-->

Kim Kardashian azuiliwa na watu wenye silaha Paris

Nyota wa televisheni nchini Marekani Kim Kardashian alishambuliwa na kuzuiliwa na watu waliokuwa na silaha katika hoteli moja mjini Paris, taarifa zinasema. Msemaji wake anasema nyota huyo wa uigizaji wa vipindi vya maisha ya uhalisia alizuiliwa na watu waliokuwa wamejifanya maafisa wa polisi na ambao walikuwa wamejifunika nyuso zao. "Ameshtushwa sana na tukio hilo lakini hajaumizwa," msemaji wake amesema.
Mumewe Kanye West amekatisha ghafla tamasha ambayo amekuwa akishiriki mjini New York. Kanye West alikuwa akitumbuiza katika tamasha ya Meadows Music and Arts Festival na amesitisha ghafla utumbuizaji na kuwaambia mashabiki kwamba alikuwa na "dharura ya kinyumbani". Mtoto wa Kim na Kanye West aitwa Saint West Kim Kardashian aonywa ngono za kila mara "Nawaomba radhi, nina dharura ya kinyumbani na inanibidi kukomea hapa kwa sasa," West aliwaambia mashabiki. Kardashian West alikuwa ameenda Paris, pamoja na mamake Kris Jenner na dadake Kendall Jenner, kuhudhuria maonyesho ya mitindo. Alihudhuria maonyesho ya Givenchy Jumapili jioni.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments