-->

Majaji wafisadi wakamatwa Nigeria, fedha zakamatwa

Wapelelezi nchini Nigeria wamekamata mamia kwa maelfu ya dola fedha taslimu na mali nyingine katika msururu ya upekuzi kupambana na ufisadi uliowalenga majaji waandamizi. Hatua hiyo imezusha shutuma kali kutoka kwa chama cha majaji na makundi ya kutetea haki za binaadamu. Wakati wa operesheni hiyo ya kitaifa, ambayo ilifanywa jana, polisi pia waliwatia mbaroni majaji kadhaa ijapokuwa idadi yao haijabainika. Katika taarifa, Idara ya Huduma za Taifa imesema ilikamata dola 800,000 fedha taslimu wakati wa operesheni hiyo ambayo ilifanywa kwa misingi ya "madai ya rushwa na utovu wa nidhamu miongoni mwa majaji". Fedha zilizokamatwa zilikuwa katika sarafu mbalimbali, za Nigeria na za kigeni. Rais Muhammadu Buhari alichaguliwa mwaka jana, kutokana na ahadi yake ya kupambana na rushwa.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments