Urusi yaionya Marekani na kuitaka isiishambulie Syria
Urusi imeionya Marekani isichukue hatua yoyote ya kijeshi, dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Syria.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Moscow, alieleza kwamba kuingilia kati kwa namna hiyo, kutasababisha yale aliyoeleza kuwa matokeo yatayotikisa Mashariki ya Kati nzima.Alisema, iwapo mshirika wa Urusi nchini Syria, Rais Bashar al-Assad, atatolewa madarakani, kutafuata pengo, ambalo haraka, litajazwa na magaidi.
Matamshi hayo yametolewa wakati wa mvutano mkubwa baina ya Urusi na Marekani, kuhusu mashambulio ya mabomu yanayoendelea, dhidi ya Aleppo.
Disqus Comments