-->

Merkel aahidi kuisaidia Mali kupambana na ugaidi

Akifanya ziara yake ya kwanza nchini Mali, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, ameahidi kuisaidia nchi hiyo kupambana na Ugaidi akisema kuwa tatizo hilo bado ni kubwa nchini humo Alisema ana wasi wasi kuwa makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi kati ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha Kaskazini mwa nchi bado hayajatekelezwa. Kwa sasa Ujerumani ina wanajeshi 430 nchini Mali kama sehemu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali (MINUSMA) Merkel aliwasili nchini Niger leo asubuhi wakati wa awamu ya pili ya ziara yake kwenye nchi tatu, ambayo ataikamilisha nchini Ethiopia.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments