Guterres kuchukua nafasi ya Ban Ki Moon
Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa baada ya kupata hakikisho kutoka kwa wanachama watano wakudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Idhinisho hilo lisilo rasmi litathibitishwa leo Alhamisi katika kura rasmi, kabla ya kupelekwa katika mkutano mkuu kwa ajili ya kuchaguliwa kwa kauli moja.
Antonio Guterres ambaye ni balozi wa Umoja wa Mataifa, ametumika kama Kamishna mkuu katika shirika la Wakimbizi kwa miaka 10.
Iwapo ataidhinishwa, atashika nafasi hiyo mwaka mpya, muda ambao Katibu mkuu wa sasa Ban Ki Moon atastaafu.
Uteuzi wake huo umekuja licha ya jitihada zilizokuwa zikichiukuliwa kuweza kumpata Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Mwanamke.
Disqus Comments