizo mpaka alipopitwa na Serena Williams mwaka huu. Sharapova aligundulika kutumia dawa hizo karibia mwezi mmoja tokea zilipofungiwa januari 2016.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments