-->

News Serengeti Boys yatimkia Rwanda

Leo September 22, kikosi cha timu ya taifa ya vijana U17 maarufu kama Serengeti Boys kimesafiri asubuhi kuelekea Rwanda kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville.
Serengeti Boys ilipata ushindi wa magoli 3-2 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa taifa hivyo kubakiza mechi moja tu ya ugenini ambayo itaamua kama vijana hao wa kitanzania watafuzu kucheza fainali za Afrika kwa vijana zinazotarajiwa kupigwa Madagascar.
Kocha mkuu wa Serengeti Bakari Shime jana alisema, watanzania hawatakiwi kuwa na hofu juu ya kikosi chao na matokeo waliyopata kwenye uwanja wa nyumbani kwasababu anawaandaa vijana kupata matokeo wakiwa ugenini Congo Brazzaville.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments