-->

Rigobert Song alazwa hospitalini Cameroon

Nyota wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song amekimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua kiharusi. Song, 40, ambaye ni mjomba wa aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, West Ham na Charlton Athletic Alex Song, alichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi 137. Taarifa zinasema alikuwa nyumbani kwake Odza, Yaounde alipopatwa na kiharusi na akakimbizwa hospitalini siku ya Jumapili. Song, ambaye alikuwa nahodha wa Indomitable Lions, ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chad, kazi aliyokabidhiwa mwishoni mwa mwaka jana. Ndiye mchezaji aliyechezea timu ya taifa ya Cameroon mechi nyingi zaidi. Wachezaji wengine nyota wa Cameroon, akiwemo Samuel Eto'oo, wamemtakia afueni ya haraka. "Namtakia ndugu yangu mkubwa ujasiri na uponaji wa haraka," ameandika kwenye Twitter na Instagram.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments