Urusi na Marekani zashindwa kukubaliana kuhusu Syria
Nchi hizo zimeshindwa kufikia muafaka juu ya namna ya kufufua makubaliano ya kusitisha mapigano Syria. Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, sasa aelekea kukata tamaa kuhusu amani kurejea
Hayo yamejitokeza katika Syria mkutano ambao mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika mzozo wa Syria Stefan de Mistura ameuita wenye machungu, mgumu na wenye kukatisha tamaa.
Kundi la kimataiafa linaloiunga mkono Syria, ikiwemo Marekani, Urusi na mataifa mengine yenye nguvu, lililikutana kandoni mwa mkuno wa mwaka wa Umoja wa Mataifa, unaowakutanisha viongozi wa ulimwengu mjini New York wakati jeshi la Syria likiwa limetangaza kuanza mashambulizi mapya ya kijeshi katika eneo linalodhibitiwa na waasi mjini Alepp
Disqus Comments