-->

Vyoo vilivyojengwa kwa vioo vyazinduliwa nchini China

China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani. Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo. Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani. Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo. Daraja refu zaidi la kioo limefunguliwa China Daraja la Uchina la vioo kufungwa wiki 2 zijazo Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi. Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments