Nigeria: Vikosi vya usalama vyadaiwa kuwaua 150 wa Biafra
Vikosi vya usalama nchini Nigeria vimewaua zaidi ya watu 150 waliokuwa wakifanya maandamano ya amani tangu mwezi Agosti mwaka 2015,kulingana na kundi moja la haki za kibinaadamu.
Amnesty International limesema kuwa jeshi la nchi hiyo lilitumia risasi na nguvu kupitia kiasi dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono Biafra ambao walikuwa wakitaka kujitenga kutoka kwa Nigeria.
Maafisa wa polisi wa Nigeria wamekana madai hayo kwamba walitumia nguvu kupitia kiasi.
Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa Amnesty International inalichafulia jina.
Ripoti hiyo ya Amnesty inatokana na mahojiano na watu 200,pamoja na zaidi ya wapiga picha 100 na wale wa video 87.
Miongoni mwa madai yaliopatikana katika ripoti hiyo ni yale ambayo Amnesty inayataja kuwa mauaji ya kiholela wakati watu 60 walipopigwa risasi katika eneo la Onitsha wakati wa siku mbili za kumbukumbu za Biafra mnamo mwezi Mei 2016.
Disqus Comments