-->

Schalke 04 bado yaendelea kupata matokeo mabaya

Schalke 04 imeshindwa kwa mara ya nne kupata ushindi katika Bundesliga msimu huu baada ya kupoteza mchezo wake jana jumapili dhidi ya Hoffenheim kwa mabao 2-1. Hoffenheim imepata ushindi wake wa kwanza katika msimu huu baada ya sare nne mfululizo wakati Lukas Rupp alipofunga bao katika dakika ya 41. Mapema Andrej Kramaric alisawazisha bao lililofungwa na Eric Maxim Choupo-Moting katika dakika ya nne kwa Schalke. Nahodha wa Schalke Benedict Howedes alikuwa na haya ya kusema: "Kwa kweli tulianza vizuri . Tulipata bao zuri kabisa. Hata hivyo baadaye tulianza kujilinda na katika hali hii hatukuwa maini sana. Tunafungwa mabao mengi ambayo ni kwa njia rahisi sna. Nashindwa kuelewa , ni vipi tunaweza kufungwa mabao kama hayo. Na hapa kwa mara nyingine tena tumeshindwa mchezo ambao hatukupaswa kushindwa, na hii inauma sana. Mlinzi wa Schalke 04 Benedickt Hoewedes akipambana na Andrej Kramaric wa Hoffenheim Mbali ya kupata mapokezi mabaya mjini Kolon , lakini wageni katika ligi ya Bundesliga RB Leipzig walipata sare muhimu kwao , wakati timu zote hizo zikibakia bila kushindwa katika mchezo wa tano wa msimu huu, baada ya kutoka sare kwa bao 1-1.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments