-->

Uyoga watunza msitu wa Nou nchini Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi zinazopoteza misitu kwa kasi duniani kulingana na takwimu za benki ya dunia (world bank) na wanasema ikiendelea kwa kasi hiyo kwa miaka hamsini ijayo, Tanzania itakuwa haina misitu tena. Lakini katika msitu wa Nou uliopo Manyara,kaskazini mwa Tanzania,baadhi ya wanakijiji wanaouzunguka msitu huo wameanzisha mbinu ya kutumia uyoga kama njia mbadala ya kujipatia kipato na kuokoa msitu huo
Ingawa Uyoga umekuwa ukitumika katika maeneo haya tangu zamani lakini ulikuwa hautumiki kama zao la kibiashara mpaka wakazi wa eneo hilo walipohamasishwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Farm Africa na kuanza kuona faida za kilimo cha uyoga.
Lawrence Kileo ambaye ni afisa uwezeshaji kutoka shirika la Farm Afrika, mkoa wa manyara anasema tangu wanakijiji hao wapate elimu juu ya ulimaji wa kisasa wa uyoga ,watu wengi wamehamasika kufanya biashara hiyo na hata soko la uyoga limekua kwa kasi ndani ya Manyara na nje ya mji huo,na sasa uyoga unatumika kama mbadala wa nyama na unawapa kipato kikubwa zaidi ya ukataji miti". Huku meneja wa misitu ,halmashauri ya Mbulu mkoa wa Manyara,William Kaaya anasema ushirikiano kati yao na jamii inayozunguka msitu huo ndio siri ya mafanikio katika utunzaji mazingira ya msitu wa Nou. Mbinu hii imekuja mara baada ya ongezeko kubwa la uhitaji wa mbao kutoka nje ya maeneo ya msitu huo,na kuwafanya wakazi wa eneo hilo kuona ukataji wa miti ndio njia rahisi na muhimu katika kijipatia kipato.
Mbegu za uyoga zenye thamani ya dola moja zinawapa faida ya dola arobaini ndani ya mwezi mmoja,hivyo shughuli za ulimaji uyoga zinaonekana kuwapa faida zaidi tofauti na ukataji miti holela.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments