NYUMBA YA MAAJABU
[MTUNZI;Atuganile Ilikuwa ni siku ya furaha sana walipohamia kwenye hii nyumba nzuri na ya kupendeza, tena iliyovutia katika macho ya watu wengi sana.
Mke alisikika akimuuliza mume wake,
“Ibra, uliwezaje kuwekeza pesa nyingi za kununua nyumba nzuri kama hii?”
“Mke wangu Sophia, kwakweli mambo ya Mungu ni mengi sana, hata mimi sikutegemea kupata nyumba kama hii kwa ile pesa ambayo nilikuwa nayo. Kwakweli tushukuru tu kwa kupata mwanga wa maisha”
“Nadhani sasa mipango yetu itatimia mpenzi”
“Ndio mke wangu kwa hapa lazima mipango itimie”
“Hivi tulipanga kuzaa watoto wangapi vile?”
“Watatu tu wanatosha mke wangu”
“Baby kwa jinsi nyumba ilivyokubwa kwanini tusifanye wanne!”
“Wewe ndio mzaaji mke wangu kwahiyo vyovyote tu inawezekana”
Sophia akakumbatiana na mume wake kwa furaha kwani hii ilikuwa ni moja ya ndoto zake kwenye maisha.
Baada ya wiki moja, Sophia aliamua kwenda kuwatembelea majirani zake wa sehemu aliyokuwa akiishi mwanzoni. Alifika na kuwakuta wakiendelea na shughuli za hapa na pale kama kawaida, moja kwa moja aliamua kwenda kwa rafiki yake wa pekee Siwema ambapo alikaribishwa vizuri sana na rafiki yake huyo.
“Yani Sophia kama usingekuja kunisalimia kwakweli ningekuona ni mtu wa ajabu sana.”
“Hivi Siwema naachaje kuja kukusalimia wewe! Nitakuwa nimerogwa basi, tena nitakuwa ni binadamu asiye na wema wala shukrani”
“Eeh hebu kwanza niambie shoga yangu mmehamia wapi maana si kwa mbwembwe zile za kuondoka hadi vigoda vyako umeacha”
“Shoga mwenzangu, yani wewe ni shoga yangu wa damu kwakweli na kukuficha siwezi. Kwakweli mwenzio nadhani kuna vitu Ibra alikuwa ananificha”
“Kivipi? Na vitu gani hivyo alivyokuwa anakuficha?”
“Hivi unaweza kuamini kwamba Ibra amenunua nyumba na gari!”
“Mmh kwa hela gani? Katoa wapi hiyo pesa ya kununua nyumba na gari?”
“Tena ninavyokwambia nyumba ni nyumba haswa shoga yangu wala sio nyumba uchwara, nitakupeleka na wewe ukajishangalie maajabu ya mume wangu Ibra”
“Mmmh kwahiyo shoga biashara ya mamantilie hufanyi tena?”
“Naanzaje kufanya biashara ya mama ntilie kwenye nyumba ile! Shoga hujaiona na wala sijisifii tu, kwakweli Ibra ana pesa, mpango wangu kwasasa ni kuzaa tu nicheze na wanangu pale maana nikichelewa nitakuta mwana si wangu”
“Shoga tusiandikie mate wakati wino upo, ujue umenitamanisha sana, naomba twende sasa hivi na mimi nikajishuhudie huo mjengo. Ngoja nijiandae fasta twende.”
Sophia akakubaliana na Siwema pale kwahiyo akamsubiri ajiandae ili aweze kwenda nae.
Siwema na Sophia walifika kwenye nyumba husika ambapo nje tu ya nyumba hiyo Siwema alibaki kushangaa na kuduwaa kwani hakutegemea kama ile nyumba ipo vile kama alivyoikuta.
“Khee jamani Sophia mbona umeokota dodo kwenye muharobaini shoga yangu, hebu jibebeshe mimba mapemaa maana hapa utashangaa ushaibiwa shoga yangu”
“Yani hapa ninachotaka ni kuzaa tu, yani toka nimeuona huu mjengo na dawa za uzazi wa mpango nikaziacha pale pale saivi nawaza watoto wa kucheza nae kwenye nyumba hii”
“Hongera sana shoga yangu ila kuwa makini na Ibra maana asije akakuletea mke mwenza bure”
“Thubutuu huyo mke mwenza atapitia mlango gani!! Labda sio Sophia niliyepo humu ndani”
“Nakuaminia Sophia, kama uliweza kumchunga Ibra kule uswahilini ndio ushindwe kumchunga kwenye huu mjengo”
“Hapo sasa, yani hapa Ibra hazungushi amefika hapa Kigoma mwisho wa reli”
Sophia alikuwa akifurahi tu na shoga yake huyu, na leo walipika pamoja na kula pamoja hadi joini ambapo mume wa Sophia aliwasili kutoka kwenye mihangaiko yake ambapo alimkuta Siwema pale kasha Siwema akawapa hongera zao na kuwaaga.
“Hongera sana shemeji yangu Ibra, ila mimi ndio naomdoka shemeji”
“Mmh shemeji jamani ndio haraka haraka hivyo!”
“Shemeji nilikuwepo hapa tangu muda ila nitakuja tena maana ndio nishapapenda tayari ila saizi wacha niende”
Basi Ibra hakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kumuaga tu huyu Siwema.
Kisha Sophia akatoka na kwenda kumsindikiza rafiki yake huyu,
“Kwakweli Sophia usizembee, pale ndio umshikirie vizuri Ibra yani umgande kama ruba maana ule mjengo si mchezo shoga yangu. Yani wambea wa mtaa watanikoma nitakavyokuwa najidai kuhusu wewe Sophy.”
Sophia akacheka tu kwani alikuwa akifurahia kile alichokuwa akiambiwa na Siwema.
“Usicheke tu Sophy ila yafanyie kazi maneno yangu”
“Ondoa shaka dada, mambo yataiva tu maana hata mimi nimetamani kuwa na watoto kwasasa”
Wakabadilishana mawazo pale kasha Siwema akapanda daladala na kuagana vyema huku Sophia akisisitiza kuwa awasalimie majirani zao wengine.
Sophy alirudi nyumbani kwake, kwavile giza nalo lilianza kuingia ikabidi aandae chakula cha usiku, na kilipokuwa tayari alikaa na mumewe na kuanza kula huku wakitabasamu.
“Mmmh Sophy muda wote unatabasamu tu mke wangu”
“Hivi naachaje kutabasamu Ibra!! Bahati tuliyoipata ni kubwa sana mume wangu kwakweli sikutegemea kama ipo siku tutaishi kwenye nyumba nzuri na kubwa kama hii, si unajua tulizoea chumba kimoja tu yani jiko hapo hapo, viti, vyombo, kitanda hapo hapo yani shaghalabhagala lakini sasa hivi eti tunaishi maisha ya kitajiri namna hii lazima nitabasamu mume wangu.”
Wakamaliza kula kasha Sophy akatoa vile vyombo na kuvipeleka jikoni huku akitaka kuviosha kwanza ndimbo aende kulala na mumewe, ila Ibra alimfata kule jikoni na kumwambia,
“Sophy mke wangu, vyombo utaviosha kesho bhana hebu twende tukalale”
Sophy akatabasamu kisha akaacha vile vyombo na kuongozana na mumewe hadi chumbani ambako muda mwingi walionekana wakitabasamu.
Kisha wakaenda kuoga pamoja na kurudi kitandani, Ibra alimkumbatia Sophy na kumuuliza tena,
“Hivi ulisema tuzae watoto wangapi vile?”
“Wanne mume wangu au wewe hupendi”
“Mmmh hakuna kitu ambacho unakipenda wewe halafu mimi nisikipende, si unajua jinsi nikupendavyo Sophy! Yani mimi na wewe letu ni moja mke wangu”
“Tena napenda wawili wawe wa kike halafu wawili wa kiume”
“Wow ni mpango mzuri sana hakuna tatizo, tutazaa kadri Mungu atakavyo tujaalia Sophy wangu.”
Wakatabasamu kisha wakalala kama kawaida.
Kulipokucha, kama ilivyoada Ibra aliamka mapema sana kisha akajiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kazi zake, Sophy alitaka kujaribu kuinuka ili kumuandalia mambo mbalimbali mumewe ila ibra alimzuia na kumtaka mkewe aendelee kupumzika tu ambapo naye alifanya hivyo kwani alielewa ni jinsi gani Ibra alimpenda.
Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, Sophy nae aliamka na kwenda kuoga ili kujiandaa kwa mambo ya hapa na pale.
Akaenda jikoni kwa lengo la kutaka kuosha vyombo vya jana na kujiandalia chakula cha asubuhi, ila alishangaa kuona vyombo vilishaoshwa na vilipangwa vizuri kabatini.
Hali hii ikamfanya Sophia ajiulize kuwa huenda Ibra alimzuia kuamka muda ule ili afanye kile kitu cha kumsahangaza. Kwakweli Sophia alitabasamu kwa jambo hili kwani aliweza kuona ni jinsi gani Ibra anampenda sana.
“Najua Ibra ananipenda sana ila safari hii kazidisha mapenzi jamani mmh yani amefikia hatua hata ya kunitaka mimi nilale halafu yeye akaosha vyombo, haya ni mahaba tena motomoto kwakweli nina kila sababu ya kumzalia watoto Ibra wangu. Kipindi kile nilikuwa najibana kuzaa sababu ya maisha duni ila kwasasa nina kila sababu ya kuzaa kwakweli.”
Kisha akajiandalia chakula pale na kuanza kukila halafu naye akatoka kwa lengo la kwenda kwenye mihangaiko yake mbalimbali.
Wakati yupo nje ya nyumba hiyo kuna mmama alipita na kumsalimia Sophia kisha Yule mama akamuuliza Sophia kama ndiye anayeishi mule ndani,
“Unaishi humo ndani dada?”
“Ndio mama”
Sophia akahisi kuwa huyu mama labda anamuona kuwa haendani na hiyo nyumba, ikabidi amuulize
“Kwani vipi mama yangu! Kuna tatizo?”
“Hapana ila sisi ni majirani kwahiyo ni vyema tukafahamiana, mimi naitwa mama Jane na wewe je?”
“Mimi naitwa Sophia, na hapa naishi na mume wangu yeye anaitwa Ibra”
“Basi ni vizuri, karibu kwangu nyumba ya jirani tu hapo”
“Asante nitakaribia”
“Karibu sana, usiogope kitu sisi ni majirani tu na ni vyema kufahamiana ingawa kufahamu watu waishio humo huwa ni ngumu sana”
“Usijali utatufahamu tu”
Kisha Sophia akaagana na huyu mama halafu yeye kuendelea na safari zake.
Jioni ya siku hiyo Sophia akiwa ndani na mumewe akamsimulia kuhusu huyo mama aliyekutana nae wakati anatoka na vile alivyozungumza nae,
“Kwakweli ni vizuri kufahamiana na majirani ukizingatia tangia tumefika hapa hakuna jirani tuliyemsogelea kumsalimia”
“Basi tutafanya hivyo mume wangu. Ila kitu kingine sasa mmmhh”
Sophy akatabasamu kwanza kabla ya kuongea na kumfanya Ibra amuulize,
“Kitu gani hiki mpaka umeguna Sophy?”
“Mmh naona mapenzi yamenoga mume wangu hadi leo umeosha vyombo!”
Ibra akacheka kisha akasema,
“Mmh acha kunichekesha Sophy yani na uvivu huu mimi nikaoshe vyombo kweli!!”
“Sasa nani kaviosha vile vyombo asubuhi?”
“Nikuulize wewe uliyebaki nyumbani”
Sophia akakaa kimya kwa muda kwanza kwani hakuelewa hapo.
ophia akakaa kimya kwa muda kwanza kwani hakuelewa hapo, akamuangalia mumewe kanakwamba amwambie kuwa alichokuwa anakisema kilikuwa ni utani tu kisha akamwambia tena,
“Acha masikhara Ibra”
“Wewe ndio uache masikhara, unajua fika kuwa mimi ni mvivu wa kimataifa haya sasa huko kuosha vyombo ningeanzia wapi? Hebu kaandae chakula tule kwanza”
“Lakini Ibra….”
“Lakini nini Sophy? Wewe kaandae chakula tule bhana, mada zingine achana nazo usifikirie ni rahisi hivyo mimi kuosha vyombo”
Sophia akaenda jikoni huku akiwa na mawazo sana ila kuna wakati alihisi kuwa Ibra anatania tu kwani kule ndani walikuwa wao wawili tu kwahiyo akahisi kuwa ni lazima Ibra ndio aliosha hivyo vyombo ila anajigelesha tu, alijiaminisha hivyo huku upande mwingine akiwa na mashaka kiasi.
“Kesho nitampigia simu Da’ Siwema nimsimulie, Yule ni mtu mzima anaelewa vizuri sana”
Kisha akaendelea na uandaaji wake wa chakula cha usiku.
Akapeleka mezani na kuanza kula na mumewe Ibra,
“Yani leo nimechoka Sophy maana nimejikuta nikiwa na kazi nyingi sana”
“Pole mume wangu ila ndio ukubwa huo”
“Kweli kabisa ukubwa jalala maana sio kwa kuchoka huku”
Walipomaliza kula, leo Sophia hakutaka kuacha vyombo vichafu kwahiyo alienda kuviosha na kuvipanga kisha kwenda chumbani kulala na mume wake ambapo alimkuta ameshalala tayari.
“Mmmh kweli leo Ibra kachoka jamani maana yupo hoi kabisa”
Kisha na yeye akatafuta usingizi pale na kulala, alipopitiwa na usingizi tu akajiwa na ndoto.
Kwenye ndoto hii alijiona yeye akiwa mjamzito ila mumewe alionekana kutokuifurahia kabisa ile mimba na alionekana kuongea maneno machafu sana ya kumkaripia,
“Aliyekwambia ubebe mimba nani? Na utaenda kuzalia kwake huyo mtu, sitaki ujinga mimi”
Sophia akashtuka sana kutoka kwenye ule usingizi huku akiilaani ile ndoto na kuona kuwa ni kitu cha ajabu sana kwake kwani haikuwa rahisi kwa Ibra kuikana mimba yake kiasi hicho ila ndoto hiyo ilimfanya asipatwe na usingizi tena hadi panakucha.
Ibra alipoamka tu, Sophy nae alikuwa macho na swali la kwanza ambalo Sophy alimuuliza Ibra ilikuwa ni kuhusu mimba.
“Hivi kwa mfano mimi nikiwa na mimba yako je utafurahi mume wangu?”
“Sophy, ninavyokupenda hivi naachaje kufurahi? Pia nahitaji mtoto Sophy wangu, na mimi napenda niitwe baba. Nakupenda sana mke wangu, najua watoto ndio watakamilisha furaha yetu mpenzi.”
“Asante Ibra”
Kisha Ibra akaanza kujiandaa pale halafu akamuaga Sophy kwa kumbusu kwernye paji la uso.
Ibra alipoondoka tu, Sophy nae akaamka na kwenda kukaa sebleni ili kujipotezea mawazo mbalimbali huku akiona wazi kuwa ile ndoto ni uchizi tu na ni kitu cha kusadikika.
“Ndoto zingine kama zimetumwa loh! Ndoto gani sasa ile? Yani Ibra kabisa akane mimba thubutuu, yani ile ndoto ishindwe na ilegee ujinga ujinga sitaki.”
Muda ulipoenda kidogo akampigia simu Siwema na kuanza kuzungumza naye kuhusu kilichotokea jana na vile ambavyo Ibra alimjibu kuwa hakuosha hivyo vyombo.
“Hayo ndio mahaba mdogo wangu, mwenzako Ibra anakupima tu lakini vyombo kaosha mwenyewe, we unadhani ataosha nani wakati ndani mpo wawili tu?”
“Ndio hapo dada nimeshindwa kuelewa kwakweli maana mimi nimekuta vimeoshwa halafu ni yeye aliyesema nisivioshe halafu anakataa kuwa hajaviosha loh!”
“Anakuchanganya akili tu huyo mdogo wangu, kwani wanaume hujawajua tu, wanapenda kutupima Sophy mdogo wangu. Hata usiwe na shaka mwaya mwenzio saivi anakuonyesha mahaba kimya kimya”
“Kweli dada haya ni mahaba maana ila hapendi kuosha vyombo, hata niumwe ataviacha hadi nipone ila kuona ameosha safari hii tena nikiwa mzima kabisa kweli ni mahaba”
“Ndio mapenzi hayo mdogo wangu hata usistaajabu sana, hapo ndio kupendwa yani wewe jiongeze tu.”
Sophia akafurahia sana ushauri aliopewa na Siwema kwani aliona ushauri huo ukimfaa sana, kisha akaagana nae kwenye simu na kuendelea na mambo mengine.
Wakati akifanya shughuli zake za hapa na pale mule ndani, akasikia hodi na kwenda kufungua mlango ambapo alimkuta Yule mama ambaye walikutana siku ya nyuma huku akiwa ameambatana na binti aliyeonekana kufanana nae sana, Sophia akawakaribisha vizuri sana watu hao ndani kwako huku akitabasamu,
“Karibuni sana jamani”
“Asante tumekaribia Sophy”
Wakaingia ndani huku Yule mama akianza utambulisho kwa binti aliyeongozana nae,
“Huyu ni binti yangu anaitwa Jane”
“Wow ndiomana umefanana nae sana mama, hongera kwa kuwa na binti mzuri”
Huyu mama akatabasamu kidogo kisha akaendelea,
“Nimeona ni vyema akufahamu jirani yetu ili hata siku akiwa mbweke nyumbani basi aje akutembelee, unajua huyu mtoto ametoka kumaliza kidato cha nne kwahiyo tunangoja matokeo tu kwasasa. Mara nyingi anashinda nyumbani kwahiyo akija kuongea ongea hapa si vibaya.”
“Umefanya jambo jema mama maana hata mimi huwa na upweke sana maana huwa nashinda mwenyewe mahali hapa, pia hongera sana Jane kwa kuhitimu kidato cha nne.”
“Unampa hongera ya bure tu huyu, akili yake yenyewe sijui kama atafaulu huo mtihani, na akifeli ndio atakaa nyumbani atafute mume aolewe tu”
“Jamani mama usiseme hivyo inakuwa kama unamuombea mabaya mtoto”
“Mabaya kajiombea mwenyewe hata sio mimi, mtu gani alikuwa anajijua kabisa kuwa ana mitihani ila ndio tamthilia sijui michezo kila kitu anakijua yeye na hatma yake inakuja kwakweli naona kabisa zero ikimuangalia.”
Jane alionekana kuwa kimya kabisa kwani ilionyesha wazi hakupendezewa na maneno ya mama yake, ili kuondoa ule mzozo ilibidi Sophia abadilishe mada kisha akaenda jikoni na kuwaletea wageni juisi huku wakizungumza mawili matatu.
Muda kidogo Ibra alirudi hata kumshangaza Sophia kwani alionekana kuwahi sana siku hiyo na alionekana kuwa na uchovu.
Sophia akamkaribisha mumewe na kumtambulisha kwa wale wageni ambao walifahamiana na kusalimiana, ingawa Ibra alikuwa amechoka ila alivunga kidogo kwenda chumbani ili wale wageni wasijihisi vibaya, ila huyu mama nae aliaga muda ule ule kwahiyo Sophia akatoa zile glass na kupeleka jikoni kisha akamuaga mumewe na kwenda kuwasindikiza wale wageni, ambapo Sophia alienda nao hadi nyumbani kwao ili kuweza kupafahamu wanapoishi watu hao.
Sophia aliweza kuona mazingira ya uswahili anayoishi huyu mama ila hakushangaa sana kwavile ndio mazingira ambayo hata yeye amekulia na ameyaishi kwa kipindi kirefu sana.
“Sophia, ukiwa na tatizo usisiste kuja, hapa ni kama nyumabani kwenu tu kwahiyo usiogope chochote”
“Usijali mama tupo pamoja”
Sophia hakukawia sana kwani aliaga na kuondoka.
Aliporudi nyumbani kwake hakumkuta Ibra pale sebleni na moja kwa moja akahisi kuwa Ibra atakuwa ameenda chumbani kupumzika tu, kisha nae akaenda chumbani alipo Ibra kwani alipenda kujua ni kwanini mumewe amechoka kiasi kile.
Alimkuta Ibra amejilaza kitandani, akamfata na kumsogelea karibu mumewe kisha akakaa pembeni yake na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
“Vipi tena Ibra mume wangu, nini kimekukumba baba?”
“Kwakweli hata sielewi ila nimechoka mwili na viungo vyote”
“Pole sana mume wangu, ngoja nikuandalie chakula ule kwanza ndipo ulale”
“Usijali kuhusu hilo, nilishaenda jikoni nimepakua chakula na nimekula tayari”
“Dah nisamehe mume wangu jamani”
“Usijali kitu mke wangu, wale ni wageni wetu sote kwahiyo hata usijali na ndiomana hata mimi sikuona tataizo kwenda jikoni na kujipakulia chakula”
“Pole sana mume wangu, basi ngoja nikakuandalie maji uoge”
“Kwakweli sijisikii kuoga kwasasa subiri nipumzike kwanza ndio nitaoga”
Sophia alitulia kwa muda akiitafakari hali ya mume wake kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Ibra kuwa vile alivyokuwa.
Alienda sebleni huku akihisi kuwa huenda Ibra akawa na malaria ila ndio hivyo anajikaza kwavile ni mwanaume, kisha akaelekea jikoni na kufunua sofuria alilopikia chakula na kukuta kweli kilipakuliwa kwamaana hiyo ni kweli Ibra amekula kile chakula kisha akaangalia Ibra alipoweka sahani aliyotoka kula nayo ila hakuona sahani wala nini hapo ndipo aliposhangaa na kwenda tena sebleni kuwa huenda ameiacha huko ila hakuona sahani yoyote chafu, wazo likamjia kuwa aangalie na zile glasi ambazo wageni wamenywea juisi ila hakuziona pale zaidi aliziona zimeshawekwa kabatini tena zikiwa safi kabisa,
“Mmh huyu Ibra si anaumwa huyu sasa iweje ameosha vyombo vyake alivyolia na zile sahani jamani wakati mtu ni mgonjwa? Haya ni maajabu mapya kwangu, sasa nitamuulizaje na anaumwa? Ila lazima nimuulize?”
Sophia akatoka jikoni na kuelekea chumbani tena alipo Ibra kwa lengo la kumuuliza kulikoni maana hakuelewa kabisa.
Alimkuta Ibra akiwa bado anagalagala tu kitandani kwani hata usingizi haukumjia, kisha akamuuliza,
“Mume wangu leo umechoka sana ila kwanini umeosha vyombo ulivyolia chakula?”
“Sophy, toka lini hunijui mimi jamani! Mimi naoshaje vyombo mke wangu, kwanza naumwa halafu wewe unaniletea habari zingine kwanini unakuwa hivyo Sophy?”
“Samahani mume wangu ila ningependa twende hospitali”
“Sijisikii kwenda hospitali kwakweli, tafadhali niache nipumzike”
Sophia hakumuelewa Ibra kabisa na akahisi huenda Ibra ana malaria ambayo imempanda kichwani na ndiomana amekuwa vile alivyokuwa.
Sophia aliamua kuinuka tena ili atoke mule chumbani ila kabla hajafika malngoni alijihisi kichefuchefu na kumfanya aanze kukimbilia chooni ili atapike ila kabla hajafika chooni alijikuta kashatapika tayari kwahiyo chooni alienda kama kumalizia tu na alitoka akiwa amechoka sana ila hakuweza kuvumilia kuangalia yale matapishi yake yaliyotapakaa chumbani kwao karibia na mlanngo wa chooni, hivyobasi Sophia akaenda jikoni kuchukua tambala na maji kwa lengo la kufuta matapishi yale.
Ila aliporudi chumbani ili afute alikuta yale matapishi yalishafutwa na pale palishakaushwa kabisa, kwakweli Sophia alichoka gafla, akamuangalia Ibra pale kitandani ila Ibra alionyesha kutokuwa na habari yoyote kwani alikuwa amejilaza vile vile.la aliporudi chumbani ili afute alikuta yale matapishi yalishafutwa na pale palishakaushwa kabisa, kwakweli Sophia alichoka gafla, akamuangalia Ibra pale kitandani ila Ibra alionyesha kutokuwa na habari yoyote kwani alikuwa amejilaza vile vile.
Sophia hakuelewa kwakweli yani hakuelewa kabisa, akaenda tena pale kitandani alipokuwa amejilaza Ibra na kumshtua, ambapo Ibra aliongea kwa kulalamika,
“Sophia jamani mbona hivyo mke wangu? Kwanini unanifanyia hivi lakini si nimekwambia kuwa najisikia vibaya! Sasa kwanini hutaki mwenzio nipumzike jamani unanifanyia mambo ya ajabu, kwanini kunishtua shtua kila muda?”
“Samahani Ibra lakini nani kazoa matapishi yangu?”
“Matapishi?”
“Ndio, kwani hukunisikia wakati natapika?”
“Sijakusikia bhana, unanisumbua tu Sophy hebu acha nipumzike”
Ibra akageuka tena na kulala, kwakweli Sophia hakuelewa chochote alijikuta akijishika tama tu kwa mawazo kwani aliona kama vile Ibra anamchanganyia mada huku nayeye akizidi kujiuliza kuwa kama sio Ibra anayefanya hayo je yatakuwa yanafanywa na nani? Hapo ndio ilikuwa ngumu kabisa kwa yeye kuelewa.
Akajikuta akikaa pale kitandani huku akitafakari kwa muda mrefu sana bila ya kupata majibu hadi akapata wazo la kumpigia simu tena Siwema ili amuulize ila aliona kamavile ni kumsumbua tu huyo Siwema, kwahiyo akatulia kimya kwa muda mrefu kidogo kisha akainuka pale na kuelekea jikoni kwa lengo la kuandaa vizuri mlo wa usiku.
Akiwa jikoni alijiuliza sana kitu kilichopelekea yeye kutapika ni nini,
“Hivi ni kwanini nimetapika ikiwa siumwi wala nini? Ni kitu gani kimepelekea mimi kutapika?”
Alijiuliza bila ya kupata jibu la aina yoyote ile kwahiyo akaamua kuandaa chakula tu.
Alipomaliza kuandaa chakula alitoka jikoni na kuelekea sebleni ambapo alimkuta mumewe amekaa na kwakweli alionekana kuwa sawa kabisa kwasasa tofauti na mwanzo,
“Khee Ibra kumbe umeamka tayari!”
“Ndio nimeshaamka”
“Eeh unajisikiaje na hali!”
“Nipo salama kabisa mke wangu”
“Basi ngoja nikakuandalie maji ya kuoga”
“Hata usijali mke wangu nimeshaoga labda ulete chakula tule”
Basi Sophia hakutaka kuhoji zaidi kwahiyo akaenda kuleta chakula kisha yeye na mumewe wakaanza kula chakula hicho huku wakizungumza mambo mawili matatu,
“Kwahiyo Ibra saivi unajiona umepona kabisa!”
“Ndio nimepona kwani nilikuwa naumwa sana eehh!”
“Yani hadi mimi ulinitia mashaka mume wangu mpaka hofu ilinitawala kabisa”
“Hata usiwe na mashaka mke wangu maana mimi ni mzima kabisa kabisa”
“Basi vizuri mume wangu kama ndio hivyo”
“Ila nakushukuru sana Sophy kwa mapenzi yako unayonionyesha na jinsi unavyonijali”
Sophia akatabasamu huku wakiendelea kula kile chakula, walipomaliza kama kawaida Sophia alitoa vyombo na kutaka kwenda kuviosha ila Ibra alimuita na kumfanya Sophia asioshe vyombo vile.
“Sophy mke wangu napenda nikae na wewe tupumzike pamoja”
“Naelewa mume wangu ila huwa sipendi kulala na vyombo vichafu ndani ndiomana huwa napenda kuviosha pindi tunapomaliza kula”
“Ngoja nikuulize swali, kwani kesho unaenda wapi?”
“Nipo tu siendi popote”
“Sasa tatizo liko wapi hapo? Utaosha hata kesho, mi napenda tukae tuzungumze na tupumzike pamoja”
Ikabidi Sophia atumie nafasi hii kumuuliza Ibra kuhusu matapishi yake,
“Hivi Ibra hukunisikia wakati natapika?”
“Kwani unaumwa?”
“Hapana ila nilitapika”
“Mmmh sijakusikia kwakweli”
“Mmmh kwahiyo nani alizoa matapishi yangu?”
“Mmmmmh Sophy acha habari hizo bhana tumetoka kula, hebu tubadilishe mada”
Sophia hakuwa na jinsi zaidi tu ya kufata matakwa ya Ibra na kisha wakaamua kwenda kulala, Ibra alipopitiwa na usingizi Sophia akakumbuka vile vyombo akaona ni vyema akavioshe ili asipate tena maswali ya kujiuliza kuwa vyombo vimeoshwa na nani, kwahiyo akatoka mule chumbani na kwenda jikoni kwa lengo la kuosha vyombo.
Alivikuta vyombo vipo pale pale jikoni na kisha akaanza kuviosha, muda kidogo alikuja Ibra kutoka chumbani huku akitikisa kichwa baada ya kumkuta Sophia akiosha vyombo,
“Ona sasa mke wangu halafu unakazana kuuliza nani kaosha vyombo wakati unaamkaga mwenyewe usiku wa manane kuviosha jamani unakuwa kama mwanga, majukumu gani hayo ya usiku wa manane?”
“Unajua nini Ibra sikupenda nipate tena shida ya kudadisi juu ya mtu aliyeosha vyombo ndiomana nimeamua kuviosha mwenyewe”
“Kwakweli umenishangaza Sophy yani nashtuka kitandani sikuoni kumbe upo jikoni unaosha vyombo, jamani mke wangu kwanini unakuwa hivyo jamani? Nadhani mtu yeyote atakayesikia hili lazima ashangae, kwani kuna umuhimu gani wa kuosha vyombo usiku kamavile hapatakucha?”
Ibra alionekana kutokupendezwa kabisa nah ii tabia aliyoiona leo kwa Sophy kwani yeye alipenda anapogeuka kitandani basi amkute mkewe akiwa pembeni,
“Basi nisamehe mume wangu, nakuahidi hii hali haitajirudia tena kama nikishindwa kuosha muda ambao tumemaliza kula basi nitakuwa nasubiria hadi kesho yake. Nisamehe tafadhari”
Basi akavimalizia na kuviacha pale juu huku akipanga kuviweka kabatini kesho yake kwani hakutaka kumkwaza mume wake zaidi.
Wakaongozana pamoja kuelekea chumbani ambapo Ibra alionekana kutokuwa na usingizi sana kwani yote ilitokana na vile alivyolala jioni ya siku hiyo, kwahiyo walivyofika tu kitandani Ibra akaanzisha maongezi tena.
“Hivi ulisema kuwa leo umetapika eeh”
“Ndio nimetapika”
“Basi kama hiyo hali itaendelea itabidi twende hospitali”
“Kama ikijirudia tutaenda mume wangu, asante kwa kunijali”
“Unajua Sophy mi nakupenda sana na kwakweli sipendi kuona ukisumbuka wala kuhangaika mke wangu ndiomana unaniona mara nyingine nafoka”
Kisha akamsogelea karibu na kumkumbatia ili waweze kulala, na kweli usingizi ukawapitia hadi palipokucha ambapo kama kawaida Ibra aliamka na kujiandaa kisha kumuaga mkewe na kwenda zake kazini.
Sophia nae kama kawaida yake alipoamka alienda moja kwa moja jikoni ambapo alikuta vile vyombo alivyoviosha usiku vikiwa tayari vimepangwa kabatini,
“Yani huyu Ibra ananikatazaga mimi ili afanye yeye ila ni sawa tu maana yupo kwenye harakati za kunionyesha upendo”
Alipofikilia hayo akaenda kuandaa chai na kunywa halafu akaenda kuloweka nguo ili afue, baada ya kuziloweka alirudi sebleni ili akae angalau kidogo halafu ndio akafue ila alivyokaa pale sebleni akapatwa na usingizi wa gafla uliomfanya alale hadi kujisahau kuwa alipanga kwenda kufua nguo zake.
Ibra alirudi nyumbani na kugonga sana ila kwa bahati nzuri tu alikumbuka kuwa anafunguo za ziada kwenye gari lake kisha akaenda kuchukua funguo zile na kufungua milango ambapo alimkuta Sophia akiwa amelala tena hajitambui kabisa, ikabidi Ibra ndio amshtue Sophia kutoka kwenye ule usingizi aliokuwa amelala ambapo Sophia alionekana kushtuka sana.
“Kheee Sophia ndio kulala gani huko hadi umejisahau yani nimegonga na kugonga ila wapi”
Ila Sophia alionekana kuchoka sana hata akajikuta anashindwa kumjibu mumewe kwa wakati, hadi alipotulia kidogo kama kurudisha akili yake vile ndio akaweza kumjibu mume wake,
“Yani hata sijielewi ila nimechoka balaa”
“Mmh hata kupika umepika kweli wewe?”
“Kwakweli sijapika wala sijafanya chochote kile yani hata sijielewi”
“Pole sana mke wangu basi twende tukajimwagie upate nguvu kisha twende tukale hotelini maana hamna namna tena”
Sophia akakubali na kuzidi kuuona upendo wa Ibra juu yake kuwa Ibra anampenda na kumuhurumia sana kwani ile iliweza kuonyesha ni kwa kiasi gani alipendwa na Ibra.
Walipomaliza kujiandaa wakatoka na kuelekea hotelini kama ambavyo Ibra alisema ili kuweza kula, waliagiza chakula na kuanza kula ila gafla Sophia akapatwa na kichefuchefu na kujikuta akikimbilia nje kutapika, Ibra alivyoona vile akamuomba muhudumu awafungie kile chakula kisha akaenda kumuangalia mke wake,
“Kwani unajisikiaje Sophy”
“Najisikia vizuri tu”
“Vizuri wakati umetapika jamani! Itabidi kesho twende hospitali tukaangalie afya yako”
Sophia akakubali kisha akaja Yule muhudumu na kuwapa chakula chao ambapo Ibra alilipia na kuondoka na mke wake.
Walipofika nyumbani waliweka kile chakula na kuanza kula tena ila Sophia alionekana kula kwa kujivuta vuta sana,
“Lazima unaumwa Sophy ingawa wewe mwenyewe unajiona kuwa mzima”
“Ni kweli kabisa najiona kuwa mzima mimi”
“Hata kama unajiona ni mzima lazima kesho twende hospitali maana hii hali ni mbaya mke wangu”
“Sawa nimekuelewa kwa hilo”
Walipomaliza kula, Ibra alibeba vile vyombo na kuvipeleka jikoni kisha akamtaka mke wake kuwa waende kulala,
“Ila sina usingizi Ibra”
“Hata kama, ila mi nakuomba twende tu chumbani”
Kisha wakaelekea chumbani na moja kwa moja wakaenda kitandani ambapo ibra alikuwa akimuangalia sana mke wake kwani aliona wazi kuwa lazima atakuwa anaumwa tu ila anajikaza.
Kulipokucha, asubuhi na mapema Ibra akamuamsha mke wake ili aweze kujiandaa na waweze kwenda hospitali ambapo Sophia alifanya hivyo ila alipomaliza kujiandaa akamwambia mume wake,
“Lakini unajua Ibra mi siumwi kabisa na wala hata sijisikii vibaya”
“Unaweza ukajiona kuwa huumwi kumbe ugonjwa upo ndani kwa ndani, usifikiri ni kitu rahisi kutapika vile Sophia usiwe mbishi kwani mi nakuona kabisa kuwa unaumwa”
“Na hospitali tutaenda kujielezaje sasa?”
“Tutajieleza kama hali halisi ilivyo”
“Ila bado mimi sidhani kama naumwa kwani nahisi ni uchovu wa jana tu”
“Uchovu wa jana umefanya kazi gani?”
Sophia akafikiria kidogo na kukumbuka kuwa aliloweka nguo,
“Mmmh jana nililoweka nguo ila sikuzifua mmh si zitanuka jamani maana nilisahau kabisa”
“Basi usijali tutafua pamoja tukirudi”
Sophia akatabasamu kisha akatoka na mume wake kwa lengo la kwenda huko hospitali, ila alipofika malangoni akakumbuka kitu kwenye zile nguo alizokuwa ameloweka jana yake ikabidi amwambie mumewe amsubiri akachukue.
Alipofika uwani ambako aliloweka zile nguo alikuta zote zikiwa kwenye kamba tena zilionekana kukauka kabisa, kwakweli Sophia akashangaa sana na kumita Ibra kwa nguvu ili kumuonyesha kile anachokiona.
Ibra nae alifika kwa haraka sana kama alivyoitwa na Sophia, kisha Sophia akamuonyesha nguo kwenye kamba ambapo Ibra aliuliza kwa mshangao
“Kwani vipi Sophy?”
“Nguo kafua nani?”
“Nguo kafua nani kivipi?”
“Kwani wewe huoni nguo kwenye kamba?”
“Naziona ndio kwani tatizo nini?”
“Nani kazifua sasa wakati mimi niliziloweka tu!”
Ibra alikuwa akimshangaa tu mkewe ambapo kabla hata hajasema chochote, Sophia alianguka chini na kuzimia.Ikabidi Ibra ambebe mke wake na kwenda kumpakia kwenye gari kisha kumpeleka moja kwa moja hospitali huku akihisi kuwa pengine mkewe ana maralia imempanda kichwani ndiomana anaongea mambo yasiyoeleweka.
Walifika hospitali na moja kwa moja kupokelewa na wahudumu wa hospitali ile ambapo muda kidogo tu Sophia alionekana kuzinduka na kuwa sawa kiasi ambapo Ibra aliingia na mkewe kwa daktari na kuelezea kwa kifupi matatizo ya mke wake ambapo daktari aliwatajia vipimo vya kupima.
Walimaliza kufanya vipimo na wakaa mapokezi wakisubiri majibu na kuitwa na daktari. Muda wote Ibra alikuwa akimtazama mkewe kwani alimuona kama mtu mwenye matatizo sana kwa kipindi hicho, Sophia alimuuliza mumewe,
“Mbona unaniangalia sana bila ya kusema chochote?”
“Kwakweli sina usemi mke wangu ingawa kuna mambo mengi sana najiuliza kuhusu wewe”
“Kama mambo gani?”
“Nadhani tutaongea zaidi tukirudi nyumbani, ngoja kwanza daktari atupe majibu ya vipimo ulivyofanyiwa”
Muda kidogo daktari aliwaita na walipoingia ofisini tu daktari alianza kwa kumpongeza Ibra,
“Hongera sana bwana Ibra, mkeo ni mjamzito”
Ibra akatabasamu kiasi kisha akamuuliza daktari,
“Kwahiyo tatizo lake ni mimba tu au kuna lingine?”
“Hakuna lingine lolote, ni mimba tu. Tena itakuwa vyema kama mkiwahi kuja kuanza na kliniki ili kujua maendeleo ya mtoto aliyeko tumboni”
“Sawa daktari, kwahiyo hakuna tiba yoyote anayoweza kupatiwa?”
“Mr. Ibra, mimba si ugonjwa wa kutibiwa huwa ni hali tu inatokea kwa mwanamke kutokana na kile kitu tofauti kinachojitengeneza kwenye mwili wake. Cha muhimu kujua kuwa mkeo ana mimba na unatakiwa kuwa nae karibu sana ili uweze kumsaidia baadhi ya mambo. Mkianza kliniki mtajifunza mengi zaidi kwahiyo mzingatie hilo.”
“Sawa basi tumekuelewa daktari, tutafanyia kazi ushauri wako”
Kisha daktari akampatia Sophia dawa za vitamin ambazo zingemsaidia kiasi kwa hali aliyokuwa nayo kwa kipindi hicho halafu wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwao.
Walipokuwa njiani kurudi wanapoishi, wakamuona mtoto mdogo barabarani kwa makadirio anaweza akawa kwenye miaka mitatu, alionekana kusimamisha gari yao kanakwamba anaomba msaada ila Ibra alipita bila kusimama ambapo mbele Sophia alimshika mkono na kuonyesha kutokufurahishwa na kitendo cha Ibra cha kumpita mtoto Yule aliyeonekana kutaka msaada.
“Hivi Ibra inamaana Yule mtoto hukumuona?”
“Aaah Sophy, mtoto mdogo kama yule anawezaje kusimama barabarani na kusimamisha gari jamani!! Mambo mengine tutumie akili ya ziada tu mke wangu”
“Sijapenda Ibra yani sijapenda kabisa kabisa”
“Kwahiyo unatakaje?”
“Turudi ili tujue ana tatizo gani”
“Hivi unajua kama hata majambazi wanawatumiaga watoto wadogo mke wangu! Tusije tukajitafutia matatizo bure jamani”
“Hata kama turudi tu kwakweli, hivi wewe huna hata huruma jamani! Mtoto mdogo vile unaanza kumuwekea imani za majambazi mmh! Turudi tafadhari.”
Ibra hakutaka kumkwaza mke wake tena ukizingatia kwa ile hali yake ya ujauzito aliyoambiwa na daktari, hivyobasi akarudisha gari nyuma kwa lengo la kumfata Yule mtoto.
Walifika pale ambapo Yule mtoto aliwasimamaisha na walimkuta pale pale ambapo Ibra alisimamisha gari kisha Sophia akashuka na kumchukua Yule mtoto kisha akapanda nae kwenye gari na kujaribu kumuuliza anapoelekea ambapo Yule mtoto aliwaonyesha kwa kidole tu anapoelekea kisha Ibra akaondoa gari na kuanza kwenda alipoonyesha Yule mtoto.
Walifika mahali kisha Yule mtoto akasema,
“Simama hapa hapa”
Ibra alisimamisha gari ila kwa hofu kiasi kwani hakutegemea kama Yule mtoto anaweza kuonngea ukizingatia mwanzo aliwaonyesha kwa mkono tu.
Kisha Sophia akafungua mlango kwa vile alikuwa amempakata mtoto huyo na kumshusha akizani labda kuna maelekezo mengine Yule mtoto atayatoa, ila Yule mtoto alivyoshuka tu aliwatazama na kuwaambia,
“Asanteni kwa kunikaribisha rasmi kwenye maisha yenu”
Akapunga mkono kisha akaondoka kwa kukimbia ambapo kwa sekunde chache tu alipotea kwenye macho yao.
Ibra na Sophia wakatazamana kisha Ibra akamuuliza mkewe,
“Hivi umemuelewa huyu mtoto?”
“Mmmh hata sijamuelewa”
Ibra nae akaguna kisha akaondoa gari mahali pale na kuendelea na safari yao ya kurudi nyumbani.
Walipofika nyumbani ilionyesha wazi kuwa Ibra alichoshwa kabisa na Yule mtoto ambaye walikutana nae njiani kwani ilikuwa ngumu sana kwake kuelewa msaada ambao Yule mtoto aliuhitaji kutoka kwao, kisha akamuuliza tena mke wake
“Hivi Yule mtoto ulimuelewa?”
“Hapana hata sikumuelewa”
“Safari ijayo usiwe na roho ya huruma kiasi kile itatuponza, huruma muda mwingine sio nzuri”
“Lakini tumepungukiwa na nini mume wangu kumsaidia Yule mtoto jamani? Hata Mungu atatuongezea thawabu”
“Thawabu zipo ila si kwa staili ile ya Yule mtoto, natumaini hakuwa na nia mbaya juu yetu”
“Mtoto Yule bhana hawezi kuwa na nia mbaya kwakweli”
“Sawa”
Kisha Ibra akabadilisha mada na kumpongeza mke wake kwa mimba aliyobeba,
“Hongera sana mke wangu, sasa furaha yetu itaenda kukamilika”
Sophia akatabasamu kisha akamsogelewa mumewe na kumkumbatia kwani aliona mawazo yake yakianza kutimia juu ya wao kuwa na watoto wa kutosha mule ndani.
“Hongera na wewe pia mume wangu maana hii ni furaha yetu wote”
“Yani sipati picha kumshika mwanangu akizaliwa maana nitafurahi sana kumuona kwakweli, itakuwa furaha kubwa sana ya maisha yangu”
“Mimi je! Nitafurahi sana sana maana sasa nitakuwa nimepata mtu wa karibu, siku ya kwanza kumshika na kumnyonyesha nitafurahi sana”
Walionekana kutabasamu na kufurahia ambapo muda huu ibra alionekana kumuuliza mkewe kuwa atapendelea kula chakula gani maana alitaka kujitolea siku hiyo kupika kwaajili ya mke wake, Sophia akatabasamu na kumjibu mumewe kuwa atakula chakula chochote tu.
“Leo nitakupikia mwenyewe Sophy, tafadhali wewe pumzika tu hapo nipike fasta fasta tule”
Sophia akatabasamu na kukaa kwenye kochi huku akihisi kuwa mumewe anafanya mbwembwe tu kwani alijua muda wowote atamshtua kuwa akapike mwenyewe, Ibra alienda jikoni na kumuacha Sophia pale sebleni ambapo kwa muda mfupi kabisa Sophia alipitiwa na usingizi pale pale kwenye kochi.
Wakati Sophia amelala pale kwenye kochi akajiwa na ndoto ambapo kwenye ndoto hiyo akamuona Yule mtoto waliyemkuta kule njiani, alionekana akitabasamu huku akimuangalia Sophia na kumwambia,
“Nitakuwa nakusaidia kazi zote ngumu na hata zile nyepesi zikiwa nyingi nitafanya mimi, napenda ukarimu wako ila huyo mtoto ajaye atakuwa ni ndugu yangu mimi sababu yeye nitampenda zaidi”
Sophia alijikuta akimuuliza huyu mtoto,
“Kivipi?”
Huyu mtoto alionekana akicheka tu bila kuongeza neon la ziada na kumfanya Sophia ashtuke sana kwenye ile ndoto na kujikuta kama akipiga kelele hivi ambapo Ibra alimfata mbio na kumuuliza kuwa kuna tatizo gani.
“Vipi Sophy mke wangu ni nini tatizo?”
“Mmh nimeota ndoto hata siielewi”
“Ndoto gani hiyo?”
“Nimemuota Yule mtoto tuliyemkuta njiani”
“Sophy mke wangu nakuomba uachane na habari za Yule mtoto kwani naona wazi zitakuchanganya tu, yani fanya hivi kwenye akili yako kuwa hatujawahi kukutana na Yule mtoto maana bila ya hivyo sidhani kama itakuwa rahisi kumsahau. Bora ujiwekee kuwa hatujawahi kukutana nae kabisa, Yule mtoto hafai kumuweka akilini kwani hakuwa mtoto wa kawaida kabisa”
“Kwanini unasema hakuwa mtoto wa kawaida?”
“Wewe fikiria hata alipoingia tu kwenye gari alionyesha kuziendesha akili zetu na kujikuta tukifanya anavyotaka yeye kamavile kumpeleka pale alipopataka tena kwa maelekezo ya kidole tu, kwakweli Yule mtoto si wa kawaida hatutakiwi kumuweka akilini mke wangu.”
“Sawa nimekuelewa mume wangu”
“Twende basi tukale”
“Mmh hata nina hamu ya kula basi!!”
“Njoo tule hivyo hivyo mdogo mdogo”
Ikabidi Sophia asogee na mumewe mezani na kuanza kula, kwakweli alimpa hongera mumewe kwa chakula kile maana kilikuwa kitamu sana,
“Asante ingawa nimekipika kawaida tu yani hata mimi mwenyewe nashangaa kuwa kitamu hivi”
Sophia akatabasamu kwani mumewe alimshangaza sana kusema kuwa hata yeye anashangaa utamu wa chakula wakati kakipika mwenyewe.
Walipomaliza kula, Sophia alitoa vile vyombo na kuvipeleka jikoni kisha akaviosha ambapo muda huo Ibra alikuwa sebleni.
Sophia alipomaliza kuosha vile vyombo, iakamjia kumbukumbu ya zile nguo chafu ambazo aliziloweka pia ikamjia kumbukumbu ya vile alivyozikuta kwenye kamba kuwa zilishafuliwa na kuanikwa, ni hapo hapo akakumbuka kuwa hiyo ndio sababu iliyomfanya azimie hapo kabla.
Kwahiyo alipotoka jikoni tu, moja kwa moja akaelekea uwani ambako huwa anafua nguo zake, alipofika uwani safari hii hakuona nguo yoyote cahafu wala za kwenye kamba hakuziona. Akapata wazo la kwenda chumbani kuangalia, ambapo alifika chumbani na kufungua kabati alikuta zile nguo zote zilishakunjwa na kupangwa kabatini, kwakweli Sophia akaguna na kujiuliza kidogo.
“Inamaana Ibra ndio kafanya haya mambo? Ndio lazima tu atakuwa yeye tu maana hakuna mwingine wa kufanya haya.”
Kisha Sophia akatoka chumbani na kurudi sebleni na kwenda kukaa karibu na Ibra kisha akamwambia,
“Asante mume wangu kwa kunisaidia udobi”
“Udobi? Udobi gani tena?”
“Si zile nguo chafu umezifua zote na kuzianua kisha umezipanga kabatini”
“Mmh mbona kama sikuelewi!”
“Hunielewi kivipi wakati zile nguo umeshaanuwa na kupanga kabatini”
Ilionyesha Ibra alikuwa haelewi kitu kwakweli, ikabidi Sophia amshike mkono na kumpeleka mpaka uwani pa kufulia ambapo hapakuwa na nguo yeyote kwenye kamba, kisha akampeleka chumbani na kufungua kabati ambapo ilionyesha nguo zikiwa zimepangwa vizuri kabatini, Ibra akamtazama Sophia na kumuuliza
“Nani kafanya yote haya?”
“Unaniuliza mimi tena! Si wewe hapo”
“Sijafanya hiki kitu mimi”
Wakajikuta wakitazamana kwa muda kidogo, huku wakiwa na hofu kwa mbali.lionyesha Ibra alikuwa haelewi kitu kwakweli, ikabidi Sophia amshike mkono na kumpeleka mpaka uwani pa kufulia ambapo hapakuwa na nguo yeyote kwenye kamba, kisha akampeleka chumbani na kufungua kabati ambapo ilionyesha nguo zikiwa zimepangwa vizuri kabatini, Ibra akamtazama Sophia na kumuuliza
“Nani kafanya yote haya?”
“Unaniuliza mimi tena! Si wewe hapo”
“Sijafanya hiki kitu mimi”
Wakajikuta wakitazamana kwa muda kidogo, huku wakiwa na hofu kwa mbali. Kila mmoja alihisi kuwa mwenzake kuna kitu anamficha hivyo wakajikuta wakiwa kimya kwa muda.
Ibra akaona ni vyema kupotezea hayo mambo ili asije akalumbana na mke wake bure, kwahiyo alichokifanya ni kumshika mkono na kurudi nae sebleni kisha kuanza kuongea nae mambo mbalimbali kuhusiana na mipango yake.
“Sophy mke wangu, inatakiwa katika akili zetu sasa tuanze kupanga mipango kuhusu mtoto wetu ajaye, kwanza kabisa nakushukuru sana mke wangu kwa hiyo zawadi uliyoibeba tumboni mwako kwaajili yangu”
Sophia akatabasamu kwani maneno ya mume wake yalimpa faraja sana, kisha nae akamwambia mumewe,
“Hata mimi nina furaha sana kwani ile ndoto yetu ya kuwa na watoto wane naiona ikitimia kabisa.”
“Kwahiyo umepanga mdogo wake huyu aje baada ya muda gani?”
“Yani huyu akifikisha miaka miwili tu namletea mdogo wake”
“Lakini nasikia kwenye uzazi wa mpango huwa wanasema angalau watoto wapishane miaka mitano mitano ili kila mmoja apate yale malezi ya kutosha ya kitoto”
Sophia akacheka kidogo na kumwambia mumewe,
“Achana na hayo mambo ya wataalamu na hao wa uzazi wa mpango mume wangu, katika maisha kila mtu huwa anajipangia mambo yake mwenyewe, kwetu tumezaliwa tisa tena mama alituachanisha kidogo sana, mwingine kampita mwenzie miaka miwili, mwingine mmoja, mmoja na nusu lakini wote tumekuwa vizuri tu hatuna kasoro wala dosari yoyote kama unavyotuona.”
“Kasoro ipo Sophy”
“Kasoro gani?”
“Kwanza kabisa kwenu mmezaliwa wengi kushinda uwezo wa wazazi wenu, pili mlipishana karibu sana. Angalia mlivyo ni nani aliyebahatika kusoma kwenu hata aweze kuitwa msomi labda”
Sophia akanuna kiasi kisha akamuuliza Ibra,
“Kwahiyo kusoma ndio kasoro? Mbona nyie mpo wachache kwenu na hata hamjasoma kivile!”
“Ni kweli kwetu tupo wachache na hatujasoma hivyo ni kutokana na uwezo wa wazazi wetu ila uchache tuliokuwa nao umefanya tuweze kupambana na ugumu wa maisha. Kwakweli kwa upande wangu kaka zangu wote wamejikwamua kimaisha, kumbuka tupo watano nyumbani kwetu. Kaka zangu watatu walishajikwamua kimaisha, dada nae alijitahidi kujikwamua na sasa kaolewa huku akiendeleza gurudumu la maisha yani nilibaki mimi tu nyuma ambapo nami nimekomboka kwa sasa tena nimewapita wote kimaisha. Haya kwa upande wa kwenu yani mwenye afadhari ni wewe tu, angalia akili za dada zako zilivyo na Yule mdogo wako wa mwisho ni nini anafanya. Kaka zako je, bangi bangi na wao hapo kuna maendeleo gani ya kuwa wengi ambao hamueleweki? Kwa walivyo wazazi wenu wangewazaa wachache na uhakika wasingeshindwa kuwasomesha”
Sophia akanuna zaidi na kumuuliza tena Ibra tena kwa kupaniki,
“Tungekuwa wachache mimi ningekuwepo? Nakuuliza wewe ningekuwepo? Maana mimi kuzaliwa kwetu ni mtoto wa nane ndio akazaliwa Yule mdogo wangu, mara nyingine ujifikiriage kabla ya kuongea mambo ya kijinga jinga.”
Kisha akainuka kwa hasira na kuelekea chumbani.
Ikabidi Ibra ainuke na kumfata mkewe chumbani ili aweze kumbembeleza ambapo akamkuta akilia,
“Jamani mke wangu usichukulie hasira yale yalikuwa ni maongezi tu wala sikuwa na nia mbaya”
“Hukuwa na nia mbaya wapi wakati unaisema familia yangu!”
“Nisamehe mke wangu tafadhali, nakupenda sana Sophy”
“Yani mi kusema watoto wapishane miaka miwili miwili umeona ndio ishu, kuna watu wanahangaika na wake zao huko sababu hawataki kuzaa zaa watazeeka ila mimi niliyejitolea kwako unaniona mjinga poa bwana.”
“Tafadhali mke wangu nisamehe, nakuomba nisamehe sana”
Ibra akapiga na magoti kumuonyesha mkewe kuwa anajutia kitu alichoongea, kitendo cha Ibra kupiga magoti kikampa Sophia faraja na kujikuta akitabasamu na kufanya afurahi na mume wake.
Kwavile ilikuwa ni jioni, Ibra akamuomba mkewe watoke kidogo wazunguke zunguke maeneo ya karibu kama kufanya zoezi la kutembea tu ambapo Sophy alikubali kisha akabadili nguo na kuwafanya watoke sasa.
Walipokuwa nje ya nyumba yao, Ibra aliona kuna upande ambao hajawahi kutembelea toka walipohamia kwenye nyumba ile na kumuomba mkewe waelekee upande ule kidogo, kisha wakatoka pale na kuanza kuelekea ule upande.
“Ila tusiende mbali sana nitachoka mwenzio”
“Usijali Sophy, tunatembea kwa stepu hakuna haja ya kwenda mbali sana.”
Wakiwa njiani wakaonana na Jane ambapo Sophia alisimama kwa tabasamu na kusalimiana na huyo Jane,
“Shikamooni”
“Marahaba, mbona hukuja tena nyumbani wakati uliniahidi kuwa utakuwa unakuja”
Jane akatabasamu kidogo kisha akasema,
“Kesho nitakuja dada hata usijali”
Waliongea kidogo pale na kuagana nae.
Alipoondoka, Sophia akamuuliza mumewe kama anamkumbuka Yule Jane,
“Mmh hata simkumbuki”
“Ndio Yule binti wa Yule mama jirani yetu ambaye mwanzoni kabisa nilikutana nae pale getini kwetu, na siku amekuja na binti yake hata wewe uliporudi uliwakuta”
“Aaah nishawakumbuka, si unajua tena kichwa hiki kina mambo mengi”
“Loh naona kweli mambo mengi maana hata hili ulikuwa hukumbuki kweli mambo yanakutinga”
Kisha wakaendelea na matembezi yao ya hapa na pale, kuna mahali palikuwa na kimlima kidogo ambapo Ibra akashauri warudi tu kwani alihisi kupanda kile kimlima kutamfanya mkewe achoke sana,
“Turudi nyumbani Sophy”
“Aah jamani, tusogee sogee kidogo yani mi ndio ushanitamanisha na kutembea, twende tukaishie pale kwenye kimlima”
“Ila si unaona giza nalo limeanza kuingia”
“Ndio naona ila tuishie hapo kwenye kimlima”
Ibra hakumpinga kwavile aliyekuwa akimuonea huruma ni yeye mwenyewe, kwahiyo wakaendelea mbele kidogo na kuanza kupandisha kale kamlima.
Walipofika juu kidogo kulikuwa tena na kamteremko kakushuka chini ila kuna kitu kilimshtua Sophy kwa kule chini na kumfanya amkumbatie mumewe kwa nguvu,
“Nini tena Sophy?”
“Ona kule chini”
Ibra alipoangalia akamuona tena Yule mtoto wa mchana akiwatazama kamavile anaomba msaada, Ibra akamshika mkewe mkono na kurudi nae nyuma kisha kugeuza na kuanza kurudi nyumbani huku akiongea,
“Yani mimi nikikataa kitu ujue lazima kuna tatizo ona sasa bora hata tungerudi pale pale nilipokataa”
Sophia hakujibu chochote zaidi ya kukokotana na kurudi nyumbani.
Walifika nyumbani, ila Sophia alidai kuchoka sana na kuelekea chumbani kulala ambapo ibra nae alielekea chumabani na kulala pembeni ya Sophia kwa kumkumbatia ili aweze kuwa na amani.
Wakati usingizi umemkolea kabisa Sophia akajiwa na ndoto, akamuona tena Yule mtoto akiwa pale pale chini kidogo ya kile kilima ambapo kwenye ndoto hii Sophia alijiona akimfata Yule mtoto alipo na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, kisha Yule mtoto akamwambia,
“Sina ubaya na wewe Sophia, una moyo wa kujali halafu una upendo sana ila tatizo ni huyu mume wako hana huruma kabisa. Je ungependa nimfanye nini?”
Sophia akawa kama anamshangaa huyu mtoto na kumuuliza,
“Umfanye nini kivipi na kwanini?”
“Mumeo ana roho mbaya sana Sophia, sipendi watu wasio na huruma wakati mimi huwa nakusaidia mambo mengi sana. Niambie basi nimfanye nini?”
“Hapana usimfanye chochote mume wangu”
“Usiwe na huruma hivyo Sophia kwa mtu asiye na huruma, yani mimi hata ukiniambia nimuue sasa hivi huyu mumeo namuua”
Sophia akashtuka kutoka kwenye ile ndoto na kupiga kelele huku jasho jingi likimtoka na kufanya Ibra nae ashtuke na kumuuliza mkewe kuwa tatizo ni nini,
“Vipi Sophy?”
Sophia alikuwa akihema juu juu na kumjibu mumewe,
“Nimeota ndoto mbaya sana”
“Mmmh pole mke wangu, hiyo ndoto inahusu nini?”
“Nimemuota tena Yule mtoto eti alitaka kukuua wewe”
Ibra akatabasamu kwavile hakuwa mtu wa hofu kwa mambo kama hayo haswa ya kuhusu ndoto, kisha akamwambia Sophia,
“Mke wangu, usiwe na wasiwasi juu yangu halafu ndoto za namna hiyo zisikutishe sana. Mimi ni mwanaume jasiri siwezi kuteketea kirahisi hivyo. Pia naomba Yule mtoto umtoe mawzzoni mwako mke wangu tafadhali”
Kisha Ibra akainuka na mkewe na kwenda kuoga ili angalau kupata nguvu mpya na kuondoa uchovu uliopita hata iwasaidie kuanza upya usingizi.
Walimaliza kuoga na kurudi tena kulala.
Kulipokucha, Ibra aliamka na kujiandaa kwenda kwenye mahangaiko yake kisha akamuaga mke wake na kumwambia kuwa endapo kutatokea tatizo lolote basi asisite kumpigia simu.
“Usijali nitakujulisha mume wangu”
Kisha Ibra akmbusu mkewe kwenye paji la uso na kumuaga.
Sophia hakuweza kuendelea kulala kwani muda ule ule aliamka na kwenda sebleni akiwa amejikalia tu kisha muda kidogo akafanya kazi zake za hapa na pale kisha kupumzika tena.
Akiwa pale sebleni alisikia hodi na kwenda kufungua ambapo aliyeingia alikuwa ni Jane hivyo kumfanya Sophia afurahi sana kwa kupata kampani ya muda ule.
“Bora Jane umekuja maana nilikuwa mpweke sana”
“Ndiomana nikaamua kutimiza ahadi yangu”
Sophia alimkaribisha vizuri sana Jane na kukaa pamoja sebleni huku wakizungumza mambo mbalimbali, ambapo Sophia alimuuliza Jane,
“Hivi huwa unafanya nini ukiwa nyumbani mwenyewe, ukiachana na kazi za nyumbani”
“Kwakweli dada mi napenda sana kusoma stori haswa stori za kutisha”
“Kheee wa ajabu wewe sasa stori za kutisha unazipendea nini?”
“Yani mi huwa napenda tu halafu huwa naona kama kweli vile”
“Basi mimi katika vitu ambavyo sipendi ni kusoma stori haswaa za kutisha sababu huwa naona ni uongo mtupu. Waandishi wanaandika vitu vya kidhahania yani havina ukweli wowote.”
“Mmh ila vingine vina ukweli dada, mfano mamabo ya misukule”
Sophia akacheka sana,
“Yani Jane na usomi wako wote bado unaamini kuhusu misukule! Hakuna kitu kama hicho duniani, tatizo lako hizo stori zimekukaa kichwani, ushawahi kuona msukule wewe? Zaidi ya kuona kwenye sinema na kusoma kwenye stori, hakuna kitu kama hicho”
“Lakini dada mara nyingi wanaoandika stori huwa ni mambo ambayo yapo kwenye jamii ndiomana yameandikwa”
“Aaah ni propaganda tu hizo ili wapate wasomaji wengi hakuna ukweli wowote”
“Ila kuna mambo ni mazuri na yanatufundisha kwakweli, mimi toka nianze kusoma hizi stori nimejifunza mambo mengi sana. Kwanza siwezi kulala bila kumuomba Mungu maana usiku wetu umezingirwa na mambo mengi, na pia nikiamka lazima nimshukuru Mungu na kuomba aniongoze siku hiyo ingawa mara nyingine nasahau kuomba nikiamka kwakweli”
Hapo hapo akajicheka tena na kusema,
“Aah hata leo yenyewe nimeshau kusali, kwakweli Mungu anisamehe tu”
Sophia nae akacheka na kumwambia,
“Hebu acha masikhara yako Jane, yani mi mtu haniambii kitu kuhusu mastori ya uongo yani siwezi kupoteza muda wangu nifatilie.”
Kisha wakabadili mada na kuanza kuongelea mambo mengine.
Mchana ulipofika Sophia alijisikia uchovu sana na kumuomba Jane akamsaidie kupika,
“Mdogo wangu Jane naomba msaada tafadhali”
“Sema chochote dada nitafanya”
“Jikoni kuna ndizi nilizimenya na nyama ipo kwenye friji, unaweza kwenda kupika ili tule”
“Aah usijali dada, jikoni ndio wapi?”
Sophia akamuonyesha Jane mlango wa jikoni ambapo Jane aliinuka na kuelekea jikoni.
Alipoingia alienda moja kwa moja na kufungua friji ambapo hakuona nyama yoyote ila alipoangalia kwenye jiko aliona sufuria imefunikwa vizuri kabisa akaamua kusogea na kufunua, kwanza akasikia harufu nzuri sana ya chakula na alipoangalia aliona ni ndizi zikiwa zimepikwa vizuri kabisa tena zikiwa na nyama na bado zilikuwa za moto. Kwakweli Jane alishangaa kiasi na kujiuliza,
“Hivi kaniambia nije nipike au nimsaidie kupakua jamani! Mbona chakula alishapika tayari! Nadhani kaniambia nije nipakue.”
Kisha akachukua bakuri kubwa na kupakua halafu akapeleka mezani na kuweka sahani halafu akamfata Sophia na kumwambia tayari.
Sophia akamuangalia kwa makini na kumuuliza,
“Tayari nini?”
“Tayari chakula kipo mezani”
“Mmh usinitanie Jane, haiwezekani zile ndizi ziwe zimeiva! Hebua acha utani”
Akaelekea na Jane mezani ila bado Sophia hakuamini na kumuangalia vizuri Jane kisha akamuuliza,
“Je wewe ni binadamu wa kawaida?”
Jane akamshangaa Sophia kwa swali lile.
Itaendelea kama kawaida……………..!!!!!!!!!!!!!!! Toa maoni na kucoment
NYUMBA YA MAAJABU: 5
Ilionyesha Ibra alikuwa haelewi kitu kwakweli, ikabidi Sophia amshike mkono na kumpeleka mpaka uwani pa kufulia ambapo hapakuwa na nguo yeyote kwenye kamba, kisha akampeleka chumbani na kufungua kabati ambapo ilionyesha nguo zikiwa zimepangwa vizuri kabatini, Ibra akamtazama Sophia na kumuuliza
“Nani kafanya yote haya?”
“Unaniuliza mimi tena! Si wewe hapo”
“Sijafanya hiki kitu mimi”
Wakajikuta wakitazamana kwa muda kidogo, huku wakiwa na hofu kwa mbali. Kila mmoja alihisi kuwa mwenzake kuna kitu anamficha hivyo wakajikuta wakiwa kimya kwa muda.
Ibra akaona ni vyema kupotezea hayo mambo ili asije akalumbana na mke wake bure, kwahiyo alichokifanya ni kumshika mkono na kurudi nae sebleni kisha kuanza kuongea nae mambo mbalimbali kuhusiana na mipango yake.
“Sophy mke wangu, inatakiwa katika akili zetu sasa tuanze kupanga mipango kuhusu mtoto wetu ajaye, kwanza kabisa nakushukuru sana mke wangu kwa hiyo zawadi uliyoibeba tumboni mwako kwaajili yangu”
Sophia akatabasamu kwani maneno ya mume wake yalimpa faraja sana, kisha nae akamwambia mumewe,
“Hata mimi nina furaha sana kwani ile ndoto yetu ya kuwa na watoto wane naiona ikitimia kabisa.”
“Kwahiyo umepanga mdogo wake huyu aje baada ya muda gani?”
“Yani huyu akifikisha miaka miwili tu namletea mdogo wake”
“Lakini nasikia kwenye uzazi wa mpango huwa wanasema angalau watoto wapishane miaka mitano mitano ili kila mmoja apate yale malezi ya kutosha ya kitoto”
Sophia akacheka kidogo na kumwambia mumewe,
“Achana na hayo mambo ya wataalamu na hao wa uzazi wa mpango mume wangu, katika maisha kila mtu huwa anajipangia mambo yake mwenyewe, kwetu tumezaliwa tisa tena mama alituachanisha kidogo sana, mwingine kampita mwenzie miaka miwili, mwingine mmoja, mmoja na nusu lakini wote tumekuwa vizuri tu hatuna kasoro wala dosari yoyote kama unavyotuona.”
“Kasoro ipo Sophy”
“Kasoro gani?”
“Kwanza kabisa kwenu mmezaliwa wengi kushinda uwezo wa wazazi wenu, pili mlipishana karibu sana. Angalia mlivyo ni nani aliyebahatika kusoma kwenu hata aweze kuitwa msomi labda”
Sophia akanuna kiasi kisha akamuuliza Ibra,
“Kwahiyo kusoma ndio kasoro? Mbona nyie mpo wachache kwenu na hata hamjasoma kivile!”
“Ni kweli kwetu tupo wachache na hatujasoma hivyo ni kutokana na uwezo wa wazazi wetu ila uchache tuliokuwa nao umefanya tuweze kupambana na ugumu wa maisha. Kwakweli kwa upande wangu kaka zangu wote wamejikwamua kimaisha, kumbuka tupo watano nyumbani kwetu. Kaka zangu watatu walishajikwamua kimaisha, dada nae alijitahidi kujikwamua na sasa kaolewa huku akiendeleza gurudumu la maisha yani nilibaki mimi tu nyuma ambapo nami nimekomboka kwa sasa tena nimewapita wote kimaisha. Haya kwa upande wa kwenu yani mwenye afadhari ni wewe tu, angalia akili za dada zako zilivyo na Yule mdogo wako wa mwisho ni nini anafanya. Kaka zako je, bangi bangi na wao hapo kuna maendeleo gani ya kuwa wengi ambao hamueleweki? Kwa walivyo wazazi wenu wangewazaa wachache na uhakika wasingeshindwa kuwasomesha”
Sophia akanuna zaidi na kumuuliza tena Ibra tena kwa kupaniki,
“Tungekuwa wachache mimi ningekuwepo? Nakuuliza wewe ningekuwepo? Maana mimi kuzaliwa kwetu ni mtoto wa nane ndio akazaliwa Yule mdogo wangu, mara nyingine ujifikiriage kabla ya kuongea mambo ya kijinga jinga.”
Kisha akainuka kwa hasira na kuelekea chumbani.
Ikabidi Ibra ainuke na kumfata mkewe chumbani ili aweze kumbembeleza ambapo akamkuta akilia,
“Jamani mke wangu usichukulie hasira yale yalikuwa ni maongezi tu wala sikuwa na nia mbaya”
“Hukuwa na nia mbaya wapi wakati unaisema familia yangu!”
“Nisamehe mke wangu tafadhali, nakupenda sana Sophy”
“Yani mi kusema watoto wapishane miaka miwili miwili umeona ndio ishu, kuna watu wanahangaika na wake zao huko sababu hawataki kuzaa zaa watazeeka ila mimi niliyejitolea kwako unaniona mjinga poa bwana.”
“Tafadhali mke wangu nisamehe, nakuomba nisamehe sana”
Ibra akapiga na magoti kumuonyesha mkewe kuwa anajutia kitu alichoongea, kitendo cha Ibra kupiga magoti kikampa Sophia faraja na kujikuta akitabasamu na kufanya afurahi na mume wake.
Kwavile ilikuwa ni jioni, Ibra akamuomba mkewe watoke kidogo wazunguke zunguke maeneo ya karibu kama kufanya zoezi la kutembea tu ambapo Sophy alikubali kisha akabadili nguo na kuwafanya watoke sasa.
Walipokuwa nje ya nyumba yao, Ibra aliona kuna upande ambao hajawahi kutembelea toka walipohamia kwenye nyumba ile na kumuomba mkewe waelekee upande ule kidogo, kisha wakatoka pale na kuanza kuelekea ule upande.
“Ila tusiende mbali sana nitachoka mwenzio”
“Usijali Sophy, tunatembea kwa stepu hakuna haja ya kwenda mbali sana.”
Wakiwa njiani wakaonana na Jane ambapo Sophia alisimama kwa tabasamu na kusalimiana na huyo Jane,
“Shikamooni”
“Marahaba, mbona hukuja tena nyumbani wakati uliniahidi kuwa utakuwa unakuja”
Jane akatabasamu kidogo kisha akasema,
“Kesho nitakuja dada hata usijali”
Waliongea kidogo pale na kuagana nae.
Alipoondoka, Sophia akamuuliza mumewe kama anamkumbuka Yule Jane,
“Mmh hata simkumbuki”
“Ndio Yule binti wa Yule mama jirani yetu ambaye mwanzoni kabisa nilikutana nae pale getini kwetu, na siku amekuja na binti yake hata wewe uliporudi uliwakuta”
“Aaah nishawakumbuka, si unajua tena kichwa hiki kina mambo mengi”
“Loh naona kweli mambo mengi maana hata hili ulikuwa hukumbuki kweli mambo yanakutinga”
Kisha wakaendelea na matembezi yao ya hapa na pale, kuna mahali palikuwa na kimlima kidogo ambapo Ibra akashauri warudi tu kwani alihisi kupanda kile kimlima kutamfanya mkewe achoke sana,
“Turudi nyumbani Sophy”
“Aah jamani, tusogee sogee kidogo yani mi ndio ushanitamanisha na kutembea, twende tukaishie pale kwenye kimlima”
“Ila si unaona giza nalo limeanza kuingia”
“Ndio naona ila tuishie hapo kwenye kimlima”
Ibra hakumpinga kwavile aliyekuwa akimuonea huruma ni yeye mwenyewe, kwahiyo wakaendelea mbele kidogo na kuanza kupandisha kale kamlima.
Walipofika juu kidogo kulikuwa tena na kamteremko kakushuka chini ila kuna kitu kilimshtua Sophy kwa kule chini na kumfanya amkumbatie mumewe kwa nguvu,
“Nini tena Sophy?”
“Ona kule chini”
Ibra alipoangalia akamuona tena Yule mtoto wa mchana akiwatazama kamavile anaomba msaada, Ibra akamshika mkewe mkono na kurudi nae nyuma kisha kugeuza na kuanza kurudi nyumbani huku akiongea,
“Yani mimi nikikataa kitu ujue lazima kuna tatizo ona sasa bora hata tungerudi pale pale nilipokataa”
Sophia hakujibu chochote zaidi ya kukokotana na kurudi nyumbani.
Walifika nyumbani, ila Sophia alidai kuchoka sana na kuelekea chumbani kulala ambapo ibra nae alielekea chumabani na kulala pembeni ya Sophia kwa kumkumbatia ili aweze kuwa na amani.
Wakati usingizi umemkolea kabisa Sophia akajiwa na ndoto, akamuona tena Yule mtoto akiwa pale pale chini kidogo ya kile kilima ambapo kwenye ndoto hii Sophia alijiona akimfata Yule mtoto alipo na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, kisha Yule mtoto akamwambia,
“Sina ubaya na wewe Sophia, una moyo wa kujali halafu una upendo sana ila tatizo ni huyu mume wako hana huruma kabisa. Je ungependa nimfanye nini?”
Sophia akawa kama anamshangaa huyu mtoto na kumuuliza,
“Umfanye nini kivipi na kwanini?”
“Mumeo ana roho mbaya sana Sophia, sipendi watu wasio na huruma wakati mimi huwa nakusaidia mambo mengi sana. Niambie basi nimfanye nini?”
“Hapana usimfanye chochote mume wangu”
“Usiwe na huruma hivyo Sophia kwa mtu asiye na huruma, yani mimi hata ukiniambia nimuue sasa hivi huyu mumeo namuua”
Sophia akashtuka kutoka kwenye ile ndoto na kupiga kelele huku jasho jingi likimtoka na kufanya Ibra nae ashtuke na kumuuliza mkewe kuwa tatizo ni nini,
“Vipi Sophy?”
Sophia alikuwa akihema juu juu na kumjibu mumewe,
“Nimeota ndoto mbaya sana”
“Mmmh pole mke wangu, hiyo ndoto inahusu nini?”
“Nimemuota tena Yule mtoto eti alitaka kukuua wewe”
Ibra akatabasamu kwavile hakuwa mtu wa hofu kwa mambo kama hayo haswa ya kuhusu ndoto, kisha akamwambia Sophia,
“Mke wangu, usiwe na wasiwasi juu yangu halafu ndoto za namna hiyo zisikutishe sana. Mimi ni mwanaume jasiri siwezi kuteketea kirahisi hivyo. Pia naomba Yule mtoto umtoe mawzzoni mwako mke wangu tafadhali”
Kisha Ibra akainuka na mkewe na kwenda kuoga ili angalau kupata nguvu mpya na kuondoa uchovu uliopita hata iwasaidie kuanza upya usingizi.
Walimaliza kuoga na kurudi tena kulala.
Kulipokucha, Ibra aliamka na kujiandaa kwenda kwenye mahangaiko yake kisha akamuaga mke wake na kumwambia kuwa endapo kutatokea tatizo lolote basi asisite kumpigia simu.
“Usijali nitakujulisha mume wangu”
Kisha Ibra akmbusu mkewe kwenye paji la uso na kumuaga.
Sophia hakuweza kuendelea kulala kwani muda ule ule aliamka na kwenda sebleni akiwa amejikalia tu kisha muda kidogo akafanya kazi zake za hapa na pale kisha kupumzika tena.
Akiwa pale sebleni alisikia hodi na kwenda kufungua ambapo aliyeingia alikuwa ni Jane hivyo kumfanya Sophia afurahi sana kwa kupata kampani ya muda ule.
“Bora Jane umekuja maana nilikuwa mpweke sana”
“Ndiomana nikaamua kutimiza ahadi yangu”
Sophia alimkaribisha vizuri sana Jane na kukaa pamoja sebleni huku wakizungumza mambo mbalimbali, ambapo Sophia alimuuliza Jane,
“Hivi huwa unafanya nini ukiwa nyumbani mwenyewe, ukiachana na kazi za nyumbani”
“Kwakweli dada mi napenda sana kusoma stori haswa stori za kutisha”
“Kheee wa ajabu wewe sasa stori za kutisha unazipendea nini?”
“Yani mi huwa napenda tu halafu huwa naona kama kweli vile”
“Basi mimi katika vitu ambavyo sipendi ni kusoma stori haswaa za kutisha sababu huwa naona ni uongo mtupu. Waandishi wanaandika vitu vya kidhahania yani havina ukweli wowote.”
“Mmh ila vingine vina ukweli dada, mfano mamabo ya misukule”
Sophia akacheka sana,
“Yani Jane na usomi wako wote bado unaamini kuhusu misukule! Hakuna kitu kama hicho duniani, tatizo lako hizo stori zimekukaa kichwani, ushawahi kuona msukule wewe? Zaidi ya kuona kwenye sinema na kusoma kwenye stori, hakuna kitu kama hicho”
“Lakini dada mara nyingi wanaoandika stori huwa ni mambo ambayo yapo kwenye jamii ndiomana yameandikwa”
“Aaah ni propaganda tu hizo ili wapate wasomaji wengi hakuna ukweli wowote”
“Ila kuna mambo ni mazuri na yanatufundisha kwakweli, mimi toka nianze kusoma hizi stori nimejifunza mambo mengi sana. Kwanza siwezi kulala bila kumuomba Mungu maana usiku wetu umezingirwa na mambo mengi, na pia nikiamka lazima nimshukuru Mungu na kuomba aniongoze siku hiyo ingawa mara nyingine nasahau kuomba nikiamka kwakweli”
Hapo hapo akajicheka tena na kusema,
“Aah hata leo yenyewe nimeshau kusali, kwakweli Mungu anisamehe tu”
Sophia nae akacheka na kumwambia,
“Hebu acha masikhara yako Jane, yani mi mtu haniambii kitu kuhusu mastori ya uongo yani siwezi kupoteza muda wangu nifatilie.”
Kisha wakabadili mada na kuanza kuongelea mambo mengine.
Mchana ulipofika Sophia alijisikia uchovu sana na kumuomba Jane akamsaidie kupika,
“Mdogo wangu Jane naomba msaada tafadhali”
“Sema chochote dada nitafanya”
“Jikoni kuna ndizi nilizimenya na nyama ipo kwenye friji, unaweza kwenda kupika ili tule”
“Aah usijali dada, jikoni ndio wapi?”
Sophia akamuonyesha Jane mlango wa jikoni ambapo Jane aliinuka na kuelekea jikoni.
Alipoingia alienda moja kwa moja na kufungua friji ambapo hakuona nyama yoyote ila alipoangalia kwenye jiko aliona sufuria imefunikwa vizuri kabisa akaamua kusogea na kufunua, kwanza akasikia harufu nzuri sana ya chakula na alipoangalia aliona ni ndizi zikiwa zimepikwa vizuri kabisa tena zikiwa na nyama na bado zilikuwa za moto. Kwakweli Jane alishangaa kiasi na kujiuliza,
“Hivi kaniambia nije nipike au nimsaidie kupakua jamani! Mbona chakula alishapika tayari! Nadhani kaniambia nije nipakue.”
Kisha akachukua bakuri kubwa na kupakua halafu akapeleka mezani na kuweka sahani halafu akamfata Sophia na kumwambia tayari.
Sophia akamuangalia kwa makini na kumuuliza,
“Tayari nini?”
“Tayari chakula kipo mezani”
“Mmh usinitanie Jane, haiwezekani zile ndizi ziwe zimeiva! Hebua acha utani”
Akaelekea na Jane mezani ila bado Sophia hakuamini na kumuangalia vizuri Jane kisha akamuuliza,
“Je wewe ni binadamu wa kawaida?”
Jane akamshangaa Sophia kwa swali lile.
Itaendelea kama kawaida……………..!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 6
Sophia akamuangalia kwa makini na kumuuliza,
“Tayari nini?”
“Tayari chakula kipo mezani”
“Mmh usinitanie Jane, haiwezekani zile ndizi ziwe zimeiva! Hebu acha utani”
Akaelekea na Jane mezani ila bado Sophia hakuamini na kumuangalia vizuri Jane kisha akamuuliza,
“Je wewe ni binadamu wa kawaida?”
Jane akamshangaa Sophia kwa swali lile.
Kwakweli Jane hakuweza kumjibu Sophia kwani lile swali pia halikuwa la kawaida na hata hivyo Sophia hakuonekana kawaida kabisa kwani alionekana ni mtu mwenye mashaka na Yule Jane.
Wakiwa bado wanatazamana, wakashtushwa na hodi na kufanya Sophia aende kufungua ambapo aliyeingia alikuwa ni mumewe Ibra ila muda huo huo Jane nae hakuweza kukaa kwani aliaga juu juu na kuondoka zake hata Ibra aliweza kuelewa kuwa lazima kuna tatizo kwavile hakuuelewa ule uagaji wa Jane na kuondoka.
Ibra akamuangalia mkewe na kumuuliza kuwa ni nini tatizo, Sophia akaamua kumueleza mumewe jinsi ilivyokuwa hadi kupelekea hali ile, Ibra akasikitika na kumuangalia mkewe kisha akamwambia,
“Unajua mke wangu kila siku napenda kukwambia kuwa uwe unafikiria kwanza kabla ya kuongea jambo lolote maana maneno yako huwa katika hali ya ukali sana. Nilivyokuzoea mimi ni tofauti na mwingine alivyokuzoea.”
“Hivi unafikiri ningemuulizaje jamani? Tatizo Ibra hukuwepo, yani mtu nimemwambia muda huo huo kuwa akapike halafu muda huo huo anaenda jikoni na kuniambia chakula tayari! Inakuingia akilini kweli? Nakwenda mezani nakuta kweli ameshaandaa chakula mmh! Kwakweli kwa upande wangu imekuwa ngumu sana kujizuia kwa hiyo hali jamani maana haiwezekani tena haiwezekani kabisa.”
Ibra akaongozana na mkewe mpaka mezani na kuangalia zile ndizi pale mezani kisha akachukua kijiko na kuzionja, halafu akakaa kimya kwa muda na kusema
“Mmmh ndizi tamu sana hizi sijapata kuona yani na njaa yangu hii hebu kaa hapo tuanze kula”
“Ila upikaji wake ni wa kustaajabisha mume wangu”
“Achana na mambo ya upikaji, mi nakujua Sophy mke wangu usikute ulimuagiza binti wa watu akapike halafu ukapitiwa na usingizi, mtu anakwambia chakula kimeiva unashtuka na kuona ni muda huo huo kwavile ulipitiwa na usingizi, hebu kaa tule”
Ibra akaweka chakula kwenye sahani na kuanza kula vizuri kabisa huku akimsisitiza Sophia nae aweze kula ambapo Sophia aliamua kula kutokana na vile ambavyo mumewe alimsisitiza.
Kwakweli chakula kilikuwa kitamu sana na kufanya waifurahie ladha ya kile chakula lakini bado Sophia alikuwa na mashaka sana juu ya upikaji wa kile chakula hata imani yake juu ya Jane ikapungua kabisa.
Walipomaliza kula, Ibra akamshauri mkewe kuwa waende wakamuombe msamaha Jane,
“Mmmh sijui atanifikiriaje sasa!”
“Usijali twende kisha mi nitazungumza nae maana mi ndio nakufahamu vizuri wewe”
Basi wakakubaliana na kuinuka wakielekea kwakina Jane.
Walipofika walimkuta mama Jane akiwa nje akichambua mboga, ikabidi Sophia ajichekeleshe kidogo na kuulizia kama Jane yupo,
“Jane karudi ila kapitiliza moja kwa moja chumbani, ngoja nimuite”
Mama Jane akamuita Jane kisha Sophia akakaa karibu na huyu mama akimsaidia kuchambua ile mboga, Jane alipotoka moja kwa moja Ibra akamuomba pembeni ili azungumze nae ambapo alisogea na Ibra kwaajili ya mazungumzo,
“Jane samahani kilichotokea kati yako na mke wangu naomba umzoee tu”
“Mimi sina tatizo nae ila sikumuelewa tu alivyokuwa akifoka na kuonyesha kunishangaa”
“Pole sana mdogo wangu, unajua nini huyu Sophy huwa ana matatizo ya kusahau anaweza fanya jambo kisha akasahau halafu muda mwingine anasahau muda sababu ya kusinzia naomba umsamehe sana”
“Mmh mi sikujua hilo, ila kama ana tatizo la kusahau basi sasa naweza kuelewa kwanini alikuwa akifoka vile. Nimemsamehe na wala sina mashaka nae”
“Kama umemsamehe ni vizuri, na usisite kuja kuendelea kututembelea tafadhali maana pale nyumbani huwa anabaki mwenyewe na upweke.”
“Ilimradi nimeshagundua tatizo lake basi haitanisumbua tena”
Kisha Ibra akamuita mkewe na kuwapatanisha ambapo Sophia na Ibra wakaaga baada ya lile tukio na kuondoka, huku Sophia akimsisitiza Jane aende kumtembelea tena kesho yake.
Walipoondoka tu, mama Jane akamuita binti yake ili kujua kilichoendelea kwani haikuwa kawaida kwa Jane kufatwa vile nyumbani kwao.
Jane hakumficha mama yake, akamueleza kila kitu ambacho kimetokea siku hiyo.
“Mmh kwahiyo chakula alishapika akasahau na kukwambia wewe ukapike?”
“Ndio hivyo mama, maana alinipa maelekezo sijui nyama ipo kwenye friji niitoe kisha niipike na ndizi, kuingia jikoni hakuna nyama kwenye friji ila nilipofunua sufuria nakuta ndizi zilishapikwa tayari tena zimenona balaa dah kafanya nimeondoka bila hata ya kula hata kidogo.”
“Kama ndio hivyo basi kusahau kwake ni babkubwa maana mmh! Mtu unasahau kabisa kama ulishapika, ila ni bora mumewe anajua tatizo la mke wake.”
“Ndio, kaniambia nimchukulie kama alivyo sababu ni tatizo lake la kusahau”
“Mmh haya mwanangu ila siku nyingine uwe makini na maneno yake”
Jane akakubaliana pale na mama yake kisha akarudi zake ndani huku akiamini kuwa Sophia alipika zile ndizi ila amesahau kutokana na tatizo lake la kusahau.
Ibra na Sophia walipofika nyumbani moja kwa moja Ibra akakumbuka kitu,
“Aaah! Hata nimesahau kumshukuru Yule binti kwa chakula kitamu, kwakweli anajua sana kupika”
Sophia akamuangalia mumewe na kumuuliza,
“Inamaana anajua kupika kushinda mimi?”
“Mmh mke wangu jamani huo sasa ni wivu, mimi nimemsifia tu wala sijasema kama amekupita wewe. Hata hivyo hakuna anayekufikia wewe mke wangu kwa chochote wala lolote”
Sophia akatabasamu kwani hizi sifa alizopewa na mumewe zilimfanya ajisikie vizuri sana, kisha Sophia akainuka na kuelekea meza ya chakula halafu akamuuliza mumewe,
“Wakati tunaondoka hivi tulitoa vyombo mezani kweli?”
“Mmh mi sikumbuki ila mezani nilikuacha wewe halafu niakenda kukaa kwenye kochi kwani vipi?”
“Kwa kumbukumbu zangu sikumbuki kama nilitoa vyombo kwakweli ila naona vimeshatolewa je nani kavitoa?”
“Aah Sophia jamani unakoelekea mke wangu siko kabisa yani mmh wewe kila kitu kwako kipo nyuma mbele. Kuna mtu aliniambia kuwa wanawake wajawazito huwa na tabia ya kusahau kwakweli leo naamini maneno yake. Hebu njoo kwanza mke wangu tujadili mambo ya msingi. Leo nimerudi mapema hata huniulizi kwanini mapema ila kila muda unazuka na jipya sijui ndio maisha gani haya mke wangu.”
Sophia akaamua kusogea pale sebleni na kukaa na mumewe ingawa katika kichwa chake kilikuwa na maswali mengi sana ila aliamua kuyapuuzia kwa muda, kisha akamuuliza mumewe kuhusu kuwahi kurudi kwake,
“Eeh mbona leo umewahi kurudi sana?”
“Kwanza kabisa leo nilipokuwa kazini mawazo yangu yote yalikuwa juu yako kwani nilikuwa nikiwaza juu ya upweke ambao utakuwa nao. Ndiomana nimewahi kurudi ili nikuliwaze mke wangu.”
Sophia akatabasamu kwavile aliyapenda sana maneno ya mumewe ya kumbembeleza, kisha Ibra akaendelea kuongea,
“Halafu nimepata wazo mke wangu, kwanini tusiwe na msichana wa kazi humu akusaidie saidie”
“Msichana wa kazi! Wa nini mimi? Kwakweli huwa sina imani na hao wasichana wa kazi mume wangu jamani nisije nikaibiwa bure bora ufikirie jambo lingine”
“Uibiwe nini mke wangu?”
“Nitaibiwa wewe”
“Mmh yani huo wivu wako majanga loh! Basi itabidi ukamshawishi mdogo wako Tausi aje hapa au unaonaje?”
“Hapo sawa, basi tutapanga ili nikaongee na mama nije nae hapa huyo Tausi anisaidie saidie ukizingatia hasomi wala nini”
Wakakubaliana pale kisha Ibra akaamua kwenda kuoga kwanza kuondoa uchovu wa siku hiyo ambapo alipomaliza kuoga akamwambia na mke wake nae akaoge, Sophia akainika na kwenda kuoga ila alikuwa na mawazo mengi sana mule bafuni haswa kwa mambo ambayo yanamtokea halafu hayaelewi elewi, alikuwa akijiuliza vitu vingi sana bila ya kupata majibu.
Alipotoka bafuni alimkuta Ibra akiwa kitandani amejilaza ambapo Ibra alimuita mke wake huyu ili aende pale kitandani na wajumuike nae.
Sophia alisogea karibu na alipo mumewe ila alimuangalia tu na kufanya Ibra amuulize,
“Sophy mke wangu mbona wanitazama tu kama hujui nilichokuitia? Unajua nimekumiss sana mke wangu”
Kisha Ibra akamsogelea kwa karibu Sophia na kumkumbatia huku akimpapasa, iala Sophy alionekana kutofurahishwa kabisa na kumfanya Ibra amuulize kwa kumshangaa,
“Vipi Sophy mke wangu nini tatizo?”
“Sijisikii”
“Hujisikii kivipi?”
“Kwani mtu akisema hajisikii huelewi au?”
Halafu Sophia akainuka pale kitandani na kuelekea sebleni, kitendo hicho kilimfanya Ibra amshangae sana mke wake na moja kwa moja akafikiria kuwa ni mimba iliyomfanya awe katika hali ya namna ile kwani katika maisha yao ya kawaida haijawahi kutokea hata mara moja Sophia kuongea maneno ya vile wala kumbishia mume wake katika tendo lile.
Ibra alitulia tu pale chumbani akitafakari na kujiuliza kuwa imekuwaje kuwaje maana ilikuwa ngumu kwake kuelewa.
Sophia alienda sebleni na kukaa kwenye kochi ila alijikuta akijifikiria sana kwa alichomjibu mumewe na moja kwa moja kujiona kuwa ana makosa, kwanza alijishangaa pia kuweza kumjibu mumewe vile wakati hajawahi hata siku moja kumkatalia hata kama akiwa hajisikii kweli.
“Mmh hivi Ibra atakuwa ananifikiriaje jamani loh! Kwanini nimefikia hatua ya kumjibu vile wakati ni mume wangu? Nina kila sababu za kwenda kumuomba msamaha maana jambo nililofanya si la kawaida kwakweli.”
Hivyobasi akainuka na kurudi tena chumbani ila alipoingia chumbani na kumuangalia Ibra pale kitandani hakumuona na kufanya ajiulize kuwa Ibra ameelekea wapi maana kama angetoka basi lazima angepita pale sebleni na yeye angemuona ila hakumuona kutoka, akajaribu kuita ila hakuitikiwa na Ibra. Moja kwa moja akahisi kuwa huenda Ibra yupo chooni hivyo akaamua kwenda chooni kumuangalia, ila alipofungua mlango wa choo hapakuwa na mtu yoyote na kumfanya Sophia apatwe na hofu moyoni.
Akaamua kwenda kukaa tena kitandani, alifika na kukaa huku akiwa na mawazo mengi sana alijiinamia kwa muda kisha akaamua kujitupa kitandani huku akiwaza alipokwenda Ibra. Ila alipojitupa tu alishtuka sana kwani alihisi kuwa kuna mtu amemlalia, kitendo hicho kilimfanya Sophia ageuke kuangalia ni nini akamuona ibra akiwa amelala tena hana habari kabisa.
Kwakweli Sophia alishtuka zaidi kwani mwanzoni hakumuona huyu Ibra hapo kitandani, akashangaa imekuwaje kuwaje.
Itaendelea kama kawaida…………..!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 7
Akaamua kwenda kukaa tena kitandani, alifika na kukaa huku akiwa na mawazo mengi sana alijiinamia kwa muda kisha akaamua kujitupa kitandani huku akiwaza alipokwenda Ibra. Ila alipojitupa tu alishtuka sana kwani alihisi kuwa kuna mtu amemlalia, kitendo hicho kilimfanya Sophia ageuke kuangalia ni nini akamuona ibra akiwa amelala tena hana habari kabisa.
Kwakweli Sophia alishtuka zaidi kwani mwanzoni hakumuona huyu Ibra hapo kitandani, akashangaa imekuwaje kuwaje.
Aliamua kumtingisha Ibra na kumuamsha ambapo Ibra aliamka huku akimshangaa Sophia kwa kumuamsha kwa nguvu vile,
“Yani kwa muda mfupi tu Ibra ndio umelala usingizi wa kiasi hicho? Kwanza niambie ulienda wapi?”
“Kwenda wapi kivipi?”
Ibra alikuwa akimshangaa mkewe, kisha Sophia akamueleza vile ambavyo yeye alikwenda sebleni na alivyorudi chumbani bila ya kumkuta pale kitandani na alipojaribu kumuita na kumuangalia sehemu mbalimbali bila ya kumuona na vile alivyofika pale kitandani na kushtukia kuwa amelala.
Kwakweli Ibra alijikuta akicheka tu huku akimuangalia mkewe mpaka Sophia akapata hasira na kumuuliza Ibra kwa ukali,
“Sasa kinachokuchekesha?”
“Jamani Sophia mke wangu kwakweli naona sasa hiyo mimba imeanza kukuendea kombo maana si kwa mambo unayoyafanya mmh!! Hivi inakuingia akilini kweli eti mimi usinikute hapa kitandani halafu urudi tena unikute, jamani aah! Mi nilikuwa nimelala hapa maana siwezi kubishana na wewe ukizingatia ushakataa ninachokitaka, ila uzuri ni kuwa natambua hali yako na ndiomana nikaamua kulala tu ila hilo swala lako la kutokuniona na kuniona ndio linanichekesha kwakweli”
Ingawa Ibra aliongea hayo ila ilikuwa ngumu sana kumuingia akilini Sophia ukizingatia ni jambo ambalo anajua wazi limetokea hata kama ikiwa ni kupoteza kumbukumbu basi si kwa staili ile.
“Sogea tulale mke wangu”
Ibra akamkumbatia Sophia na kumsogeza karibu yake ili wapate kulala kwani aliweza kuona kuwa mawazo ya Sophia hayakuwa sawa kwa muda huo.
Kulipokucha kama kawaida Ibra aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye shughuli zake, kma kawaida yake akamuaga Sophia kuwa anatoka ila kabla hajatoka Sophia akamzuia kutoka na kufanya Ibra amshangae na kumuuliza,
“Mbona unanizuia Sophy?”
“Usiende kazini leo sitaki kubaki peke yangu”
“Jamani Sophy mke wangu kwa staili hii tutaendelea kweli? Tutapata wapi pesa kwa ajili yetu na mwanetu mke wangu? Kwanini uwe hivyo jamani!”
“Nisamehe Ibra ila sijisikii kubaki mwenyewe”
“Basi inuka twende kwakina Jane tumuombe urudi nae hapa na ushinde nae, tafadhali tufanye hivyo mke wangu maana kazi nayo ni muhimu pia kwenye maisha yetu haya”
Sophia akakubali juu ya hilo, kisha akainuka pale kitandani na kutoka pamoja na mumewe wakielekea kwakina Jane.
Walifika na kuwagongea hata mama Jane alishangaa kuwaona asubuhi yote ile pale nyumbani kwake, ikabidi watumia Kiswahili cha kumvutia ili aweze kum,ruhusu Jane kwenda muda huo na Sophia nyumbani kwake. Mama Jane alielewa na kwenda kumuamsha Jane kisha kumwambia kuhusu ujio wa wakina Sophia.
“Mmh mama asubuhi yote hii jmani?”
“Naelewa kama ni asubuhi mwanangu ila hawa ni majirani zetu inapaswa kuwa nao karibu.”
Jane akaamka na kutoka nje kisha kuwasalimia Sophia na Ibra halafu akawaambia akaoge kwanza ajiandae ndio aende, ila Sophia aksamuomba Jane,
“Beba tu nguo, twende ukaoge nyumbani Jane”
Jane akafikiria kidogo na kukubali, kisha akaenda kuchukua nguo na kutoka halafu wakaingia kwenye gari ya Ibra ambapo aliwaacha pale nyumbani kwake kisha yeye kuelekea kwenye shughuli zake.
Sophia na Jane waliingia ndani ambapo kabla ya yote Jane aliomba kuonyeshwa uwani ili aweze kuoga na kujisafisha, Sophia alifanya hivyo kisha nay eye akaenda kuoga maana hata yeye alikuwa bado hajaoga kisha walipomaliza wakaandaa chai na kunywa halafu wakaanza stori za hapa na pale ambapo kwanza kabisa Sophia alimuomba msamaha Jane kwa kile ambacho kilitokea.
“Usijali dada nimeshakusamehe”
Sophia akatabasamu ingawa kiukweli bado alikuwa na maswali mengi sana moyoni mwake kuhusu hali halisi ya maisha yaliyopo pasle.
Muda kidogo Jane alianza na stori zake,
“Basi bhana jana usiku nimesoma stori hiyo inatisha hadi nikaogopa kulala, yani usingizi ukachelewa kuja balaa ndiomana mpaka saizi nina usingizi”
“Yani wewe kwa stori zinazotisha hujambo, hivi unazipendea nini jamani? Mwenzenu stori ambazo hazina uhalisia wala huwa sizifagilii”
“Uhalisia upo dada, unajua mara nyingine mtu unaweza ukalala halafu ukaota ndoto mbaya sana na usipokuwa makini ile ndoto inakutokea kwenye maisha halisi”
“Sasa kuhusu ndoto mbaya unakuwaje makini hapo?”
“Unajua inatakiwa ukiota ndoto mbaya ukishtuka tu Sali ili Mungu akuepushe nay ale mabaya uliyoyaota”
“Mmmh ila Jane wewe unanifurahishaga sana, hayo mastori yako ya kutisha ndio yamekufundisha hivyo? Kitu kama kipo kipo tu hata mtu ufanye nini”
“Ila na wewe dada kwa kupinga sikuwezi mmh. Ila kwakweli nina usingizi sana, nataka nilale tu hapa hapa kwenye kochi.”
“Hakuna shida wewe lala tu”
Sophia alitulia akiangalia runinga huku Jane akiwa amejilaza kwenye kochi.
Wakati jane akiwa amelala hoi kabisa, Sophia akasikia kama vyombo vikilia jikoni na kumfanya ashtuke sana huku akisikilizia kwa makini, kadri alivyozidi kusikiliza ndivyo mlio wa vyombo ulivyozidi kwakweli uoga ukamshika na kumfanya amshtue Jane kutoka usingizini ambapo Jane alishtuka sana huku akimuangalia Sophia kwa mshangao.
Sophia akamuuliza Jane kwa uoga flani hivi,
“Umesikia hiko?”
Ila muda huo ile sauti ya vyombo haikusikika tena na kumfanya Jane azidi kumshangaa Sophia kwavile yeye hakusikia kitu chochote kile.
“Sisikii chochote”
Sophia akakaa kimya kwa muda na kupumua kwa nguvu kanakwamba kitu ambacho kilikuwa kimetokea kilikuwa kikubwa sana, kisha Jane akamuuliza
“Kwani kulikuwa na kitu gani kikilia?”
Sophia alijikuta akishindwa kumjibu Jane kwani mdomo wake ulijawa na uzoito gafla.
Walikaa pale wakitazamana ambapo Jane aliamua tena kujilaza kwenye kochi ila Sophia aliogopa hata kwenda chooni kwa muda huo.
Mida ya mchana Jane alishtuka na kudai kuwa kwasasa usingizi umeisha na anaweza akafanya vitu vingine, kwavile Sophia aliogopa kwenda jikoni kutokana na mlio wa vyombo akaamua kumuomba Jane akapike chakula ili waweze kula.
“Mmh dada usije ukanifanyia kama mambo ya jana!”
“Hapana siwezi kufanya hivyo”
“Haya ngoja niende huko jikoni, ila unataka nipike nini?”
“Kuna maini kwenye friji, uyachukue halafu upike na wali”
“Hakuna tatizo”
Jane akainuka na kuelekea jikoni ili aweze kuandaa hiko chakula, ila alipofika jikoni kama alivyoona jana ndivyo alivyoona leo kuwa sufurua zimefunikiwa jikoni, akasogea na kufunua akaona maini yakiwa yameungwa vizuri sana tena yakiwa bado yamoto, kisha akafunua sufuria lingine ambapo napo akaona wali ukiwa umepikwa vizuri sana.
Jane akatabasamu na kujiuliza zaidi kuhusu tatizo la Sophia,
“Yani anapika mwenyewe halafu anasahau, basi hapo nikienda kumwambia mbona umeshapika atashtuka sana bora leo nisimwambie. Ngoja nirudi nimwambie vinachemkia nione kama anaweza kukumbuka kuwa ni yeye mwenyewe ndio alipika”
Kisha Jane akatoka jikoni na kwenda sebleni ambapo alimwambia Sophia kuwa ameacha vinachemkia, akamuona Sophia akipumua kidogo kwavile aliona kuwa siku hiyo hakuna maajabu yaliyotokea halafu wakaendelea kupiga stori mbili tatu ambapo Jane alimuuliza Sophia kuhusu swala lake la kupoteza kumbukumbu,
“Hivi tatizo lako la kupoteza kumbukumbu lilianza lini dada?”
“Tatizo la kupoteza kumbukumbu! Mi sina tatizo la kupoteza kumbukumbu”
Jane akacheka kisha akasema,
“Ama kweli mgonjwa huwa hajijui, yani dada hujui kabisa kama una tatizo la kupoteza kumbukumbu?”
“Sina hilo tatizo Jane, niamini jamani hilo tatizo sina kabisa”
“Haya basi ngoja nikusimulie kitu, kuna stori moja nilisoma kuhusu misukule yani unaweza ukaishi na misukule ndani bile kugundua”
Sophia akashtuka kidogo na kumuuliza Jane,
“Kuishi nayo kivipi”
“Unaweza ukashangaa unakaa kwenye nyumba labda umepanga kumbe mwenye nyumba ana misukule yake basi ukikaa unashangaa kama mtu kapita halafu humuoni huyo mtu kumbe ndio hiyo misukule”
“Uwiii mbona yanatisha hayo mambo!”
“Pole dada nilisahau kama hizi stori huzipendi”
“Kweli sizipendi ila ngoja kwanza, mtu unawezaje kugundua kama misukule ipo ndani na unawezaje kuiepuka?”
“Ila dada wewe si ulisema kuwa haya mambo ni ya kufikirika halafu hupendi stori za kufikirika, naomba niishie hapo, au umesahau kama ulisema kuwa hakuna misukule duniani ni stori tu wanazitunga”
Kisha Jane akainuka na kuelekea tena jikoni huku akiwa amemuacha Sophia akiwa na maswali mengi sana. Cha kwanza aliwaza uwepo wa misukule na matukio ambayo huwa anayaona kwenye ile nyumba kwani kwa kifupi yalikuwa yakimstaajabisha.
Jane akarudi tena na kumwambia kuwa ameshaandaa chakula mezani ila Sophia alijikuta akitaka kufahamu mengi sana kuhusu hiyo misukule na kujikuta akimuuliza maswali Jane ambapo jane akamuomba wakaulizane maswali hayo wakati wanakula.
Sophia alielekea mezani na kujiwekea chakula huku Jane nae akiwa amejiwekea cha kwake kisha Sophia akamuuliza tena Jane ila Jane bado alimpa masharti.
“Si vyema kuongea wakati wa kula dada, inatakiwa tumalize kwanza kula halafu ndio tutaendelea na maongezi”
Walikuwa wakila pale ila kichwa cha Sophia kilijawa na maswali mengi sana.
Walipomaliza kula jane alipeleka vile vyombo vyote jikoni kisha wakarudi kukaa sebleni ambapo Sophia akaanzisha tena maswali yake,
“Tafadhali Jane naomba unijibu maswali yangu”
“Haya niulize sasa nikujibu”
“Je misukule inaweza kufua nguo?”
“Kufua nguo! Mmmh! Sijui labda mwenye ile misukule akiiongoza”
“Sasa misukule inaweza kufanya vitu gani?”
“Mi ninachojua misukule inaweza ikala chakula chako ndani, huwa inapelekwa kulima nadhani hata mwenye misukule akiamua kuwa iwe inafua inaweza kufanya kazi hizo maana wale ni binadamu wa kawaida ila tu huwa wanaondolewa ufahamu”
“Basi niambie mtu unawezaje kujua kuwa unaishi na misukule na vipi unaweza kuiepuka?”
“Kuhusu kuishi nayo unaweza kugundua kama kukuta vitu vimefanyika ndani ndivyo sivyo ila kuiepuka sijui maana mi mwenyewe ile stori sijaimalizia”
“Mmh je misukule inaweza ikamdhuru mtu?”
“Misukule haina ufahamu dada, sidhani kama inaweza ikamdhuru mtu”
Sophia akawa kimya kwa muda ambapo Jane akaendelea kuongea,
“Kweli leo nimeamini kuwa kumbukumbu zako huwa zinapotea maana nakumbuka ulivyonikanusha kuhusu hizi stori halafu leo wewe ndio umekuwa wa kwanza kutaka kujua undani wake mmh kweli dada unasahau sana”
“Unajua nini Jane, kiukweli hizo stori mimi huwa siziamini ila kuna mambo flani hivi yananichanganya ndiomana nikakuuliza ila siku moja utayajua tu”
Wakiwa wanazungumza pale, Ibra nae akawa amerudi kutoka kwenye mihangaiko yake ambapo Sophia alimkaribisha mumewe na moja kwa moja akaenda kumpakulia chakula kwanza huku Ibra akimshukuru sana jane kwa kuweza kushinda na mkewe kwa muda wote toka ameondoka,
“Usijali kaka, mi nipo pamoja nanyi”
Sophia akamkaribisha mumewe mezani ambapo Ibra alikula chakula kile huku akikisifia sana kuwa ni kitamu, kisha akauliza
“Nani kapika?”
“Jane huyo”
“Khee huyu mtoto anajua kupika sana”
Sophia akatabasamua tu, baada ya Ibra kumaliza kula Sophia akatoa vile vyombo na kwenda kuviweka na vingine vichafu pale jikoni kisha akarudi sebleni ambapo Jane nae hakutaka kukaa zaidi kwani aliaga na kufanya Sophia na mume wake kuinuka na kumsindikiza ila hawakumfikisha hadi kwao, kisha Ibra akamuomba Jane uwepo wake kesho yake tena.
“Tafadhali Jane naomba kesho tuje tukufate tena ushinde na mke wangu”
“Hakuna tatizo kaka”
Kisha wakarudi na kumuacha Jane nae akielekea kwao.
Walirudi ndani huku Sophia akifurahia uwepo wa mume wake,
“Kwakweli nafurahi siku hizi unawahi sana kurudi”
“Lazima niwahi kurudi mke wangu maana siwezi kukuacha na hali yako hiyo”
Sophia akamuacha mumewe akaoge kisha yeye akaelekea jikoni ili aoshe vyombo na aweze kukaa na mumewe kuzungumza mawili matatu.
Alipoingoia jikoni alishangaa sana kuona vyombo vyote vimeoshwa na vimeshapangwa kabatini kwakweli alijikuta akipiga kelele na kumfanya Ibra amfate kwa haraka sana,
“Vipi Sophia nini tena mke wangu?”
“Misukule”
“Misukule! Misukule imefanyaje?”
Ibra alikuwa akimshangaa mkewe na kuangaza macho yake huku na kule kuangalia kama kuna chochote.
Itaendelea kama kawaida……………………….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 8
Alipoingoia jikoni alishangaa sana kuona vyombo vyote vimeoshwa na vimeshapangwa kabatini kwakweli alijikuta akipiga kelele na kumfanya Ibra amfate kwa haraka sana,
“Vipi Sophia nini tena mke wangu?”
“Misukule”
“Misukule! Misukule imefanyaje?”
Ibra alikuwa akimshangaa mkewe na kuangaza macho yake huku na kule kuangalia kama kuna chochote.
Ila Ibra hakuona chochote mule jikoni na kumuuliza tena mke wake,
“Sophy, misukule kivipi?”
“Misukule imeosha vyombo na kuvipanga”
“Misukule imeosha vyombo na kuvipanga? Wee Sophy akili yako iko sawa kweli? Unajua misukule wewe?”
Ibra alikuwa akimshangaa mke wake na kumuona kama ni mtu aliyekuwa akichanganyikiwa maana mambo aliyokuwa akiongea hayakuwa na mantiki yoyote ile.
Aliamua kumuinua mkewe pale chini na kuelekea nae chumbani kwani alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi.
Walipokuwa chumbani sasa, Ibra aliamua kumuacha kwa muda kitandani kisha yeye kwenda kuelekea kuoga kama alivyokuwa amepanga.
Kwakweli Sophia hakujielewa kabisa na kuhisi hadithi za Jane za kuhusu misukule zikianza kumuingia akilini vilivyo na kuona ni kweli ile nyumba yao ina misukule maana kila akiangalia yale matukio kengele ya hatari ndivyo ilivyozidi kulia katika ubongo wake.
Wakati akiwaza hayo akasikia kama mlango wa sebleni ukifunguliwa na kufungwa kanakwamba kuna mtu kaingia au katoka ila akajiuliza kuwa itawezekanaje ikiwa alishafunga mlango huo wakati wanaingia ndani, kwakweli uoga ulimshika mpaka pale Ibra alipotoka bafuni kuoga na kumkuta mkewe akiwa amejikunyata.
Ibra alimfata mkewe na kukaa naye karibu kisha akamkumbatia na kumuuliza kwa ukaribu zaidi,
“Kwani nini tatizo mke wangu? Unajua Napata shida sana kukuelewa!”
“Ibra hata mimi sielewi kwakweli yani sielewi kabisa kabisa”
“Unajua kwangu inakuwa ngumu sana kwasababu sijawahi kuishi na mwanamke mjamzito maana inawezekana haya ni mambo ya kawaida kwa wajawazito ila mimi sielewei kwakweli. Inabidi unifafanulie mke wangu kuwa ni mambo gani yanakusibu au ni vitu gani unaviona ili nijue tunaanzia wapi kupata ufumbuzi”
“Tatizo Ibra nikisema huniamini, hebu sikia tulitoka hapa tumeenda kumsindikiza Jane ila kulikuwa na vyombo vichafu jikoni, tumerudi ili nikavioshe nakuta vyote vimeoshwa wakati humu ndani tupo mimi na wewe tu. Nimekaa hapa nasikia mlango wa sebleni ukilia sasa hayo mambo yanamaana gani mume wangu?”
“Mmh kama hayo mambo ni ya kweli basi kuna makubwa”
“Mi nahisi kuna misukule humu ndani”
“Hebu Sophia tusiongelee hizo habari maana usiku huo unakuja tutashindwa kulala”
Kisha Ibra akamuomba mkewe ajiandae ili angalau watoke waende mahali wapate kubadilisha hali ya hewa.
Sophia alipomaliza kujiandaa, yeye na mumewe wakatoka mule ndani na kufunga milango vizuri kabisa kisha wakapanda kwenye gari yao na moja kwa moja Ibra akaelekea na mkewe hotelini ili kutimiza lengo lake la kubadilisha hali ya hewa ila kichwani alikuwa na maswali mengi sana ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati ule.
Kikubwa alichowaza ilikuwa ni kama Sophia anaongea ukweli kuhusu yale matukio basi lazima kuna kitu kinaendelea kwenye ile nyumba yao, pia akawaza kuwa kama ni kweli basi huenda majirani zao ni wachawi.
Ibra alikuwa kimya tu huku akinywa juisi taratibu ambapo Sophia akamuomba kuwa kesho yake ampitishe kwa Siwema ili akamsalimie,
“Basi kesho asubuhi unavyoondoka naomba mi ukaniache kwa Da’ Siwema nikamsalimie maana nimemkumbuka sana.”
“Mmh kwa nikujuavyo wewe utataka kumwambia mambo yanayotokea nyumbani, tafadhari usimwambie kabla hatujayafanyia ufumbuzi”
“Wala hata sina nia hiyo ya kumwambia, mi nataka nikamsalimie tu”
Ibra alikubaliana na mke wake ingawa alielewa wazi lengo la mkewe ni nini ukizingatia huwa hawezi kukaa na kitu moyoni, wakazungumza zungumza pale kisha wakarudi nyumbani.
Wakati wanarudi kama kawaida wakamuona Yule mtoto akisimamisha gari yao kama ile siku ya kwanza ila kwakweli leo Ibra hakutaka huu ujinga kabisa na akapita kamavile hajaona chochote na kufika mbele akasema kuwa hawtoenda tena kula kwenye ile hoteli kwani aliona kamavile inamahusiano ya moja kwa moja na Yule mtoto ambaye wanamkutaga njiani.
Walifika nyumbani na moja kwa moja wakaenda kulala kwani Ibra hakutaka kupoteza muda wa kujiwekea mawazo ya tofauti.
Kulipokucha kama walivyopanga, Ibra alijiandaa huku Sophia nae akijiandaa kisha wakatoka kwa pamoja na kufunga milango kama kawaida.
Ibra alimpeleka Sophia mpaka kwa Siwema na kumuacha hapo, ambapo Sophia alimgongea Siwema ila alikaa kwa muda bila ya kufunguliwa na kumfanya aamue kukaa nje ya nyumba hiyo akimsubiri huyo Siwema.
Baada ya masaa kama mawili, Siwema alitoka ndani tena alionekana akiwa amechoka choka hivi na alipomuona Sophia alimshangaa sana na kumuuliza
“Khee Sophia mbona asubuhi subuhi! Umefika hapa saa ngapi?”
“Nimefika muda tu dada, nimegonga weee ila hujanifungulia ndio nikaamua kukaa hapa nje.”
“Pole sana kwakweli hata sikusikia kugonga kwako jamani, karibu Sophy. Kwanza najishangaa leo kuchelewa kuamka kiasi hiki jamani”
Siwema akamkaribisha Sophia ndani kisha wakakaa pamoja huku Siwema akitamani kujua kilichompeleka Sophia mahali pale kwani haikuwa kitu cha kawaida kwa Sophia kwenda pale tangu alipohama.
“Vipi kwema lakini?”
“Kwema tu dada”
“Kwahiyo naweza kwenda kuoga kisha tukaendelea na maongezi ya hapa na pele?”
“Ndio dada wala hata usijali kitu”
Siwema aliinuka na kwenda kuoga ili kuondoa uchovu wake kisha akaandaa chai na kuanza kunywa, ila Sophia alipokunywa kidogo tu alikimbia nje na kutambika hivyobasi kumfanya Siwema awe na mashaka juu ya afya ya Sophia.
“Vipi mdogo wangu au twende hospitali?”
“Hapana dada, nadhani nimetapika kutokana na mimba niliyonayo”
“Wow, una mimba Sophy!”
“Ndio dada”
“Kwakweli hiyo ni khabari njema, hongera sana mdogo wangu. Cha msingi kwasasa ni kuzingatia chakula bora ili kuufanya mwili wako upate afya na nguvu. Kula matanda kwa wingi na mboga za majani”
“Asante dada”
“Vipi umeshaanza kliniki?”
“Bado sijaanza ila nitaenda kuanza”
“Ni vyema ukaanza kliniki mapema mdogo wangu kwani inasaidia kujua ukuaji wa mtoto na pia kuangalia mwenendo mzima wa afya yako”
“Hakuna tatizo dada huko kliniki nitaenda tu ila yaliyonileta hapa leo sio hayo ni mengine kabisa”
“Mmh yapi hayo tena Sophy?”
Sophia akaanza kumueleza Siwema kuhusu mambo ambayo ameyaona hivi karibuni katika nyumba yake, pia akamuelezea kuhusu Jane jinsi walivyozoeana na jinsi ambavyo Jane amekuwa akimsimulia kuhusu habari za misukule. Pia akamsimulia kuhusu kile chakula ambacho Sophia alihisi kuwa kimepikwa na Jane kwa dakika mbili, na kumueleza alivyofahamiana na mama Jane hadi yeye kuwa karibu na huyo Jane.
Siwema akapumua kidogo na kumuangalia Sophia kisha akamuuliza,
“Hivi mpaka hapo hujaelewa mchezo mzima unaondelea mdogo wangu?”
“Kivipi dada?”
“Hebu kwanza niambie huyo Jane anajishughulisha na nini?”
“Jane kamaliza kidato cha nne kwahiyo huwa yupo nyumbani tu akisubiri matokeo”
“Mmmh mdogo wangu hapo akili kichwani mwako, huyo binti kwanza hashindwi kukupiku kwa mumeo ukizingatia kila mumeo anapokula chakula chake anakisifia kuwa kitamu sana, kwanza umenieleza hapa kuwa huyo binti wala hawana matumaini nae kuwa atafaulu au la kwahiyo mama yake hashindwi kumlengesha kwa Ibra ili angalau hata awe mke wa pili ampunguzie majukumu”
“Jamani dada mbona hayo mapya sasa, inamaana na haya maajabu ya ndani kwangu yanasababishwa na yeye?”
“Ndio, hisia zangu zinanituma kuwa huyo binti atakuwa mchawi yani ingawa simjui ila naona kabisa kuwa ni mchawi, na yote anayafanya ili kukutisha na nyumba yako. Anataka uiogope nyumba yako na ikiwezekana uondoke ili ajilengeshe kwa Ibra. Yani usipokuwa makini utashangaa anaolewa nay eye, si vizuri kuokoteza majirani mdogo wangu mwisho wa siku unapata ya kuyapata kama hivi”
“Mmh au ndiomana ananitishia na stori zake za misukule?”
“Ndio, anataka uoanishe matukio na stori zake ili upatwe na uoga halafu mwisho wa siku uone nyumba mbaya na uikimbie nyumba yako aingie yeye. Hivi unafikiri ni nani asiyetamani kuishi kwenye jumba la kifahari kama lilre? Nani asiyependa maisha ya raha unayopewa wewe na mumeo?Hakuna Sophy, kila mwanamke anatamani kuishi vizuri kwa furaha na amani unatakiwa uwe makini sana”
“Nashukuru dada ila nitafanyaje kumuepuka?”
“Kwanza kabisa mzuie kuja nyumbani kwako, halafu pili kuna mtaalamu nitakupeka atatupa dawa ili tumzuie kabisa kabisa kukanyaga na mauchawi yake.”
“Kwahuyo mtaalamu tutaenda lini sasa?”
“Nadhani itakuwa vyema tukienda kesho, wataalamu hawaibukiwi hovyo hovyo. Inatakiwa kudamka asubuhi na mapema na kuelekea huko.”
Wakaendelea na stori mbali mbali huku Siwema akimfundisha Sophia namna ya kutunza mimba aliyokuwa nayo na jinsi ya kumtunza Ibra hata katika hiko kipindi cha ujauzito wake.
Jane kama ambavyo aliongea na wakina Sophia jana yake na jinsi ambavyo walimuomba kuwa na siku hiyo aende nyumbani kwao ili akampe kampani Sophia, alipoamka tu alienda kujiandaa kisha kumuaga mama yake kuwa anaenda nyumbani kwa Sophia,
“Mmmh kushakunogea tayari!”
Jane akatabasamu kisha akamuaga mama yake na kuelekea huko kwa Sophia.
Alipofika, alikuta geti liko wazi kabisa na kushangaa kuwa imekuwaje wamesahau hata kurudishia geti lile akajiuliza na kuingia kisha akalirudishia huku akiongea
“Usikute dada Sophy bado hajatoka nje maana si kawaida hili geti kuwa bwamu kiasi hiki”
Alipofika mlango wa ndani aligonga ila hakufunguliwa na kujaribisha kufungua ambapo nao ulifunguka na kumfanya Jane aingie ndani na kukaa pale sebleni huku akiita.
“Dada, dada, dada Sophy”
Ila hakujibiwa, moja kwa moja akahisi kuwa huenda Sophia ameenda Sokoni ila kwanini hakufunga milango? Akajipa jibu kuwa huenda aligundua kuwa atafika ndiomana hakufunga milango.
Alikaa kaa pale na kuamua kuwasha video huku akimsubiri Sophia arudi ila wakati akiangalia alijikuta akipitiwa na usingizi na kulala pale pale kwenye kochi.
Ibra alipomaliza shughuli zake aliamua kumfata Sophia kule nyumbani kwa Siwema ili aweze kurudi nae nyumbani, alimkuta mkewe akiendelea na maongezi mbalimbali na Siwema ambapo naye alijumuika kidogo kisha kuaga.
“Ila kabla ya yote shemeji napenda kukupongeza kwa ujauzito alionao mdogo wangu”
Ibra alitabasamu kidogo na kushukuru huku akitoka nje na Sophia, ila Sophia akamuuliza tena Siwema,
“Vipi hiyo kesho nije au wewe utakuja nyumbani?”
“Itakuwa vyema kama ukija Sophy”
Kisha Sophia na Ibra wakapanda kwenye gari na safari ya kurudi kwao ikaanza.
Wakiwa kwenye gari Ibra alimuuliza mkewe,
“Kwahiyo siku hizi habari itakuwa ni hii ya kuletana kwa Siwema au?”
“Mmmh jamani Ibra si leo na kesho tu, au kama utashindwa basi nitakuja mwenyewe”
“Haya basi usinune maana na wewe siku hizi kitu kidogo tu unanuna, ila tabia yako sijaipenda”
“Ipi tena?”
“Yani mimba change hivyo umeshaanza kuitangaza mmh!”
“Jamani Ibra kwani kuna ubaya gani kumwambia Da’ siwema jamani wakati ni kama ndugu yangu!”
“Sawa umefanya vyema ila kiukweli mimba haitangazwi, acha itajitangaza yenyewe”
Sophia akanyamaza kwani aliona kamavile ni marumbano kidogo na mume wake.
Wakiwa wanaendelea na safari yao, ibra akapita karibia na njia ya ile hoteli ambapo mbele kidogo walikaona kale katoto ial leo kalionekana kamelala chini na kumfanya Sophia ashtuke sana kisha Ibra akamwambia,
“Achana na habari za hako katoto, hakana jema na maisha yetu wala usishtuke. Safari ijayo sitapita tena njia hii”
Wakaendelea na safari yao hadi walipofika kwenye nyumba yao.
Sophia alishuka na kufungua geti kisha Ibra akaingiza gari ndani halafu wakafunga geti na kufungua mlango wa kuingia ndani, kwakweli Sophia alishtuka sana kumuona Jane akiwa amelala kwenye kochi na kuita Ibra kwa nguvu aliyekuwa akipaki gari lake vizuri.
Ibra aliingia ndani huku nae akishangaa kwani halikuwa jambo la kawaida, Sophia alishikwa na hasira sana na kumsogelea Jane pale kwenye kochi na kumkurupua kwa kumpiga ambapo jane nae alishtuka kama chizi na kuanza kupiga kelele za mwizi tena kwa nguvu kabisa.
Itaendelea kama kawaida………………….!!!!!!!! NYUMBA YA MAAJABU: 9
Ibra aliingia ndani huku nae akishangaa kwani halikuwa jambo la kawaida, Sophia alishikwa na hasira sana na kumsogelea Jane pale kwenye kochi na kumkurupua kwa kumpiga ambapo jane nae alishtuka kama chizi na kuanza kupiga kelele za mwizi tena kwa nguvu kabisa.
Zile kelele zilifanya watu waanze kukusanyika nje ya nyumba ya Ibra, kitu ambacho Ibra hakuona kuwa ni sahihi na kuanza kumtuliza Jane aliyekuwa na mawenge ya usingizi, kisha kutoka nae nje na kuwaomba watu msamaha kuwa hakuna jambo lolote baya ila Sophia alitamani wale watu wampige Jane kwani alikuwa sawasawa na mwizi kuingia kwenye nyumba ya watu wakati wao wamefunga milango, watu walipoanza kutawanyika kwakweli bado ilikuwa ngumu sana kwa Sophia kukubaliana na uwepo wa Jane mahali pale,
“Tafadhali Ibra, huyo binti sitaki kumuona yani sitaki kumuona kabisa huyo binti ni mchawi, nimesema sitaki kumuona yani naweza kumfanya kitu kibaya”
Ilibidi Ibra amuombe Jane aende kwao, kwakweli Jane aliondoka huku analia kwani hakuipenda ile kauli ya Sophia ya kumuita kuwa yeye ni mchawi.
Ingawa Jane alikuwa akiondoka huku analia ila bado Sophia aliokota kitu chini na kumpiga nacho Jane kwa nyuma na kufanya Jane aanguke, kwakweli Ibra alishangaa sana kwani ilikuwa ni kitendo cha ghafla ambacho hakukitarajia kabisa kufanywa na mke wake Sophia.
“Khee Sophia umefanya nini sasa? Mbona unataka kuleta mabalaa tena jamani?”
Ibra akamkimbilia Jane pale chini na kujaribu kumuinua ila Jane alikuwa akitokwa na damu puani, kitu ambacho kilimuogopesha Ibra na kuona wazi mkewe amemdhuru Jane. Ibra aliamua kumbeba Jane na kukimbilia kumpakiza kwenye gari yake ili kumkimbiza hospitali ambapo Sophia nae alipanda kwenye hilo gari kisha Ibra akatoa gari lile na hata wakasahau kufunga milango kwani ilikuwa kama kuchanganyikiwa.
Walipofika hospitali walipokelewa na wahudumu kama kawaida kisha Jane kukimbizwa wodini na daktari kuitwa ambapo ilibidi Ibra amuombe daktari amtibie Yule mgonjwa huku akimpa pesa ili asiambiwe maswala ya PF3,
“Ila hii kitu tunafanya kinyume na utaratibu maana hairuhusiwi kisheria”
“Tafadhali nakuomba daktari nisaidie naomba”
Daktari akaanza kumchunguza Jane ni kitu gani kimempata mpaka kupelekea atoe damu puani kwani ilikuwa ikitoka nyingi huku Jane akiwa amepoteza fahamu.
Kwakweli Ibra alikuwa kama kachanganyikiwa huku akingoja hatma ya Jane kwa wakati huo, ila Sophia yeye alikuwa kwenye gari tu wala hakushika kufatilia kam Jane atatibiwa au la kwani moyoni mwake alijikuta akiwa amemchukia Jane kupita maelezo ya kawaida na ukizingatia yale maelezo aliyopewa kuhusu uchawi wa jane na vile walivyomkuta ndani ndio kabisa vikamfanya Sophia aamini kuwa Jane ni mchawi tena ni mchawi aliyekubuhu ndiomana kila siku anamletea stori za ajabu ajabu ili kumtisha na mambo yake ya kishirikina.
Ibra alirudi kwenye gari na kumuangalia mke wake kisha akamuuliza,
“Hivi Sophia una mapepo au kitu gani? Akili yako ni nzima kweli?”
“Usiniulize hayo maswali kwasababu ya Yule firauni Jane, laity ungejua kwamba Yule binti hafai kiasi gani wala hata usingenilaumu yani tena ungenisifia mna kunisapoti kuwa tummalize kabisa”
“Jamani Sophia ni roho ya wapi hiyo uliyonayo? Kwakweli sio mke ambaye nilikuzoea mimi jamani sio kabisa kabisa, kwakweli Sophia unanishangaza tena unanishangaza sana”
Kisha Ibra akashuka tena kwenye lile gari ili kwenda kusikilizia hali ya Jane inaendeleaje.
Alimkuta daktari ndio ametoka kwenye kile chumba walichompeleka Jane kisha akamfata daktari huyo na kumuuliza kuwa imekuwaje kuhusu Jane.
“Anaendelea vizuri ingawa aliumia sehemu za nyuma ila kuna dawa tutawapa ili awe anakunywa kwaajili ya kumrudisha katika hali ya kawaida.”
“Kwahiyo tutaweza kurudi nae nyumbani?”
“Yeah itawezekana ingawa muda utakuwa umeenda sana kwani sasa tumemuweka mapumziko kwa muda”
Ibra alkakubaliana na maneno ya daktari kisha akatoka nje na kwenda kukaa kwenye gari huku akisubiria muda uende ila alimkuta Sophia akiwa amejilaza mule kwenye gari, hakutaka kumsumbua na kumuacha alale tu.
Ibra nae alikuwa kimya mule kwenye gari huku akitafakari mambo mbali mbali kwani akili ya mke wake hakuielewa kwakweli ingawa hakuelewa zaidi kuhusu Jane kuwa amewezaje kuingia ndani ilihali walifunga milango yote asubuhi wakati wa kuondoka? Akabaki na maswali mengi sana kichwani bila ya kupata majibu ya aina yoyote ile.
Kwenye mida ya saa nne usiku ndipo waliporuhusiwa kuondoka na Jane ambaye alikuwa amezinduka muda huo hata fahamu nazo zilikuwa zimemrejea, wakapatiwa na dawa ambazo zitazidi kumsaidia Jane.
Ibra alifungua mlango wa nyuma ambapo Jane alipanda kwani pale mbele alikaa Sophia na hata hivyo hakuweza kuwaweka Sophia na Jane mahala pamoja kwa muda huo kwani alijua wazi kuiwa bado Sophia ana kinyongo na Jane.
Ibra aliondoa gari, na alipofika mahali alisimamisha na kuagiza chips ili waweze kula wakifika nyumbani kwani alijua wazi kuwa ni ngumu kupika kwa muda huo. Muuzaji aliwafungia vizuri zile chips na kuwapatia kisha safari yao ya kurudi ikaendelea, ila Jane aliwaomba wampeleke kwao moja kwa moja ambapo Ibra alimuuliza,
“Kwanini tusiende nyumbani kwanza ule halafu ndio tukupeleke kwenu!”
“Hapana nitaenda kula nyumbani na hata hivyo sijisikii kula chips”
“Ila unajua muda umeenda sana Jane, sidhani kama utakuta chakula kwenu”
“Kwetu hawanaga tabia ya kumaliza chakula chote, nitakikuta tu”
“Basi sema chakula unachotaka tukanunue hata hotelini uende nacho kwenu ukale”
Sophia akaingilia kati yale mazungumzo,
“Jamani si ameshasema anataka kwenda kwao, hebu tumpeleke maana mada zinakuwa nyingi sasa”
Ibra hakuongeza neno lolote kwani hakutaka Sophia aongee zaidi maneno mabaya na kumkwaza Jane. Moja kwa moja walimpeleka Jane nyumbani kwao ambapo Ibra alishuka na kuongozana nae huku akimuomba Jane kuwa asiseme chochote juu ya kilichotokea kwa mama yake,
“Tafadhali Jane, usimwambie chochote mama yako”
“Akiuliza nilipokuwa je!”
“Mdanganye hata tulikupeleka kutembea ila usiseme chochote kuhusu kilichotokea, nakuomba Jane”
“Sawa”
Kisha wakafika mlangoni na kugonga ambapo mama Jane ndiye aliyetoka kuwafungulia na alipowaona tu kuwa ni wao alianza kuongea,
“Yani leo mmenikwaza jamani yani toka asubuhi mpaka muda huu kweli! Jane umeondoka hapa asubuhi hadi saa hizi jamani, mtatuuwa kwa presha maana wengine hatupo sawa jamani”
Ikabidi Ibra ajaribu kumuomba msamaha pale,
“Tafadhali mama tusamehe sisi maana hatukutoa taarifa yoyote juu ya kuondoka na Jnae, kuna mahali tulienda nae kutembea ila kwa bahati mbaya ndio tumechelewa kurudi tafadhali mama tusamehe sana”
“Sawa ila mmenikwaza kwakweli”
Kisha Ibra akaagana nao pale halafu akarudi kwenye gari na kuelekea nyumbani kwao akiwa na Sophia.
Walifika na kukuta geti limefungwa vizuri ambapo Ibra alishuka na kufungua kisha akarudi kwenye gari na kuingiza gari ndani halafu akalipaki ambapo akashuka pamoja na Sophia na ule mfuko wa chips kisha akarudi kurudishia geti, alimuacha Sophia akiwa amesimama tu na alipotoka kufunga geti alimkuta kasimama vile vile na kufanya amuulize kwa mshangao,
“Khee mbona hufungui mlango wa ndani?”
“Fungua mwenyewe, mi sitaki miujiza”
Ibra alikuwa akimshangaa tu mkewe kisha akachukua funguoambazo Sophia ndiye aliyemkabidhi funguo hizo na kufungua halafu wakaingia ndani ambapo kila mmoja alikuwa na mawazo yake ya kutosha tu na kuwafanya wakae pale sebleni kwanza, Kisha Sophia akamuuliza Ibra
“Hivi kwa kumbukumbu zako wakati tunampeleka Jane hospitali tulifunga milango?”
“Mmmh kwakweli sikumbuki”
“Mi basi nakumbuka vizuri maana funguo nilikuwa nazo mimi, milango hatukufunga wala nini. Sasa jiulize ni nani kafunga?”
“Kwahiyo unataka kusema Jane kafunga?”
“Jane sio mtu mzuri mume wangu ingawaje unamtetea, yani Yule binti sio mtu mzuri kabisa. Asubuhi tumeondoka hapa na milango yote tumefunga cha kushangaza tumerudi na kumkuta ndani je alipitia wapi? Yule binti ni mchawi mume wangu wala usijitahidi kumtetea”
Ibra alikaa kimya kwanza maana hilo swala kidogo lilimchanganya na kuhusi huenda kuna ukweli ndani yake. Kisha akainuka na kwenda kuleta sahani ili waweke zile chips na kuweza kula, alipofika na sahani akachukua ile mifuki ya chips ili aweke ila wakapatwa na mshangao kwani kwenye ile mifuko hawakukuta chips wala nini.
Walijikuta wakishangaa na kutazamana kwa zamu zamu, Ibra alimuuliza mkewe
“Ni nini hiki Sophy?”
“Sasa unaniuliza mimi naelewa?”
“Makubwa haya, sijawahi kutapeliwa hivi. Inamaana wale wauzaji hawakutupimia chips au?”
“Hata usiwalaumu wauzaji, kwa macho yabgu niliwashuhudia wakipima na kuweka kwenye mifuko, tatizo ni kuwa tumenunua hizi chips tukiwa na Jane. Yule mtoto si mtu mzuri itakuwa amezichukua kiuchawi”
“Mmh naanaza kuamini sasa, au ndiomana alikataa kuja huku na kujifanya hataki kula chips!”
“Ndion hivyo Ibra, binti gani asiyependa chips? Jiulize tu utapata jibu, kwanza walivyo na dhiki pale kwao eti huwa hawana tabia ya kumaliza chakula chote loh wakati huwa wanakula hadi wanagombaniana mmh! Leo tumeingia choo kibaya mume wangu”
“Sasa tutakula nini?”
“Yani kale katoto kabaya kanataka tulalae na njaa loh!”
Ibra akafikiria na kuona kuwa ni vyema hata wakakoroga uji ili angalau wale kitu na kwenda kulala,
“Ngoja nikakoroge uji mke wangu, kwakweli leo tumepatikana dah!”
Ibra alienda jikoni na kuanzakukoroga uji ambao baada ya muda ulikuwa tayari kisha akaanza kunywa na mkewe,
“Kheee kwani huu uji umeweka nini?”
“Sijaweka chochote zaidi ya sukari tu”
“Mmh mbona mtamu hivi?”
“Hata mimi mwenyewe nashangaa, halafu hata haujachelewa kuiva yani”
Wakanywa na kumaliza, kisha Sophia akapeleka vyombo jikoni halafu yeye na mumewe wakaelekea chumbani kwa lengo la kulala, ila Sophia alidai amechoka sana kiasi kwamba hata kuoga anaona uvivu.
“Kwakweli nimechoka, mi siogi bhana leo”
“Shauri yako ila uchafu unafanyaga watu waote ndoto mbaya”
“Mmh ushaanza maneno yako”
“Sio hivyo, ukumbuke wewe una mimba utamfanya mtoto nae awe mchafu kwasababu yako”
“Aah yani mi sijisikii kabisa kuoga yani”
“Kama hujisikii sikulazimishi maana kuoga ni hiyari ya mtu”
Kisha Ibra akaenda kuoga ila aliporudi alimkuta mkewe akiwa ameshalala muda mfupi uliopita ambapo naye akaungana nae na kulala nae.
Ibra alimsogelea mkewe na kumkumbatia ambapo alipofanya hivyo, Sophia alishtuka kamavile kapatwa na jambo baya kwani alisema kwa nguvu
“Niache”
Kwakweli Ibra alimshangaa ila Sophia alikuwa akihema sana huku jasho likimtoka,
“Khee Sophia umepatwa na nini si umelala sasa hivi tu jamani”
“Hata sielewi”
Huku akihema sana, Ibra alijaribu kuwa nae karibu ili kumfanya arudi kwenye hali ya kawaida kwani alihisi kuwa huenda ameota ndoto mbaya ya gafla.
Baada ya muda kidogo wakaamua tena kulala na kulala pamoja.
Kulipokucha leo Sophia ndio alikuwa wa kwanza kuamka na kumuamsha mumewe ambapo Ibra nae akaamka kisha kwa pamoja wakaenda kuoga, wakati wanajiandaa Ibra akamuuliza mkewe
“Kwahiyo na leo tena kwa Siwema?”
“Sio lazima unipeleke maana naona unataka kuniwekea vikwazo”
“Ila Sophy mke wangu kwani umekuwaje siku hizi jamani? Unajua hukuwa hizi zamani yani tunaongea kamavile ni watu wenye maugomvi mke wangu dah!”
“Sio maugomvi, mimi nataka kuokoa nyumba yetu wewe unaona ni ujinga ndiomana naongea hivi”
“Haya unataka kuiokoaje hii nyumba?”
“Hii nyumba imeingiliwa na adui Jane kwahiyo lazima niiokoe”
“Sawa ila je kuiokoaje?”
“Wee subiri tu nitakupa majibu badae”
“Haya twende nikupeleke huko kwa Siwema”
Wakamaliza kujiandaa na kutoka kisha safari ikawa ni kuelekea nyumbani kwa Siwema kwanza kisha ndio Ibra aende kwenye safari zake zingine.
Walifika nyumbani kwa Siwema ambapo Sophia alishuka kisha Ibra akaondoka zake, moja kwa moja Sophia alienda kugonga mlango wa Siwema ambaye hakukawia kutoka na kusalimiana na Sophia kisha akamwambia amsubiri ajiandae haraka haraka waende.
“Karibu ndani basi unisubirie”
“Aaah acha tu nikusubirie hapa hapa nje bhana”
“Kama unaona ni sawa basi sawa, ngoja nijiandae haraka haraka”
Siwema akaingia ndani kujiandaa kwani alikuwa tayari ameshaoga, Sophia nae akainuka na kuusogelea mti wa mpera pale karibu na kwa Siwema ili kuangalia kama una mapera ili achume japo moja atafune ingawaje anajua wazi kuwa ule mti hauna historia ya kuwa na mapera.
Alipokuwa chini ya ule mti, alishtuliwa na bibi mmoja ambaye alikuwa anapita mahali hapo na kumfanya Sophia ashtuke sana huku akimuangalia bibi huyo, Yule bibi akamwambia Sophia
“Pole kwa kukushtua”
Sophia alimuangalia kwa muda kidogo kisha akamjibu,
“Asante”
“Huu mti wa mpera si mzuri”
“Kwanini?”
“Huwezi kupata pera hata moja hapo kwavile huu mti umechezewa sana”
“Khee unaujua huu mti wewe?”
Huyu bibi akacheka kidogo na kusema,
“Naujua sana huu mti, hata nyumba yako naijua”
Sophia alimshangaa na kumuuliza,
“Nyumba yangu unaijua kivipi?”
“Nyumba yako ni ya maajabu”
Sophia akashtuka na kuzidi kumshangaa huyu bibi.
Itaendelea kama kawaida……………………..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 10
“Huu mti wa mpera si mzuri”
“Kwanini?”
“Huwezi kupata pera hata moja hapo kwavile huu mti umechezewa sana”
“Khee unaujua huu mti wewe?”
Huyu bibi akacheka kidogo na kusema,
“Naujua sana huu mti, hata nyumba yako naijua”
Sophia alimshangaa na kumuuliza,
“Nyumba yangu unaijua kivipi?”
“Nyumba yako ni ya maajabu”
Sophia akashtuka na kuzidi kumshangaa huyu bibi, kisha akamuuliza kwa mshangao
“Nyumba yangu ya maajabu kivipi”
Mara Siwema akamuita Sophia ambapo Sophia alimtazama Yule bibi na kwenda alipoitwa na Siwema, kisha Siwema akamwambia Sophia
“Yani unapoteza muda wako kabisa unaongea na Yule bibi!”
“Kwani ana tatizo gani dada?”
“Yule bibi ni mwanga yani kashindikana nakwambia, ni mchawi hakuna mfano. Unavyomuona hakuna hata mtu mmoja anayezungumza nae mtaani kwake yani Yule bibi hafai tena hafai kabisa kabisa”
“Alikuwa ananiambia eti nyumba yangu ni ya maajabu”
“Mmh usimsikilize kabisa, alikuwa anajaribu kukuteka tu kwakweli Yule bibi hafai mdogo wangu”
“Halafu kasema eti ule mpera wako umechezewa sana na kamwe hauwezi kuzaa mapera”
“Sophy, achana na Yule bibi yani kuhusu huo mpera ndio kauandama balaa achana nae kabisa. Tena bahati yako hajagundua kuwa una mimba maana hakawiii kuvuruga mimba za watu Yule.”
“Mmh dada tuondoke asije akaniletea makubwa bure, nampenda mwanangu”
Kisha wakatoka pale na kuanza safari yao ya kuelekea kwa mtaalamu.
Walifika kwa mtaalamu na kukuta watu wengi sana wakisubiri kuingia humo, ikabidi wapange foleni na wao ili zamu yao ikifika waweze kuingia. Kwa upande wa Sophia hii ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kwenda kwa mganga wa kienyeji kwahiyo ile hali aliishangaa sana,
“Kheee kumbe ndio kunakuwaga na watu wengi hivi!”
“Na hapa bado, ndiomana jana nikakataa na kukwambia kuwa muda umekwenda sana maana nilijua lazima tungekuta foleni kubwa zaidi”
“Mmh! Kwahiyo waganga wote ninaowasikiaga ndio huwa wanajaza watu hivi?”
“Hapana si wote, mara nyingi watu hujaa kwa wataalamu wa ukweli maana mtu unakuwa umeona mafanikio na kuwaambia wengine, ila kwa upande wa wale matapeli hata hawanaga watu wengi kivile wanadanganya sana na watu wamewashtukia hawaendi”
“Mmh yani sijawahi kwenda kwa waganga mie kwakweli Yule Jane kaninyoosha”
“Mama yenu nae hajawahi kweli? Maana mi mama yangu ndio kanifundisha haya mambo, yeye sasa ni kitu kidogo tu anaenda kwa mganga. Kwani Jane umeonana nae tena?”
“Tena ngoja nikusimulie kisanga cha jana”
Sophia akaanza kumueleza Siwema yale yaliyotokea jana waliporudi nyumbani kwao na kumkuta Jane ndani ilihali walifunga milango wakati wa kutoka hadi kuhusu kuyeyuka kwa zile chips.
“Kheee huyo mtoto mbona mchawi kiasi hicho! Hadi namchukia kabla sijamuona jamani loh, yani milango ulifunga sasa ndani kaingiaje? Na hizo chips uwiiii huyo mtoto ni wa kumuogopa kama ukoma. Tena ikiwezekana tumuombe mtaalamu atupe dawa ya kummaliza kabisa huyo binti maana si kwa uchawi huo jamani.”
“Ndio hivyo yani toka nimfahamu mambo ya ajabu nayo yanaongezeka jamani, nilikuwa siamini mambo ya uchawi ila Yule mtoto kaninyoosha. Alikuja na gia ya kunisimulia stori zake za kutisha hadi nikaanza kuiogopa nyumba yangu kumbe ana malengo yake.”
“Huyo mtoto ni wa kumuepuka kabisa yani tukipata dawa ya kummaliza nitashukuru sana”
Muda wao ukafika na kuwafanya waingie kwa mtaalamu ambaye aliwapokea kwa kicheko na kuwafanya wawe kimya kimshangao, ambapo muda kidogo mtaalamu akaanza kuwaambia,
“Tatizo lenu nalijua, mmekuja kwasababu ya binti mmoja anayewasumbua akili zenu anaitwa Jane”
Kwakweli Sophia alishangaa sana jinsi huyu mganga alivyoweza kugundua tatizo lao kwa urahisi kiasi kile, kisha Siwema akamwambia mganga
“Yani huyo binti anatutesa sana babu tafadhali utusaidie”
“Mnataka tumfanye nini?”
“Naomba tummalize kabisa maana hata hatutaki kumuona machoni petu babu, tafadhali tusaidie”
“Basi mimi nitawapatia dawa ya kuweza kummaliza na hatoonekana tena mbele yenu”
“Asante babu”
Basi Yule mganga akachukua unga unga na kuufunga kwenye karatasi vizuri kabisa kisha akawapa huku akiwaambia masharti ya ile dawa,
“Dawa hii mnatakiwa kumkaribisha Jane nyumbani kwenu, ukiona anakaribia kuja unainyunyuzia mlangoni. Kisha akija ataingia ndani, halafu nenda kamchukulie kinywaji chochote juisi, soda au maji muwekee hiyo dawa mpelekee anywe yani akinywa tu kwisha habari yake hamtasikia cha Jane wala ujinga gani”
Sophia akaguna kidogo,
“Mmh nitawezaje kumshawishi Jane aje nyumbani wakati jana nilimtimua?”
Yule mganga akatoa jani dogo kisha akampa Sophia na kumwambia,
“Chukua jani hili, ukiwa unaenda huko alipo Jane litafune halafu ukifika zungumza nae aje nyumbani hawezi kukataa hata kidogo maana jani hili huwa linawavuta wachawi, halafu akija unafanya hiyo dawa kisha mchezo unaisha”
Sophia akachukua lile jani na kuona sasa kazi itakuwa rahisi sana katika kumshawishi Jane ili akampatie dawa ya kummaliza kabisa.
Kisha wakaweka pesa na kuondoka kwenye kile kijumba cha mganga, kwakweli Sophia alifurahi sana na kujikuta akipanga mipango ya kummaliza Jane wakati mumewe hayupo.
“Yani dada nitahakikisha kesho naikamilisha hii kazi ila sitaki Ibra agundue maana anavyojifanya anahuruma na Yule binti balaa tupu”
“Ibra nae ndiomana mwisho wa siku yanamtokea puani jamani maana anatetea hadi maradhi mmh!”
“Ila dada inamaana atafia nyumbani kwangu?”
“Mi nadhani akishakunywa tu mtimue arudi kwao maana nahisi atakaa kaa hata dakika tano ndio afe kwahiyo wewe mtimue arudi kwao.”
“Basi nitafanya hivyo dada yani simpendi Yule binti balaa, amenifika hapaa kwakweli simpendi jamani dah”
“Unahaki ya kutokumpenda kwakweli maana hakuna mtu nayewapenda wachawi kwa maisha yao ukizingatia wanatutesa sana”
Safari yao sasa ilikuwa ni kurudi nyumbani kwa Siwema ambapo Sophia aliona ni vyema akamsubirie mumewe huko.
Leo Ibra aliwahi kutoka kwenye shughuli zake ila alipoenda kwa Siwema ili akamchukue mkewe hakuwakuta wote wawili na kufanya aondoke tena ili akazunguke zunguke kidogo huku akipanga kurudi tena badae.
Ila akapata wazo la kwenda kumuangalia Jane nae anaendeleaje maana hakujua hali yake tangu ile jana walipomuacha pale kwao, moja kwa moja Ibra akaelekea nyumbani kwakina Jane na ikawa vyema kwani alimkuta Jane akiwa nje amepumzika tu.
Ibra alienda pale alipo Jane na kumsalimia kisha kumpa pole kwa kilichotokea na kuanza kumuuliza kuwa anaendeleaje.
“Vipi hali yako lakini Jane”
“Niko safi tu, naendelea vizuri”
“Vipi lakini dawa unatumia?”
“Ndio natumia dawa vizuri tu”
“Pole sana yani kwakweli jana dah hata mimi sielewi elewi vizuri kwakweli, kwani ulipofika nyumbani jana ilikuwaje hadi ukaingia ndani?”
“Mimi nilivyofika jana nilikuta geti likowazi nikaingia na kulirudishia kidogo kwani nilijua dada amesahau kufunga kama kawaida yake ya kusahau. Nilipofika mlangoni nikagonga ila sikufunguliwa, nikajaribu kufungua mlango nikakuta uko wazi na kufanya niingie ndani ila nilimuita dada bila ya kuitikiwa ila kwa haraka haraka nikahisi labda dada ameenda sokoni na kusahau kufunga milango kwahiyo nikakaa kumsubiri. Ila sielewi ilikuwaje maana nilipatwa na usingizi mzito sana hadi nyie ndio mmenishtua halafu nilikuwa na maruwe ruwe ya usingizi na kuhisi labda pamevamiwa ndiomana nikaanza kupiga kelele za mwizi”
Maelezo haya ya Jane yalimfanya Ibra awe na mawazo kiasi kwani hakuelewa kuwa ilikuwaje Jane akute mlango wao uko wazi wakati walifunga.
“Kwanza kabisa Jane usitufikirie vibaya maana asubuhi tulivyoondoka milango ilifungwa kabisa na mke wangu ndiomana tuliporudi jioni alipatwa na mshangao sana kuwa wewe umeingiaje ndani”
“Sasa kama milango ,mlifunga unafikiri mimi ningeingiaje ndani? Inawezekana mkeo alisahau kama kawaida yake na kufikiri kuwa alifunga”
Ikabidi Ibra ajivunge hapo hapo kwani alijua wazi aking’ang’ania kauli yake ya kusema milango walifunga wakati huyu Jane kasema alikuta wazi atakuwa fika anamkandamiza huyu Jane kwa kumuhisi vibaya.
“Kweli bhana Jane, inawezekana kabisa ni mke wangu aliyesahau kufunga na kudai kuwa alifunga maana mke wangu ni msahaulifu sana ila tafadhali naomba unisamehe mimi Jane”
“Nimekusamehe ila kwa stahili hii nahisi siku moja nitatolewa roho na mke wako kwa matatizo yake ya kusahau. Mi nadhani ni vyema kama nisije kwenu tena”
“Hapana Jane, wewe ndio faraja ya mke wangu ila hujui tu. Tafadhali usitufanyie hivyo.”
Ibra akajaribu kumbembeleza Jane ili asijione vibaya kuwa anchukiwa na mkewe kwani bila kufanya hivyo alijua ni rahisi sana kwa Jane kugundua kuwa Sophia ana chuki za wazi sana juu yake. Kisha Ibra akaaga na kuondoka zake kuelekea kwa Siwema sasa.
Alipofika kwa Siwema aliwakuta nao ndio wamerudi muda huo huo ila hakutaka kupoteza sana muda na kumuomba mkewe kuwa warejee nyumbani ambapo walienda kupanda gari yao kisha safari ya kurudi kwao ikaanza, njiani Sophia alimuuliza mumewe
“Vipi leo hatununui chips?”
“Kwahiyo una hamu na chips?”
“Ndio au unahisi zitayeyuka kama jana?”
“Aaah achana na habari za jana Sophy, ngoja tununue”
Ibra akasimamisha gari na kununua hizo chips kisha safari yao kuendelea.
Walipofika nyumbani tu, kitu cha kwanza Sophia alichukua sahani na kuweka zile chips na kumuomba mumewe kuwa wale huku akimwambia,
“Si unaona leo hazijayeyuka”
“Unamaanisha nini Sophy?”
“Jana tulinunua tukiwa tumeambatana na mtu mbaya mume wangu”
“Aah Sophy jamani wale ni majirani zetu tena yatupasa tuwaombe msamaha”
“Labda nitamuomba msamaha huyo Jane siku akiwa kaburini”
“Sophy usiongee maneno hayo mke wangu”
Waliendelea kula na walipomaliza tu, Ibra alimuuliza mkewe kuhusu alipoenda na Siwema,
“Tulienda kutembea tu, kupunga upepo na kubadilisha mazingira”
“Mmh ila Sophy usipende sana kumuamini Siwema maana Yule ni mswahili sana”
Sophia akatabasamu tu kwani aliona mumewe kamavile anampigia mbuzi gitaa tu, wakaenda kukaa sebleni huku wakitazama luninga ila mara kidogo tu ile Tv ikazimika na kufanya washtuke kwani ilikuwa kama mtu kaizima hivi, Sophia akamuuliza mumewe kwa mshangao
“Ni nini hiki?”
Ibra nae akashangaa tu, ila ile Tv ikawaka tena na kuwafanya washtuke zaidi. Kwakweli kitendo hiki kilimfanya Ibra anyanyuke na kuizima ile Tv huku akimuomba mkewe waende chumbani tu.
Sophia akamuuliza mumewe,
“Kwani unaelewa hapo ni nini tatizo?”
“Sijui ila nahisi inataka kuharibika, nitamleta fundi aiangalie kuwa tatizo ni nini ila twende chumbani tu tukajiandae kulala”
Walienda chumbani na kuoga kisha kulala.
Kulipokucha kama kawaida Ibra alijiandaa na kwenda kwenye shughuli zake, kisha Sophia nae akaamka na kujiandaa kisha akelekea kwakina Jane kwani alishajipanga kutimiza anachokitaka kwa siku hiyo.
Kama alivyoambiwa na Yule mganga yani alipokaribia tu kwakina Jane akatafuna kile kijani kisha akafika na kumuulizia Jane ambapo walienda kumuitia, Jane alitoka na kushangaa aliyemfata pale kwao kisha akamsikiliza lengo lake ambapo Sophia alimwambia kuwa anamuomba nyumbani kwake. Jane alitaka kukataa ila akakumbuka maneno ya Ibra kuwa yeye ndio faraja ya huyu Sophy mke wa Ibra kwahiyo Jane akakubali na kumwambia kuwa akioga tu ataenda.
Akaagana nae pale, kisha Sophia akawa anarudi nyumbani kwake huku akifurahia kuhusu Yule mganga kuwa ni kiboko kwani hakutegemea kama Jane angekubsali kirahisi namna ile.
Sophia alipofika tu kwake, akachukua ile dawa na kuinyunyuzia mlangoni kisha akaenda jikoni na kuweka juisi kwenye glasi kisha kuweka na ile dawa ili Jane akija tu ampe juisi hiyo.
Muda kidogo Jane nae aliwasili ambapo cha kwanza kabisa alipofika mlangoni alishangaa kuona kama unga unga na kumuuliza Sophia,
“Dada ni nini hiki mlangoni?”
“Wewe pita tu kuna vitu vilianguka”
KwakweliSophia hakupendezwa kabisa na hili swali la Jane kwani alizidi kujidhihirisha kuwa ni mchawi, Jane aliingia ndani na kukaa pale sebleni kisha Sophia akaenda jikoni kumletea ile juisi.
Wakati Sophia akitoka jikoni na ile juisi akamshangaa Jane akiwa ametulia kabisa akiangalia Tv ambayo yeye hakuiwasha kwavile alikuwa akimsubiri fundi atakayeletwa na mumewe, kwahiyo Sophia alimuuliza Jane kwa mshangao,
“Kwanini umeiwasha hiyo Tv Jane ni mbovu”
“Sijaiwasha dada, nimeshangaa imewaka tu”
Sophia alimuangalia Jane kwa jazba sana tena kwa mshangao mkubwa.
Itaendelea kama kawaida……………………..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau
NYUMBA YA MAAJABU: 11
Muda kidogo Jane nae aliwasili ambapo cha kwanza kabisa alipofika mlangoni alishangaa kuona kama unga unga na kumuuliza Sophia,
“Dada ni nini hiki mlangoni?”
“Wewe pita tu kuna vitu vilianguka”
KwakweliSophia hakupendezwa kabisa na hili swali la Jane kwani alizidi kujidhihirisha kuwa ni mchawi, Jane aliingia ndani na kukaa pale sebleni kisha Sophia akaenda jikoni kumletea ile juisi.
Wakati Sophia akitoka jikoni na ile juisi akamshangaa Jane akiwa ametulia kabisa akiangalia Tv ambayo yeye hakuiwasha kwavile alikuwa akimsubiri fundi atakayeletwa na mumewe, kwahiyo Sophia alimuuliza Jane kwa mshangao,
“Kwanini umeiwasha hiyo Tv Jane ni mbovu”
“Sijaiwasha dada, nimeshangaa imewaka tu”
Sophia alimuangalia Jane kwa jazba sana tena kwa mshangao mkubwa sana kwani aliona akimtungia maneno tu muda ule, akamuuliza tena
“Inamaana imejiwasha?”
“Mi sijui, nilihisi labda umeme ulikatika na ukasahau kuizima sasa ndio umerudi na kuwaka moja kwa moja”
“Haiwezekani yani ni haiwezekani kabisa, hata hivyo karibu juisi”
Sophia akampatia Jane ile glasi ya juisi, ambapo Jane nae aliipokea na kushukuru.
Sophia alikaa kwenye kochi huku akimsubiria Jane anywe ile juisi ila Jane alikuwa kimya kidogo huku kaishikilia ile juisi na kumfanya Sophia amuulize,
“Mbona hunywi sasa!”
“Nakunywa dada, nilikuwa naiombea kidogo”
“Kheee inamaana huniamini?”
“Hapana dada, nakuamini sana tu ila mama jana alinifundisha vitu vingi sana na ndiomana saivi nataka kuanza tena kumrudia Mungu”
“Kwahiyo amekufundisha kutokuamini watu na kuombea kila wanachokupa?”
“Usinifikirie vibaya dada ila jana kuna makala nilisoma ilinifundisha vitu vingi sana ndipo nilipomuuliza mama nae akanielezea mambo mengi, tunatakiwa kukabidhi kwa Mungu kila kitu tunachofanya. Kama ile juzi ningemuomba Mungu aniongoze basi yasingenitokea yote yale yaliyonitokea ila kwavile nilitumia akili zangu za kibinadamu ndiomana ikawa vile. Natakiwa kukabidhi kwa Mungu kitu chochote kile hata nilichokitengeneza mwenyewe”
Kisha Jane akanywa kidogo ile juisi ila alishusha glasi na kutoka nje na kuitema, kwakweli Sophia alimshangaa sana hata gadhabu yake ikazidi maradufu na kumfuata nje na kumuuliza kwa ukali,
“Yani unatema juisi niliyokupa! Kama ulikuwa hutaki si ungesema tu kwani ningekulazimisha jamani?”
“Dada jamani hebu shika na wewe uionje, hii juisi ni chungu wala sijaitema kwa kutaka”
Sophia alichukua ile juisi ila alishindwa kuionja kwavile alijua wazi kitu ambacho ameweka kwenye ile juisi, kisha akarudi sebleni na ile glasi ya juisi ambapo Jane nae alirudi pale sebleni ambapo ile Tv iliendelea kuonyesha kama kawaida.
Walipokuwa wamekaa Sophia akamuangalia tena Jane na kumuuliza,
“Inamaana hii juisi kweli ni chungu?”
“Hata wewe ionje dada ni chungu kweli labda ni kikombe”
“Toka lini juisi ya embe ikawa chungu?”
“Mi sijui dada ndiomana nimesema labda ni kikombe”
“Mmmh una mambo yako tu wewe na hata sio kwamba juisi ni chungu”
“Kama unabisha dada ionje na wewe uhakikishe nisemayo”
“Nionje ili nife!”
Jane akamshangaa sana Sophia maana juisi kaileta mwenyewe halafu yeye huyohuyo anakataa kuionja, moja kwa moja Jane akahisi kuna uwalakini kwenye ile juisi na kisha akamuuliza Sophia,
“Kwani dada umeweka nini kwenye hiyo juisi?”
“Unahisi nimeweka nini?”
“Mi sijui maana uliyetengeneza ni wewe”
“Sijaweka chochote”
“Basi labda maembe uliyotengenezea yalikuwa mabovu”
“Unayajua maembe mabovu wewe au unaongea tu”
“Dada usipaniki tafadhali”
Mara Tv ikajizima tena na kufanya watazamane ambapo moja kwa moja Jane alihisi kuwa umeme umekatika,
“Mmmh umeme umekatika nini?”
“Umeme ungekatika friji lingeendelea kuunguruma?”
“Khee dada mbona unaongea kwa hasira hivyo jamani! Mi nimeuliza tu”
“Si nilishakwambia kuwa hii Tv ni mbovu sasa maswali gani unauliza hayo”
“Basi yaishe dada”
Mara mlango ukagongwa na aliyeingia alikuwa ni Ibra, ila alishangaa uwepo wa Jane mahali pale kuwa imekuwaje kuwaje hata ikawa rahisi sana kwake kusahau kilichotokea juzi. Ila alimkaribisha vizuri tu,
“Oooh Jane nafurahi sana kukuona upo hapa na mke wangu, kwakweli karibu sana”
“Asante ila mimi ndio napaswa kukukaribisha wewe sababu ndio umenikuta”
“Ni kweli nimekukuta ila hapa ni kwangu na nina haki ya kukukaribisha”
Ibra akakaa kwenye kiti ila macho yake yalienda mezani moja kwa moja ambapo aliona glasi ya juisi, ila alishangaa kitu na kuuliza kwa mshangao,
“Kheee hii juisi nyekundi ni juisi gani?”
Sophia na Jane kwa pamoja walijikuta wakiiangalia ile juisi ambapo Jane nae aliuliza kwa mshangao,
“Mmh hii juisi si ilikuwa na rangi ya njano hapa, imekuwaje imebadilika?”
Sophia alizidi kushangaa tu bila kusema neon lolote kwani alihisi huenda ile dawa aliyoweka kwenye ile juisi ndio imeibadilisha baada ya kukaa kwa muda.
Ibra akachukua ile glasi ya juisi na kuiangalia kwa karibu ila alishtuka sana kuona kama vitu vikicheza cheza ndani ya glasi ile, ambapo aliiacha chini na kumwambia Sophia,
“Hebu angalia ndani ya hiyo glasi, hivi ni juisi kweli hiyo?”
Jane akadakia kujibu,
“Ndio ilikuwa ni juisi sema ilikuwa chungu”
Kisha na yeye Jane akachukua ile glasi kuangalia ila alichokiona kilimshtua zaidi na kumfanya aiachie ile glasi ambapo ilianguka chini na kupasuka, ila kilichotapakaa baada ya ile glasi kupasuka kiliwashtua wote kwani ilikuwa kama damu ya mtu imemwagika.
Ibra alikuwa wa kwanza kuuliza,
“Ni mambo gani haya jamani?”
Huku akiamini kuwa huenda maneno ya mke wake kuwa Jane ni mchawi ni ya kweli, alimuangalia Jsne na kumuuliza,
“Ni wewe uliyetengeneza hii juisi?”
“Hapana, mi mwenyewe nililetewa na dada ili ninywe”
Ibra akamuangalia kwa makini mkewe ila Sophia hakuweza kusema chochote kwani alikuwa akitetemeka tu na ukizingatia alikuwa anajua kinachoendelea, Ibra aliamua kumuuliza mkewe sasa
“Unaweza kuniambia hii juisi imekuwaje?”
“Sijui imekuwaje ila nitakueleza ninavyojua mimi ila naomba Jane aondoke na tuongee kifamilia”
Jane hata hakutaka kuangaliwa na kuambiwa ondoka kwani pale pale aliaga na kuondoka zake.
Ndani ya nyumba alibaki Sophia na mumewe Ibra sasa ambapo Ibra alihisi kuna kitu mkewe anakijua na kumfanya amkazanie ili amueleze kuwa ilikuwaje,
“Naomba unisamehe mme wangu, nimefanya yote haya ili kuiokoa familia yetu”
“Kuiokoa familia yetu kivipi?”
“Kwanza niahidi kuwa utanisamehe”
“Sasa Sophy nisipokusamehe wewe nitamsamehe nani? Wewe ndio mke wangu, mama wa watoto wangu na hapo ulipo umebeba mwanetu tumboni mwako hivi naanzaje kutokukusamehe kwa mfano”
“Ngoja nikueleze basi ilivyokuwa”
“Wewe nieleze tu hata usiwe na wasiwasi”
Ikabidi Sophia amueleze Ibra mlolongo mzima wa yeye na Siwema kwenda kwa mganga wa kienyeji hadi yeye kupatiwa dawa ya kumdhuru Jane ambapo ndio aliiweka kwenye hiyo juisi.
“Mmmh kama ndio hivyo basi hiyo dawa ni kiboko mke wangu, ila siku nyingine usirudie tafadhali. Kwanza nikuulize una ushahidi gani kuwa Jane ni mchawi?”
“Mume wangu ni kutokana na mambo yanayotokea humu ndani, na mganga kasema kuwa yote yanasababishwa na huyo Jane”
“Najua wewe habari za waganga huzijui vizuri mke wangu ila kwavile umeamua kujihusisha nao basi utazijua mwanzo mwisho, ila siklu nyingine usijaribu hiki kitu. Hivi mfano Jane angekufa humu ndani tungempelekaje kwao mke wangu? Tena ushukuru Mungu huyo Jane ana imani zake na Mungu wake maana angekunywa tu hiyo juisi iliyogeuka kuwa damu basi kungekuwa na habari nyingine muda huu. Tafadhali mke wangu kuwa makini sana, Siwema atakupoteza wewe”
Kisha Ibra akaenda kuchukua tambara ili kuweza kufuta pale chini ila alikuta ile damu imeganda kamavile iliwekwa kwenye barafu kwahiyo alifanya kazi ya kuigandua na kwenda kuitupa nje kisha akapasafisha kabisa pale na kutulia huku akimuangalia mkewe ambaye alikuwa kimya tu kwa muda huo. Ibra aliamua kumuuliza tena,
“Je hiyo dawa bado unayo?”
“Hapana, niliitoa yote kama nilivyoelekezwa na Yule mganga”
“Ninachokuomba mke wangu usije ukarudia tena tafadhali, saivi kuwa makini na hiyo mimba. Kwanza vipi kuhusu kuanza kliniki?”
“Nitaanza tu mume wangu hata usijali”
“Basi ukiona imefika kipindi muafaka cha kuanza useme ili niwe nakupeleka”
“Sawa hakuna tatizo”
Wakati wakiendelea kuongea, mara kidogo Tv ikajiwasha kama kawaida na kumfanya Ibra ashtuke na kumuuliza mkewe kwa mshangao,
“Si nilisema hii Tv isiwashwe jamani Sophy na jana nikaizima hadi kwenye soketi imekuwaje tena?”
“Huyo Jane wako unayemtetea ndio aliyeleta tena mauza uza ya hiyo Tv maana hata mimi nilimshangaa akajitetea kuwa imejiwasha”
Ibra akapata hasira na kuinuka kisha akaenda kuchomoa nyaya zote za Tv ili kusiwe na muunganiko wowote kati ya umeme na Tv kisha akamuomba mkewe kuwa waende chumbani.
Sophia akainuka huku akiambatana na mumewe na kuelekea pamoja chumbani, ila walipofika tu cha kwanza kabisa Ibra alimuuliza mkewe
“Eeeh leo tunakula nini”
“Hata sijui maana sijapika”
“Kwahiyo mawazo yako leo ilikuwa ni juu ya kumuangamiza Jane tu hata ukasahau lishe dah! Basi jiandae twende hotelini tukale”
Sophia alijiandaa kisha wakatoka pamoja na mumewe kuelekea hotelini kula.
Walifika hotelini na kuagiza chakula, kisha kilipoletwa walianza kula na kumaliza ambapo Ibra alifurahi kwakweli maana mkewe siku hizi alikuwa na matatizo kiasi kwahiyo alihisi labda atatapika au atakataa kula hapo hotelini, kisha akamuuliza Sophia,
“Vipi leo hujajisikia voibaya mke wangu maana umeweza kula hapa hotelini hadi nimeshangaa”
“Kwasababu tumebadilisha hoteli ndiomana nimeweza kula, lile li hoteli lako silitaki kabiosa”
“Ila si nilishasema kuwa ile hoteli hatutaenda tena kutokana nay ale wanayotutegeshea njiani, kwakweli hata mimi ile hoteli siitaki tena na kama nilivyoahidi haitokuja kutokea tena niende kwenye ile hoteli”
“Hapo sawa mume wangu maana hoteli zingine zimekaa kiushirikina tu”
“Vipi tubebe chakula kingine twende nacho nyumbani?”
“Mmh hapana jamani maana kama mimi hapa nimeshiba balaa, kesho nitapika tu”
“Basi turudi nyumbani sasa”
“Labda tununue juisi maana si unajua hata usiku haujaanza kuingia vizuri”
“Lakini si ulitengeneza juisi wewe mpaka ukampa Jane!”
“Aaah achana na ile juisi bhana, kwanza tukirudi naimwaga yote”
Ibra akacheka tu kisha wakamuita muhudumu na kumuagiza juisi ya boksi na alipoleta walibeba na kuelekea kwenye gari yao kwa lengo la kurudi nyumbani.
Wakiwa njiani ndani ya gari, wakakatisha kwenye moja ya kituo cha daladala ila gafla wakasikia sauti ikiita kwa nguvu jina la Sophia na moja kwa moja wakahisi kuwa huenda kuna mtu kwenye kituo cha daladala anayemfahamu Sophia kwahiyo Ibra akasimamisha gari yao ili kumuangalia mtu huyo. Ila gafla mlango wa nyuma wa gari yao ukafunguliwa na akaingia mtu, ambapo kwa pamoja waligeuka na kumuangalia mtu huyo, wakamuona ni Yule mtoto ambaye huwa wanamkuta njiani akiwafanyia vituko cha kwanza walishangaa sana.
Kwakweli Ibra alipatwa na hasira ya gafla kisha akashuka kwenye gari na kwenda ule mlango wa nyuma na kuufungua ambapo alimtoa mtoto huyo kwa ghadhabu kubwa sana kisha akamrusha nje ila Yule mtoto hakuanguka wala nini kanakwamba Ibra alimuondoa na kwenda kumsimamisha ila bado Ibra hakushangazwa na lile swala bali alirudi kwenye gari na kuondoa gari yao kwenye lile eneo huku akiwa amechukia sana kwani chanzo cha wao kubadilisha hoteli na njia ni huyo huyo mtoto.
Walipofika nyumbani, kabla hata ya kushuka kwenye gari ili afungue geti, wakaona kitu kama nyoka kikimalizikia kuingia ndani kwao kwa kupitia chini ya geti ila waliona mkia tu ambapo Sophia ndio alikuwa wa kwanza klushtuka na kumwambia mumewe,
“Mmh sio nyoka Yule?”
“Hata mimi nimeona kama nyoka vile”
“Duh mbona makubwa!”
Ikabidi washuke wote na kuingia kwa tahadhari ili kama ni nyoka basi wajue cha kufanya kabla ya kuingiza gari ndani, ila walipoingia tu getini waliona nyoka mkubwa akiwa amejiviringisha pembezoni mwa mlango wao wa kuingia ndani kanakwamba anawasubiria kuwa waingie nae.
Itaendelea kama kawaida………………………!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 12
Ikabidi washuke wote na kuingia kwa tahadhari ili kama ni nyoka basi wajue cha kufanya kabla ya kuingiza gari ndani, ila walipoingia tu getini waliona nyoka mkubwa akiwa amejiviringisha pembezoni mwa mlango wao wa kuingia ndani kanakwamba anawasubiria kuwa waingie nae.
Kwakweli hapakuwa na mwenye ujasiri kati yao wa kuweza kuendelea mbele, Ibra alimuangalia mkewe na kumuuliza,
“Tutafanyaje sasa?”
“Wewe ni mwanaume unatakiwa ujue cha kufanya”
“Yani uanaume kwa joka lote lile, mbona hunitakii mema mke wangu!”
“Sasa tutafanyaje?”
“Nadhani tuondoke tukatafute hoteli ya kulala kwa leo, lile joka tushughulike nalo kesho maana giza nalo hilo limeshaingia, hakuna namna hapa. Tutampata nani muda huu wa kutusaidia kulimaliza joka kubwa vile?”
Ikabidi wakubaliane kufanya hivyo maana haikuwa kitu rahisi kwa wao kupambana na lile joka, na kwa jinsi giza lilivyoingia haikuwa rahisi kusema utatafuta watu ili waweze kulimaliza joka lile.
Wakarudi nje na kupanda kwenye gari yao kisha kuondoka na kuelekea hoteli nyingine ya karibu ili kuangalia ustaarabu wa kupata chumba na kulala, kwa bahati nzuri walipata chumba kwenye hoteli ambayo walienda kwa muda huo.
Ila mpaka wanaingia ndani kila mmoja alikuwa na mawazo yake kuhusu lile joka waliloliacha nje ya nyumba yao, Sophia alimuuliza mumewe,
“Hivi joka kubwa kama lile linaweza kutokea wapi mjini hapa?”
“Kwakweli hata mimi sielewi Sophy maana sio hali ya kawaida kabisa ile, tena mjini hapa jamani kukutana na nyoka kama Yule mmmh!”
“Mi nahisi ametumwa Yule mume wangu”
“Inawezekana kabisa unayoyasema maaana si kitu rahisi kwa mjini hapa kukutana na nyoka mkubwa kiasi kile”
“Sasa unahisi tufanyeje?”
“Kwakweli hata sijui, nahisi kuchanganyikiwa tu”
“Mmmh mi nahisi kesho twende kwa da Siwema atupeleke kwa yule mganga ili aweze kutusaidia kwa hili, yani Yule nyoka ni wa kutumwa kabisa kabisa si jambo la kawaida mume wangu”
“Unafikiri nitabisha? Hata siwezi kubisha mke wangu, yani sibishi chochote kwakweli katika maisha yangu sijawahi kuona nyoka mkubwa kama Yule zaidi ya kuona kwenye sinema tu. Kwakweli haya ni makubwa, na kama ni uchawi basi ni uchawi wa wazi wazi kabisa yani”
Sophia alilidhika na kauli ya mumewe ya kukubali kwenda kwa mganga ili pia aweze kuwaeleza zaidi kuhusu Jane kwani alipenda mumewe nae aelewe kwa kina ubaya wa Jane anayemtetea kila siku.
Ibra aliona ni vyema wakapumzisha mawazo hivyobasi akamuomba mkewe walale tu ili kesho yake waamkie huko kwa Siwema, Ibra alimsogelea mkewe pale kitandani na kumkumbatia ili wapate kulala kwa pamoja. Na haikuchukua muda wote wawili wakajikuta wakipitiwa na usingizi.
Sophia alianza kupatwa na ndoto ambapo katika ndoto hiyo aliona lile tukio ambalo liliwapata wakati wakitoka hotelini kula ambapo aliona tukio zima la Yule mtoto alivyopanda kwenye gari yao na jinsi Ibra alivyomshusha kwa ghadhabu, ila kwenye hii ndotro alimuona huyu mtoto akiwaambia kuwa,
“Nitawakomesha”
Sophia alijikuta akishtuka kutoka usingizini huku jasho jingi likimtoka ambapo Ibra nae alishtuka huku akimshangaa mkewe na kumuuliza kuwa imekuwaje tena,
“Ndoto mume wangu”
“Ndoto! Ndoto gani?”
Gaf;la wakasikia mtu akiita jina la Sophia kwa nguvu toka nje ya hoteli hiyo ambapo Sophia alitaka kuitika ila Ibra alimziba mdomo na kumkataza.
“Usipende kuitika unapoitwa usiku, je unajua anayekuita ni nani na ana lengo gani na wewe?”
Sophia akahema kwa nguvu sana na kumuuliza mumewe,
“Hivi kwanza kuna mtu anayenifahamu huku?”
“Ndio ushangae sasa, hakuna anayekufahamu je utakuwa unamuitikia nani? Hata kama ukiwa mahali kwa watu wanaokufahamu tafadhali mke wangu usipende kuitika usiku, yani wewe chukulia kwamba anayeitwa sio Sophia wewe, chukulia kwamba kuna Sophia wengi sana ulimwenguni huenda kuna mmoja ndiye anayeitwa lakini sio wewe.Usiitike kabisa mke wangu”
Ile sauti ya kumuita Sophia nayo ilikazana na kumfanya Sophia kuingiwa na uoga ila mumewe alijaribu kuongea nae na kujitahidi kumtoa ile hali ya uoga ili awe katika hali ya kawaida kabisa na ahisi kuwa anayeitwa sio yeye.
Sauti ile iliita na kuita ila mwishowe ikafifia kabisa na kuwa kimya ila bado Sophia hakulala na kumfanya Ibra nae asiweze kulala kwani alikuwa akimpa maneno ya kumfanya mkewe asijisikie vibaya hata kidogo.
Kwavile hawakuwa na usingizi, ikabidi Ibra amuulize Sophia kuhusu kile alichokiota ambapo Sophia alimueleza lile tukio aliloliota na jinsi mwishoni alivyoambiwa na Yule mtoto, kidogo Ibra akapata wazo jipya na kumwambia Sophia,
“Unaona sasa, unakumbuka ule mchana ilikuwa sauti kama ile tuliyosikia ikikuita na tuliposimamisha gari ndio akapanda yule mtoto wa maajabu halafu saizi unaota tena na sauti inaanza kukuita tena, je huwezi kuona kuwa matukio yanawiana hayo!”
“Mmh halafu kweli mume wangu, bora umenikataza kuitika”
“Ndio hivyo, nadhani alitaka uitike ili awe na uhakika na chumba tulicholala. Ondoa mashaka mke wangu, tulale kwa amani sasa maana hawajui tumelala chumba kipi”
“Kwahiyo kama ni watu wabaya basi wamechemka”
“Tena wamechemka haswaaa”
Ibra akamkumbatia mkewe kisha wakaanza kuutafuta usingii na hatimaye wakalala tena.
Kulipokucha, waliamka mapema sana na kwenda kuoga ili kujiandaa kutoka pale hotelini, ambapo walitumia muda mfupi tu kujiandaa kwani hawakuwa na mengi ya kufanya.
Wakati wanatoka pale hotelini walishangaa kuna mahali watu wengi sana wamejaa na kufanya washuke kwenye gari yao na kwenda kushuhudia kuwa ni kitu gani kimetokea, waliposogea walishangaa kumuona binti mmoja pale chini akiwa ameuwawa kikatili sana ila muda mfupi tu walifika maaskari ambao ilionyesha walipewa taarifa kuhusu Yule mtu aliyeuwawa mbapo walimfunika na kumpakiza kwenye gari yao na kuondoka na baadhi ya watu kwa maelezo zaidi.
Ibra alikuwa akishangaa sana na kufanya nae aulize kwa kina kama sehemu hiyo huwa kuna matukio yoyote ya ajabu,
“Eti kaka, kwani hapa huwa kuna matukio ya hivi?”
“Kwakweli kaka haijawahi kutokea yani ndio mara ya kwanza na kila mmoja anashangaa maana hatujawahi kupatwa na matukio ya hivi halafu ubaya zaidi ni kuwa haijulikani ameuliwa na kitu gani”
“Mmh ndugu zake wamepatikana?”
“Kwakweli ilikuwa ngumu kumtambua ila kuna binti mwingine alipita hapa na ameweza kumtambua, hivyo amekimbia kwao kuwaita ndugu zake nadhani wakifika hapa itabidi waelekee moja kwa moja polisi au hospitali maana polisi wamewawahi kufika”
Muda kidogo walifika watu kama wamechanganyikiwa kabisa huku wakitaka kuonyeshwa huyo marehemu ambapo watu waliwapa maelekezo juu ya polisi waliofika na kuchukua ule mwili wa marehemu, kati ya wale watu alisikika mama mmoja akilia sana huku akionge,
“Mungu wangu jamani, naomba unisaidie asiwe binti yangu kweli jamani, yani Sophia wangu mimi hapana haiwezekani kabisa”
Wengine walimuita dereva wa bajaji aliyewapakiza wale na kuelekea nao kwenye kituo cha polisi ili waweze kuwahi kumuona huyo marehemu kabla hajapelekwa monchwari.
Sophia alimuangalia mumewe na kumuomba kuwa waondoke eneo lile kwani tayari alihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia kuwa Yule binti aliyeuwawa aliitwa Sophia pia, Ibra alimsikiliza mkewe na kisha wakaelekea kwenye gari ambapo moja kwa moja safari yao ilikuwa ni kwenda kwa Siwema na hakuna aliyeongea kwa muda huo.
Walipofika nyumbani kwa Siwema walimkuta akijiandaa kwaajili ya majukumu yake mengine, hata na yeye alishangaa ujio wao ila kwa haraka haraka akahisi kuwa huenda Yule binti ameshakufa kwahiyo ndio wamekuja kumpa habari, kwahiyo aliacha alichokuwa anafanya na kwa shauku kubwa alitulia kuwasikiliza kilichowapeleka mahali pale.
Sophia hakutaka kupoteza muda na moja kwa moja akaanza kumueleza yaliyotokea nyumbani kwao mpaka kuwafanya wao kuamua kuja kwake ili awapeleke huko kwa huyo mganga.
“Kheee mbona makubwa jamani! Je nah ii asubuhi huyo joka mmemuacha hapo mlangoni?”
“Hata nyumbani hatujaenda tena, usiku tumelala hotelini kwakweli hali ni mbaya, twende tu kwa huyo babu akatusaidie jamani”
“Basi ngoja nijiandae fasta fasta twende jamani maana haya mambo ni makubwa sana”
Siwema akaingia ndani, muda kidogo akapita tena Yule bibi ambaye alimwambia Sophia kuwa nyumba yake ni ya maajabu ila huyu bibi hakuwasalimia wala nini zaidi ya kumsemesha Sophia kwa kumwambia,
“Una bahati sana, ushukuru mumeo ana upeo mkubwa”
Sophia akamshangaa huyu bibi na kumuuliza kwa jazba,
“Kivipi”
“Usiku ule ungeitika wakati unaitwa basi sidhani kama muda huu ungekuwa hapa, ingawa umemuingiza pabaya mtu ambaye hakustahili kabisa”
“Sikuelewi ujue”
“Ni ngumu kunielewa kwasababu huwa naongea ukweli mtupu, mnatakiwa muwe karibu sana na Mungu lasivyo ile nyumba itawashinda”
“Nyumba na kuitwa usiku vina uhusiano gani?”
Kabla huyu bibi hajajibu, Siwema alikuwa kashatoka ndani na hapo hapo akaanza kumfokea Yule bibi kwa kumfukuza.
“Hivi wewe bibi una mpango gani na familia yangu? Si nilishakwambia usipite hapa nyumbani kwangu tafadhali ondoka mchawi mkubwa wewe tena ukome kukatisha hapa”
Yule bibi aliondoka bila ya kuongea chochote za ziada ingawa alionekana kuondoka akiwa amenyong’onyea, ikabidi Ibra nae amuulize Siwema kwa ukaribu kuwa Yule bibi ni vipi
“Yani Yule bibi ni mchawi hakuna mfano nawaamnbia halafu huwa anajifanya kila kitu anakijua, Sophia nilikwambia lakini usipende kumsikiliza huyu bibi hata nashangaa unavyomsikiliza jamani. Haya twendeni tusije tukachelewa foleni huko kwa babu”
Ikabidi Ibra afungue gari na wakapanda wakielekea kwa mganga wa kienyeji sasa.
Walipofika kwa mganga kama kawaida walikuta foleni kubwa tu maana mahali hapo palikuwa hapakosi watu hata mara moja.
Ila waliamua kuvumilia kwenye foleni hadi pale ilipofika zamu yao na kuingia ambapo mganga alikuwa amekaa na matunguli yake ila alikuwa kimya kabisa mpaka pale wao walipoanza kumueleza ambapo Siwema alianza kwa kumuomba msamaha kwanza,
“Babu tusamehe, nadhani tumekosea masharti na yametupata makubwa. Nje ya nyumba kuna nyoka mkubwa amefanya tushindwe kuingia ndani”
Huyu babu alianza kuongea kwa jazba,
“Mnajua nyie ni wajinga sana, tena wajinga haswaa yani mlishindwa kujiuliza kuwa kwanini ile dawa iliganda? Na nani aliwatuma muende kuitupa nje?”
Sophia nae akaanza kujitetea,
“Tusamehe babu, kwakweli hatukujua cha kufanya. Tusamehe tafadhari, tunaomba msaada wako”
“Ile dawa ni kali sana, mara nyingi mimi huitoa kwa lengo la kummaliza mchawi kwamaana ile dawa mtu akiinywa hawezi kuepuka kifo hata afanye kitu gani. Ile dawa ilitakiwa inywewe na muhusika ambapo angeinywa tu angeona habari yake kwanza wadudu wa tumboni wote wangekuwa wakubwa maradufu na hao ndio wangemuua kisha kuanza kumtoka hovyo hovyo yani kila sehemu ya uwazi kwenye mwili wake ingetoa wadudu ambao wangekuwa wakubwa sana na hakuna ambaye angeweza kukaa karibu na mwili wa marehemu huyo kisha wangeenda kumzika mapema sana. Sasa nyie mmeitupa pale nje kwenu tena ikiwa imekauka vile, ubaya wa ile dawa ikikauka tu harufu yake huwavutia viumbe jamii ya nyoka. Pale kwenu palikuwa na nyoka mdogo ambaye amekunywa ile dawa na mwisho wa siku ndio kawa vile. Hata mkirudi tena kumuona mtakuta amekuwa mkubwa zaidi ya mwanzo na huwa ni vigumu sana kuwaua nyoka waliokula ile dawa kwani ukiwasogelea tu hukimbilia kukudhuru kwanza”
Ibra alihisi kuchoka kabisa kwa maelezo haya, kisha akamuuliza Yule mganga,
“Sasa tutafanyaje babu?”
“Hapo dawa ni moja tu, tunatakiwa tutoe kafara ya ng’ombe mzima”
“Ng’ombe mzima?”
“Ndio ng’ombe mzima tutamchinja kisha damu yake tutaiweka dawa ambapo huyo nyoka ataifata hiyo damu kisha atajifia mwenyewe halafu tutachinja kondoo na mbuzi kwa lengo la kumfanya huyo nyoka atoweke kabisa”
Ibra alijikuta akiwa na mawazo lukuki maana hakujiandaa kwa hayo maswaibu ya kununua ng’ombe mzima wa kafara kisha kondoo na mbuzi. Yule mganga akawasisitizia kabisa,
“Hiyo kazi inatakiwa ifanyike leo, yani leo maana kadri huyo nyoka atakavyozidi kukaa ndio itakavyokuwa ngumu kumtoa”
“Basi babu ngoja tulete pesa kwaajili ya kununua huyo ng’ombe, mbuzi na kondoo”
Kisha wakatoka nje ambapo Ibra alikuwa na mawazo tu muda wote, alichukua simu yake na kuwapigia rafiki zake akiwaomba wamkopeshe pesa maana aliona akiitoa kwenye biazshara yake atafanya iyumbe mapema sana.
Kwa bahati nzuri aliowapigia na kuwakopa walimtumia pesa bila hata kukawia na kufanya ashukuru sana ili akakamilishe hilo zoezi na waweze kurudi kwao.
Ila Ibra alijikuta akimlaumu sana mkewe na kumuona kuwa ni mwanamke mpumbavu maana yote hayo kayasababisha yeye kwa kutaka kummaliza Jane na mwisho wa siku wamejikuta wakiingia kwenye gharama zisizo na maana.
Walienda kumtaarifu mganga kuhusu upatikanaji wa fedha kisha vile vitu vikaenda kutafutwa ili kujiandaa kwa hiyo shughuli ya kumtoa Yule nyoka nyumbani kwa Ibra.
Walipofanikiwa kupata vitu vyote, kwanza kabisa Yule ng’ombe alichinjwa pale pale nyumbani kwa mganga ambapo mganga aliweka damu ya Yule ng’ombe kwenye chupa na kuiweka na dawa.
“Yani hapa nataka tukifika tu kitu cha kwanza iwe ni kuimwaga hii damu maana haitakuwa vyema kwenda kumchinja ng’ombe mbele ya Yule nyoka.”
Kisha mbuzi na kondoo nao wakachinjwa ambapo damu yao iliwekwa kwenye chupa moja na kuchanganywa.
“Sasa akisha kunywa hii ya ng’ombe, atakufa kisha tutammwagia hii ya kondoo na mbuzi ili atoweke.”
Kisha wakaenda kupanda kwenye gari, Ibra, mganga, msaidizi wa mganga, Siwema na Sophia. Safari ilikuwa ni kwenda nyumbani kwa Ibra.
Walipofika nyumbani kwa Ibra, walishuka wote kwani Ibra alisimamisha gari yake nje kisha wakasogelea geti na kufungua kwa tahadhari, cha kushangaza sasa pale ambapo walimuacha nyoka jana walimkuta Jane amekaa tena akiwa hana habari yoyote.
Itaendelea kama kawaida………………….!!!!!!!!!!!!!!
34
NYUMBA YA MAAJABU: 13
Walipofika nyumbani kwa Ibra, walishuka wote kwani Ibra alisimamisha gari yake nje kisha wakasogelea geti na kufungua kwa tahadhari, cha kushangaza sasa pale ambapo walimuacha nyoka jana walimkuta Jane amekaa tena akiwa hana habari yoyote.
Kila mmoja alikuwa na mshangao juu ya lile, ambapo Ibra alimuita Jane kwa uoga flani kuona kama ni mtu au ni lile joka limejigeuza kuwa ni mtu, Jane nae alipoitwa aliitika na kuinuka pale kisha akaanza kuwasogelea ambapo Sophia akamwambia Jane kwa ukali
“Tafadhali Jane usitusogelee ila tuambie umeingiaje humu ndani?”
“Kuingiaje kivipi? Mi nimekuja nikakuta geti liko wazi nikaingia”
“Nyoka yuko wapi?”
“Nyoka? Nyoka gani?”
“Unatuuliza sisi tena wakati palikuwa na nyoka hapo mlangoni”
“Sijaona nyoka kwakweli na nipo hapa kama saa moja iliyopita”
“Na ni nani aliyekwambia uje leo?”
“Sijaambiwa na mtu yeyote ila kuna vitu niliviota usiku ndiomana leo nikaja ili nikuulize”
Yule mganga nae aliwatazama Ibra na Sophia na kuwauliza kuwa Yule binti ni nani ambapo Sophia alimjibu kwa makini kabisa na kwa kujiamini,
“Huyo ndio Jane Yule mchawi maarufu”
Yule mganga akamtazama kwa makini Jane kisha akatikisa kichwa halafu akawageukia wakina Sophia na kuwaambia kuwa wamwambie Yule Jane aondoke kwani atawaharibia kazi ila Ibra akahamaki na kuuliza,
“Kazi gani sasa mganga wakati huyo nyoka hayupo tena”
“Nyoka hayupo tena? Unaweza kuangalia wewe kuwepo au kutokuwepo kwa nyoka?”
“Kama yupo yuko wapi sasa?”
Sophia akamuangalia mumewe kwa jazba na kumkazia macho kisha akamwambia,
“Ibra tafadhali acha kubishana na mtaalamu”
Kisha Sophia akamtazama Jane na kumwambia,
“Jane tunakuomba uondoke tafadhali”
Jane hakutaka kubishana nao na wala hakuongea lolote zaidi ya kutoka kwenye nyumba ile na kuondoka.
Sasa alibaki mganga na wakina Sophia ambapo Siwema nae akatia chumvi kuhusu Jane,
“Mmh halafu kale katoto kanaonekana ni kachawi haswaa yani haiwezekani kawe kanajiamini kiasi kile jamani”
“Umeona dada eeeh kale katoto sio ka kawaida kabisa”
Mganga akaanza kuongea kuwa inaonekana nyoka kuna mahali kajificha kwahiyo alitakiwa afanye jitihada za kumuita kwanza nyoka huyo ili amteketeze ila katika kumuita huyo nyoka alihitaji wachinje kuku wa kienyeji watatu ili apate nguvu ya kufanya hivyo.
Kwakweli Ibra alijiona akizidi kupoteza pesa kwa uzembe wa mke wake ila hakuwa na namna yoyote ya kufanya kwa muda huo. Ikabidi atoe pesa za hao kuku kisha Yule msaidizi wa mganga akaenda kuwanunua kuku hao.
Na baada ya muda kidogo Yule msaidizi alirudi na hao kuku watatu, kisha Yule mganga akawachinja wale kuku na kuanza kama kuita ila aliita na ukapita muda mrefu sana bila ya hilo joka kujitokeza wala nini tena haikuonyesha kama kulikuwa na dalili yoyote ya kuwepo nyoka katika eneo lile, ndipo Yule mganga alipowauliza tena jina la binti aliyetoka pale.
“Yule binti niliyesema aondoke anaitwa nani?”
“Yule anaitwa Jane”
“Jamani ngoja niwaambie ninachokiona”
Wote wakatulia kumsikilizia Yule mganga anachotaka kusema, kisha Yule mganga akaanza kuwaambia
“Nimekazana hapa kumuita Yule joka lakini hajatokea, mizimu yangu imenionyesha kitu ambacho kilikuwa kimeendelea mahali hapa. Swala ni kwamba Yule binti anaelewa kila kitu tulichokuja kukifanya hapa halafu yeye hataki tukifanye. Sasa jambo alilolifanya Yule binti ni kuondoka na lile joka kwa madai kwamba ataenda kulitumia kwenye shughuli zake. Ila nyie hata msihangaike nae, mimi nampa siku tatu tu za kuendelea kunusa harufu ya dunia hii. Kazi ya kummaliza sasa nitaifanya mimi mwenyewe baada ya kunisumbua hivi, nyie ngojeni baada ya siku tatu tu mtaitwa kwenye msiba wa huyo binti. Ngoja sisi tuondoke.”
Ibra akataka kuwapeleka ila waliomba kukodiwa usafiri wa kukodi ambapo ilimbidi Ibra afanye hivyo kisha Yule mganga na msaidizi wake wakaondoka.
Ibra akiwa pamoja na Sophia na Siwema wakafungua mlango wa ndani sasa na kuingia ndani ambapo walikaa sebleni huku wakimlaani Jane mwanzo mwisho, kwakweli Sophia alionekana wazi wazi akimchukia huyo Jane,
“Kwakweli naichukia ile siku ya kwanza kumfahamu yule mama Jane maana ndio kaniletea yote haya”
“Tena inaonyesha huyo mama ni mchawi kushinda mwanae maana haiwezekani mtoto awe mchawi halafu mama asiwe”
“Najuta kuwafahamu dada maana wamenieleleza balaa”
Ibra nae akachangia yak wake sasa,
“Mimi najuta kumfahamu huyo mganga wenu maana bila yeye hizi pesa zote ziizonitoka leo zisingenitoka”
Ikabidi Siwema atetee kuhusu hiyo mada,
“Usiseme hivyo shemeji, uhai ni bora kuliko mali”
Wakaongea ongea kisha Ibra akamuitia na huyo Siwema usafiri wa kukodi ambapo nae aliondoka kwa stahili hiyo.
Ndani walibaki wawili sasa huku Ibra akiwa na swala lake lile lile la kulaumu kuhusu mganga,
“Yani inamaanisha mganga ndio amekukera kiasi hicho mume wangu!”
“Amenikera sana, kiukweli Sophia zamani ulikuwa ni mwanamke mwenye akili sana na ulikuwa na uchungu na pesa zetu. Nakumbuka hukutaka kabisa tufanye mambo ya kijinga kwani muda wote ulikuwa ukiwaza maendeleo, sasa siku hizi umekumbwa na nini mke wangu? Hebu fikiria isingekuwa wewe kwenda kwa mganga kwa mara ya kwanza na kupewa ile dawa ya kumuangamiza Jane je yote haya yangetokea? Na je huyu mganga alikuwa na ulazima gani wa kuchinja Yule ng’ombe, mbuzi na kondoo nyumbani kwake halafu huku akaja na damu tu! Kwanini asingekuja kwanza eneo la tukio na kuona hali halisi ilivyo kisha ndio awachinje? Kwakweli mmeniingiza hasara sana ten asana hadi sina hamu na huyo mganga tena”
“Nisamehe mume wangu ila mimi nilifanya yote haya kwa lengo la kuikomboa familia yetu.”
“Hapa hata ulikuwa hukomboi ila ulikuwa unatudidimiza tuwe maskini tena. Yani siamini kabisa kama leo nimepoteza milioni moja na nusu kwa ujinga tu dah!”
“Pole mume wangu”
“Ngoja tusaidiane kupika tule tupumzike”
Kisha wakaenda jikoni na kuanza kuandaa chakula ambapo Ibra alipofungua friji aliona kuna nyama na kuchukua nyama hiyo na kuanza kuikatakata kisha kuibandika wakati huo Sophia alikuwa akishughulika na mchele ili waweze kupika kwa haraka.
Haikuchukua muda mrefu sana wakawa tayari wamemaliza kuandaa chakula na kwenda kukaa mezani kisha wakakaa na kuanza kula huku wakikisifia kile chakula kuwa kitamu sana kwani kilikuwa na ladha nzuri mdomoni na kilivutia kula tu.
“Yani siku hizi humu ndani tunapika chakula kuwashinda hata wa hotelini maana chakula chetu ni kitamu balaa”
“Basi tusiwe tunakula hotelini siku hizi maana mapishi yetu ni hoteli tosha”
“Kwani huu wali umeweka viungo mke wangu?”
“Wala, ni maji, mafuta na chumvi tu”
“Mmh unavyonukia na kunoga balaa”
“Kwakweli hata mimi nashangaa chakula kilivyokitamu dah”
Walikula huku wakisifia muda wote kisha walipomaliza Sophia alitoa vyombo na kwenda na mumewe chumbani kujimwagia kisha moja kwa moja kupumzika kwani walikuwa wamechoka sana na mizunguko ya siku hiyo ukizingatia ni tangu jana na lile varangati la nyoka.
Wakiwa wamelala Sophia alijiwa na ndoto na kuwa kamavile analiona tukio lote ambalo lilitokea usiku wa jana yake wakati wamelala hotelini, alijiona akiwa anaitwa na jinsi ambavyo mume wake alimkataza asiitike. Kisha akamuona binti njiani akionyesha kushtushwa na lile jina la Sophia lililokuwa likiitwa na moja kwa moja akaonyesha kuitika huku akielekea mahali ambapo anaitwa ila mbele kidogo akakiona kile kitoto ambacho huwa wanakutana nacho njiani ila kilionyesha kuwa na sura kama ya kiutu uzima na gafla alitoa vitu vya ajabu na kumwagia Yule dada ambaye alianguka chini.
Sophia alishtuka sana na kupiga kelele ambazo moja kwa moja zilimshtua mume wake pia na kumfanya aamke kutoka usingizini huku akiuliza kwa mshangao kuwa mkewe ameona kitu gani.
Sophia alikuwa akitetemeka sana kisha akaanza kumueleza mumewe kile ambacho alikuwa amekiona kwenye hiyo ndoto,
“Mmh hayo ni makubwa mke wangu kwakweli tunatakiwa kuwa makini maana hiyo hali ni mbaya, unajua nini kwakweli kale katoto huwa sina imani nacho kabisa yani, kale katoto nahisi ni jini”
Sophia akashtuka sana na kumuangalia mumewe, kisha akamuuliza kwa mshangao,
“Jini tena mume wangu jamani dah! Mbona unaniletea habari za kutisha?”
“Sio habari za kutisha ila ndio ukweli huo mke wangu maana haiwezekani tuwe tunakutana nae njiani tena katika mazingira ya kutatanisha kiasi kile. Ila usijali mke wangu maana swala hili lazima nitalitafutia ufumbuzi tu.”
Kwakweli ile habari ya jinni ilimkosesha raha Sophia ingawa hata pale mumewe alipomtaka warejee kulala alijilaza tu bila ya kujiwa na usingizi tena kwani alijikuta akiwa na mawazo sana huku akikumbuka stori za zamani kuwa majini yanakuwaga marefu sana yani huoni mwisho wao halafu chini yanakuwa na kwato za ng’ombe ila akawa anajiuliza kuwa mbona kale katoto ni kafupi sana je ni jamii gani ya jini, alikosa jibu kabisa huku usingizi wake nao ukiwa umekata kabisa.
Masaa yakapita akiwa macho tu kwa muda mrefu kitu kilichomfanya aboreke pale kitandani hivyo akaona vyema hata awahi kuamka zaidi ya siku zote. Ilipofika saa kumi na moja alfajiri aliona ni vyema aende kukaa sebleni tu kuona kama ataweza kusinzia labda na kuweza kulipiza usingizi wake wa usiku.
Akainuka pale kitandani na kwenda mpaka mlangoni ambapo alifungua mlango ila akasikia kama sauti ya Tv ikiongea sebleni kwakweli aliogopa sana ukizingatia mara ya mwisho mumewe alichomoa nyaya zote za kwenye Tv hiyo. Sophia akarudi chumbani kwa kasi ya uoga kwani hakutaka kushuhudia kile kitu, moja kwa moja akaenda kumuamsha Ibra aliyeonekana kuwa na usingizi mzito sana.
“Ibra Ibra tafadhali amka”
“Kwani vipi Sophia kuna nini jamani? Mi si nilisema leo siendi kazini, niache nipumzike”
“Najua kama huendi Ibra ila kuna kitu nataka ushuhudie”
“Kitu gani jamani?”
Ikabidi Ibra aamke na kumuangalia mkewe kisha kumuuliza tena kuwa ni kitu gani ambapo Sophia akamuomba Ibra moja kwa moja kwa muda huo aelekee sebleni ili akaone yeye mwenyewe, Ibra akainuka na kuelekea sebleni ila hakuona chochote ambapo Sophia nae alimfata nyuma. Kisha Ibra akamuuliza Sophia kuwa kulikuwa na kitu gani,
“Mbona hamna chochote kipya hapa sebleni! Ni kinini hiko ambacho ulikiona?”
“Tv ilikuwa inaongea yani kamavile ilikuwa imewashwa”
“Uliiona kabisa ikionyesha?”
“Hapana ila nilisikia sauti ndio nikakimbilia ndani kukuamsha”
“Mmmh maruweruwe hayo mke wangu ukizingatia na ndoto ambayo ulikuwa umeota usiku. Hapa hakuna lolote la kutisha mke wangu hata usiwe na uoga wa aina yoyote ile, uwe na amani tu”
“Lakini nilisikia kabisa”
“Ilimradi hujaona ujue basi ni maruweruwe tu mke wangu. Umefanya na nini usingizi wangu wote ukatike jamani saa kumi na moja hii bado giza totoro nje”
“Nisamehe mume wangu lakini kwakweli sikuwa na jinsi zaidi ya kukuamsha tu.”
“Usijali, mi nakuelewa sana Sophy wangu”
Kisha Ibra akamuomba Sophia kuwa warudi tena chumbani kulala tu hadi saa moja maana sikunhiyo hakuwa na mpango wowote wa kutoka asubuhi asubuhi.
Wakarudi chumbani ambapo Ibra alipojilaza tu usingizi ulimchukua tena na kufanya Sophia awe macho peke yake huku akiwa na mawazo mbalimbali.
Alikuwa akijiuliza kama kweli alisikia sauti ya tv au yalikuwa ni mawazo yake tu na maruweruwe kama mumewe alivyosema ila ilikuwa ni kweli kabisa kuwa alisikia mlio wa Tv kabisa, kwa mbali yale maneno ya Yule bibi aliyekutana nae kwa Siwema na kumwambia kuwa nyumba yake ni ya maajabu yakaanza kumuingia akilini na kuona kama kuna kaukweli flani ambako alikuwa akipingana nako ila alijiuliza kuwa je hayo maajabu yanaletwa na Jane au kuna mtu mwingine anayewafanyia mambo hayo ili kuwatisha kwenye nyumba yao?
Alipokuwa akiwaza hayo, kwa mbali akasikia tena sauti ya Tv na kufanya akurupuke pale kitandani ila kwa muda huu akajipa moyo wa ujasiri ambapo aliamua kwenda sebleni na kushuhudia kabisa kama ni Tv kweli au ndio maruweruwe yake kama mumewe alivyosema.
Sophia alitoka hadi sebleni ambapo kila aliposogea ile sauti ya Tv nayo ndio ilisikika zaidi, alipofika karibu na kuchungulia alikuta ni kweli Tv iliwaka na ilikuwa ikionyesha vizuri kabisa.
Itaendelea kama kawaida……………………..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
34
NYUMBA YA MAAJABU: 14
Sophia alitoka hadi sebleni ambapo kila aliposogea ile sauti ya Tv nayo ndio ilisikika zaidi, alipofika karibu na kuchungulia alikuta ni kweli Tv iliwaka na ilikuwa ikionyesha vizuri kabisa.
Kwakweli Sophia alipatwa na uoga sana safari hii, hali hiyo ilipekea aanze kuoiga makelele na kufanya mumewe atoke chumbani mbio hadi pale sebleni.
Moja kwa moja Ibra alimuuliza mkewe kuwa amekubwa na kitu gani,
“Nini tatizo mke wangu?”
“Ona Tv inawaka”
Ibra aliiangalia ile Tv ambayo ilikuwa ikionyesha vizuri kabisa kisha akamuangalia mkewe na kusema,
“Si nilichomoa nyaya zote kwenye hii Tv mimi!”
“Ndio ushangae sasa inawaka”
Ibra akaisogelea ile Tv na kuangalia vizuri akakuta nyaya zote zimechomekwa vizuri kabisa, kisha akamuangalia tena mke wake na kumuuliza,
“Nani kachomeka tena hizi nyaya za Tv?”
“Hakuna aliyechomeka itakuwa zimejichomeka zenyewe”
Ibra akacheka kama kwa dharau hivi kisha akamwambia mkewe,
“Nyaya zinajichomekaje zenyewe Sophy mke wangu? Unajua wewe huwa unabaki hapa nyumbani hebu kumbuka nani kachomeka nyaya? Au Siwema jana alichomeka hizo nyaya?”
“Ibra hakuna aliyechomeka, mimi nina uhakika na ninachoongea. Kwakweli nimeanza kuamini maneno ya Yule bibi kuwa hii nyumba ni ya maajabu na siwezi tena kubaki humu ndani peke yangu”
“Kwamaana hiyo unataka mimi nifanyaje? Je tuwe tunaenda wote kazini au nikuletee msichana wa kazi?”
Sophia akawa kimya kwa muda bila ya kujibu lile swali la Ibra, kisha Ibra akaisogelea ile Tv na kuizima halafu akachomoa tena nyaya zote za T vile, halafu akaanza kuongea na mkewe tena
“Unajua zamani watu walipokuwa wakiniambia kuwa wamama wajawazito wana vituko sana nilikuwa siwaamini kabisa ila sasa najionea mwenyewe kwa macho yangu. Kwakweli vituko vyako Sophy imezidi sasa”
“Jamani vituko gani ambavyo mimi navifanya Ibra?”
“Hebu kumbuka toka umeshika hiyo mimba ni vituko mwanzo mwisho, mara useme vyombo vimeosha kimiujiza sijui chakula kimepikwa kimaajabu mara nguo zimejifua zenyewe. Sasa ya saivi ndio kali hii ya kujiwasha kwa Tv duh! Tutafika kweli kwa mtindo huu mke wangu? Sophy hukuwa mtu wa kwenda kwa waganga ila kupindi hiki umeenda hadi kwa mganga na kuniletea makubwa zaidi, kiela chetu kimekwenda na maji. Ulitaka umuue Jane, hivi unaweza kuua wewe? Hiyo roho umeitoa wapi mke wangu? Wewe sio Sophy niliyekuzoea jamani!”
“Ibra najua unanishangaa kwavile mambo mengi ni mimi ninayeyaona ila ungeona na wewe ungeelewa kwanini nakuwa hivi”
“Kwahiyo unataka turudi yale maisha ya zamani? Unataka yale maisha yaw ewe kutembeza karanga na kurudi na mia tano ndani? Unayataka maisha yale ya kukosa hata hela ya kula ndani? Mumeo nimepambana na kufanya maisha yetu yabadilike ili angalau mke wangu uweze kuishi yale maisha ambayo wanawake wengine wanaishi ila matokeo yake ndio haya kukosa amani ndani! Nilikuwa najiuliza sana kwanini wanaume wengine huwarudisha wake zao nyumbani hadi watakapo jifungua ila sasa nimepata jibu kabisa, kwakweli wewe Sophia ni miongoni mwa wanawake wanaotakiwa kurudi nyumbani kwao hadi uatakapojifungua”
Sophia hakuongea chochote kwani kauli ya mumewe kuwa anastahili kurudi kwao hadi atakapojifungua ilimkera sana ukizingatia maisha ya kwao aliyajua mwanzo mwisho.
Ibra alirudi tena chumbani ambapo moja kwa moja akaenda kuoga huku akili yake ikimueleza kuwa lazima Sophia alienda sebleni na kuchomeka nyaya za Tv kisha akaiwasha na kujifanya kuwa imejiwasha ili kumfanya yeye awe anaamini maneno yake kuwa kuna maajabu katika nyumba hiyo.
Ibra alikuwa akioga huku akiwaza cha kufanya kwa huyu mkewe kwani alimuona kama anaanza kuchanganyikiwa na akili, alimaliza kuoga na kurudi chumbani alianza kuvaa huku akiongea peke yake,
“Kwakweli kama mimba zenyewe ndio hivi sijui kama nitaweza jamani, ndio kwanza mimba ya mtoto wa kwanza je akifika mpaka huyo wan ne anayehitaji yeye dah sijui kama sitabaki kijiti mimi kwa mawazo jamani mmh! Mwanamke ananieleleza huyu sijapata kufikiria.”
Wakati akiwaza hayo, salimsikia Sophia akimuita tena kwa sauti ya juu kabisa na kumfanya atoke na kuelekea Sophia alipo ambapo alimkuta jikoni,
“Eeh kuna nini kipya huku jikoni?”
“Vyombo vya jana vimeoshwa vyote”
Safari hii Ibra hakushtuka wala nini bali alicheka tu na kumwambia mkewe,
“Kama vimeoshwa si ndio vizuri umepunguziwa kazi au unaonaje mke wangu!”
“Ibra unachukulia masikhara wewe, sasa hutaki hata kujiuliza kuwa vimeoshwa na nani ikiwa ndani tuko wawili tu mimi na wewe!”
“Ingekuwa tunakuta vyombo visafi vimechafuliwa hapo sasa ndio ningechukua hatua ila kukuta vyombo vichafu vimeoshwa sasa nichukue hatua gani wakati kazi zetu zinajifanya zenyewe tu. Hakuna hata sababu ya kushtuka kwa hilo mke wangu kuwa kawaida tu”
Sophia alimuangalia mumewe kwa hasira kiasi na kuhisi kuwa mumewe kuna vitu anafahamu kuhusu yanayotokea ila amemficha tu maana muda wote yeye ndio anaonekana kuridhishwa kabisa na kinachotokea.
Kisha akamuuliza anapoelekea maana alimuona akiwa amemaliza kujiandaa kabisa,
“Kwahiyo ndio unataka kwenda wapi?”
“Nataka kwenda kumleta fundi wa Tv”
“Kipindi kile ulisema hivyo hivyo ila mpaka leo kimya haonekani fundi wala nini”
“Fundi ningemletaje na yale majanga yako? Tatizo lako kila leo unazua jipya yani hatupumui humu ndani.”
“Kwahiyo mimi unaniacha na nani?”
“Nilikuuliza nikuletee msichana wa kazi au uende kwenu ukapumzike? Hakuna ulilonijibu sasa unafikiri mimi nasemaje tena!”
“Ila mimi si nilishakwambia sitaki msichana wa kazi nataka aje mdogo wangu”
“Sophy, mdogo wako Yule Tausi unamjua vizuri kabisa kwakweli siwezi kumleta hapa maana mambo yatakuwa ni yale yale tu. Lini Tausi ametulia nyumbani? Hebu usitake kuleta makubwa zaidi. Cha muhimu hapa ni mdada wa kazi tu.”
“Sawa siwezi kukupinga si umeamua bhana, sasa tutampatia wapi huyo mdada wa kazi?”
“Tutampata tu hata usijali, ngoja nianze kuulizia kwa wadau mbali mbali.”
“Ila kwa leo mimi sibaki hapa peke yangu”
“Kwahiyo unataka nikusubiri twende wote kwa fundi?”
“Ndio nisubiri”
“Mmh kweli kazi ninayo, haya kajiandae nakusubiri”
Ilibidi Ibra akae sebleni akimngoja mkewe amalize kujiandaa waende huko kwa fundi.
Sophia alipomaliza kujiandaa alitoka, kisha yeye na mumewe wakatoka nje ambapo Ibra aliona ni vyema wakamfate fundi kwa miguu tu kwani hapakuwa na umbali wowote,
“Ni vyema maana itakuwa pia ni zoezi tosha kwangu”
Wakaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida tu ila mbele kidogo walimuona binti kajiinamia tena alionyesha wazi kuwa alikuwa akilia, kwakweli Sophia huruma ilimjaa kwa binti Yule na kumuomba mumewe kuwa wamsogelee na wamuulize kuwa alikuwa na tatizo gani ila kama kawaida ya Ibra na roho yake ngumu alikuwa akipinga,
“Sophy, kila mtu ana matatizo yake hapa duniani utayaulizia ya wangapi jamani?”
“Ibra jamani mbona huwa huna huruma! Unakuwa na roho mbaya hivyo kwanini?”
“Roho mbaya kushinda wewe uliyekuwa unataka kumuua Jane!”
“Jamani hayo mambo si yaliisha! Hebu tukamuulize Yule binti inaonekana ana matatizo”
Ibra aliamua kukubaliana na mkewe kisha wakamsogelea Yule binti ambaye ni kweli alikuwa akilia, Sophia akainama na kumuuliza kuwa ana matatizo gani
“Nina matatizo mengi sana dada yani hapa nilipo hata kula sijala njaa nayo inaniuma sana”
Sophia akaingiwa na imani na kumuomba mumewe kuwa warudi na binti huyo nyumbani kwao ili waweze kumpatia chakula na awaeleze yale yaliyomsibu ili kama wataweza kumsaidia zaidi basi wamsaidie. Ibra hakupinga swala hilo kisha wakamsaidia Yule binti kuinuka na kuanza kuelekea nae nyumbani kwao.
Walifika na kuingia nae ndani ambapo Sophia alienda kupasha kile chakula cha usiku na kumpatia ili ale, kisha na wao wakapakua cha kwao na kuanza kula kwani walikuwa wakienda kwa fundi wakati hata kula walikuwa hawajala.
Walikuwa kwa pamoja pale na kumaliza kisha wakatulia kabisa kusikiliza kuwa huyu binti alikuwa na matatizo gani, Sophia alianza kwa kumuuliza,
“Kwanza kabisa unaitwa nani na ni kitu gani kilichokupata mpaka ukawa umekaa pale unalia?”
“Mimi kwa majina naitwa Neema, kwakweli nina matatizo sana yani tangu alipokufa mama yangu nimekosa kabisa furaha ya maisha kwani nilikuwa nikiishi na bibi tu ila ndugu wote walikuwa hawanitaki nyumbani”
Akainama tena na kuanza kulia ambapo Sophia alimsogelea na kumbembeleza,
“Pole sana Neema jamani dah pole sana, eeh ikawaje?”
“Tatizo la sasa ni kuwa Yule mtetezi wangu yani bibi yangu nae amekufa na kuniacha na ukiwa halafu ndugu wakanifukuza. Nimejikuta nikitangatanga tu kisha nilipanda gari la mizigo lililoniacha mjini ila nimejikuta sina pa kuelekea na hata sijui cha kufanya”
“Khee jamani binadamu wabaya sana, pole sana. Ngoja na sisi tuangalie namna ya kukusaidia Neema”
“Nitashukuru sana jamani maana sina uelekeo mimi”
Ibra akaona ni vyema amuache Sophia na huyo Neema ili yeye aende huko kwa fundi, kwahiyo akawaaga pale na kutoka nje ambapo kabla hajaondoka Sophia alimfata nje na kumuuliza kuhusiana na wao kumsaidia binti huyo.
“Unaonaje tukiishi na huyu binti mume wangu?”
“Sophy, tutazungumza nikirudi ngoja saivi nishughulikie hili swala la fundi”
“Sawa basi badae”
Ibra akaondoka na kumfanya Sophia arudi ndani.
Sophia alienda kukaa karibu na Yule binti ili hata kujaribu kuongea nae kama ataweza kuishi hapo nyumbani kwao,
“Je tukikwambia ukae hapa na sisi unaonaje?”
“Nitafurahi sana dada, unaonekana una roho nzuri sana dada yangu”
“Usijali, jisikie huru kabisa yani jisikie upo nyumbani. Ila kazi za nyumbani unaweza kufanya?”
“Hakuna kazi ambayo mimi inanishinda, maisha niliyokulia yamefanya niwe naweza kazi zote dada yangu kwahiyo hata usiwe na hofu kuhusu mimi.”
Sophia alijikuta akiwa na huruma sana kwa huyu binti na pia akivutiwa nae sana na kuona lile swala lake na mumewe la kuhitaji mdada wa kazi limepata ufumbuzi kwa stahili hiyo.
Muda kidogo Ibra alirudi akiwa na kijana ambaye alimtambulisha kuwa ni fundi, Yule kijana moja kwa moja alienda kuiangalia ile Tv kisha akaanza kuwaorodheshea matatizo ya ile Tv n kuhitaji wampatie pesa ili aende akanunue vifaa kwaajili ya kurekebisha Tv hiyo.
“Inahitajika kama laki moja na nusu hapa ili tatizo lisijirudie tena, yani msingekuwa makini siku moja ingewalipukia hii”
“Ila mbona gharama sana mtu wangu?”
“Ndio hivyo, ni kutokana na kifaa ambacho kimeharibika huwa kinauzwa gharama sana tena hapo nimekupunguzia sababu wewe wangu bhana, yani hela ya ufundi hapo nitachukua elfu kumi tu maana laki na arobaini yote nitaenda kununulia hicho kifaa”
Ibra akafikiria kidogo, ila kwavile hapendi malalamiko ya kila siku kuhusu ile Tv aliamua kujitoa muhanga kwa kutoa hiyo pesa ili amkabidhi huyo fundi kwaajili ya kununua hicho kifaa. Ila kabla fundi hajapokea ile pesa, huyu Neema akamwambia Ibra,
“Kaka hata usitoe hiyo pesa maana hii Tv sio mbovu”
“Kwani wewe hii Tv unaijua?”
“Siifahamu ila moyo wangu unaniambia kuwa hii Tv sio mbovu”
Kisha akamuangalia Yule fundi na kumwambia,
“Kwanini unakuwa muongo hivyo? Au ukubwa wa hii nyumba ndio unafanya na wewe utake kuponea hapa! Hebu waambie ukweli kuwa hii Tv sio mbovu na wala hakuna kifaa chochote kilichoharibika, sema ukweli”
Huyu fundi alionekana akitetemeka na kujieleza kuwa ni kweli ile Tv haikuwa mbovu ila yeye alishikwa na tama ya pesa tu na ndiomana akasema vile, Ibra alimshangaa sana huyu fundi kwani alikuwa ni kati ya watu aliowaamini sana, kisha huyu fundi aliondoka bila kuaga.
Ibra alimuangalia Neema na kumshukuru kisha akamuuliza kuwa amejuaje kuwa ile Tv sio mbovu na amejuaje kuwa Yule fundi ni muongo,
“Bibi yangu alinifundisha kuwa mtu muongo akiongea macho yake huwa anapepesa pepesa, sasa nilipomuangalia huyo fundi nikamuona akipepesa macho na moja kwa moja nikagundua kuwa ni muongo.”
Sophia aliyekuwa amekaa kimya kwa kipindi chote nae aliamua kuchangia mada kwa kumshukuru sana Neema maana ilikuwa kama amewasaidia katika kupoteza pesa zingine, ila bado alimwambia kuwa ile Tv ina tatizo la kujiwasha na kujizima ndiomana wakaita fundi awasaidie.
“Msijali, ilimradi mimi nipo hapa hilo tatizo halitajitokeza tena”
Sophia hakuongeza neno zaidi ya kwenda kumuonyesha Neema chumba ambacho atakuwa analala kwa kipindi chote atakachokuwa anaishi hapo.
Alimpeleka kwenye chumba ambacho kilikuwa na kitanda na godoro tu kisha Sophia akatoka na kumuacha huyo Neema kwenye chumba hicho, Sophia alienda chumbani kwake na kumchukulia Neema mashuka ili aweze kutandika vizuri pale kitandani na kufanya papendeze kulala.
Sophia akiwa na mashuka yake mkononi kwa lengo la kumpelekea Neema, aliingia kwenye kile chumba na kumkuta Neema akiwa amesimama tu ila kitanda kilikuwa kimetandikwa vizuri kabisa tena kwa mashuka mazuri.
Itaendelea kama kawaida…………!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 15
Sophia akiwa na mashuka yake mkononi kwa lengo la kumpelekea Neema, aliingia kwenye kile chumba na kumkuta Neema akiwa amesimama tu ila kitanda kilikuwa kimetandikwa vizuri kabisa tena kwa mashuka mazuri.
Kwakweli Sophia alishangaa sana na kumtazama Neema kwa mshangao zaidi ila huyu Neema hakuonekana na hofu yoyote ile na kufanya Sophia amuulize,
“Neema, kitanda kimetandikwa na nani? Na je mashuka yametoka wapi hayo?”
Neema hakujibu ila naye alimuuliza swali Sophia,
“Kwani umeyapenda dada haya mashuka?”
Sophia alizidi kushangazwa kwani hakutegemea na yeye kuulizwa swali badala ya kujibiwa swali lake kwahiyo ilikuwa kamavile ni kitu kinachomchanganya zaidi, kisha kabla hajaongeza neno lolote akamshangaa tu Yule Neema akimpokea yale mashuka na kisha kumshukuru sana kwa kumletea,
“Asante dada kwa haya mashuka kwani nayo ni mazuri sana dada yangu”
Bado Sophia hakuweza kuongeza neno lolote zaidi ya kutoka mule chumbani na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake kwani hata sebleni alipitiliza, Ibra alikuwa ametulia tu pale sebleni akimuangalia mkewe akipitiliza chumbani na kuhisi kuwa huenda kuna vitu ambavyo mkewe alivisahau huko chumbani kwani kwa matarajio yake alihisi kuwa mkewe alipomaliza kupeleka yale mashuka angerudi pale sebleni waweze kuzungumza.
Muda kidogo ni Neema aliyetoka na kwenda kukaa sebleni ambapo alimtazama tu Ibra bila ya kuongea chochote kile, Ibra nae hakuchukua muda mrefu akainuka pale sebleni na kuelekea chumbani.
Alipofika chumbani alimkuta mkewe akiwa amelala kabisa kamavile ni muda mrefu aliingia kulala, mija kwa moja Ibra alihisi kuwa ni uchovu wa mimba ndio umemfanya mkewe awe katika ile hali kwani haikuwa kawaida yake hapo zamani, ila Ibra nae alipanda kitandani na kujilaza karibu na mkewe ambapo kwa muda mchache tu naye usingizi ulimpitia.
Walipokuja kushtuka muda tayari ulikuwa umeshaanda tena aliyeanza kushtuka alikuwa ni Ibra na kumuamsha mkewe,
“Sophy, Sophy tumelala sana mke wangu amka”
Sophia nae aliamka na kuanza kujinyoosha kwa uchovu huku akijihisi kuchoka sana, kwa pamoja wakainuka na kutoka chumbani ambapo walimkuta Neema akiwa pale sebleni tena alionekana kuyazoea sana mazingira yale kupita maelekezo kwani alikuwa sawa na binti ambaye amekuwa pale kwa siku zote. Ambapo walipofika tu sebleni aliwakaribisha mezani kuwa chakula tayari, hakuna aliyehoji kati yao kuwa ni nani aliyemwambia Neema kupika au kumuelekeza cha kupika bali walielekea mezani wote na kuanza kula huku huyu Neema akiwa anaendelea na shughuli zingine.
Alianza Sophia kukisifia kile chakula kuwa ni kitamu sana huku akiyasifu mapishi ya Neema kuwa ni binti aliyefundwa vyema, Ibra nae alimsapoti mkewe kwa kummwagia sifa za kutosha huyu Neema. Hadi wanamaliza kula ilikuwa ni kumsifia Neema tu pale mezani.
Walipomaliza tu Neema alikuja na kutoa vile vyombo na kuvipeleka jikoni moja kwa moja kisha Sophia na Ibra wakarudi sebleni na kukaa ambapo neema alikuwa ameiwasha ile Tv ambayo walikuwa wakiogopa kuiwasha kwa siku zote mule ndani.
Hakuna aliyemuuliza chochote Neema kwani wote walitulia na walionekana kuridhishwa na uwepo wake mule ndani, ingawa mara nyingi sana walimuona huyu Neema akiwaangalia sana ila hawakuweza kuhoji kitu chochote kile zaidi ya kutabasamu tu.
Usiku ulipoingia zaidi, Sophia na Ibra walielekea chumbani kwao huku Neema nae akielekea chumbani kwake.
Walipokuwa chumbani, Ibra aliamua kumuuliza mkewe kilichompelekea mchana kwenda kulala bila ya kumtaarifu.
“Ilikuwaje kwani maana nilikukuta umelala hoi kabisa au ndio mambo ya mimba tena?”
“Naelewa basi! Hata sielewi, nilikujs chumbsni sijui hata kufanya nini nikashangaa usingizi ulipotokea loh yani nimelala usingizi mzito kupita maelezo ya kawaida.”
“Duh pole mke wangu, najua ni mimba hiyo inayokusumbua ila mambo yatakuwa sawa baada ya miezi kadhaa tu.”
“Na hapa tumbo halijakua vizuri je likikua sijui itakuwaje”
“Utazoea tu mke wangu ila ni vyema kama ukianza kliniki si unajua wanasema ni bora kuanza mapema!”
“Naelewa mume wangu nitaanza tu hata usijali”
“Ila unasemaga hivyo kila siku halafu wala huonyeshi huitaji wa kuanza kabisa hata sijui kwanini?”
“Ngoja tumbo litokee tokee kwanza”
“Mmh jamani Sophy, mbona watu wanaanzaga mapema unataka tumbo litokeaje?”
“Khee Ibra hao wanaoanza mapema umewaona wapi? Ushawahi kukaa na mwanamke mjamzito wewe?”
“Basi yaishe mke wangu ila ni vyema kuanza kliniki”
“Sawa nitaanza hata usijali”
Sophia akajinyoosha pale kitandani na kulala, muda huo huo ikawa kama amelala kwa muda mrefu kwani alikuwa na usingizi mzito sana na kufanya Ibra amtazame tu kisha na yeye akalala.
Ibra alipolala tu akajiwa na ndote, ile ndoto ilimuonyesha kuwa Yule nyoka mkubwa waliyemuona mlangoni kwao hakuwa nyoka kweli bali alikuwa ni huyu Neema waliyekuwa nae ndani kwani alivyokuwa akimuona kwenye ndoto alimuona akibadilika badilika mara akiwa mtu na mara akiwa joka. Kisha akamuona Jane akiingia pale ndani kwao na gafla Yule nyoka akayeyuka halafu akaonekana chini ya mti mahali ambapo ndio pale pale walipoenda kumkuta Neema akiwa amejiinamia.
Kwakweli Ibra alishtuka sana kwani hakutegemea kama anaweza kupata ndoto ya namna ile ukizingatia huyo Neema ndio wanaishi nae ndani kwa kipindi hiko, jasho lilikuwa likimtoka sana Ibra na kumfanya ashindwe kuendelea kulala kabisa kwani alikaa tu kitandani kwa muda huo, kisha akakumbuka jinsi mkewe nae anavyopataga ndoto ambazo huwa zinamfanya akose usingizi kabisa kwakweli na leo ilikuwa zamu yake yeye.
Kulipokucha Ibra aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye shughuli zake, kisha akamuamsha na mkewe kwa kumuaga kuwa anatoka kwa muda huo, hivyo Sophia aliinuka ili aweze kufunga mlango pale mumewe anavyotoka ila walipofika sebleni walimkuta Neema akiwa tayari ameshaamka, alikuwa amekaa tu akiangalia Tv ikabidi wamsalimie huku Sophia akimuuliza kuwa mbona mapema sana.
“Ndio kawaida yangu kuamka mapema huwa silali kupitiliza”
“Sawa ndio vizuri ila duh unawahi sana”
“Hata usijali kitu dada yangu”
Ibra akawaaga pale na kuondoka, ndani alibaki Neema na Sophia ambapo Sophia alirudi chumbani na kuendelea kulala.
Ibra akiwa njiani kwakweli alijikuta akikosa imani kabisa kumuacha mkewe na Neema ukizingatia mkewe ni mjamzito halafu Neema ni mgeni kwenye ile nyumba yao, akajiwa na wazo kuwa ni bora akamwambie Jane nae aende pale kwake ili awe nao pamoja kuliko mkewe kubaki mwenyewe na Yule Neema ambayo hawamfahamu vizuri.
Ibra aligeuza gari na moja kwa moja akaelekea kwakina Jane ambapo kama kawaida alimkuta mama yake Jane akiwa ndiye pekee aliyeamka huku akifanya shughuli za nyumbani kwake, hivyo akamsalimia na kuomba aitiwe Jane, ila leo mama Jane nae alifunguka
“Ila nyie mpaka mumtoe mwanangu ngeo ndio mtaona raha maana sio kwa kumuita ita huko halafu akifika kwenu mnamfanyia vituko. Au unafikiri habari zenu sikuzipata? Kwanza mwanangu Jane bado kalala labda uje badae.”
Ibra hakutaka kupingana na huyu mama ukizingatia ni kweli mambo ambayo walimtendea Jane hakuna mzazi yeyote anayeweza kuridhishwa au kufurahishwa nayo, hivyo Ibra akawa mpole tu na kumuaga huyu mama kuwa atarudi tena badae.
Ibra akaondoka pale kwakina Jane na kuelekea kwenye shughuli zake ila mawazo yake yalikuwa ni juu ya mkewe kwani alijikuta gafla akikosa amani kabisa dhidi ya uwepo wa Yule Neema pale nyumbani kwao ukizingatia na ile ndoto aliyoota ndio kabisa yani.
Sophia sasa aliamka vizuri na kwenda sebleni tena ambapo alimkuta Yule Neema akiangalia tu Tv ila kazi za mule ndani zote zilikuwa zimefanyika, Sophia alikaa nae huku akizungumza nae kwa furaha sana.
“Kwakweli Neema nimekupenda bure maana wewe ni mchapakazi sana na hata sikukutegemea kabisa kama utakuwa hivi”
“Usijali dada mbona utazidi kufurahia uwepo wangu, yani utafurahia sana na kujilaumu kuwa kwanini umechelewa kugundua uwepo wangu”
“Ni kweli kabisa maana wewe hata sio mtu wa kupigishana kelele ukizingatia unafanya kazi zako kwa wakati.”
Neema akatabasamu tu, kisha akamwambia Sophia kuwa hata chai alishamuandalia mezani ambapo Sophia alienda moja kwa moja kunywa chai ile ambapo alikuta ni chai ya maziwa, chapati na mayai. Sophia alikunywa bila hata ya kuhoji kuwa vile vitu vimenunuliwa muda gani hadi kupikwa kwani alihisi huenda mumewe alinunua bila hata ya kusema.
Alipomaliza kunywa chai alirudi chumbani kuoga ili kupata nguvu mpya ambapo alioga na kwenda kukaa kitandani huku akijikuta akifikiria mambo mawili matatu.
“Inamaana Neema zile chapatti kazipika au kazinunua? Kama kazipika unga ametoa wapi? Na kama amezinunua basi pesa alipewa na nani? Hivi Ibra anaweza kutoa pesa bila ya kunishirikisha kweli? Vipi kuhusu yale mayai mmh! Itakuwa ni ibra tu ila hatahivyo chakula kilikuwa kitamu sana.”
Sophia akatulia na kuanza kuvaa kisha akatoka tena na kwenda sebleni ambapo Yule Neema alikuwa pale pale sebleni akiwa ametulia akiangalia Tv tu, ambapo Sophia alimuuliza
“Huchoki Neema kuangalia Tv?”
Neema akatabasamu tu na kudai kuwa anapenda sana kuangalia Tv kuliko kitu chochote na kama akichoka basi ataizima, Sophia hakutaka kuongea zaidi kwani alihisi anaweza kumfanya Neema achukie bure ukizingatia hoja yake ilikuwa ni kumwambia kuwa tv inahitaji kupumzika kwani sio vizuri kuwa inaonyesha muda wote.
Walikaa pale sebleni kwa muda kidogo na hata mchana iliwakutia pale pale, muda kidogo Neema akamwambia Sophia kuwa chakula cha mchana kilikuwa tayari mezani, Sophia alimuangalia na kumuuliza kuwa amekipika muda gani kwani kwa kumbukumbu zake walikuiwa wote hapo sebleni kwa muda wote pamoja.
Neema akatabasamu na kumwambia Sophia,
“Tulikuwa wote ndio ila wewe muda mwingi ulikuwa unasinzia, mimi nimeenda kupika nimekula hata hujajua. Pole dada, ila ni hali yako hiyo ndio imekufanya hivyo”
“Kheee kwani unajua kama mimi nina mimba! Nani kakwambia?”
“Si ngumu kumgundua mwanamke mjamzito tena ikiwa mtu unauzoefu nao ndio kabisa yani, mi hata mtu mwenye mimba ya siku moja namjua sembuse hiyo mimba yako ya miezi mitatu jamani”
Sophia akashtuka kuona kuwa Neema amejua hadi muda wa mimba yake kuwa ina miezi mitatu,
“Khee umejuaje kama mimba yangu ina miezi mitatu?”
“Mimi hata mimba ya siku moja nagundua kutokana na kukaa sana karibu na bibi yangu, tena mimba yako wewe hiyo miezi mitatu ipo wiki ya mwisho maana wiki ijayo itaanza mwezi wa nne. Yani usijali chochote, mimi nilishaisoma hali yako dada nenda kale upate nguvu maana mimba inataka uwe unakula hata kwa kujilazimisha ila uwe unakula ili kumfanya mwanao akue vizuri”
Sophia hakuongea zaidi ila aliinuka na kwenda mezani kula ambapo alikula vizuri sana tofauti na siku zingine ambavyo huwa anakula kwa kujivuta vuta, alikuwa akifurahia tu utamu wa kile chakula kwa muda ule.
Alipomaliza kula alirudi pale sebleni na kukaa tena na Neema ambaye alionekana makini sana katika kuitazama ile Tv kamavile kuna vitu vya maana anavyovitazama kwani alionekana kuwa makini mno.
Sophia akamuuliza tena Neema kuwa anapendea nini kutazama Tv muda wote na kumuuliza kuwa kama hachoki kutazama vile.
“Si nilishakujibu dada kuwa napenda kuangalia Tv kuliko kitu chochote kile kwahiyo wewe usijali, au hupendi niwe naangalia?”
“Hapana, wee angalia tu Neema”
Sophia aliamua kujivunga tu kwa muda huo ingawa kiukweli hakupenda kwavile aliona Tv inakosa muda wa kupumzika.
Ibra aliwahi kutoka kazini siku hiyo kwani alihitaji kuzungumza na Jane na pia kumuomba awe anaenda nyumbani kwake pindi yeye akiwa kazini, kwahiyo moja kwa moja safari yake ilikuwa ni kuelekea kwakina Jane. Alipofika kwa bahati nzuri alimkuta Jane akiwa mwenyewe nje ya nyumba yao na kumuomba kwaajili ya mazungumzo,
“Jane samahani nimekuita kwa pembeni kwavile naogopa mama yako asije akaniona bure. Tafadhali twende wote nyumbani kwangu nataka kuongea nawe kidogo tu”
Jane akaingia kwenye gari ya Ibra bila hata kuhoji maswali ya ziada, kisha Ibra akaendesha gari ambapo alipokaribia na nyumbani kwake alilisimamisha na kuzungumza kidogo na Jane.
“Kwanza unaendeleaje maana mama yako asubuhi alifoka sana hata sijui alijuaje”
“Dunia haina siri, siku ile nimepiga kelele kuna watu walimueleza mama na vile nilivyorudi naumwa mama aliniuliza sana mwisho wa siku sikuweza kuendelea kumficha na nikaamua kumwambia ukweli”
“Sawa hakuna tatizo Jane hata hivyo tulifanya makosa sana, ila kuna kitu kimoja nilikuwa naomba unisaidie”
“Kitu gani hicho?”
“Pale nyumbani tumepata msichana wa kazi ila mimi nimejikuta kutokumuamini kwakweli, sasa nilikuwa naomba pindi nikiwa kazini uwe unaenda pale nyumbani mara kwa mara kumuangalia mke wangu na ikiwezekana hata uwe unashinda pale pale”
Jane akajifikiria kidogo ila hakukataa na kumfanya Ibra afurahi kisha akamuomba kwa muda huo aingie nae ndani ili angalau amfahamu huyo mdada wa kazi waliyempata.
Ibra alisogeza gari yake mpaka getini kabisa kisha akashuka pamoja na Jane kuelekea ndani, na walipofika Ibra alifungua mlango wa ndani na kuingia ambapo Sophia na Neema walikuwa pale pale sebleni.
Ila Jane alipomuona Neema alishtuka sana na kufanya wote wamshangae kilichomshtua kiasi kile.
Itaendelea kama kawaida……………….!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
34
NYUMBA YA MAAJABU: 16
Ibra alisogeza gari yake mpaka getini kabisa kisha akashuka pamoja na Jane kuelekea ndani, na walipofika Ibra alifungua mlango wa ndani na kuingia ambapo Sophia na Neema walikuwa pale pale sebleni.
Ila Jane alipomuona Neema alishtuka sana na kufanya wote wamshangae kilichomshtua kiasi kile.
Jane alianza kurudi kinyumenyume na kuwafanya washangae zaidi huku Ibra akimuuliza kuwa tatizo ni nini au ni kitu gani kakiona, ila Jane hakusema chochote na alionekana akizidi kurudi kinyumenyume na alipofanikiwa kufika nje alionekana akiondoka kwa kukimbia kabisa eneo lile.
Walibaki wakimshangaa na kutazamana tu, kisha Sophia akamuuliza mume wake
“Umetoka nae wapi Yule na kwanini aogope vile na kukimbia?”
Ibra alikosa jibu ila Neema alionekana akicheka na kisha kuwajibu yeye,
“Hivi unafikiri angeweza kuingia Yule na kukaa pamoja na mimi!”
“Kwanini asiweze?”
“Yule mtoto ni mchawi halafu alikuwa amekuja na vitu vyake vya kichawi, sasa kuniona mimi ameogopa sana sababu mimi ni mtu safi na siwezi kuingiliwa na wachawi. Ndiomana ameshindwa hata kunitazama mara mbili hapa”
Sophia akamuangalia mumewe na kumwambia,
“Umesikia sasa, Yule Jane ni mchawi ila nikisema mimi unaona kamavile namuonea haya sasa leo umesikia kwa macho yako tena licha ya kusikia umeweza kujionea mwenyewe jinsi alivyojawa na hofu hadi kukimbia. Kwakweli Neema amekuja kuikoa familia yetu mume wangu”
Ibra hakuongea chochote kwani hata yeye hakutegemea kabisa lile swala la Jane kumkimbia Neema ambaye wao wanaishi nae ndani, alijikuyta akiwa na maswali pamoja na mawazo mengi sana katika kichwa chake. Ila Sophia alijitahidi kwa muda huo kumuweka mumewe sawa ambapo akamwambia akae ili atulize akili, ila Ibra kabla hajakaa akakumbuka kuwa gari yake alikuwa ameiacha nje ya geti kabisa na hivyo kumwambia mkewe asubiri akaiingize kwanza.
Ila alipotoka ndani tu alikuta ile gari ikiwa imeshaingizwa ndani ya geti huku geti likiwa limefungwa vizuri kabisa, kwakweli akili ya Ibra ilikuwa kamavile inavurugika kwa muda huo kwani alijikuta akiwa haelewi elewi kabisa, kitendo hicho kilimfanya asimame sana pale nje bila ya kuingia ndani ikabidi Sophia amfate nje maana aliona akikawia.
“Si ushaingiza gari, mbona umesimama tu?”
“Hii gari sijaiingiza mimi”
“Sasa nani ameiingiza jamani mume wangu?”
“Hata mimi nashangaa sielewi kabisa”
“Mmh twende ndani bhana itakuwa umejisahau tu”
“Hapana siwezi kujisahau kiadsi hiki Sophy dah! Akili yangu haipo sawa kabisa”
Kisha akaingia ndani na moja kwa moja akaelekea chumbani ambapo Sophia aliamua kwenda kumfata huko chumbani.
Ibra alionekana kujiinamia tu kitandani kwani ilionyesha wazi kuwa alikuwa na mawazo mengi sana, ikabidi Sophia aendelee kumpa moyo mumewe na kuwa karibu naye ili angalau aweze kumsaidia katika kumpunguza mawazo aliyokuwa nayo.
“Ni vitu gani unawaza kiasi hikomume wangu?”
“Wewe acha tu Sophy, kewakweli akili yangu haipo sawa kabisa”
“Pole sana, basi itabidi uoge ili angalau uchangamshe akili. Tafadhali Ibra mume wangu naomba ufanye hivyo”
Ibra alimuelewa mkewe na kuamua kufanya hivyo ambapo moja kwa moja alienda bafuni kuoga. Ila alipokuwa mule bafuni kila akifumba macho inamjia picha ya Yule joka pamoja na picha ya Neema kwakweli akajikuta akipatwa na uoga kupita maelezo ya kawaida. Kitendo hicho kilimfanya atoke bafuni kwa haraka bila hata ya kuoga vizuri.
“Khee mume wangu umetoka hadi na povu sikioni”
“Wee acha tu Sophia, kuna muda nitakueleza na utanielewa vizuri tu”
“Nieleze saizi mume wangu ili tushauriane cha kufanya”
“Hata kama nikikueleza saizi sijui kama utanielewa mke wangu, nitakueleza tu pindi akili yangu itakapotulia”
“Basi twende ukale mume wangu”
“Hiko chakula nani kapika?”
“Amepika Neema”
“Mmh kama Neema hapana, sijisikii kula kwakweli”
“Kheee makubwa, sasa maana ya mdada wa kazi ndani ni nini jamani mume wangu?”
“Mdada wa kazi ni mtu wa kutusaidia kazi za humu ndani ila sio mpaka chakula cha mumeo apike mdada wa kazi”
Sophia alimshangaa sana mumewe kwani hakutegemea kama angeongea maneno kama hayo, aliona kuwa Ibra ni mwanaume asiye na huruma kwani anajua fika hali ya Sophia kuwa ni mjamzito ila bado alihitaji kupikiwa chakula naye, kwakweli Sophia alikuwa amechukia kwa kiasi kisha akainuka na kumwambia,
“Ngoja nikakuandalie chakula mwenyewe basi ili ufurahi”
“Unaenda kuniandalia chakula gani?”
“Wali”
“Sitaki wali, nataka ugali”
Kisha Sophia akatoka mule chumbani na kumuacha Ibra akiwa mwenyewe amejiinamia tu kwa mawazo.
Sophia alienda moja kwa moja jikoni huku akiwaza kuhusu Ibra kutokuwa na huruma na hali yake,kisha akaona ni vyema amsongee tu huo ugali kwa haraka kisha amuandalie na mboga ya haraka aweze kula.
Akabandika sufuria ya kusongea ugali, kisha akaenda kufungua friji ili aangalie kama kuna mboga ya aina yoyote. Alipofungua ile friji alishangaa kwa muda kwa kila mboga aliyoifikiria kichwani mwake ilikuwepo mule akajiuliza kuwa ni Ibra alinunua mboga hizo au imekuwaje, ila moja kwa moja alihisi ni Ibra tu kwani hakuna mwingine ambaye angenunua zile mboga kama sio Ibra.
Akatoa samaki ambao walikuwa wamekaushwa vizuri ili awaunge na kumuandalia Ibra mezani, ila alipokuwa anageuka na wale samaki akashangaa kumuona Neema akiwa ameweka vizuri ugali kwenye sahani na kufanya amuulize kwa mshangao,
“Khee Neema umeingia saa ngapi humu jikoni?”
“Nimeingia wakati wewe unatafuta mboga kwenye friji ndio nikaamua nikusaidie kusonga huu ugali maana maji yalikuwa yanachemka.”
“Umejuaje kama yale maji yalikuwa ya ugali?”
“Kheee dada, ukizoea kupika basi itakuwa rahisi sana kujua kila aina ya pishi na ndiomana nimejua kwa haraka sana kuwa yale maji yalikuwa ya ugali na ugali huo tayari. Lete hao samaki nikupikie haraka wakati unaenda kuandaa huu ugali mezani”
Sophia hakuongeza neno bali alimpa Neema wale samaki kisha akabeba ule ugali na kuupeleka mezani huku akiwaza kuwa neema amewezaje kusonga ugali kwa muda mfupi kiasi kile! Akajiuliza,
“Ingawa ugali ni chakula cha haraka kupika ila mmh ndio kwa muda mfupi vile?”
Hakupata jibu na kurudi jikoni ambapo alimkuta Neema ameshamaliza kuunga wale samaki na alishawaandaa kwenye bakuli, Sophia alishtuka ila alishindwa kuuliza chochote ambapo alichukua ile mboga na kwenda kuweka mezani kisha akaenda kumuita mume wake.
“Chakula tayari Ibra”
“Mmh umepikia kompyuta au?”
“Kwanini?”
“Mbona kimekuwa haraka sana!”
“Nakujali mume wangu na ndiomana nimeharakaisha”
“Sio swala la kunujali Sophia ila umetumia muda mfupi sana”
Kisha Ibra akainuka na kwenda mezani kula ambapo alikula huku akimsifia mkewe kuwa amepika chakula kitamu sana, Sophia alikuwa akitabasamu tu ingawa alielewa wazi kuwa zile sifa alipaswa apewe Neema maana ndiye aliyepika chakula kile, ila hakumwambia mumewe kwavile alikataa kula chakula kilichopikwa na Neema.
Ibra alipomaliza kula alimuuliza Sophia,
“Mbona huyu Neema muda wote namuona akiangalia Tv tu, hivi hachoki?”
“Kasema anapenda kuangalia Tv kuliko kitu chochote kile na ndiomana mimi huwa namuachaga tu aangalie, tena mara nyingine utakuta anaangalia na wala hata hajitingishi yani sijui kukaa vile hachoki”
“Labda hachoki, ila kwa mimi siwezi kwakweli kuangalia Tv muda wote siwezi. Sasa huko kupika na kazi zingine za hapa atakuwa anazifanyaje?”
“Kazi anafanya vizuri ila ndio akishafanya anarudi tena kwenye Tv”
“Mmh basi sawa”
Ibra akainuka na kurudi tena chumbani kwao kwani hakutaka hata kukaa sebleni. Ila Sophia alienda kukaa na Neema ambaye muda wote alikuwa makini kuangalia Tv tena kuna kipindi alionekana kutokupepesa hata macho na kumfanya Sophia ajiulize zaidi kuwa huyu Neema hachoki.
Walikaa pale hadi giza lilipoingia na kuwasha taa za ndani, kisha Sophia akainuka na kuelekea chumbani alipo mumewe.
Alimkuta akiwa amejiinamia tu kama ambavyo alijiinamia mwanzo,
“Kheee hayo mawazo Ibra sasa yamezidi jamani. Tushirikishane hutaki sasa hata sijui ndio nini wakati mimi ndio mkeo”
Ibra muda huu alimuuliza swali Sophia,
“Hivi Sophy una uhakika kuwa Jane ni mchawi?”
“Jane ni mchawi ndio tena ni mchawi aliyekubuhu”
“Mmh sio kwamba anasingiziwa?”
“Hivi mume wangu huyo Jane ana lipi labda la kusingiziwa? Hata kama kusingiziwa ndio watu wote hawa wanamsingizia? Tuseme mimi namsingizia, da’ Siwema je anamsingizia? Yule mganga je? Na Neema je anamsingizia? Yule Jane hata hasingiziwi mume wangu ni mchawi kweli, na bora tumepata kiboko yake humu ndani maana hatokanyaga tena nyumba hii na mauchawi yake”
“Dah! Nashindwa kuamini kwakweli maana mi ninavyomuona Jane ni wa kawaida tu”
“Kwani unafikiri mchawi ukimuona unamjua kwa haraka hivyo? Huwezi kumjua sababu anakuwa ni mtu wa kawaida tu halafu wanajifanyaga wana roho nzuri balaa kumbe roho zao ni za kichawi. Kwakweli mume wangu tunatakiwa kushukuru sana uwepo wa huyu Neema humu ndani”
Kisha Sopy akamuomba mumewe waende sebleni wakapate chakula cha usiku,
“Ila najisikia kushiba sijui kama nitaweza kula”
“Sasa ungependa chakula gani kwa usiku huu?”
“Labda ningepata mkate tu na chai au maandazi tu na chai maana nimeshiba mke wangu”
“Basi twende tukanunue mkate, tuchemshe chai tunywe mume wangu”
Wakakubaliana kufanya hivyo, kisha kwa pamoja wakatoka mule chumbani.
Walipofika sebleni walimkuta Neema akiwa pale pale kwenye Tv ila alipowaona tu akawakaribisha waende mezani, Sophia akamuuliza alichoandaa
“Itakuwa vyema kama mkisogea pale wenyewe muone nilichowaandalia”
Sophia akamshika mumewe mkono na kwenda nae mezani ambapo walikuta Neema amewaandalia maandazi na chai, Sophia akatabasamu na kumwambia mumewe
“Hakuna haja tena ya kwenda dukani mume wangu kwani chakula ulichohitaji kipo tayari”
“Amejuaje kama tunahitaji chakula cha hivi muda huu?”
“Labda kwavile kaona tumekula jioni”
Kisha Sophia akamsihi mumewe akae pale mezani na waweze kula kile chakula ambapo Ibra alifanya hivyo na kukaa pale mezani halafu wakaanza kula ila Ibra alimuuliza Sophia kuwa huyo Neema amekula muda gani,
“Ngoja nimuite umuulize mwenyewe”
Sophia akamuita Neema ambaye aliwafata pale mezani na kuwasikiliza walichomuitia, Ibra akamuuliza Neema
“Mbona huji kula na sisi?”
“Mimi nimekula jikoni kwahiyo sina njaa tena”
“Usije sema tunakutenga, tafadhari siku nyingine tuwe tunakula pamoja umesikia Neema”
“Sawa msijali nimewaelewa tutakuwa tukila pamoja ila tatizo ni kuwa hamtashiba”
“Hatutashiba kivipi?”
Neema akacheka na kujibu kamavile mtu anayetania,
“sababu nakula sana”
Sophia akacheka pia na kumwambia,
“Ungekuwa unakula sana si vyakula vingekuwa vimeisha humu ndani jamani, Neema bhana tuwe tunakula pamoja ndio vizuri”
“Sawa dada nimekuelewa nitakuwa nafanya hivyo”
Kisha akarudi tena kwenye kuangalia Tv na kuwaacha Sophia na ibra wakiendelea kula.
Walipomaliza kula, Ibra akamwambia mkewe kuwa anaona vyema yeye akalale tu kwani amejawa na uchovu sana,
“Sawa mume wangu,na mimi nitakuja kulala muda sio mrefu”
Ibra akaenda chumbani kisha Sophia akaenda sebleni kukaa na Neema huku akijaribu kumuuliza kuwa ameionaje siku,
“Neema siku ya leo umeionaje na maisha ya humu ndani umeyaonaje kwa ujumla?”
“Nimeipenda na kuifurahia sana siku ya leo kwani inaonyesha wazi kuwa maisha yangu humu ndani yatakuwa ni yenye furaha”
“Na vipi ule ujio wa Yule Jane?”
“Yule hawezi kuja tena hapa, popote ninapokuwa hakuna mtu mbaya anayeweza kusogea ndiomana Yule alikimbia mwenyewe maana asingeweza kukaa na mimi karibu”
“Nafurahi kusikia hivyo maana alikuwa ananikera sana Yule binti, ngoja nikutakie usiku mwema ingawa sijui utaenda kulala saa ngapi”
“Muda sio mrefu na mimi nitaenda kulala hata usijali dada”
Sophia akaelekea chumbani ambapo alimkuta mumewe akiwa amelala hoi kabisa kisha nae akajiunga kwenye kulala pembeni ya Ibra.
Usiku wa manane Ibra alishtuka kutoka usingizini ambapo alihisi kamavile tumbo lake limevurugika hivyo akaamka na kukaa kitandani ila aliona ni vyema anywe maji hivyo akainuka na kuelekea jikoni ili akachukue maji. Ila alipofika sebleni alishangaa kumuona Neema akiangalia Tv ila kwavile mkewe alimwambia kuwa Neema anapenda sana Tv hakushangaa zaidi ila aliona ni vyema amuulize kuwa hana usingizi au imekuwaje.
Ibra akamsogelea Neema na kumuuliza,
“Vipi mpaka saizi, huna usingizi?”
Neema aliinua sura yake na kumuangalia Ibra, kwakweli Ibra hakuweza kumtazama Neema mara mbili kwani macho ya Neema yalikuwa yakiwaka moto na kumfanya Ibra apige kelele za uoga kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
Itaendelea kama kawaida……!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 17
Neema aliinua sura yake na kumuangalia Ibra, kwakweli Ibra hakuweza kumtazama Neema mara mbili kwani macho ya Neema yalikuwa yakiwaka moto na kumfanya Ibra apige kelele za uoga kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Ila kelele zile za Ibra hazikufika popote zaidi ya kuishia mule mule ndani kwani Ibra alianguka chini muda huo huo na kuwa kama mtu aliyepatwa na usingizi mzito sana.
Mtu ambaye alishtuliwa na kelele zile alikuwa ni Sophia ambaye alishtuka usingizini ila alijikuta gafla hajali kuhusu zile kelele na kumfanya ajigeuze na kulala vizuri zaidi ambapo nay eye alipatwa na usingizi mzito kushinda wa mara ya kwanza.
Alipopitiwa na ule usingizi safari hii Sophia alipatwa na ndoto ambapo alijiona mahali na mbele yake alimuona mtoto mdogo ambaye sura yake ilionekana kufanana nae sana kitu kilichomfanya Sophia amwite Yule mtoto ‘mwanangu’ ila alipojaribu kumsogelea Yule mtoto alisogezwa mbele zaidi, kisha kuna sauti ikamwambia Sophia,
“Ni kweli mtoto huyu ni mwanao ila hautaweza kumshika wala kumgusa zaidi zaidi utakuwa unamuona tu wakati umelala”
Sophia akajikuta akihoji kwenye ile ndoto peke yake,
“Kwanini nisiweze kumshika wala kumgusa wakati ni mwanangu mwenyewe?”
“Pole sana Sophia, ila hii ni zawadi yetu sisi. Tunapenda sana watoto”
Sophia alijikuta akiumizwa sana kwani kila alipoitazama sura ya Yule mtoto ilionyesha simanzi kubwa, iliyomfanya Sophia asiweze kukubaliana na ile hali kwahiyo akaanza kumfata Yule mtoto ambapo alishtuka usingizini kabla ya kumkaribia Yule mtoto na tayari palikuwa pameshakucha.
Sophia alikaa kitandani akitafakari kuhusu ile ndoto na je kwake ilikuwa na umuhimu gani, alijikuta akilishika tumbo lake na kusema,
“Uwe salama mwanangu, nakupenda sana”
Kisha akamuangalia Ibra aliyekuwa hoi na usingizi na kumfanya amuamshe kwani muda wa kujiandaa kwenda kazini ulikuwa umewadia, Ibra alishtuka sana ila alionekana kuwa na uchovu uliopitiliza, Sophia akamuuliza mumewe
“Kheee mbona umechoka sana mume wangu?”
“Dah yani hata sijielewi kwanini nimechoka hivi”
Kisha akainuka na kwenda kuoga halafu akarudi kuvaa ila kuna vitu vilionekana kumweka kwenye mawazo sana, alijikuta akijiuliza kuwa alichokiona usiku wa jana kilikuwa ni kweli au ni ndoto tu iliyompitia, akajikuta akisema kwa sauti
“Kama ilikuwa ni kweli basi nilichukua maamuzi gani? Na kama ni ndoto kwanini nilipiga kelele? Au zile kelele nazo zilikuwa ni ndoto?”
Ibra alikosa jibu ila kwavile Sophia alimsikia Ibra anachojihoji aliamua kumuuliza kuwa ni kitu gani ambapo Ibra kabla ya kujibu akamuuliza Sophia,
“Hakuna kelele zozote ulizozisikia usiku Sophy?”
“Kuna kelele nilizisikia usiku tena ilikuwa kama sauti yako hivi”
“Sasa ulipozisikia ulichukua hatua gani na mimi nilikuwa wapi kwa wakati huo?”
“Nilishtuka kutoka usingizini ila wewe nilikuona pembeni yangu ukiwa hoi na usingizi hivyo nami nikajigeuza na kuendelea kulala. Kwani ni vipi mume wangu?”
“Hakuna kitu mke wangu ila akili yangu ikiwa sawa nitaweza kueleza kile ninachofikiria kichwani”
Sophia ilibidi amkubalie tu mumewe kwani kumpinga pinga alishachoka tayari, kwavile Ibra alikuwa kashamaliza kujiandaa akamuomba tu mkewe amsindikize nje kama kawaida yao.
Ibra na Sophia walitoka hadi sebleni ambapo walimkuta Neema kisha kusalimiana nae na Ibra kuwaaga ila Neema akamuomba kitu,
“Kaka kabla hujaondoka itakuwa ni vyema ukanywa chai kwanza, leo nimeamka mapema sana ili nikuandalie chai naona unashinda na njaa kwa muda mrefu”
“Dah asante Neema ila nimechelewa muda huu”
Sophia nae ikabidi aanze kumsisistiza mumewe,
“Kwani kunywa chai inachukua muda gani Ibra jamani, si ungekunywa tu ili uwe na nguvu huko uendako jamani mume wangu!”
“Ni kweli msemayo ila naomba chai nianze kunywa kesho maana leo nimeshachelewa”
“Jamani kaka sio vizuri hivyo jamani, yani nimeandaa kwaajili yako”
“Nisamehe bure Neema”
Kisha Ibra akaenda kufungua mlango na kuondoka kwani hakutaka kuendelea kukaa hapo ili wasije kumpa vishawishi zaidi wakati tayari alikuwa na mawazo yake kichwani.
Ndani alibaki Sophia na Neema ambapo Sophia akasema ni vyema hiyo chai akanywe yeye ila Neema akamkataza na kumwambia yak wake bado hajamuandalia.
“Hakuna shaka Neema ila chai si chai tu!”
“Yeah chai ni chai tu ila kuna chai bora kwa mama mjamzito, tulia nikuandalie. Sitaki unywe hii sababu utashiba na kushindwa kunywa chai bora kwaajili yako, subiri nikuandalie dada na mwenyewe utafurahia”
Sophia hakuhoji sana kisha akaelekea chumbani kwa lengo la kuoga na kuweka chumba chao vizuri.
Ila alipokuwa chumbani alifikiria sana kwani hakuona kama kunakuwa na tofauti ikiwa kuna wajawazito wanaokunywa chai za pamoja na familia zao, akajiuliza sana kuwa kwanini Neema amemkataza kunywa ile chai ila hakupata jibu, kwa upande mwingine alihisi kuwa pengine kuna kitu ambacho Neema ameweka kumdhuru mume wake ila akajiuliza kwanini amdhuru maana hakuona kama kuna sababu yoyote kwa Neema kufanya hivyo, ikabidi apuuzie yale mawazo yake.
Alipomaliza shughuli zake alitoka na kumkuta Neema kama kawaida akiwa amekaa kuangalia Tv, ila kabla nay eye hajakaa kujumuika na Neema akamwambia kuwa asikae kwanza aende mezani kwa lengo la kunywa chai ambapo Sophia alifanya hivyo na kukuta akiwa ameandaliwa chai ya maziwa na chapati psmoja na nyama ya kurosti. Sophia alikunywa kisha akarudi kukaa sebleni na kumuuliza maswali Neema,
“Samahani Neema kuna kitu naomba nikuulize”
“Niulize tu dada hakuna tatizo”
“Hivi maziwa yamenunuliwa muda gani humu ndani? Inamaana Ibra analeta vitu bila ya kuniambia?”
“Mbona maziwa yapo mengi dada ndiomana mimi nimeyapika tena kwa afya yako ni vizuri sana ukinywa mara kwa mara”
“Swala ni kwamba yaliletwa lini? Unajua hujawahi kunidai hela ya mboga hata siku moja ila kila siku tunakula vizuri tu je hizi mboga zinatoka wapi na huyo Ibra kazileta muda gani?”
Safari hii Sophia hakujibiwa chochote ila gafla akapatwa na usingizi na kulala pale kwenye kochi kwani usingizi ule ulikuwa ni usingizi mzito sana.
Ibra alifanya shughuli zake leo huku akiwa na mawazo sana, alijikuta akiwaza mambo mbali mbali haswa lile swala la kuona macho ya Neema yakitoa moto lilimkosesha raha kwani alizidi kujiuliza kuwa ile ilikuwa ni ndoto au ni kitu gani, swala la Jane kukimbia pia lilimpa mawazo na kumfanya awahi kufunga shughuli zake siku hiyo ili aweze kwenda kwakina Jane kuzungumza nae kuhusu kilichomkimbiza kiasi kile.
Alipomaliza tu kufunga, aliingia kwenye gari yake na safari yake ilikuwa moja kwa moja kwakina Jane ambapo alimkuta Jane akiwa ametulia tu nje kwao, kisha akamuita pembeni na kusalimiana nae halafu kuanza kuzungumza kuhusu jambo lililompeleka mahali pale.
“Jane kwanza kabisa samahani kwa kilichotokea jana kwani sikutarajia kama ungekimbia kiasi kile”
“Nisamehe mimi kaka ila kwakweli sikuweza kuendelea kuwepo pale kwenu na sidhani kama nitaweza kuja tena”
“Hebu niambie kwanza kilichokukimbiza wewe ni nini, na kwanini ulishikwa na uoga kiasi kile? Na kwanini useme huwezi kuja tena pale kwetu?”
“Siwezi kuja kwasababu ya Yule mgeni wenu siwezi kabisa yani siwezi”
“Ndio uniambie kwanini?”
“Siwezi tu, nadhani damu yake na yangu haviendani”
“Hebu Jane niambie ukweli maana kwa mujibu wa Yule binti ndani ni kuwa wewe ni mchawi”
Jane akacheka kicheko cha mshangao na kusema,
“Kheee mimi mchawi! Huo uchawi niutolee wapi mimi ikiwa hata mama yangu hajui kuhusu uchawi? Mimi mwenyewe narogwa je mchawi huwa na yeye anarogwa? Hapa nilipo huwa naonekana sijielewi sababu nimesharogwa sana. Na kama amewaambia hayo maneno Yule mgeni wenu basi jueni kwamba yeye ndio mchawi na sio mtu mzuri kabisa.”
“Kwanini unasema hivyo na nipe sababu ya kukimbia kwako”
“Sikia kaka nikwambie kitu, mimi sina akili ya darasani ila nina akili ya maisha, na akili hii nimeipata kwa kuangalia maisha ya watu mbalimbali na kusoma makala mbalimbali. Mimi ni mpenzi wa kusoma hadithi za kutisha na kusisimua ila humo nimejifunza vitu vingi sana. Kuna makala mengi huwa yanaeleza kuwa unapokutana na mtu mbaya kwa mara ya kwanza basi mwili wote husisimka na nywele kusimama. Sasa mimi nilipomuona Yule mgeni wenu hiyo hali ndiyo imenikuta kwa mara ya kwanza katika maisha yangu na aliponiangalia nilihisi kutetemeka mwili mzima ndiomana sikuweza kukaa pale na kuamua kukimbia”
“Kwamaana hiyo Yule ni mtu mbaya?”
“Sijui kwa nyie mnamuonaje ila kwa mie hapana kwakweli Yule si mtu wa kawaida, sijawahi kupatwa na ile hali katika maisha yangu yani ilikuwa ndio mara ya kwanza. Nakumbuka mama alinifundisha kuwa nikikutana na kitu kibaya niondoke eneo lile huku nikiomba Mungu anisaidie maana siwezi jua kuwa kitanipata nini na ndivyo nilivyofanya”
“Bado sikuelewi Jane kwahiyo Yule ni mtu mbaya mule ndani?”
“Mmh kwani nyie mmemtoa wapi kaka?”
Ikabidi Ibra amueleze Jane jinsi yeye na mkewe walivyokutana na Neema na mpaka kumkaribisha nyumbani kwao na kuamua kuwa awe mdada wa kuwasaidia kazi za ndani.
“Mmmh kaka kweli kabisa mnamchukua mdada wa kazi ambaye hamfahamu hata nyumbani kwao je akipata matatizo mtafanyaje?”
“Kwakweli hatuna la kufanya kwani ilikuwa ni katika kumsaidia ukizingatia kasema kuwa ndugu zake hawamtaki, na sijui katokea kijiji gani huko”
“Basi kabla ya yote mlitakiwa mumpeleke kwa mjumbe ili ajue kuwa kuna mtu asiye na kwao mnaishi nae na lolote likiwapata mtakuwa salama maana mlishatoa taarifa. Maisha yanataka umakini sana, unamchukua mtu awapikie, awafulie, aangalie nyumba yenu halafu hamjui kwao mnategemea nini? Kuna mtu duniani asiye na kwao? Mngeenda kwanza kwa mjumbe”
“Ila Jane umeniambia jambo la msingi sana ambalo hata sikulifikiria kabisa, licha ya kusema ni mtu mbaya na nini na nini ila hilo swala la kwa mjumbe ni la muhimu sana ambalo nilikuwa nimelisahau kabisa yani. Asante mdogo wangu.”
“Hata usijali kaka ila mimi kuja kwenu tena hapana, ila ngoja kuna kitabu nikuletee ukakisome unaweza kuwa na mawazo mapya ya maisha”
Jane akaelekea ndani kwao na kutoka na kitabu kidogo kisha akamkabidhi Ibra, kitabu kile kiliandikwa juu yake “Fahamu kuhusu majini” Ibra akashtuka sana na kumuuliza Jane,
“Unamaana gani kunipa hiki kitabu! Hivi unajua kuwa majini ni viumbe wa ajabu sana ambao huwezi kustahimili kukutana nao! Au unamaana kuwa Neema ni jinni? Uliona wapi jini anapika, anaosha vyombo, anafua, analala uliona wapi?”
Kisha Jane akakichukua tena kile kitabu na kumwambia Ibra,
“Hiki kitabu ni tofauti kabisa na unavyokifikiria lakini najua ipo siku utakihitaji na utakisoma na kukielewa, kwa leo acha nikae nacho mwenyewe ila zingatia swala la kwenda kwa mjumbe kwanza”
Jane akamuaga Ibra na kurudi ndani kwao kwani hakutaka kuongea nae zaidi halafu alihisi kama kichwa kikimgonga hivi.
Ibra alirudi kwenye gari yake na kupanda huku akitafakari kwa muda kabla ya kuondoka pale kwakina Jane kwani lile wazo la Jane la kumshauri kuwa wampeleke Neema kwa mjumbe kwanza lilikuwa likifanya kazi katika akili yake, kisha akataka kuondoa gari yake ili aondoke ila kabla ya kuondoka kuna mdada alitoka ndani kwakina Jane na kumfata Ibra na kuanza kumgongea kwenye kioo ambapo ikampasa Ibra afungue kioo cha gari yake ili amsikilize ila Yule dada aliongea kwa kufoka,
“Umemfanya nini Jane?”
“Kumfanya nini kivipi?”
“Katoka kuongea na wewe hapa karudi ndani analalamika kuwa kichwa kinamuuma sana na analia tu”
Ibra akashangaa sana na kumfanya ashuke kwenye gari kisha kuongozana na Yule dada mpaka ndani ambapo Jane alionekana akigalagala chini huku akilalamika kuhusu maumivu ya kichwa, Ibra akatoa wazo kuwa ni vyema wakampeleka hospitali hivyo akasaidiana na Yule dada ili wamkongoje waende nae huko hospitali ili kujua kinachomsumbua Jane ni kitu gani.
Wakati wanatoka akatokea mama Jane na mmama mwingine ambao kwa pamoja walishangaa na wakaelezwa hali halisi ya Jane na kuwa wanamuwaisha hospitali ila Yule mama mwingine alisema Jane arudishwe ndani ili aweze kumfanyia maombi ambapo Ibra hakuweza kupingana nao kisha wakamrudisha Jane ndani kisha Ibra alitoka nje na kuwaacha.
Ibra akiwa nje alijiuliza maswali mengi sana kuwa wale watu wako vipi yani wanathamini sana maombi kuliko afya ya ndugu yao, akatingisha kichwa kwa kusikitika.
“Badala mtu wamuwaishe hospitali eti wenyewe wanataka wamuombee kwanza, ngoja niondoke zangu mie”
Ibra akarudi kwenye gari yake kisha akaondoka eneo lile na kuelekea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake aliona nyumba ikiwa kimya sana kanakwamba ndani hapakuwa na mtu yeyote, kisha akaingiza gari na kufungua mlango wa sebleni ambao ulifunguka kama kawaida na kuingia ndani. Akamuona mkewe akiwa amelala hoi kwenye kiti tena alionekana hajitambui kabisa, kisha Ibra akamuuliza Neema bila hata ya salamu
“Vipi huyo kafanyaje?”
Neema alimuangalia Ibra bila ya kumjibu kitu chochote na kufanya Ibra amuulize tena,
“Neema si naongea na wewe, kafanyaje huyo?”
Safari hii Neema naye alimuuliza swali Ibra ila swali lake lilikaa kibabe sana na alionekana kujiamini kupita maelezo,
“Na wewe unataka?”
Ibra alijikuta akitetemeka kwa uoga huku akihofia kitu ambacho anaweza kufanyiwa na huyo Neema kwani alikosa ujanja gafla.
Itaendelea kama kawaida………..!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 19
Akatoka hadi sebleni ambapo aliangaza macho yake huku na kule ili kumuona Neema ila hakumuona na kumfanya ashangae kwani kawaida ya Neema ni kukaa pale sebleni akiangalia Tv, Ibra alipotazama Tv aliikuta ikiwaka na kuona kuwa ile ni sababu tosha ya kumtimua Neema kuwa anaachaje Tv inawaka wakati yeye hayupo pale sebleni.
Ibra akasogea sasa karibu, alipotazama kwenye kochi alishtuka sana baada ya kuona kuna nyoka amekaa juu ya kochi akiwa amejiviringisha na kichwa amekiinua juu.
Kwakweli Ibra aliishiwa na ujasiri gafla na kujikuta akipiga kelele kwani hakujua afanye kitu gani kwa muda huo, kelele za Ibra zilimshtua Sophy na kumfanya atoke mbio ili ajue kuwa mumewe amepatwa na nini ila nae alipofika pale sebleni alipatwa na uoga wa hali ya juu baada ya kumuona Yule nyoka kwenye kochi na kujikuta akimkumbatia mumewe kwa nguvu huku akiita jina la Neema kanakwamba wanamuhitaji Neema aweze kuwasaidia.
Muda kidogo Neema alitokea na moja kwa moja akamuamuru Yule nyoka atoke nje, kisha akaenda kufungua mlango ambapo Yule nyoka alijitoa pale kwenye kochi na kutoka nje kidsha Neema akafunga mlango na kuwatazama Ibra na Sophia ambao walikuwa kimya kabisa kwani walikuwa wakitetemeka kwa uoga.
Kisha Neema akawaambia kwa kujiamini
“Njooni mkae tuzungumze”
Sophia akadakia,
“Hapana Neema, labda utueleze kwanza Yule nyoka katokea wapi?”
Neema akacheka na kuwaambia,
“Yule sio nyoka ni mtu”
Wote wawili wakashangaa kuwa ni mtu kivipi, kisha Neema akaendelea kuwaeleza,
“Yule ni Jane”
Sophia na Ibra wakashtuka sana kwani hawakutegemea kabisa kuwa Yule nyoka anaweza kuwa Jane, kwahiyo wakauliza
“Ni Jane kivipi?”
“Yote kayataka huyu kaka Ibra, aliyekutuma leo uende kwakina Jane ni nani? Na huyu nyoka alikuja kwa lengo la kuwadhuruu, mshukuru sana uwepo wangu.”
Ibra akashangaa kiasi kuwa huyu Neema amejuaje kuwa yeye alienda kwakina Jane na iweje Jane ajigeuze nyoka wakati alishasema kuwa huyu Neema si mtu mzuri, akajikuta akikosa swali wala jibu. Ni Sophia pekee aliyeweza kuuliza zaidi,
“Inamaana hatorudi tena?”
“Hawezi kurudi kwasababu mimi nipo”
Kisha Ibra akamshika mkewe na kurudi nae chumbani huku akiwa na mawazo lukuki.
Wakiwa chumbani Sophia aliamua kumuuliza Ibra,
“Mume wangu huko kwakina Jane ulienda muda gani? Ni nani aliyekushauri uende huko jamani! Mbona unapenda kutafuta matatizo Ibra? Hivi uambiwe na nani kuwa Jane sio mtu mzuri ndio uamini jamani mmh!”
Ibra alikuwa kimya kwanza kwani bado kuna mambo mengi sana yalikuwa yakizunguka akili yake haswa kuhusu huyu Neema na Jane je ni nani wa ukweli kati yao? Ila kwa upande mwingine alimuamini zaidi Jane kuliko Neema, kisha akapanda kitandani na kulala bila ya kuongea ya zaidi na mkewe, hivyo akamfanya Sophia nae apande kitandani na kulala pia.
Wakiwa wamelala, Ibra akajiwa na ndoto ambapo kwenye ndoto ile alikuwa akiona vitu ambavyo vipo kwenye nyumba yao, kwanza kabisa alijiona yupo ndani na kutoka sebleni ambapo akamuona Neema mmoja akiwa jikoni na Neema mwingine akiwa sebleni na gafla Yule Neema wa sebleni akageuka na kuwa nyoka kisha Neema wa jikoni akatoka na kumfukuza Yule nyoka halafu akamuangalia Ibra na kutabasamu kisha akamwambia,
“Mimi ndio Neema, kunikwepa huwezi…….”
Ibra akashtuka kutoka usingizini huku akihema ila akaisikia sauti ya Neema ikiendelea kuongea,
“Na kunifukuza pia huwezi, nimejipa jina hili kwa makusudi kwani huwezi ukaniepuka kamwe”
Kisha akasikia kicheko cha Neema ambapo Ibra akajawa na hofu sana huku akimuamsha mkewe ili nae aweze kusikia ila Sophia alipoamaka hakusikia chochote kwani hata ile sauti ya kicheko haikuendelea tena, Sophia akamuuliza mume wake
“Tatizo ni nini mume wangu jamani?”
“Sophia mke wangu haya ni majanga”
“Majanga! Majanga kivipi?”
“Nimeota ndoto mbaya sana ila yenye uhalisia ndani yake”
“Uhalisia kivipi na ni ndoto gani?”
“Sophia mke wangu, sijielewi sijielewi kabisa. Hebu angalia saa hapajakucha kweli?”
Sophia akaangalia muda na kumwambia mumewe,
“Ni saa nane kamili mume wangu”
“Dah muda hata hauendi pakuche jamani, mimi hata sijui kama nitaweza kulala tena, nitakaa macho tu”
“Hapana usikae macho tulale, hizo ni ndoto tu. Hivi unakumbuka kipindi kile mimi nilipokuwa nikiota ota ulikuwa unaniambiaje Ibra? Basi jua kwamba hizo ni ndoto tu hata zisikupe mawazo tulale mume wangu”
“Tatizo huelewi kuhusu hizi ndoto mke wangu”
“Hata wewe ulikuwa huelewi pia kuhusu ndoto nilizokuwa naota mimi ila napenda kukwambia tena mume wangu kuwa hizo ni ndoto tu zisikutishe”
Sophia alijitahidi kumshawishi mumewe ili waendelee kulala ambapo Ibra nae alijitahidi aweze kulala ila usingizi ulimpiga chenga kwa muda huo.
Kulipokucha kama kawaida, Ibra aliamka na kwenda bafuni kuoga ila kila alipokuwa akioga na kufumba macho aliona sura ya Neema na kumfanya apate hofu kama aliyoipata majuzi yake hivyo akatoka bafuni kwa haraka sana na kumuamsha mkewe ili angalau avae huku akizungumza na mke wake.
Sophia aliamka na kumtazama mume wake ambaye alionekana hata kuoga hakuoga vizuri siku hiyo,
“Ila oga yako siku hizi mume wangu majanga tupu, unatoka na povu jamani”
“Sophia naamini kuna muda utanielewa tu mke wangu”
“Kunieleza hutaki sasa sijui nitakuelewaje”
“Nitakueleza tu hata usijali”
Sophia akamuangalia mume wake kwa makini sana ila hakuweza kumwambia zaidi kwani alijua ni wazi hapendi kuulizwa sana kitu ambacho alisema atamueleza. Kisha Ibra akamwambia Sophia kuwa amsindikize nje kwani ndio alikuwa akienda kwenye shughuli zake ambapo Sophia alifanya hivyo na walipofika sebleni tu ikawa kama jana kuwa Neema alishaandaa chai ili Ibra anywe na akamuomba afanye hivyo kabla ya kuondoka,
“Hapana Neema nimeshachelewa”
“Unajua hata usiku hujala kaka!”
“Naelewa ila hata usijali”
Kisha Ibra akatoka nje na kufuatiwa na mkewe ambaye alitoka nae hadi nje kabisa akimwambia asubiri alitoe gari kwanza, na alipolitoa gari tu alimwambia mkewe apande ili azungumze nae kidogo ambapo Sophia alifanya hivyo,
“Sophy mke wangu, mimi naenda kwenye shughuli zangu ila tu nakuomba kuwa makini sana na huyu Neema, kuwa nae makini kwenye kila kitu kuanzia chakula anachokupikia yani kila kitu. Nakupenda mke wangu, kuna mengi tu nahitaji kuyafatilia kwa undani kuhusu huyu mtu humu ndani”
Kisha akamuaga mke wake na kumbusu kwenye paji la uso, ambapo Sophia akashuka kwenye ile gari halafu yeye akaondoka zake.
Sophia alirudi ndani na kumkuta Neema akiwa kimya pale sebleni ambapo jambo la kwanza kabisa Neema akamuuliza Sophia alichokuwa akizungumza na Ibra,
“Mmh Neema ni mambo ya kawaida tu ya kifamilia”
“Ila hata mimi ni mmoja ya wanafamilia yenu kwahiyo natakiwa kujua vyote vinavyoendelea humu ndani, natakiwa kufahamu kila kitu”
“Hakuna tatizo ila utafahamu taratibu”
“Napenda kuwekwa wazi na kila kinachoendelea hapa ndani, haijalishi amekwambia kuhusu nini ila unapaswa kunieleza”
Kwavile Neema alionekana kumng’ang’ania Sophia amueleze ikamfanya Sophia aamue kuwa kumweleza ukweli vile ambavyo amezungumza na mumewe kwenye gari, Sophia alipomaliza tu kumueleza alishangaa Neema akicheka na kusema,
“Nimefurahi sana kuona Sophia unasema ukweli, basi nakuahidi kuendelea kushirikiana na wewe bega kwa bega na wala usiwe na hofu juu yangu kama unavyoambiwa na mumeo. Tafadhari yapuuzie maneno yake, kinachomsumbua zaidi ni kuwa anafika kwakina Jane na wanamuharibu kisaikolojia”
Sophia akatabasamu tu ingawa kiukweli hakupenda kumwambia Neema kile alichozungumza na mumewe ila ndio hivyo alikuwa ameshamwambia.
Ibra akiwa katika shughuli zake, kuna rafiki yake alipita na kujikuta akizungumza nae mawili matatu kwani hawakuonana kwa kipindi kirefu sana. Pia rafiki yake alimdokeza kuhusu biashara mpya ambayo inaingiza sana faida na kumfanya Ibra atamani kuhusu biashara hiyo kwani alipenda sana kujaribu vitu kwaajili ya kujiongeze kipato tena ukizingatia kuna mambo mengi yaliingia katikati na kufanya pesa yake iyumbe kwahiyo alifurahi sana kuonana na huyo rafiki yake na kuelezewa kuhusu hiyo biashara.
Rafiki huyu wa Ibra alitamani sana kupafahamu nyumbani kwa rafiki yakekwanza kwani toka amehamia huko hakuwahi kufika,
“Utapafahamu tu Lazaro hata usijali”
“Tena ikiwezekana iwe leo ndugu yangu si unajua duniani hapa mambo mengi sana!”
“Yeah naelewa, basi tutapita mara moja upafahamu kisha twende huko kwenye biashara unayosema.”
“Sawa hakuna tatizo na kwa hakika hii biashara utaipenda sana ndugu yangu”
Wakakubaliana na kuondoka mahali hapo wakielekea nyumbani kwa Ibra kwanza kisha waende kwenye hiyo biashara ambayo Ibra aangalie inavyokwenda na kama ataweza kuifanya na kuendelea kujiongezea kipato.
Walipofika nyumbani kwa Ibra kwakweli Lazaro alishangaa sana ile nyumba ya rafiki yake kuwa kapata wapi pesa ya kuweza kumiliki nyumba yote ile,
“Mjini mipango Lazaro”
“Kweli mjini mipango yani kwa stahili hii mmh! Nimeshangaa kwakweli maana sio kawaida kabisa. Nakumbuka nilikuwa na uwezo kukuzidi ila nyumba yangu mimi ni ya kawaida tu ila mwenzangu upo kwenye mjengo wa maana. Hongera sana kaka”
“Nashukuru ndugu yangu, karibu sana”
Walishuka kwenye gari na kisha Ibra akafungua mlango wa ndani na kumkaribisha Lazaro ndani ambapo walimkuta Sophia na Neema wakiwa sebleni wamekaa kama kawaida, Ibra akawasalimia ila Lazaro alimsalimia Sophia tu ambapo Ibra akamshtua kuwa huyu mwingine hajamuona ila Lazaro akahamaki tu,
“Yupi huyo?”
“Inamaana humuoni hapo?”
Ibra alimuonyesha alipo Neema ila Lazaro bado hakuonyesha kama amemuona mtu yeyote eneo hilo na alikuwa akimshangaa tu Ibra huku akimwambia,
“Hebu acha masikhara Ibra unataka nimsalimie nani tena wakati nimemuona shemeji tu”
Sophia akamaliza mjadala kwa kuwakarabisha wakae, ila bado ibra hakulizishwa na hali ile na kufanya ajaribu kumuuliza kitu Neema aone kama kweli Lazaro hajamuona huyu Neema.
“Neema hujamuona huyu mgeni na wewe?”
Neema akamtazama tu Ibra bila ya kumjibu chochote huku maongezi mengine yakiendelea pale sebleni ambapo Lazaro aliwalalamikia kuwa nyumba yao inaonekana kuwa ni nzito sana,
“Hii nyumba ni nzuri ila ni nzito sana”
“Nzito kivipi?”
“Mnatakiwa mtafute watu wa maombi ili muifanyie maombi nyumba yenu ikae sawa”
Sophia akaguna na kuuliza,
“Mmh maombi tena?”
“Ndio maombi ni muhimu sana maana naona nyumba yenu ni nzito jamani”
Ibra akamtazama mkewe kisha akamtazama Neema ambaye alionekana yupo makini sana kutazama Tv, kisha Ibra akamuuliza Neema
“Unasikia kinachoongelewa huku?”
Neema alikuwa kimya tu na alimuangalia kisha akaendelea kuangalia Tv, Ibra akachukia sana na kumfanya ainuke na kwenda kuzima Tv moja kwa moja kwenye soketi ya kuingiza umeme kisha akarudi tena kukaa.
Ila Lazaro nae aliaga na kumuomba aende nyumbani kwake, Ibra akamuuliza kuhusu wao kwenda kule kwenye biashara.
“Sitaweza kwenda tena maana hapa nilipo kichwa kimeanza kunigonga naomba niondoke tu”
Lazaro akainuka na kufanya Ibra nae ainuke ili amsindikize, walipotoka nje Lazaro alionekana kuwa na kizunguzungu kikali sana ambapo ilibidi Ibra ampakie kwenye gari yake na kuitoa nje kabisa huku akitaka kumpeleka hospitali ila Lazaro aligoma na kuhitaji kurudishwa tu nyumbani kwake ambapo ikabidi Ibra afanye hivyo.
Sophia alibaki ndani na Neema huku akijiuliza kimoyomoyo kuwa kwanini Neema alikuwa hamjibu chochote Ibra halafu bado alionekana kimya kabisa ingawa Tv ilikuwa imezimwa na Ibra kwa hasira.
Sophia aliamua kumuongelesha yeye sasa ili aone kama atajibiwa kitu chochote,
“Neema mbona kimya sana mdogo wangu?”
Neema alikuwa kimya tu hakujibu chochote kile na kumfanya Sophia azidi kumshangaa kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Neema kufanya hivyo. Sophia akainuka pale alipokaa na kusogea alipo Neema ili kumshtua kwa kumshika kabisa, ila aliposegea ili amguse gafla akashangaa kuwa pale hapakuwa na mtu yoyote yani Neema hakuonekana gafla.
Kwakweli Sophia alipigwa na butwaa kwani muda wote alikuwa akimuona Neema mahali hapo halafu tena gafla Neema ametoweka, alijikuta akitetemeka tu na kuwa kama mtu asiyejielewa.
Itaendelea kama kawaida………………….!!!!!!!
NYUMBA YA MAAJABU: 20
Neema alikuwa kimya tu hakujibu chochote kile na kumfanya Sophia azidi kumshangaa kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Neema kufanya hivyo. Sophia akainuka pale alipokaa na kusogea alipo Neema ili kumshtua kwa kumshika kabisa, ila aliposegea ili amguse gafla akashangaa kuwa pale hapakuwa na mtu yoyote yani Neema hakuonekana gafla.
Kwakweli Sophia alipigwa na butwaa kwani muda wote alikuwa akimuona Neema mahali hapo halafu tena gafla Neema ametoweka, alijikuta akitetemeka tu na kuwa kama mtu asiyejielewa.
Akiwa anajitetemekea pale mara akamuona Neema akitoka chumbani na kuja pale sebleni na ndio hapo uoga ulipomzidia na kujukuta akishindwa kustahimili na kuanguka chini na kuzimia.
Sophia akiwa amezimia alijiona sehemu ya mbali sana, alijiona mahali akiwa amekaa mwenyewe halafu mbele yake aliwaona watoto watatu wakimuangalia kwa huruma sana na kumfanya nay eye apatwe na huruma kisha akainuka pale alipokuwepo na kuanza kuwafata ila kila alipowasogelea nao walizidi kwenda nyumba kisha akajikuta akisogea na kusogea bila ya kuwafikia na kumfanya sura yake ikiingiwa na simanzi zaidi.
Muda kidogo akajikuta ameshtuka na kujiona yupo sebleni kwenye kiti huku pembeni yake akiwepo Neema ambaye alimpa pole baada ya kushtuka, kisha Sophia akamuuliza Neema kuwa ni kitu gani kilitokea
“Sijui ni kitu gani dada ila ulianguka gafla tu”
Sophia alijaribu kuvuta kumbukumbu nyuma ili kuweza kukumbuka kilichomtokea ila hakuweza kukumbuka kitu chochote kile, alijikuta akiangaza tu macho yake huku na kule ila Neema alimuomba anyanyuke na aende kula chakula cha mchana ili kupata nguvu kwavile alikuwa hajala chochote toka alivyokula asubuhi.
Sophia akainuka na kwenda moja kwa moja mezani kula chakula alichoandaliwa na Neema na kuanza kula chakula kile.
Ibra alimrudisha Lazaro hadi nyumbani kwake ambapo walipokelewa na mke wa Lazaro kisha Lazaro akamuomba mkewe amfanyie maombi maana hali yake haikuwa sawa, mke wa Lazaro hakujifikiria mara mbili na moja kwa moja alianza maombi.
Ibra alikuwa kimya kabisa akiwatizama huku yale maombi yakiendelea mpaka kuna muda ambao Lazaro alidai kuwa anajihisi nafuu sasa na anaweza kuzungumza, kisha akamuangalia rafiki yake na kumwambia,
“Ibra pendelea kufanya maombi kwenye nyumba yako”
“Maombi gani ambayo napaswa kuyafanya? Maana mimi sijazoea hayo mambo kwakweli”
“Hivi unajuu ukuu wa Mungu Ibra? Nyumba yako imetawaliwa na mambo mabaya, sio kwamba nakuonea wivu hapana ila kuna vitu nimevihisi kwenye nyumba yako”
Ibra akafikiria kidogo na kumuuliza rafiki yake huyu,
“Hivi wakati naongea na Yule Neema mbona ulikuwa hunisikilizi?”
“Mimi sijamuona huyo Neema ndani kwenu na wala sijakusikia kama kuna muda umeongea nae zaidi ya kuning’ang’aniza nimsalimie mtu nisimuona”
Mke wa Lazaro alisikia yale maongezi na kutamani kujua zaidi kuhusu huyo mtu ambapo Ibra aliamua kuwaeleza kwa kifupi jinsi walivyokutana na Yule Neema hadi kwenda nae nyumbani kwake, ila mke wa Lazaro nae alimuuliza kama kuna taratibu zozote alizofanya ili kumtambulisha huyo Neema kwa mjumbe na kuwafanya wawe huru nae nyumbani kwao,
“Yani hapo ndio kwenye tatizo, Yule Neema hataki kabisa twende nae kwa mjumbe yani kashatugomea kabisa kasema tungetaka kumpeleka kwa mjumbe basi tungeenda nae toka mwanzoni”
“Mmh shemeji poleni sana, lakini katika maisha hakuna kitu kibaya kama kuishi na mtu usiyemfahamu maana huwezi jua hi mtu wa aina gani na ndiomana kuna utaratibu ili kitakachokupata chochote au kumpata huyo binti watu watajua ni jinsi gani wanakusaidia. Kusaidia mtu njiani sio tatizo ila tatizo ni kutofata taratibu”
“Basi labda kama mtaweza shemeji mje siku moja nyumbani kwangu na kunisaidia kumshawishi Yule binti niweze kwenda nae kwa mjumbe maana mie amenikatalia kabisa na nimeshindwa hata kufanya hivyo”
Mke wa Lazaro alimkubalia Ibra ila Lazaro aligoma kwenda tena nyumbani kwa Ibra,
“Ndugu yangu tafadhali nisamehe bure tu ila sitaweza kuja tena nyumbani kwako, kama nilivyokwambia tafuta watu wa maombi kwanza”
“Usijali, mimi nitaenda, siku ukipata muda shemeji njoo unifate niende huko kwako”
“Sawa mke wangu ila ile nyumba inahitaji uwe na umakini wa hali ya juu”
Wakakubaliana pale kisha Ibra akaaga na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana kwani hakuelewa kuwa nyumba yake imekumbwa na kitu gani hadi kushauriwa na watu juu ya maombi. Kwanza kabisa alikumbuka maneno ya Jane kisha akakumbuka alichoambiwa na Lazaro pamoja na mke wa Lazaro kwakweli akili yake ilikuwa ikitembea bila ya majibu yoyote yale hadi alipofika nyumbani kwake bado alikuwa na mawazo.
Ibra aliingia ndani na kumkuta Neema akiwa pale sebleni ambapo alimsalimia kisha akamuuliza alipo mke wake,
“Yupo chumbani kalala”
“Mbona kalala mapema sana”
“Labda ni uchovu tu”
“Sawa, ila Neema mbona muda ule wakati yupo mgeni nilipokuwa nikikuuliza kitu ulikaa kimya tu?”
Neema akamuangalia Ibra na kutabasamu hivyo akafanya Ibra azidi kupatwa na maswali mbalimbali kisha akamuuliza tena,
“Mbona unatabasamu?”
“Yule rafiki yako hawezi kurudi tena hapa”
“Kwanini?”
“Sio mtu mzuri Yule na amekuonea wivu sana wewe kumiliki nyumba kama hii kwani hata yeye ametamani ingekuwa yake”
“Kwahiyo ndio ulishindwa kunijibu sababu ananionea wivu?”
“Huwa sipendi kuongea na watu wabaya, nimeshawaambia hili mara nyingi sana mwenzenu siwezi kuzungumza na watu wabaya”
“Sawa, ila kwanini pia hupendi twende kwa mjumbe?”
“Mimi sio kwamba sipendi, nyie mkipata muda tu twendeni sina tatizo juu ya hilo kabisa”
Ibra alishangaa sana leo kujibiwa kirahisi hivi na huyu Neema kwani haikuwa kawaida yake ukizingatia ukizungumzia tu swala la mjumbe alikuwa mkali sana ila leo alionekana kukubali kwa haraka zaidi. Kisha Ibra kaelekea chumbani alipo mkewe na kumkuta kweli amelala na hivyo kumuamsha kwanza, Sophia aliamka kama mtu aliyekuwa amezidiwa sana na usingizi na kumfanya Ibra ampe pole kwa kumuamsha kwa haraka vile.
“Kwani kuna kitu gani mume wangu?”
“Hakuna kitu ila nilikuamsha ili angalau nikusalimie, halafu ndio uendelee kulala”
Sophia hakujibu cha zaidi kwani alijilaza tena pale kitandani na ilionekana usingizi kumchukua kwa muda huo huo. Ibra alitulia akitafakari kisha kuamua kwenda kuoga ambapo alienda kuoga kwa haraka sana na kurudi tena chumbani ila akashangaa pale kitandani hakumuona tena mkewe na kumfanya ashtuke kuwa mkewe atakuwa ameenda wapi kwani alimuacha hapo akiwa maelala fofofo.
Ibra akavaa haraka haraka na kwenda sebleni kumuangalia mabapo alimkuta Neema tu pale sebleni na kumuuliza,
“Dada yako kaenda wapi?”
“Kwani hayupo chumbani?”
“Nilimkuta amelala lakini nimetoka kuoga gafla simuoni tena”
“Aah acha masikhara bhana kaka, sasa atakuwa ameenda wapi?”
“Sijui kwakweli na ndiomana nimekuja kukuuliza wewe labda umemuona kuwa ametoka”
“Hapana mimi sijamuona, na ninachojua yupo chumbani kwenu amelala”
“Chumbani hayupo nielewe hivyo Neema”
“Je unaniruhusu twende pamoja tuakamuangalie huko chumbani”
“Twende ukaone”
Neema alitabasamu kisha akainuka pale kwenye kiti na kuongozana na Ibra hadi chumbani kwao, walipofika tu pale chumbani Sophia alionekana kitandani na kumfanya Neema amwambie Ibra,
“Si huyo hapo amelala jamani, nikusaidie kumuamsha?”
Ibra akatingisha kichwa kwani tayari uoga ulishamjaa moyoni, Neema alisogea kwenye kitanda na kukaa kisha akamgusa Sophia ambye alishtuka kutoka usingizini na kuamka kabisa huku akimshangaa Neema kuwa ameingiaje kwenye chumba chao.
“Usijali dada, ni kaka kaniruhusu kwa lengo la kukuamsha wewe”
“Sawa hakuna tatizo Neema nimeshaelewa”
Sophia alikaaa pale kitandani kisha Neema akainuka na kutoka ambapo Ibra alisogea alipo mkewe na kumuangalia kwa makini sana ambapo Sophia pia alimuangalia mumewe kwa macho makali huku akimuuliza,
“Kwanini umemruhusu Neema aingie chumbani kwetu? Inamaana wewe hukuweza kuniamsha mwenyewe hadi aje Neema?”
“Unanilaumu bure mke wangu, kwa hali ilivyokuwa sikuweza kuacha kumlaumu aingie humu chumbani”
“Halafu badae unaanza kulalamika ooh hatumfahamu vizuri na umemruhusu mwenyewe kuingia mpaka chumbani”
“Nisamehe kwa hilo mke wangu”
Kisha Sophia akainuka na kuelekea bafuni kwa lengo la kujimwagia maji kwanza ili aweze kupata nguvu.
Sophia akiwa bafuni gafla alipiga kelele na kurudi chumbani huku akilia na kumfanya Ibra ashangae sana kuwa ni nini kinamsumbua,
“Vipi mke wangu nini tatizo tena?”
“Sielewi, sielewi, sielewi Ibra”
“Huelewi kitu gani tena Sophy jamani, kwani kuna nini au umeona kitu gani?”
“Sijui hata ni kitu gani kwakweli sijui Ibra”
“Khee sasa makubwa haya, yani ukimbie ulie na usielewe unacholilia wala kilichokikimbiza kweli? Ni kitu gani umeona?”
“Nitakw\mbia tu mume wangu ila naomba unisindikize tu nikanawe vizuri”
Hilo halikuwa tatizo kwa Ibra ila tatizo ni kuwa mke wake amekumbwa na kitu gani huko bafuni ndio kulimkosesha jibu kabisa. Kisha akainuka nae na kuelekea nae bafuni ambako kulionekana kuwa kawaida tu halafu Sophia akajimwagia maji haraka haraka na kutoka nje.
Ibra alikaa huku mkewe akivaa nguo, kisha akaamua kuzungumza nae tena kuwa ni kitu gani kilimtokea bafuni wakati akioga na kumfanya akimbie na hata kuanza kulia,
“Nimekwambia sielewi Ibra yani sielewi kabisa”
“Sasa huelewi kivipi Sophy yani inawezekana vipi mtu kupatwa na jambo usilolielewa?”
“Sijui ila sielewi”
“Basi ngoja nikuulize hivi, umeona nini huko bafuni?”
Kabla hajajibu wakagongewa mlango na Neema ambaye alikuwa akiwaita ili waweze kula chakula ila leo Sophia alikuwa wa kwanza kusema kuwa anajihisi kushiba sana na kumfanya Ibra nae kusema kuwa ameshiba, hivyo Neema hakuwagongea tena na ukimya nao ukatawala ambapo Ibra alimwambia mkewe kuwa ni bora walale tu kwa muda huo.
“Ila leo nimelala sana Ibra hata sidhani kama nitapata usingizi saizi”
“Pole mke wangu ila inatakiwa ulale maana ni usiku huu si unajua tena mambo ya usiku”
“Naelewa ila sina usingizi mume wangu”
Wakiwa wanabishana kuhusu swala la kulala gafla umeme ukakatika na kufanya kuwe na giza la haswaa chumbani kwao na kumfanya Sophia amkumbatie kwa nguvu Ibra kwa uoga aliokuwa nao kwa muda huo,
“Itabidi tuwashe tochi ya simu sasa”
Ibra akaanza kupapasa ilipo simu yake ila hakufanikiwa kuipata na kushangaa kuwa siku hiyo aliweka wapi simu yake, akajaribu kuinuka huku akiwa ameshikiliwa na Sophia na kuendelea kapapasa sehemu mbalimbali na mwisho wa siku hawakuwa na la kufanya zaidi ya kumuita Neema ambaye alienda na kuwapelekea mshumaa pamoja na kiberiti ili ikitokea umeme umekatika tena wawashe tu.
Walimshukuru sana Neema na muda kidogo umeme nao ukarudi, Ibra alikuwa kashika ule mshumaa na kiberiti kisha Sophia akamuuliza mumewe
“Hivi wakati umeme umekatika hadi tukamuita Neema humu ndani, je alifungua mlango wa chumbani kwetu saa ngapi na ametoka saa ngapi?”
“Kwanini umeuliza hivyo Sophy?”
“Maana sikumbuki kama mlango ulifunguliwa ila ninachokumbuka ni kuwa Neema alileta mshumaa na kiberiti, pia sikumbuki muda aliotoka ila tu nimeona umeme umerejea”
“Hata mimi sikumbuki mke wagu ila nakuona sasa ufahamu umeanza kukurudia”
Kisha Ibra akamuomba mkewe kwa muda huo waweze kulala tu kwani hakuona umuhimu wa wao kuanza kumzungumzia Neema kwa muda huo.
Kulipokucha Sophia alikuwa wa kwanza kuamka kwa safari hii, kisha akamuamsha mumewe na kumwambia kuwa angepena siku hiyo amuandalie chai yeye mwenyewe ili aweze kunywa kabla ya kuondoka,
“Leo umeota nini mke wangu?”
“Nimeamua tu Ibra sababu nakupenda na pia naijali afya yako”
Ibra aliinuka na kwenda kuoga kisha Sophia alitoka chumbani kwao, alipofika sebleni alimuona Neema akiwa amekodolea macho kwenye Tv kisha yeye akaenda jikoni ambako alimkuta Neema akiosha vyombo na kufanya Sophia aanze kupiga kelele.
Itaendelea kama kawaida…………..!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABU: 21
Ibra aliinuka na kwenda kuoga kisha Sophia alitoka chumbani kwao, alipofika sebleni alimuona Neema akiwa amekodolea macho kwenye Tv kisha yeye akaenda jikoni ambako alimkuta Neema akiosha vyombo na kufanya Sophia aanze kupiga kelele.
Ila Neema huyo huyo ndio alimfata Sophia na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, ila Sophia alikuwa akitetemeka tu na kushindwa kujibu,
“Jamani dada nini tatizo, niambie tafadhari”
Sophia alizidi tu kutetemeka mpaka pale Ibra alipoingia jikoni pia kwani na yeye alishtushwa na kelele za Sophia, ni hapa Sophia alipomkimbilia mume wake na kumkumbatia ambapo Ibra nae alimuuliza kuwa tatizo ni nini,
“Sielewi, sielewi naomba twende chumbani”
Ikabidi Ibra amshikilie mke wake na kwenda nae chumbani ambapo Sophia alionekana kupooza sana kwani hakuweza kuongea ya zaidi.
“Niambie basi Sophia, tatizo ni nini?”
“Hata sielewi Ibra ila ningependa nikuombe kitu”
“Kitu gani?”
“Leo unapotoka naomba tutoke wote kisha mimi ukaniache kwa Da’Siwema”
“Kheee habari za Siwema zimeanza tena! Haya hakuna tatizo, jiandae basi”
Sophia aliinuka na kwenda bafuni ambapo alioga haraka haraka kisha kuvaa na kumuomba mumewe kuwa waondoke.
Walipokuwa wanatoke, Neema alikuwa pale sebleni ambapo Ibra alimuaga Neema kuwa yeye na mke wake wanatoka
“Mmh kaka leo mnaniacha mwenyewe!”
“Ukiona hivi ujue tumeshakuamini”
Neema akatabasamu kisha wakaondoka na kwenda kupanda gari yao moja kwa moja na safari ikaanza, Ibra alitamani sana kujua kilichompata mkewe jikoni na kumfanya apige kelele kiasi kile ila bado Sophia alikuwa mgumu kusema na kumfanya Ibra akubaliane na hali halisi tu.
Walifika nyumbani kwa Siwema kisha Ibra akamshusha mkewe na kumuaga ambapo moja kwa moja Sophia alienda kumgongea Siwema, haikuchukua muda mrefu akafunguliwa mlango
“Kheee kumbe ni Sophia, karibu sana yani hata sikukutegemea kama ungekuja leo”
“Imenibidi tu kuja dada yangu maana nina majanga ya kutosha tu”
“Majanga? Majanga gani tena? Hebu njoo uingie ndani tukae tuzungumze kwanza”
Wakaingia ndani ambapo walikaa huku Siwema akiwa na hamu ya kujua hayo majanga yanayomsumbua rafiki yake,
“Kwanza kabisa dada yangu, siku hizi mume wangu simuelewi kabisa nyumbani kutokana na mambo anayoyafanya”
“Anafanya mambo gani hayo?”
“Mara agome kula yani mambo shaghalabaghala, kisha kuna kitu kinaendelea ndani kwetu ila huwa hasemi hata nikimuuliza vipi ila na mimi kuna kitu leo nimekiona na nimeshindwa kumwambia kabisa hadi nimekuja kwako”
“Kitu gani umekiona na mambo gani yanayoendelea kwenu?”
Sophia aliamua kumueleza jinsi walivyokutana na Neema njiani na jinsi walivyoenda nae nyumbani kwao na jinsi walivyomshawishi kwenda kwa mjumbe akakataa na kile alichokishuhudia asubuhi,
“Mmh mbona makubwa hayo Sophy, una uhakika kweli kuwa ni yeye aliyekuwepo hapo sebleni na jikoni?”
“Nina uhakika kabisa dada maana nilikuwa na akili zangu timamu kabisa na sikuwa na usingizi kabisa.”
“Sasa mbona nashindwa kuelewa jamani, je kwa fikra zako unahisi ni nini mpaka ikawa hivyo?”
“Kwakweli sijui maana hata mimi nimeanza kutokumuelewa Yule Neema kabisa”
“Je Yule Jane nae huwa anaendelea kuja pale kwenu?”
Ikabidi Sophia amueleze kidogo juu ya kilichotokea kwa Jane alipomkuta Yule Neema na kisha Jane kusema kuwa hatorudi tena pale.
“Mmh inamaana huyo Neema ana nguvu kumshinda Jane?”
“Yani kama Neema ni mchawi dada basi atakuwa ni mkubwa wa wachawi”
“Sasa wewe unataka tufanyaje mdogo wangu”
“Nataka unisaidie Yule Neema atoke pale ndani dada yangu maana ananipa mashaka sana”
“Duh! Ila hebu twende kwanza nyumbani kwako nikamshuhudie huyo Neema mimi mwenyewe”
Sophia akaona kuwa hilo ni swala la muhimu sana, hivyo kukubaliana na Siwema ambaye alienda kujiandaa kisha kutoka na Sophia na kuanza safari.
Walifika nyumbani kwa Sophia na kuingia ndani ambapo Yule Neema alikuwa pale sebleni amekaa tu akiangalia Tv kisha akawakaribisha kwa uzuri sana.
“Karibuni jamani, karibuni sana”
Wakakaa kisha Neema akaenda jikoni na kuwaletea glasi za juisi na kuwaandalia ili waweze kunywa ambapo walikunywa huku wakiendelea na maongezi mengine ila baada ya kunywa ile juisi tu wote wawili yani Siwema na Sophia wakapatwa na usingizi mzito sana na kuwafanya walale pale pale sebleni.
Ilichukua muda mrefu sana wakiwa wamelala bila ya kuwa na habari ya aina yoyote ile, na aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Siwema ambapo alimuona Neema akitabasamu tu Ila yeye alikuwa akijishangaa kwani hakutegemea kama angelala kwenye kochi muda ule.
“Dah kumbe nililala”
“Pole sana kwa uchovu dada”
“Asante yani sikutegemea kabisa kama ningelala kiasi hiki”
“Ndio mambo ya uchovu yalivyo, mtu unaweza kujishangaa ukilala sehemu yoyote ile haswa ikiwa na utulivu”
Kisha Siwema akamuangalia Sophia na kujaribu kumshtua,
“Kheee yani huyu ndio hajitambui kabisa”
“Muache tu ataamka mwenyewe si unajua mimba nayo inamsumbua dada”
“Naelewa ila kama amelala sana au ni mimi ndio nililala kabla yake?”
“Ndio ulilala kabla yake, hata hivyo mjamzito anatakiwa apate muda wa kupumzika ndimana nakwambia muache ataamka mwenyewe”
Siwema aliitikia tu huku akijifikicha macho yake, muda kidogo Ibra nae aliwasili kutoka kwenye shughuli zake na kuwakuta pale sebleni ila Sophia akiwa amelala vilevile, ikabidi Ibra asalimiane na Siwema kwanza,
“Ila shemeji una tabia mbaya yani umemleta mwenyewe Sophy nyumbani halafu hata kusubiri tusalimiane imekuwa shida mmh!”
“Nisamehe bure shemeji yangu nilikuwa nawahi kibaruani”
“Sawa, za majukumu lakini!”
“Nzuri tu, ila huyu nae kwanini anapenda kulala sebleni siku hizi”
“Tena amelala muda mrefu balaa”
Ikabidi Ibra amsogelee Sophia na kuanza kumuamsha ila Neema alikazania msimamo wake kuwa wamuache ataamka mwenyewe kwani si vizuri kuwasumbua wajawazito, Siwema akaingilia kati
“Hata kama si vizuri kuwasumbua wajawazito ila huyu amelala muda mrefu sana jamani, tumuamshe tu”
“Nisikilizeni mimi, muacheni alale hadi atakapoamka mwenyewe”
Kwakweli Ibra alikuwa hapendezewi na kauli za huyu Neema kuwa wamsikilize yeye kama nani wakati aliyelala pale ni mke wake, Ibra alimuangalia Neema kwa jicho kali sana kisha akaendelea kumuamsha Sophia, ambapo Neema aliing’ang’ania ile ile kauli yake ya kusikilizwa na kumfanya Ibra aongee kwa hasira sasa,
“Tukusikilize wewe kama nani wakati aliyelala hapa ni mke wangu!”
Neema akamwambia,
“Mdomo uliponza kichwa, endelea kumuamsha”
Siwema alikuwa kimya tu kwani hata yeye kwa muda huu alishindwa kumuelewa huyu Neema moja kwa moja kwani halikuwa jambo la kawaida kwa msichana wa kazi kubishana na bosi wake kamavile ambvyo Neema alikuwa akibishana na Ibra.
Ingawa Ibra alikazana kumuamsha Sophia ila hakuamka, ndiohapo Ibra akashikwa na hasira zaidi na kumuuliza Neema kwa ukali,
“Umemfanya nini mke wangu Neema?”
“Kwani wewe unahisi nimemfanya nini?”
Neema alijibu kwa dharau kabisa na kumzidisha hasira Ibra ambapo alijikuta akinyanyua mkono wake na kutaka kumzaba kibao Neema ila ule mkono kabla haujatua kwenye shavu la Neema tayari alikuwa ameudaka na kumwambia,
“Usithubutu maana utajutia maisha yako yote hadi unaingia kaburini”
Ibra aliutoa mkono wake kwenye kiganja cha mkono wa Neema na kuushusha chini kisha akakaa karibu na mke wake huku akiwa amejiinamia tu.
Ikabidi Siwema aanze kumbembeleza shemeji yake ili angalau apunguze hasira alizokuwa nazo ambapo kwa muda huo kimya kidogo kilitawala mule ndani.
Iliingia jioni kabisa ambapo Sophia alishtuka kutoka katika ule usingizi mzito sana huku akiangaza macho yake na kuwa kama mtu aliyechoka sana, alimuangalia Siwema, akamuangalia mume wake ambapo nao walikuwa wakimtazama tu kisha akajikuta akiwauliza,
“Mbona mnaniangalia hivyo jamani?”
“Umelala kwa muda mrefu sana Sophy hadi ukatupa mashaka ndiomana unaona tukikuangalia tu”
“Kheee kumbe nimelala kwa muda mrefu eeehh ila dah nimechoka sana”
Ibra akamsogelea mkewe na kuanza kumpa pole kwani kiukweli alikwa anaonekana kama mtu aliyechoka sana na kupoteza muelekeo kabisa ila Siwema nae aliamua kuaga kwani ni muda mrefu tu alikuja akingoja Sophia aamke ndipo aage na kuondoka.
“Ila kwanini Da’Siwema leo usingelala hapa hapa?”
“Hapana Sophy sikujipanga kulala, nitakuja kulala siku nyingine”
Kisha Ibra akainuka pamoja na Sophy kwa lengo la kumsindikiza Siwema ambapo Neema nae alimuaga halafu wakaondoka.
Njiani Siwema akaanza kuongelea kuhusu Neema,
“Jamani, mi mwenzenu tatizo kubwa nililoliona kwa Yule binti ni kiburi na huenda hao ndugu zake hawamtaki sababu ya kiburi maana anaonekana kuwa na kiburi cha hali ya juu”
“Sasa unatusaidiaje kwa hilo shemeji?”
“Mmh sijui hata tufanyaje ila ningeprnda siku mje nae nyumbani kwangu kisha mmuache nmkomeshe maana mie watu wenye kiburi vile huwa nawakomesha”
“Hilo wazo zuri shemeji tena ningependa tulifanyie kazi kesho tu maana mie amesha nichosha”
“Jitahidini mfanye hivyo, yani mie nikikaa nae siku mbili tu Yule ananyooka mbona maana huwa sipendi ujinga mie”
Wakaona hilo ni wazo jema sana na wote wakakubaliana kufanya hivyo, kisha Siwema akapanda daladala halafu wao wakaanza safari ya kurudi kwao taratibu.
Walifika na kuingia ndani ambapo kwa safari hii walienda moja kwa moja chumbani kwao huku wakifurahia sana lile wazo walilopewa na Siwema.
“Nilikwambia Ibra tukienda kwa Siwema tutapata suluhisho”
“Kweli kabisa Sophy ila tusiongee sana ili kesho iwe rahisi kukamilisha mpango wetu.”
“Sawa hakuna tatizo.”
Kichwani mwa Ibra ilikuwa ni kumpeleka Neema moja kwa moja kwa Siwema yani asirudi tena nyumbani kwao ili kama kufukuzwa basi akafukuzwe huko huko kwa Siwema kwahiyo hilo swala lilimfanya atabasamu muda wote kwa wakati huo.
Wakaongea ongea mule ndani, muda kidogo wakagongewa mlango kuwa chakula tayari, kwavile walikuwa tayari na mipango yao kichwani hawakuona tatizo lolote kwa wao kwenda kula kisha wakatoka na kwenda kula ambapo kwa siku ya leo Ibra alimuomba Neema ale nao pamoja,
“Ila mimi nimeshakula jikoni”
“Hata kama umekula jikoni Neema ila ukija na kujumuika pamoja nasi japo kwa kula kidogo tu itakuwa vizuri”
Neema hakuwabishia na akaenda mezani kukaa pamoja nao ambapo akajipakulia chakula chake kidogo tu kisha wote wakaanza kula, ila muda mwingi Ibra alikuwa akimuangalia Neema kwa lengo la kumchunguza ila kwa siku hiyo alijikuta akila huku akimshangaa huyu Neema aliyeonekana akishika shika kijiko tu bila kula ila chakula kilionekana kupungua kwenye ile sahani ya Neema kanakwamba kinaliwa ingawa muda wote aliokuwa akimuangalia hakuna muda ambao aliweka chakula mdomoni.
Kwakweli hiki kitendo kilimstaajabisha sana Ibra ila hakutaka kuongea jambo lolote lile kwani aliona ni kamavile watazua jambo jipya. Walipomaliza kula, vyombo vilitolewa mahali pale kisha Ibra na mkewe wakaelekea tena chumbani ila Ibra alikuwa akijiuliza vitu vingi sana na kujikuta akiamua kumuuliza Sophia,
“Hivi inawezekana vipi mtu kushikashika kijiko huku chakula kwenye sahani kinaisha bila kuliwa, inawezekana vipi? Je mtu huyo ni wakawaida kweli?”
“Unazungumzia nini Ibra?”
“Aaah ngoja tuachane na hayo ila kuna wakati utanielewa zaidi”
Ibra akamuomba mkewe walale ingawa kiukweli alikuwa na mawazo sana ukizingatia hakuuelewa kabisa ule ulaji wa Neema.
Kulipokucha kama kawaida waliamka na kujiandaa kisha kwa pamoja wakatoka hadi sebleni na kumkuta Neema akiangalia Tv kama kawaida kisha Sophia akaanza kuzungumza naye,
“Neema, leo ningependa twende wote kwa yule rafiki yangu wa jana ili ukufahamu nyumbani kwake na iwe rahisi kuwasiliana hata kikitokea kitu chochote nyumbani hapa”
“Kwahiyo ndio twende muda huu dada!”
“Ndio twende saizi ili tuwahi kurudi”
Neema akawaomba wasubiri ajiandae kwanza, na wao wakamruhusu kufanya hivyo huku wakifurahi kwani hawakutegemea kama angekubali kirahisi namna ile. Muda kidogo Neema alitoka akiwa tayari amejiandaa kisha safari ikaanza.
Wakiwa njiani Sophia akakumbuka Yule mtoto ambae walikuwa wakikutana nae njiani,
“Unamkumbuka Yule mtoto mume wangu, hivi siku hivi yuko wapi?”
“Hata sijui alipotelea wapi dah alikuwa ananikera sana”
Sophia akacheka tu huku Neema nae akicheka kanakwamba na yeye amewahi kumuona huyo mtoto.
Walifika nyumbani kwa Siwema na kushuka ambapo kwa muda huo walimkuta Siwema akiwa nje na shughuli zake za asubuhi ambapo aliwakaribisha ndani vizuri sana kisha wote wakaingia ndani. Muda kidogo Ibra akaaga kuwa anahitaji kwenda mahali na mke wake kisha watamfata Yule Neema badae ambapo Siwema aliwakubalia vizuri kwani mpango wao ulikuwa mmoja ila hata Neema nae hakubisha, kisha Sophia na Ibra wakatoka na kurudi kwenye gari yao huku wakifurahi sana na safari ya kurudi ikaanza.
“Nimefurahi sana kuutua ule mzigo”
“Hunifikii mimi mume wangu yani nimefurahi kupita maelezo ya kawaida”
“Sasa cha kufanya tukifika nyumbani ni kufunga minguo yake yote tuitoe nje”
“Halafu hata huwa nashangaa kuwa zile nguo kazitoa wapi wakati tulivyomuokota hakuwa hata na chochote mjinga Yule”
“Ni kweli ila cha msingi tumeutua mzigo”
Waliwasili nyumbani na kuingia ndani ila pale sebleni Tv ilikuwa inawaka tu na kufanya watazamane,
“Hivi tuliondoka bila ya kuzima Tv?”
“Inawezekana mume wangu si unajua tena tulikuwa na furaha ya kuondoa ule mzigo”
Kisha Ibra akachukua rimoti ya Tv na kutaka kuizima, ila kabla hajaizima akasikia sauti,
“Usizime kaka bado naangalia”
Walishtuka na kugeuka, wakamuona Neema akitokea jikoni.
Itaendelea kama kawaida……….!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
Usiku mwema wapendwa wangu, shukrani sana kwa kuniombea mema.
NYUMBA YA MAAJABU: 22
Kisha Ibra akachukua rimoti ya Tv na kutaka kuizima, ila kabla hajaizima akasikia sauti,
“Usizime kaka bado naangalia”
Walishtuka na kugeuka, wakamuona Neema akitokea jikoni tena akiwa hana habari kabisa, kwakweli si Ibra wala si Sophia aliyeweza kustahimili hali ile kwani walijikuta wakitetemeka tu ila walimshangaa huyu Neema kwani naye alionyesha kuwashangaa na wao. Ibra aliamua kujikaza kiume huku akiuliza kwa sauti ya kutetemeka,
“Ne-ne-neema umefikaje hapa?”
“Kivipi kaka”
Neema alijibu kwa kujiamini kabisa, kisha Ibra akajikakamua tena na kusema;
“Si-si-situmekuacha kwa Siwema wewe!”
Neema akacheka kisha akawatazama kwa muda mrefu na kuwafanya wakae chini bila ya kutarajia, Ibra na Sophia walikuwa wakiangaliana tu kwa uoga na bila ya kufanya chochote huku Neema akiendelea na shughuli zake.
Ulipita muda wakiwa pale sableni bila ya kufanya chochote kile, Neema akawafata muda huu na kuwaambia,
“Mnatakiwa kuwa makini sana kwani mimi kabla hamjapanga kitu chochote juu yangu tayari nakuwa nimeshakijua, pia ni nyie wenyewe mlinionea huruma na kunikaribisha nyumbani kwenu kwamaana hiyo siwezi kutoka mahali nilipokaribishwa kwa upendo. Pia nikiingia mahali nimeingia yani kutoka msahau kabisa”
Sophia akamuangalia mumewe kisha akauliza,
“Kwahiyo Yule tuliyempeleka kwa da’Siwema ni nani?”
Neema akacheka na kumwambia Sophia,
“Niulize mimi maana ukimuuliza mumeo ni kama unajisumbua tu, na bata nikiwaambia zaidi nitakuwa nawachanganya tu bora nisiwaambie, au mpigieni simu huyo Siwema wenu awaambie”
Ibra alichukua simu huku akitetemeka na kumpigia Siwema ambapo Siwema alipokea simu ile na kusema.
“Yule mtu wenu mliyemleta hayupo”
“Ameondoka muda gani?”
“Nadhani muda sio mrefu”
Kisha simu ikakatika na kufanya Ibra atazamane tena na mkewe ila walijishangaa sababu hakuna aliyeweza kuinuka wala hakuna aliyeweza kufanya chochote kwani wangeweza kwa mufda huo wangeondoka pale nyumbani kwao. Waliazamana kwa muda ila gafla wakapatwa na usingizi wa ajabu.
Ibra alikuwa wa kwanza kuamka huku akiwa amechoka sana, pembeni yake alikuwepo mkewe Sophia na kufanya Ibra ajaribu kurudisha kumbukumbu za haraka na kweli aliweza kukumbuka mambo yote kasoro tu hakukumbuka wamewezaje kwenda chumbani kulala kwani kwa kumbukumbu zake ni kuwa walilala pale pale sebleni kwao.
Ibra akaona ni vyema amuamshe mke wake ingawa ilikuwa ni usiku, na alipomuamsha mkewe aliamka ila alionekana kuwa na usingizi sana
“Ibra jamani kuna nini tena acha nilale”
“Khee yani Sophy umesahsau yote yaliyotokea mke wangu hadi unapzata nguvu ya kulala kiasi hiko!”
“Nimechoka sana mume wangu jamani”
Sophia akajigeuza upande wa pili na kulala vizuri zaidi, Ibra alimshangaa mkewe ila hakuweza kufanya chochote kwa muda huo zaidi ya kumkumbatia na kulala tena hadi palipokucha.
Asubuhi hii Ibra alikuwa wa kwanza tena kuamka huku akiwa anakumbuka matukio yote yaliyotokea jana yake kasoro tu ni kuwa waliingiaje chumbani na kulala, Ibra alijishika kichwa huku akiwa na mawazo sana, muda kidogo Sophia nae aliamka na kusalimiana na mumewe kisha Ibra akamuuliza;
“Sophy una kumbukumbu yoyote kwa kilichotokea jana?”
“Ndio nakumbuka”
“Unakumbuka nini?”
“Nakumbuka tulikuja na Siwema hapa na ametushauri kuwa tumpeleke huyu Neema nyumbani kwake ili akamfunze adabu kwani anaonekana kuwa na kiburi sana”
“Mmmh Sophy mke wangu hayo ni mambo ya juzi”
“Ya juzi kivipi Ibra wakati ni jana tu. Hebu twende tujiandae tumpedleke au umeghairisha!”
“Kuwa mwelewa Sophy hayo unayoyasema ni ya juzi, ngoja nikueleze ya jana”
Kisha Ibra akaanza kumueleza mkewe kuhusu yale yaliyotokea jana ila Sophia alionekana kustaajabu na kushangaa sana huku akihisi kuwa huenda mume wake anaota kwani yeye hakuwa na kumbukumbu yoyote ile ya jana.
“Ibra unaota au? Huyu Neema bado hatujampeleka kwa da’Siwema yani ndio leo tunataka kumpeleka mume wangu nahisi umeanza kuchanganyikiwa”
“Sophy itakuwa ni wewe ambaye umechanganyikiwa maana nakumbuka ulipiga kelele juzi hadi ikafikia kukupeleka kwa Siwema kisha akaja hapa na kutushauri kuwa huyu binti tumpeleke nyumbani kwake kisha jana tukafanya hivyo na ndio hayo majanga yakatokea. Kwakweli mke wangu huyu Neema sio mtu mzuri kabisa inatakiwa tufanye jitihada za kumuondoa, nadhani atakuwa amekusahaulisha tu”
“Haiwezekani mume wangu, ila ili kuvunja utata basi tumpigie simu da’Siwema ili tujue kati ya mi na wewe nani anakosea”
Ibra alikubali kwani alihisi kuwa ndio njia pekee ya kumsaidia mkewe kurudisha kumbukumbu za jana. Wakampigia simu Siwema naye hakukawia kupokea baada ya salamu tu Siwema akawauliza;
“Mlisema mtamleta huyo Neema huku leo imekuwaje tena mbona kimya?”
Ibra akapatwa na butwaa kuwa hawa watu wamepatwa na nini ikiwa mambo hayo yalikuwa jana, kwakweli Ibra hakuendelea kuongea na kukata ile simu huku akijiuliza maswali lukuki, kisha akainuka na kwenda bafuni kuoga labda aweze kuiweka akili yake sawa.
Ibra alipokuwa bafuni aliwaza sana na kujiuliza vitu vingi huku akijiuliza kuwa kamakweli anaota au ni vipi maana matukio yote ya jana anayakumbuka sasa imekuwaje hawa wenzie hawakumbuki chochote!
Akajimwagia maji huku akiangaza macho yake kulia na kushoto ila alikuwa hajielewi kabisa kwani ilikuwa kama masikhara vile ila ndio hivyo wenzie wote hawakukumbuka kilichotokea, akapata wazo kuwa akimaliza kuoga basi aende kwakina Jane akazungumze nae kwani alihisi huenda akamsaidia kwa mawazo aliyokuwa nayo kwa muda huo.
Alipomaliza kuoga na kuvaa akatoka na kumkuta mke wake sebleni akiwa na Neema tena akionekana hana hofu yoyote ile kabisa, Ibra hakutaka kuongea sana zaidi ya kumuaga mke wake kuwa anatoka kidogo.
“Sawa ila nadhani ule mpango wetu wa kwenda kwa da’Siwema umehairisha”
“Hapana ila tutaongea zaidi nikirudi badae”
Kisha Ibra akatoka na kuwaacha pale ndani Sophia na Neema, muda kidogo Neema akamuuliza maswali Sophia;
“Kwani dada, kaka ana matatizo gani maana hata kunisalimia hajanisalimia”
“Achana nae huyo akili yake huwa inatawaliwana mawazo ya ajabu ajabu tu”
“Kama mawazo gani?”
“Achana nae Yule hata asikuumize kichwa, hebu tufikirie mambo mengine”
Kimya kidogo kikatawala kisha Sophia akakumbuka kitu na kusema;
“Mara nyingi Ibra amekuwa akinikumbushia nikaanze kliniki, naomba kesho nikumbushe niende Neema”
“Hata usijali dada na wala usijisumbue kwenda huko kliniki kwani kipi kipya wanachofanya? Mi ninaweza kukufundisha vyote na ukawa salama zaidi ya kwenda huko kliniki”
“Mmh nasikia ni muhimu, sijui kuna dawa za kunywa na sindano za kuchoma”
“Dada usijisumbue yani usijisumbue kabisa ngoja nitakufanyia kitu wewe mwenyewe utapenda kuliko hata kwenda huko kliniki”
Sophia akatabasamu kwani kuna wakati alihisi kama ni mzigo hivi kwenda kuanza kliniki kwahiyo alivyoambiwa hivyo na Neema akafurahi sana.
Ibra alifika nyumbani kwakina Jane na kumkuta Jane akiwa nje na shughuli zake, akamuita naye Jane hakusita kusogea alipo Ibra na kumsalimia kisha maongezi yao yakaanza,
“Unajua Jane kilichonileta hapa ni kuhusu Yule Yule mdada aliyepo ndani kwetu kwakweli amezidi kutushangaza na kutuonyesha maajabu tu.”
“Eeeh kivipi kaka?”
“Kwanza kabisa kumpeleka kwa mjumbe ilishindikana yani alitufanyia vituko sio vya nchi hii, inakuwa kama ni ndoto hivi lakini ndio ukweli ulivyo. Halafu alichokifanya jana ndio kimenitisha zaidi mpaka nimekuja kwako mdogo wangu kupata ushauri”
“Mmh pole sana, kwahiyo jana ndio kafanyaje tena?”
Ibra akamsimulia Jane vile ambavyo ilikuwa, kwakweli Jane alishangaa sana na kumuuliza kwa makini Ibra kama hayo matukio ni ya kweli au ni ndoto tu.
“Jane, hii sio ndoto yani nina uhakika kabisa na haya matukio ni kweli kabisa ila nadhani Yule mtu amevuruga akili ya mke wangu hata amekuwa haelewi chochote jamani.”
“Dah pole sana, ila mi kwa ushauri wangu nadhani itakuwa vyema ukamchukue mjumbe uende nae hapo nyumbani kwenu”
“Lakini sasa mjumbe wa huku ni nyie ndio mmemzoea labda twende wote ili tumshawishi kwenda nae nyumbani”
“Sawa kaka hakuna tatizo, ngoja nijiandae”
Ibra akatulia pale nje akisubiri Jane amalizie kujiandaa, muda kidogo simu yake ikaanza kuita alipoiangalia kuwa nani anapiga akakuta ni Siwema kisha akaipokea,
“Shemeji nimepata mahali kuna mtaalamu huyo mahili inabidi tumpeleke huko huyo mdada wenu wa kazi ili asitumiwe tena na huyo Jane”
“Samahani Siwema, hivi unaelewa kweli unachokizungumzia?”
“Kivipi shemeji?”
“Kumbuka jana ulivyosema kwenye simu na leo asubuhi ulivyosema”
“Ya jana nakumbuka ndio na ndiomana nimeenda kutafuta mtaalamu ila leo sijawasiliana na nyie yani ndio muda nimekupigia shemeji kukujulisha”
“Mmmh asubuhi si tumekupigia simu wewe na tukaongea!”
“Shemeji acha masikhara basi, simu mmepiga muda gani jamani hadi nisikumbuke? Hatujaongea asubuhi bhana”
“Mmh basi ngoja badae nitakupigia tuongee vizuri”
Ibra akakata ile simu huku akitafakari kwani aliona kamavile Siwema kachanganya mada tu kwani kwa kumbukumbu zake walimpigia simu asubuhi ili kupata uthibitisho kwa mkewe kuwa ilikuwa kweli na si ndoto ingawa majibu ya Siwema kwa hiyo asubuhi ilionyesha kamavile haikuwa kweli. Ibra alitafakari sana bila ya majibu na alihisi kichwa kumuuma tu.
Jane alipotoka ndani wakaanza safari ya kuelekea kwa mjumbe bila ya kupoteza muda zaidi.
Sophia akiwa amekaa na Neema ndani muda huu, Neema akamwambia kuwa anataka kumpima vipimo kama vya kliniki kwahiyo akamuomba aelekee nae chumbani kwake.
“Kwahiyo chumbani kwako ndio vizuri Neema?”
“Ndio dada twende”
Sophia akainuka na kwenda na Neema hadi chumbani kwake, kisha Neema akamwambia Sophia kuwa apande kitandani naye alifanya hivyo. Neema akaanza kushika shika tumbo la Sophia huku akimwambia kuwa nimeshika kichwa cha mtoto, mara nimeshika miguu yake basi Sophia akawa anafurahi tu. Kisha Sophia akamuuliza Neema;
“Je unaweza kuhisia jinsia ya mtoto?”
“Aaah naweza ndio ila subiri ukilala ukiamka nitakwambia jinsia yake, ila mtoto anaonekana kuwa mtamu sana huyu”
“Mtamu!! Kivipi mtamu?”
“Sio utamu utamu, namaanisha ni mzuri sana”
“Sikukuelewa mwanzo”
“Basi ndio nielewe, ila cha kukwambia kwasasa nenda kalale kwanza umpumzishe mtoto”
“Sawa kungwi wangu”
Wote wakacheka, kisha Sophia akainuka na kuelekea chumbani kwake ambapo alipojiweka tu kitandani ukampitia usingizi mzito sana.
Ibra na Jane walifika kwa mjumbe na bahati nzuri walimkuta na kumsalimia kisha Ibra akaelezea shida yake ambapo mjumbe alimsema kwanza,
“Hivi nyie vijana mkoje? Yani unamuokota mtu na kukaa nae siku zote hizo bila ya kutoa taarifa! Kwa mfano akikufia utakimbilia wapi?”
“Nisamehe kwa hilo baba yangu kwakweli nimefanya kosa, ila nakuomba sana twende nyumbani ukamuone”
“Kwanza ni utaratibu wa wapi huo kuwa mimi ndio nije huko badala ya nyie kuja?”
Ikabidi Jane amuombe pale, na mwisho wa siku mjumbe alikubali na kuongozana nao hadi nyumbani kwa Ibra, ila walipofika walishangazwa na ukimya wa ile nyumba kwani ilikuwa ni kimya sana na wakagonga kwa muda mrefu bila ya kufunguliwa;
“Mmmh au wametoka? Na kama wametoka kwanini hawakunipa taarifa jamani!”
Ikabidi Ibra amuombe msamaha pale Yule mjumbe kisha mjumbe akaondoka zake, halafu Ibra akaondoka na Jane na kukaa huko kwa muda ili kuvuta masaa yaende.
Jioni Ibra alirudi nyumbani kwake na kufunguliwa mlango na Neema, swali la kwanza alimuuliza Neema kuwa walikuwa wapi mchana;
“Nilimpeleka dada kliniki”
“Kwahiyo yuko wapi saivi?”
“Nimerudi nae kachoka sana na amepitiliza kulala”
Ibra akaenda chumbani alipo mkewe huku akitafakari mambo mbalimbali bila ya jibu na alimuona akiwa amelala hoi hajitambui kabisa, kisha akasogea karibu yake na kulala nae huku akijipa imani kuwa wakishtuka ndio wataenda kula kwani usiku ulikuwa bado haujaingia.
Ilikuwa ni usiku sana ambapo Ibra alishtuliwa na sauti ya Sophia akilia, alikuwa akilalamika tumbo linamnyonga sana. Ibra alimshika mkewe na kukaa ila walipoangalia kitandani, palikuwa pametapakaa damu na kufanya uoga uwashike.
Itaendelea kama kawaida…………………..!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
NYUMBA YA MAAJABY: 23
Ilikuwa ni usiku sana ambapo Ibra alishtuliwa na sauti ya Sophia akilia, alikuwa akilalamika tumbo linamnyonga sana. Ibra alimshika mkewe na kukaa ila walipoangalia kitandani, palikuwa pametapakaa damu na kufanya uoga uwashike.
Kwakweli Ibra ndiye ambaye alishtuliwa zaidi na zile damu, huku akijaribu kumtuliza mkewe kwani yeye alipoona zile damu alikuwa akilia tu.
“Nyamaza mke wangu tujue cha kufanya”
“Inamaana damu zote hizi zinanitoka mimi?”
“Ndio mke wangu”
Sophia akaendelea kulia kwani alijiona kamavile anakaribia kufa, ikabidi Ibra anyanyuke na kuvaa haraka haraka kisha akamnyanyua mkewe na kuanza kukokotana nae ili waende hospitali, kutoka sebleni akamkuta Neema amekaa tena akiwa hana wasiwasi wowote ule ingawa aliona wazi Sophia akitokwa na damu kwani zilikuwa zikichuruzika tu.
Ibra hakumuongelesha Neema na kuendelea kumkokota mkewe ili atoke nae nje, Neema akawaangalia na kuwauliza,
“Vipi usiku huu mnaenda wapi?”
“Hivi wewe huoni midamu inayochuruzika au? Nampeleka mke wangu hospitali”
“Usimpeleke, rudi nae chumbani”
“Hivi wewe una kichaa nini, yani mke wangu anaumwa na damu zinamtoka kiasi hiki halafu unasema nisimpeleke hospitali!!”
Ibra hakumtazama zaidi Neema kwani alitoka na mkewe nje na kuacha Neema akicheka na kusema,
“Utaona faida ya kumpeleka huko, mdomo uliponza kichwa”
Ibra alifika nje na kumpakia mkewe kwenye gari kisha safari ya hospitali ikaanza.
Walifika hospitali na Sophia akapokelewa na manesi na kupelekwa moja kwa moja kwa daktari kwani hali yake ilikuwa mbaya sana, Ibra alikuwa kachanganyikiwa tu pale nje huku akijiuliza,
“Huko kliniki alikoenda mke wangu leo wamemfanya nini jamani? Yani mke wangu kwenda kliniki tu na matatizo juu yamempata dah! Mungu msaidie mke wangu apone”
Alihisi kama akili yake kutokufanya kazi kwa muda kidogo huku akingoja majibu ya daktari.
Ulipita muda akiwa anasubiri na baada ya masaa kadhaa alitoka daktari na kwenda kuongea nae, ila daktari hakusema chochote zaidi ya kumwambia kuwa aendelee kusubiri au kama anaweza basi aende nyumbani kwake na aje kesho yake kwani wao bado waliendelea kumuhudumia, kwakweli Ibra hakuweza kufanya hivyo badala yake alijikuta akizunguka zunguka hapo hospitali hadi panakucha kwani hakuweza hata kusinzia kutokana na mawazo juu ya mke wake.
Bado alikuwa akimngoja daktari amwambie kuhusu mgonjwa wake, muda kidogo daktari alitoka tena na kumfata ila daktari alimkaribisha ofisisni kwake na akaongozana nae hadi huko ofisini.
“Pole sana ndugu yangu”
Neno la pole lilimfanya Ibra presha iwe juu na kuwa kama amechanganyikiwa,
“Nini dokta mke wangu amekufa? Mungu wangu, nitawaeleza nini ndugu zake mimi! Nitabaki na nani jamani? Uwiii bora ningemsikiliza Neema! Dokta niambie ukweli”
“Usipaniki bwana Ibra, tafadhali punguza presha. Mkeo hajafa”
Ibra akapumua kidogo na kuuliza tena;
“Kwahiyo amefanyaje mke wangu?”
“Kwa bahati mbaya mimba yake imetoka……”
“Jamani mwanangu, kwahiyo tarajio la kuitwa baba kwa hivi karibuni halipo tena! Dah mwanangu jamani”
“Jikaze Ibra wewe ni mwanaume unatakiwa kuwa jasiri, mkeo kapoteza damu nyingi sana hata sijui ni kitu gani kilichosababisha mimba yake kutoka. Pole sana”
“Yani mke wangu kuanza kwenda kliniki tu na mimba imetoka? Jamani mambo gani haya?”
“Kwani mkeo kaenda kliniki lini?”
“Jana mke wangu ndio kaenda kliniki”
“Ila mimba yake inaonyesha ilikuwa kubwa tu, kwanini amechelewa hivyo kuanza kliniki? Yani miezi saba kasoro ndio anaenda kliniki!! Ila sidhani kama kliniki ndio wamemsababishia hayo matatizo kwani kule hata kama mimba ipo kwenye hatari huwa wanawapa wajawazito tahadhari ili wawe makini ila kama umekuja na kadi yake ungenipatia labda naweza gundua tatizo”
“Mimi sijui alipoweka kadi yake maana huko kliniki ameanza jana halafu leo mimba imetoka dah mwanangu jamani”
Dokta hakuwa nay a ziada zaidi ya kumpa pole tu Ibra na kumwambia kuwa mkewe hawezi kuruhusiwa kwavile amepoteza damu nyingi sana.
Ibra alitoka kwa daktari akiwa kama amechanganyikiwa kwani hakujua aanzie wapi na aishie wapi.
Alipokuwa nje ya hospitali hiyo, wazo likamjia kuwa awapigie simu ndugu zake na Sophia ingawa alijua wazi kuwa watamlaumu sana kwani hakuwahi kuwaambia habari za mimba.
“Mmh sasa nifanyaje hapo? Nikae kimya tu, mtoto wa watu akipatwa na matatizo zaidi itakuwaje? Lakini watanisema sana hata sijui nifanyaje”
Wakati ameshika simu ili awapigie akashtushwa na sauti ya Neema ambapo alishtuka sana;
“Kheee ulivyoshtuka kama umeitwa na mzimu vile”
“Aaah ahh Neema, aah umejuaje kama tumekuja hospitali hii!”
“Nimejua tu, nimemletea dada chakula ili apate nguvu na tuweze kurudi nae nyumbani”
“Ila dokta kasema ametokwa na damu nyingi sana hawawezi kumruhusu”
“Usijali, watamruhusu tu, ngoja akanywe kwanza huu uji”
Neema aliondoka pale na kuongoza moja kwa moja hadi wodi aliyolazwa Sophia ambapo Ibra alikuwa akimfata tu nyuma hata swala la kuwapigia simu tena ndugu wa Sophia akalipuuzia.
Neema alipofika akamuamsha Sophia na kumpa ule uji, baada ya muda mfupi Sophia alionekana kuchangamka sana kamavile sio Yule mtu aliyekuwa hajiwezi muda mfupi uliopita.
Muda kidogo daktari alikuja na kuwapa ruhusa ya kwenda nyumbani, wakatoka wote na kuongozana mpaka kwenye gari.
Kwakweli Ibra hakuwa na la kusema kwani haya mambo yalikuwa kwa muda mfupi sana, ila akasema tu
“Yani nilijua nampoteza mke wangu”
Neema akadakia,
“Hata usijali, nisingeweza kuacha apotee maana bado namuhitaji sana”
“Unamuhitaji kivipi?”
Neema akacheka tu ila Sophia alikuwa kimya kabisa kwani hata yeye hakujielewa ukizingatia usiku tu wa kuamkia siku hiyo alikuwa hoi akiumwa sana ila leo alikuwa ni mzima kanakwamba hajaumwa chochote kila ila muda wote alikuwa akijidadisi moyoni kuwa imekuwaje hadi mimba yake kutoka.
Walifika nyumbani na kuingia ndani ambapo Neema aliwakaribisha mezani kwa madai kwamba alishawaandalia chakula, Ibra akamuuliza tena Neema
“Ulikuwa na uhakika gani kama tunaweza kurudi leo?”
“Nilikuwa na uhakika kabisa, na ndiomana nikaja kuwafata. Unajua mimi nishazoea kuishi nanyi humu ndani kwahiyo sikuweza kuvumilia kuona mko mbali name, nikiwaambiaga nawapenda huwa hamuamini ila nataka mtambue kwamba nawapenda sana.”
Ibra na mkewe wakakaa mezani na kula kisha Sophia akahitaji kwenda kupumzika, moja kwa moja Ibra akaenda na mkewe chumbani ambapo walioga kisha wakapumzika pamoja ukizingatia hata Ibra hakulala usiku kucha kwani alikuwa na hofu na hali ya mke wake.
Wakati wamelala, Sophia akajiwa na ndoto tena ndoto hii ilikuwa ni ile ile ya watoto watatu ambao walikuwa wakionyesha sura za kuhuzunika ila safari hii kati ya wale watoto watatu kuna mmoja wapo alipunga mkono kama ishara ya kumuaga Sophia ambapo alipoanza kuondoka Sophia alianza kumkimbilia ila hakumfikia. Aliporudi aliwakuta wawili ambao nao kila alipotaka kuwashika walisogea nyuma ila sura zao zilionyesha kusononeka sana na kumfanya Sophia ashtuke kutoka kwenye ile ndoto huku akihema juu juu ila baada tu ya kushtuka, neno la kwanza kulisema ilikuwa “mwanangu” huku akishika shika tumbo lake na machozi kumtoka.
Ibra aliamka pia na kumkumbatia mkewe,
“Tutapata mwingine mke wangu, cha muhimu ni bado una uhai”
“Roho inaniuma sana Ibra yani sana, mtoto alikuwa faraja yangu, tumaini yangu, furaha yangu na ndoa yetu ila hayupo tena na sisi. Nilikuwa nafarijika sana na mwanangu ingawa alikuwa bado yupo tumboni ila ameondoka bila hata ya kumtia machoni”
Machozi yalimtiririka Sophia huku Ibra akiendelea kumbembeleza na kuamua kwenda nae sebleni ili wakaangalie Tv kwa kupoteza mawazo hayo.
Walitoka sebleni ila leo Neema hakuwepo hapo sebleni na Tv ilikuwa imezimwa kwahiyo ni wao ambao walienda na kuiwasha tena ile Tv, moja kwa moja wakakutana na igizo la Kiswahili na ilionyesha lilikuwa la kichawi. Waliangalia kidogo na kujikuta wakijadili,
“Waswahili nao kwa kuhusudu mambo ya kichawi siwawezi”
“Sio kwamba wanahusudu Sophy, ukweli ni kwamba hayo mambo yapo kwenye jamii yetu na ndiomana wanayaigiza”
“Kama ndio hivyo mbona ulinimaindi kipindi kile da’Siwema alivyonipeleka kwa mganga”
“Unajua nini Sophy tatizo hukunishirikisha mapema na ndiomana nilichukia ila hata nisingechukia kiasi kile”
“Ila kiukweli waswahili tunapenda sana kuamini haya mambo ya kishirikina ingawa Yule mganga ameshindwa kuniondolea Jane hadi leo”
“Kheee yani bado unaamini kuwa Jane ni mtu mbaya jamani”
“Ni mtu mbaya ndio, wewe unamtetea bure tu”
“Jane si mtu mbaya kabisa na ipo siku utajua umuhimu wa Jane katika maisha yetu ingawa tumeshindwa kutumia uwepo wake”
Neema nae akaja kujumuika nao pale sebleni, alikuja huku akicheka na kuwaambia
“Huyo Jane msimtetee yani siku mkimjua vizuri mtajilaumu sana”
Ibra akajibu,
“Tutajilaumu ndio kuwa kwanini hatukuwa nae karibu toka mwanzoni”
Neema akabadilisha mada,
“Hivyo mnavyoviangalia mtaenda kuviota vyote”
“Halafu kweli, yani Ibra anatetea hili igizo wakati ni uchawi mtupu”
“Mnataka mkiota muwashike watu ubaya, kuweni makini sana na vitu vya kuangalia”
Kisha Neema akawabadilishia stesheni, Ibra alikaa kimya kwa muda huku akijiuliza kuwa kwanini huyu Neema anajichukuliaga tu maamuzi kamavile yeye ndio mwenye nyumba wakati ni msichana wa kazi tu.
Muda huu Ibra akainuka na kuelekea chumbani kwao, alikaa kitandani akakumbuka kuwa wakati wanaenda hospitali hapo kitandani palikuwa pamejaa damu swali ni kuwa je Neema amefua mashuka yote na mpaka godoro? Maana hapakuonekana hata tone la damu tena, akajikuta akijiwa kama na mawazo kuwa ile damu mule chumbani iliyeyuka yenyewe akashtuka sana kwa uoga, kisha akasema
“Neema si mtu wa kawaida”
Gafla akaona maneno yakijiandika kwa chini ‘Si mtu wa kawaida kweli’
Ibra alitoa macho na kufumba kisha kufumbua tena na kupiga kelele za kumuita mke wake ambapo Sophia hakukawia kwenda chumbani alipo mumewe na kumuuliza kuwa kuna tatizo gani.
“Nini tatizo Ibra jamani, umepatwa na nini tena?”
Ibra akawa anamuonyesha Sophia yale maandishi ila gafla yalifutika na kumfanya Ibra awe kamavile mtu aliyewehuka kwa muda huo, kwakweli Sophia alikuwa akimshangaa tu mumewe kuwa amepatwa na jambo gani kwani alikuwa kama ana matatizo.
“Ibra jamani loh! Tatizo ni nini sasa?”
“Naogopa kila kitu Sophy, naogopa mimi”
Sophia akamkumbatia mumewe kwani alihisi kuwa mumewe pia bado alikuwa na mawazo ya kupoteza kiumbe chao kilichokuwa tumboni.
“Usijali mume wangu, tujipe moyo naamini tutapata mtoto mwingine”
“Sio swala la mtoto tu Sophy bali ni swala la huyu Neema”
“Mmmh mume wangu kwani ana nini jamani? Hebu tuachane nae na tuishi kwa amani, tuangalie jinsi gani tutaweza kukabiliana na mambo yaliyopo mbele yetu”
“Sophia mambo yaliyopo mbele yetu si mtihani mkubwa kama mtihani huu tulionao wa Neema”
“Mume wangu, usijichanganye akili yako kuhusu huyu Neema”
“Unajua Sophy usiwe kama mtu asiyejielewa mke wangu, hebu nikuulize ni nani alikushauri jana kwenda kliniki maana usikute hata swala la kutoka kwa mimba chanzo ni yeye”
Sophia akamuangalia mumewe na kumwambia,
“Sijaenda kliniki jana mie, nilikuwa nyumbani siku nzima”
“Mmh unaona hapo michezo ya Neema eeh!! Mke wangu fungua macho yako, kwani Neema amekufanya nini jana wakati sipo?”
Sophia akajaribu kufikiria kidogo na kukumbuka kuwa jana alipimwa mimba yake na Neema na baada ya hapo akalala usingizi mzito, akakumbuka na jinsi tumbo lilivyoanza kumuuma hadi kupelekwa hospitali.
“Mmh nimekumbuka Ibra”
Kisha akamsimulia vile ambavyo Neema alimpima mimba ile.
“Eeh unaona hapo Sophy unaona yani ni huyu huyu Neema ndio chanzo cha mimba yako kutoka mke wangu. Huyu Neema katuulia mtoto wetu dah ! Sikubali lazima nifanye kitu”
“Kitu gani Ibra?”
“Subiri”
Ibra akainuka na kumuacha mkewe pale kitandani akijiuliza maswali kuwa mume wake anataka kufanya kitu gani.
Ibra alijitoa muhanga na akajitoa ufahamu kabisa kwa muda huo ambapo akaenda moja kwa moja jikoni na kuchukua kisu, kisha akanyata sebleni hadi alipokaa Neema na kumchoma nacho mgongoni ila Neema hakushtuka hata kidogo ingawa damu zilionekana kumtoka.
Itaendelea kama kawaida………………..!!!!!!!!!!!!!!!!!
Toa maoni yako mdau.
Disqus Comments