-->

NYUMBA YA MAAJABU [24-30]

NYUMBA YA MAAJABU: 24 Ibra alijitoa muhanga na akajitoa ufahamu kabisa kwa muda huo ambapo akaenda moja kwa moja jikoni na kuchukua kisu, kisha akanyata sebleni hadi alipokaa Neema na kumchoma nacho mgongoni ila Neema hakushtuka hata kidogo ingawa damu zilionekana kumtoka. Ibra alijikuta akiduwaa na kile kisu chake sababu Neema hakushtuka wala kutingishika kanakwamba hakuna alichokichoma mahali pale, akajikuta akishindwa kupiga hata kelele huku ameshika kisu chake mkononi. Mkewe aliamua kutoka ili ajue mumewe anataka kufanya kitu gani ila alimkuta mumewe sebleni akiwa hajielewi kabisa, “Vipi Ibra umepatwa na nini mume wangu?” Ibra akanyoosha kidole alipo Neema ili mkewe aangalie zile damu na amuone jinsi Neema alivyotulia tu bila ya wasiwasi wowote ule. “Mbona hamna kitu mume wangu unanionyesha nini? Na mbona umeshika kisu mkononi?” Ibra akaanza kuongea kwa kujiuma uma, “Ina-ina-inamaana humuoni Neema hapo na damu!” “Mume wangu hebu acha kuota jamani, Neema yuko wapi hapa?” Ibra akajifikicha macho na alipoangalia kwa makini hakumuona Neema wala nini na kumfanya apatwe na uoga zaidi ukizingatia mwanzoni alimuona mahali hapo na alimchoma na kisu, akajikuta akianza kutetemeka kwani kile kisu mikononi mwake hakikuwa na damu tena na wale pale chini hapakuwa na damu tena, akajikuta akianza kuongea kwa nguvu sasa “Hapana sioti, sioti mimi ni ukweli mtupu Neema alikuwa hapa na nimemchoma na kisu. Huyu Neema ni mchawi huyu ni mchawi” Mara Neema akatokea chumbani na kuuliza kwa dharau, “Nani anayeitwa mchawi huyo?” Ibra akajibu kwa hasira huku akitetemeka, “Wewe hapo Neema ni mchawi” Neema akacheka sana na kumuangalia Ibra kisha akamwambia, “Ningekuwa mchawi ningeshawamaliza siku nyingi sana kwa vituko vyenu haswa wewe mwanaume, Ibra kuwa makini sana na mimi huwa sitaniwi” Kisha akasonya, Sophia akamuangalia Neema kwa mshangao na kusema, “Neema kuwa na adabu, huyu ni baba mwenye nyumba” Neema akacheka tena kisha akasema kwa dharau, “Baba mwenye nyumba awe huyu!!! Kwa uwezo gani alionao? Anauwezo wa kumiliki nyumba kama hii? Mnapotafuta nyumba muwe mnauliza kwanza na waliotangulia kukaa hapo” “Unamaanisha nini Neema?” “Sahau nilichosema” Kisha Neema akampuliza Sophia usoni na muda huo huo Sophia akaanguka kwenye kochi na kupitiwa na usingizi, akamfanyia hivyo na Ibra ambaye pia akapitiwa na usingizi. Kulipokucha kama kawaida Ibra alikuwa wa kwanza kuamka na walikuwa chumbani wamelala yani yeye na mke wake, Ibra aliinuka na kukaa kitandani ila kichwa chake kilikuwa kizito sana. Alijikuta akiwaza mambo mengi huku akijaribu kurudisha kumbukumbu zake nyuma na kwa bahati aliweza kukumbuka mambo yote ambayo yalitokea, akasikitika sana huku akijiuliza cha kufanya. Akamuamsha mke wake kwanza ili ajue kama nae anakumbuka chochote, Sophia aliamka na kukaa pia kisha Ibra akamuuliza; “Unakumbuka kilichotokea jana?” Sophia akawa kimya kwa muda kisha akamjibu mumewe; “Kwani kimetokea kitu gani maana sina kumbukumbu kama kuna kitu cha kustaajabisha kilichotokea” Ibra akataka kumuelezea mkewe kwa kifupi juu ya kilichotokea, ila kabla hajaanza kueleza wakasikia Neema akiwaita, Sophia akamkatisha mumewe na kumuomba kuwa wakamsikilize kwanza Neema “Ila Sophia mke wangu siku akili yako ikirudi sawa utaelewa kwanini hatupaswi kumsikiliza huyu Neema” “Jamani mume wangu hata hujui anatuitia nini usikute ni mambo ya maana hebu twende tukamsikilize” Sophia akawa wa kwanza kuinuka ikabidi Ibra nae ainuke na kumfata mkewe, kisha wakatoka hadi sebleni alipo Neema ambaye aliwasalimia kwa adabu kabisa mpaka Ibra akashangaa kuwa huyu Neema mwenye kiburi leo anajifanya ana adabu kwasababu gani, wakatulia kumsikiliza; “Jamani kuna jambo nataka kuwaeleza” Ibra alitulia zaidi kwani alijua ni maajabu mengine kwani Neema alishakuwa tishio tayari kwake, Sophia akamuuliza kwa makini zaidi, “Jambo gani hilo Neema? Tueleze tafadhali” “Jana usiku nimejiwa na ndoto mbaya sana, kwanza kabisa alitokea bibi yangu akaniambia anataka kunionyesha maajabu yaliyotokea kwangu kisha akapotea. Mara nikamuona Jane akisema kuwa kuna mambo anayafanya ili mimi nionekane mbaya kwenye macho yenu. Nikashtuka usingizini, kwakweli Jane ni mtu mbaya sana ten asana mnaweza mkachukizana na watu wengi sana kwasababu yake. Nimeamua kuwaita na kuwaeleza haya ili mjue ya kuwa sina ubaya wowote mimi” “Mmmh!!!” Ibra aliguna kwanza kwani hakuamini hata kidogo haya maneno ya Neema na wala hakufikiria kama ni maneno ambayo Neema aliyowaitia asubuhi hiyo na kwa haraka haraka akahisi kuwa Neema amefanya hivyo kwavile hataki amsimulie Sophia kile kilichotokea kwa hofu ya kumkumbusha vizuri, Ibra akamuangalia Neema na kusema “Inamaana na kilichotokea jana ni Jane ndio amefanya?” “Kipi hicho kilichotokea jana?” “Yani Neema bila hata ya aibu unajifanya kuuliza kipi kilichotokea? Kwani hujui kilichotokea?” Sophia naye akauliza, “Kwani kitu gani kilitokea?” “Mke wangu Sophy huyu Neema ni mchawi” “Mchawi? Kivipi? Au na wewe mume wangu ushachanganywa na Jane?” “Niamini mimi Sophia huyu Neema ni mchawi na ndiye aliyemuua mtoto wetu” “Kheee kivipi mume wangu wakati ni mimba imetoka!” “Kwa macho ya kawaida unaona kamavile mimba imetoka ila kiukweli imetolewa na Neema kiuchawi” Neema alikuwa kimya tu akiwasikiliza na maongezi yao kanakwamba hayupo ila alikuwepo palepale akiwaangalia, Sophia naye akamuangalia Neema na kumuuliza “Je ni kweli umesababisha mimba yangu kutoka Neema? Je ni kweli wewe ni mchawi?” Neema akacheka sana, kisha akawaambia “Ila kweli nyie mtakuwa na matatizo ya akili, yani niliyowasimulia yote yameingia kulia na kutoka kushoto duh! Mtu mwenye akili timamu anaweza kuniuliza maswali kama hayo kweli?” Neema akamuangalia Sophia kwa msisitizo zaidi ambapo Sophia akainuka na kuelekea chumbani kwao. Sophia alipokuwa chumbani aliwaza sana na kufikiria kuwa huenda mume wake ana matatizo kichwani kwani halikuwa jambo la kawaida kumuita mtu mchawi bila kuwa na uthibitisho, akainuka tena ili aende sebleni akamuombe msamaha Neema na aweze kumshawishi mume wake ili wamuombe msamaha Neema. Alipofika sebleni alimkuta Neema akiwa peke yake na kumuuliza alipo mumewe kwanza, “Ibra yuko wapi?” “Katoka” “Kaenda wapi?” “Hata hajaniaga alipoenda” “Kheee Ibra ameanza kuchanganyikiwa sasa loh! Yani kaondoka bila hata kuoga tena kifua wazi au alivaa shati gani?” “Yani hata sijui maana nilichosikia ni kuwa alifungua mlango na kutoka sababu mimi nilikuwa jikoni” “Khee makubwa haya, tafadhali Neema naomba utusamehe mimi na mume wangu kwa kukushutumu vibaya” “Hata usiwe na wasiwasi dada, mimi ni mtu muelewa sana.” “Nashukuru kwa hilo Neema ila huyu Ibra hata sijui ana matatizo gani jamani yani kuondoka bila hata kuoga loh!” Sophia alifikiria kidogo kisha akaenda tena chumbani na kuchukua simu yake akijaribu kumpigia mumewe ila simu ilianza kuitia mule mule ndani na kugundua kwamba mume wake ameacha simu ndani, akatoka tena na kuelekea sebleni kisha akamwambia Neema “Kumbe simu yenyewe kaiacha ndani, ila mie nae hata sijui nafikiria nini maana mwanzoni nilipotoka nae hapa hakutoka na simu halafu eti naenda chumbani kumpigia loh! Ila pia alitoka hajavaa shati hata sijui ameendaje huko” “Labda kaenda kuanua ya kwenye kamba huwezi jua” “Mmh halafu sijafua siku nyingi” “Una wasiwasi gani wakati mimi nipo! Yani mimi nikiwepo hutakiwi kuwa na mashaka ya aina yoyote ile sababu nitafanya kazi zote za humu dada” Kisha Neema akamuomba Sophia aelekee mezani kula huku akimsisitiza kuwa ni muhimu ale sana ili kurudisha afya yake baada ya ile mimba kutoka, Sophia hakujiuliza mara mbili na moja kwa moja alielekea mezani na kula chakula alichoandaliwa na Neema. Sophia alipomaliza kula akaenda kuoga na kujiandaa kwani alipata wazo la kwenda nyumbani kwa Siwema ili aweze kuzungumza nae kuhusu mume wake na jinsi anavyomshutumu Neema kuwa ni mchawi na anahusika na mimba yake iliyotoka. Akatoka chumbani sasa na kumkuta Neema pale sebleni kama kawaida na kuamua kumuaga, “Neema, mimi natoka kidogo” “Unataka kwenda wapi dada?” “Naenda kwa rafiki yangu mara moja” “Sawa dada, badae tutaonana” Akaagana nae pale vizuri kabisa na kuondoka, alipofika getini gafla kichwa kilianza kumgonga yani kamavile mtu anagonga na nyundo, Sophia hakuweza kwenda mbele na kusimama kwa muda kwanza kisha akaanza kurudi na kuingia ndani. Alipoingia ndani alishangaa kumkuta Neema akicheka sana, “Mbona unacheka hivyo Neema?” “Na wewe mbona umerudi?” “Kichwa kinaniuma sana tena kimenianza gafla tu” Neema akacheka tena kisha akamwambia Sophia, “Basi hunabudi kuahirisha safari yako, ni bora ukapumzike tu” “Ila sasa mbona unacheka Neema?” “Nacheka vile ninavyoweza kuziendesha akili zenu” “Unasemaje Neema?” “Nenda kapumzike na wala sijasema chochote” Sophia alielekea chumbani kwake huku akiwa na mawazo sana kwani hakuielewa kabisa ile kauli ya Neema kuwa anacheka vile anavyoweza kuziendesha akili zao, “Mmmh akili zetu anaziendeshaje huyu? Inamaana kuna kitu huwa anatufanyia?” Wazo lingine likamjia palepale kuhusu Ibra, “Hivi Ibra anaweza kuondoka bila ya kuniaga kweli! Mbona kamavile ni jambo lisilowezekana kabisa, mmh basi kabadilika sana siku hizi” Akajilaza kidogo na kupitiwa na udsingizi palepale. Wakati amelala akajiwa na ndoto, kwenye ndoto yake leo aliona watoto wadogo wawili, sura zao zilionyesha huzuni sana na kufanya nae aone huzuni pia ila alisikia sauti ikimwambia, “Je, ni yupi atapona kati yao?” Sophia akashtuka sana na kuamka, akaangaza huku na huko na kuona kuwa giza nalo lilikuwa limeingia, akafikiria kuhusu ile ndoto ila akajikuta akikumbuka kuhusu mume wakw, “Inamaana Ibra bado hajarudi?” Akainuka na kuelekea sebleni ambako alimkuta Neema ila kabla hajamuuliza Neema chochote akashangaa Neema akimwambia, “Umeamka mapema sana tena sana, inatakiwa urudi kulala” Sophia akajishangaa akirudi tena chumbani na kulala. Kulipokucha Sophia alikuwa wa kwanza kuamka na kumkuta mumewe amelala hoi pembeni yake na kumuamsha, Ibra naye aliamka kwa upesi sana tena alikuwa ni mtu anayejishangaa kwa wakati huo, kisha kwa haraka akaenda kuoga na kurudi huku akivaa haraka haraka. “Kheee kukuamsha nikuamshe mie halafu haraka ujifanye unazo wewe loh!” “Natakiwa niwahi kwenye shughuli zangu kuna wateja niliahidiana nao leo” “Ndio ulipokuwa jana!” “Kuwa jana kivipi mke wangu jamani, ngoja niwahi nikirudi tutazungumza” Ibra alimbusu mkewe kwenye paji la uso na kisha kuondoka zake. Ibra alifika kwenye shughuli zake ila kila mmoja alionekana kumshangaa kwenye eneo lile, “Unaonekana umeshiba pesa ndugu yangu yani siku zote hizo ulikuwa wapi?” “Kivipi jamani mbona siwaelewi?” Wakabaki kumshangaa tu kisha kila mmoja kuendelea na shughuli zake, Ibra alikuwa akishangaa tu biashara yake kwani ilionyesha haijafunguliwa muda kidogo na kujiuliza kuwa kwanini hakufungua siku zote hizo, wakati akifikiria hayo alifika rafiki yake Lazaro na kumkuta hapo kisha kusalimiana nae, “Kila siku nikipita hapa sikukuti Ibra, vipi ndugu yangu umekumbwa na nini?” “Hata mimi mwenyewe sifahamu kuwa nimekumbwa na nini?” “Au ndio mambo ya Yule msichana wenu wa kazi?” Kidogo Ibra akaanza kukumbuka baadhi ya mambo na kumuangalia rafiki yake kisha kumwambia, “Lazaro, nadhani Yule binti atakuwa kanifanya kitu sio bure” “Pole sana, ila huyo binti sio wa kumuendekeza inatakiwa umwambie ukweli” Muda huo huo Neema akaja pale kwenye biashara ya Ibra na kuwaambia, “Haya niambieni huo ukweli” Ibra na Lazaro waliangaliana kwa mshangao. Itaendelea kama kawaida………….!!!!!!!!!!!!!! NYUMBA YA MAAJABU: 25 Kidogo Ibra akaanza kukumbuka baadhi ya mambo na kumuangalia rafiki yake kisha kumwambia, “Lazaro, nadhani Yule binti atakuwa kanifanya kitu sio bure” “Pole sana, ila huyo binti sio wa kumuendekeza inatakiwa umwambie ukweli” Muda huo huo Neema akaja pale kwenye biashara ya Ibra na kuwaambia, “Haya niambieni huo ukweli” Ibra na Lazaro waliangaliana kwa mshangao, kwakweli walitetemeka pia kwani hakuna hata mmoja kati yao aliyemtarajia Neema kwa muda huo. Ibra alijikuta akimuuliza Neema kwa sauti iliyojaa uoga na kutetemeka “Na-na-nani aliyekuonyesha hapa kwenye biashara zangu?” “Mkeo ndio kanionyesha hapa” “Mke-mke-mke wangu mwenyewe yuko wapi?” “Huyo hapo anakuja” Kuangalia nje ni kweli alimuona Sophia akisogea pale kwenye biashara yake na kumfanya Ibra azidi kupatwa na mashaka. Sophia alifika eneo lile na kuwasalimia, Ibra alishindwa hata kuitikia salamu ya mke wake na kujikuta akimuuliza “Mbona-mbona hukuniambia kama utakuja huku leo?” “Kwani kuja mahali ambako mume wangu huwa anashinda ni dhambi au ni vibaya?” “Hapana si vibaya ila mbona hukunitaarifu?” “Hivi wewe ulivyokuwa na haraka vile ile asubuhi ningekutaarifu vipi? Kwakweli mimi sijakuelewa kuhusu ulipoelekea jana ndiomana leo nimekuja kuhakikisha kama kweli umekuja kwenye shughuli zako isije kuwa napigwa changa la macho” Lazaro akaingilia kati yale maongezi kwa kumuuliza Sophia, “Sasa shemeji, change la macho upigwe na Ibra au huyo msichana wenu wa kazi?” Neema alimuangalia Lazaro kwa jicho kali sana na kumwambia, “Na wewe hayakuhusu, fanya yako” “Unaniambiaje wewe?” “Kama nilivyokwambia na kama ulivyosikia” “Wewe usionichezee mimi sio hao wakina Ibra unaowachezea mimi ni mtu mwingine wa tofauti” Neema akamsonya Lazaro kisha akamwambia, “Kwa utofauti gani ulionao wewe!” Kisha akamsonya tena, kwavile Lazaro alikuwa ni mtu wa hasira kwakweli hasira zilimpanda palepale na kumnasa kofi Neema huku akisema, “Mke wangu mwenyewe hajawahi kunisonya sembuse wewe kikaragosi” Neema akacheka na kumwambia Lazaro tena kwa dharau zaidi ya mwanzo, “Yani umenipiga mimi kibao eeh!! Sasa nakwambia hiki kibao ulichonipiga kitakutesa wewe na familia yako na hapo ndio utaujua ukikaragosi wangu mbweha wewe” Ikabidi Ibra aingilie kati kwani aliona kamavile mzozo ungekuwa mkubwa zaidi na kumsihi rafiki yake apunguze hasira ila Neema aliendelea kuongea, “Tena umsihi sana ten asana maana hanijui vizuri huyo, sasa nitamuonyesha kuwa mimi ni nani” Kisha akamshika mkono mke wa Ibra na kumwambia, “Tuondoke” Kabla hata Sophia hajasema chochote alijikuta akifatana tu na Neema na kuondoka eneo lile. Ibra na Lazaro walibakia mahali pale kisha Lazaro akamwambia rafiki yake kuwa awe makini sana, “Kuwa makini Ibra haiwezekani wanawake wakatupanda kichwani namna hii” “Ndugu yangu, kuna wanawake wa ukweli na wanawake wa uongo, sio kila mwanamke ni mwanamke kweli. Wewe mwenyewe ulisema kuwa nyumbani kwangu si pa kawaida na umegoma kuja tena, basi pale nyumbani kwangu toka amekuja huyo Neema ndio kumekuwa na matatizo sasa utasema ni mwanamke wa kawaida Yule???” “Ila Ibra ngoja nitamuagiza mke wangu aje akupe ushauri wa kiroho maana bila ya hivyo huyu Neema atakusumnbua tu na uchawi wake” Ibra akatulia kwanza na kutafakari uchawi wa Neema bila ya jibu ukizingatia wanafanyiwa vioja kila leo, akawaza kuwa hata anavyoulizwa na mkewe kuhusu jana huenda kuna kitu kilitokea ingawa hakuwa na uhakika zaidi. Lazaro aliamua kumuaga pale rafiki yake na kuondoka huku akimsisitiza kuwa ni lazima wapate msaada wa matatizo ya huyo Neema, Ibra aliitikia huku akiendelea na mawazo yake. Akajaribu kurudisha kumbukumbu zake kwa siku ya jana ili aweze kujua kuwa alikuwa wapi, akakumbuka alivyotoka chumbani na mke wake muda Neema amewaita na jinsi alivyomsema Neema kuwa ni mchawi mbele ya macho yake, kisha akakumbuka jinsi mkewe alivyoinuka na kuelekea chumbani kanakwamba hakuna ya maana yanayozungumzwa pale. Halafu akakumbuka kuwa mkewe alivyoinuka kuna kitu alipuliziwa na Neema na kumfanya aanguke chini ndio hakukumbuka kulichoendelea hadi asubuhi yake alipoamshwa na mkewe, “Mmmh kwakweli huyu Neema ni mchawi tena mchawi kabisa aliyekubuhu, hivi tunawezaje kuishi na mtu mchawi kiasi kile kama Neema jamani yani hadi nyumba yangu naiona chungu” Wakati akiwaza hayo, alikuja rafiki yake ambaye ni mfanyabiashara mwenzie wa eneo lile aliyejulikana kama baba John ambaye kwa muda huo ndio alimshtua toka kwenye yale mawazo. “Vipi wewe umeanza kuchanganyikiwa au?” “Hapana ndugu yangu ila kuna mambo yananitatiza bhana” “Mambo gani hayo?” “Msaidizi wetu wa kazi nyumbani ni mchawi kwakweli anatutesa sana yani sina raha” “Si umtimue jomba, kwanini uendelee kufuga maradhi?” “Kumtimua si kazi rahisi, tushajaribu mara nyingi imeshindikana baba John yani nachanganyikiwa hadi sijui cha kufanya” Baba John akafikiria kidogo kisha akamwambia Ibra, “Eeeh nimekumbuka kitu, kuna mganga wa kienyeji huyo ni khatari ndugu yangu yani huyo mtu mbona ataondoka bila kuaga” “Dah itakuwa vyema sana kama utanipeleka huko ndugu yangu kwakweli nimechoka, au kamavipi tufunge unipeleke hata muda huu” “Dah kweli umechoka ndugu yangu pole sana, ngoja nimuite dogo abaki pale dukani twende” “Sawa, mimi nipo tayari ndugu yangu” Baba John akatoka na kumuacha Ibra akifunga funga ile biashara yake ili aende huko kwa mganga wa kienyeji. Ibra na baba John waliongozana hadi kwa huyo mganga ambaye baba John alimueleza Ibra, walikuta kuna mtu ndani kwahiyo wakasubiri atoke kwanza, baba John aliendelea kumsisitiza Ibra kuwa hapo wapo mahali sahihi na tatizo lao litafika mwisho. Yule mtu alipotoka waliingia wao na moja kwa moja Yule mganga alianza kuwaeleza matatizo yao; “Naona baba Jumatano umekuja na mwenzio, unahuruma sana wewe yani angekuwa ni mtu mwingine asingeweza kushirikiana na huyu kumleta huku. Sasa kijana matatizo yako tumeshayajua ila ni mazito kidogo sema tutajitahidi hivyo hivyo tukusaidie” “Nashukuru sana wazee, kwakweli naomba mnisaidie sana yani mambo yamenifika kooni sina raha sina amani wala sina furaha naomba tu mnisaidie niondokane nayo” “Sawa, sisi tutakupa dawa ila inatakiwa ufate masharti ya dawa yetu” “Nipo tayari kwa masharti yenu” “Hii dawa, ukiwa umefika nyumbani kwako yani kabla hujaingia ndani ilambe kisha ingia ndani ila ukishaingia ndani usiongee na kiumbe yeyote Yule….” “Hata mke wangu!!” “Elewa maana ya kiumbe yeyote Yule, yani usiongee chochote wewe fanya mambo yako kimya kimya tu mpaka muda wa kulala ilambe tena na ulale. Pakikucha ilambe tena yani nakwambia kile kitendo cha wewe kutoka kwenda kwenye shughuli zako ndio muda huo huo Yule kiumbe nae atafungasha virago vyake na kuondoka” “Asante sana ndugu mganga kwakweli nitafata masharti vilivyo sitakosea hata kidogo” “Jitahidi sana usikosee masharti, maana ukikosea yatakayokupata mimi simo” “Yani siwezi kukosea hata kidogo kwahiyo usijali kuhusu hilo” Wakamuaga Yule mganga na kuondoka eneo lile, wakiwa njiani ikabidi Ibra amuulize baba John; “Ndugu yangu vipi Yule mganga kakuita baba Jumatano wakati mwanao anaitwa John??” “Ibra, kwenye maisha kuna siri nyingi sana ila ngoja nikwambie kuhusu mwanangu John.” “Eeeh niambie ndugu yangu” “Mke wangu mimi alikuwa hashiki mimba ndio tukaenda kwa Yule mganga, akatufanyia dawa hadi mke wangu akapata mimba halafu mganga akasema siku mke wangu atakapojifungua huyo mtoto basi tunatakiwa tumuite huyo mtoto jina la siku hiyo, sasa mke wangu akajifungua siku ya Jumatano hapo ndio ikawa kimbembe maana sijawahi hata siku moja kusikia mtu akiitwa Jumatano ndipo tulipoamua kumuita mtoto John ila jina lake halisi ni Jumatano yani tumemuita John ili watu wasiulize ulize sana. Bora hata tungempata Jumanne wakina Jumanne wapo kuliko hiyo Jumatano. Kwahiyo huyu mganga siku zote huniita baba Jumatano sababu anajua siri iliyojificha kwa mtoto wetu” “Dah ila huyu mganga atakuwa vizuri sana, ngoja nimalize haya halafu nije tena labda anisaidie na matatizo yangu mengine” “Hata usiwe na shaka Yule mzee ni kiboko” “Basi ngoja tuzunguke kidogo hata nikirudi nyumbani muda uwe umeenda enda niweze kufata masharti vizuri” Baba John akamshauri warudi kwenye biashara ili wakamalizie muda huko, kwahiyo walikubaliana na kuongozana kwenye biashara zao. Sophia alishtuka usingizini na kuamua kwenda sebleni huku akijishika kichwa na kulalamika kuwa kinamuuma sana, Neema alimpa pole na kumwambia kuwa anywe maji mengi kitapoa. “Unajua nimeota ndoto ambayo siielewi hadi sasa” “Ndoto gani hiyo dada” “Nimeota eti mimi na wewe tumetoka hapa nyumbani na kuelekea kwenye biashara ya Ibra, halafu tukamkuta na rafiki yake ambaye uligombana nae na akakupiga kibao kisha wewe ukanishika mkono kuwa tuondoke. Nimeshangaa kuamka najikuta kitandani kumbe ni ndoto loh!” Neema akacheka na kumwambia Sophia; “Kweli hiyo ni ndoto dada yani mimi nipigwe kibao halafu nimuangalie tu huyo mtu nimechanganyikiwa au!” “Kwahiyo ingekuwa kweli ungemfanyaje?” “Ningemrudishia, yani nisingeweza kukubali kupigwa kizembe namna hiyo.” “Ila leo inaonekana nimelala sana yani hata sikumbuki muda gani nimekula” “Dada jamani itakuwa mimba nyingine hiyo inakunyemelea” “Dah bora iwe kweli maana nimemiss kushika shika tumbo langu na kuongea na mwanangu angali tumboni yani nimemkumbuka sana ungawa sikuiona sura yake” “Usijali dada, utampata mwingine tu, ila hata hivyo nakuhisi kama una mimba vile” “Mmmh Neema ndio fasta hivyo jamani, ila natamani niipate nitafurahi sana” “Ila ili uwe salama usionane kabisa na Yule Jane dada yangu.” “Nani aonane na Yule shetani yani siwezi kabisa, sijui Ibra vipi maana ndio anaonanaga nae” “Mumeo ana matatizo sana, ila dada una mimba” “Mmmh kweli Neema?” “Ndio ni kweli nimeona bora tu nikwambie” “Uwiiii Ibra atafurahi sana nikimwambia, unajua mimi huwa naamini sana maneno yako Neema. Sina hata haja ya kupima” Muda kidogo Ibra akaingia ndani ila hakuwasaliia wala nini na kupitiliza chumbani, Sophia na Neema wakaangaliana kisha Neema akamuuliza Sophia; “Kwani shemeji ana matatizo gani dada?” “Hata naelewa basi, yani kama hajatuona vile” “Hebu mfate umuulize, asipokujibu basi jaribu kumwambia swala lako la mimba na kama akiwa kimya jifanye unaumwa” “Sawa sawa, ngoja niende” Sophia akainuka pale na kuelekea chumbani alipo Ibra. Alimkuta Ibra akiwa amejilaza kitandani, Sophia akamuamsha na kumuuliza tatizo ni nini ila Ibra alikuwa kimya tu, “Jamani mume wangu nani kakuudhi jamani? Ibra wa kuninyamazia mimi wewe?” Ibra alikuwa kimya tu hakumjibu kitu chochote mke wake na wala hakuonyesha kujali vile alivyokuwa akiulizwa na Sophia. Kwakweli Sophia alikuwa anapatwa na hasira tu vile mumewe alikuwa hamjibu, kisha akamwambia “Ibra, mwenzako nina mimba” Ibra bado yupo kimya tu. “Jamani mume wangu hata kufurahia jamani, inamaana hutaki mtoto tena mume wangu!” Ibra hakujibu chochote na kuzidi kumsononesha Sophia kwani alikosa raha kabisa vile ambavyo alikuwa hajibiwi na mumewe. Kimya kikatawala mule ndani, muda kidogo Sophia alijitupa chini na kuanza kulalamika kuwa tumbo linamuuma sana huku akijinyonga nyonga na kulia, Ibra akataka kumuinua mkewe ili amuwaishe hospitali ila Sophia alikuwa anagoma kuinuka na kuendelea kujinyonga nyonga tumbo, kwakweli Ibra alihisi kuchanganyikiwa kwani alitamani kuongea Ila akikumbuka masharti aliogopa kuongea ila akiangalia hali ya mkewe alitishika zaidi, mara gafla Sophia akawa pale chini kimya kabisa na kumfanya Ibra uoga umshike zaidi na kuanza kumsukuma sukuma mkewe kama ishara ya kumuamsha ila wapi yani hakushtuka hata kidogo na kumfanya Ibra azidi kupatwa na hofu. Akaamua kumnyanyua, ila alipomnyanyua tu alishangaa damu zikimtoka Sophia kama maji, yani hapo Ibra alichanganyikiwa kupita maelezo ya kawaida na kutoka nje na mke wake. Wakati anapita sebleni alimkuta Neema amekaa huku akicheka sana ila Ibra bado aliendelea na msimamo wake wa kutokuongea chochote ila wakati anatoka akajikwaa mlangoni na kufanya yeye na mkewe waanguke chini. Itaendelea kama kawaida………….!!!!!!!!!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 27 Sophia akiwa pale getini gafla akamuona Ibra akija akiwa ameongozana na mwanamke, kwakweli Sophia hakufikiria mara mbili kwani alijikuta akijawa na hasira na moja kwa moja akaenda kumsukuma Yule mwanamke ambaye alianguka vibaya sana. Kwakweli Ibra hakuwa na la kusema zaidi ya kumkimbilia Yule mwanamke pale chini na kumshikilia huku akimlaumu mke wake, “Jamani Sophia ndio umefanya nini sasa jamani?” “Nimefanya nini? Hebu niondolee huyo Malaya wako upesi” “Utajutia kwa hiki ulichokifanya, njoo ukae nae hapa nikafate usafiri tumpeleke hospitali” Sophia akacheka kile kicheko cha hasira na kumwambia mumewe, “Yani unapoenda kutafuta huo usafiri mbebe na huyo kinyago wako uondoke nae la sivyo utakuta nimeshammaliza kitambo sana” Kwakweli Ibra hakuweza kuelewa kwa haraka kilichompata mke wake kwa muda huo mpaka kuwa hivyo, Ibra aliamua kumnyanyua mke wa Lazaro na kumweka begani kwani alikuwa akichuruzika damu ukizingatia aliangukia kwenye jiwe. Ibra akainuka na kuanza kuondoka na Yule mwanamke ila akamsikia mke wake akisema, “Na upotelee huko huko na huyo mwanamke shwaini wewe” Kisha Sophia akarudi ndani ila alipokaa akaanza kulia kwa hasira huku wivu ukiwa umemjaa kwani aliona ndio kampa ruhusa kabisa mumewe ya kufanya vile alivyofanya, alilia kwa uchungu sana ambapo Neema alimsogelea na kuanza kumbembeleza, “Yani Ibra Ibra kwanini amenifanyia hivi jamani!! Mtu kama amekuchoka si akwambie tu, bora nirudi kwetu maana sijauwa mimi jamani siwezi kuvumilia haya mateso” “Nyamaza dada, mbona haya sio mateso hata kidogo. Hivi unawajua wanaume watesaji wewe? Kwanza kwa kifupi tu nikwambie dada yangu usipende sana kumuamini mwanaume yani utajuta maisha yako yote. Mwanaume hatakiwi kuaminiwa dada yangu, madhara yake ndio hayo unalia hadi unachanganyikiwa. Tatizo lako umempenda sana ila usingempenda wala usingeumia hivyo ila mimi nitakusaidia” “Utanisaidiaje sasa Neema jamani? Sijaweza kuamini kabisa kama Ibra anaweza kunisaliti jamani kwajinsi tunavyopendana” “Sio kwa jinsi mnavyopendana ni kwajinsi unavyompenda yani nikikupa siri ya mumeo kwa hakika hutaweza kuamini. Mumeo hajatulia kabisa ni tofauti na unavyomfikiria, mimi mwenyewe amewahi kunitongoza ila kulinda heshima yenu nikamkataa kwahiyo usimuamini sana. Sasa ili kufanya moyo wako usiumie sana unatakiwa kuwa na mwanaume mwingine dada” Sophia alikaa kimya bila ya kujibu chochote kisha akainuka na kuelekea chumbani kwake ambako alienda kulia vizuri sasa sababu alikuwa mwenyewe. Ibra alifika na mke wa Lazaro hospitali ambapo alipokelewa na madaktari na kuanza kupewa matibabu, kwakweli Ibra hakuweza kuondoka kwani yeye ndio chanzo cha kila kitu. Kwahiyo alichokifanya ni kuchukua simu yake na kumpigia Lazaro ambaye kwa muda ule alipatikana hewani. Baada ya muda mfupi Lazaro aliwasili pale hospitali na kutaka kumuona mke wake ambapo aliambiwa kuwa asubiri kwanza. “Hivi kwani imekuwaje Ibra?” Ikabidi Ibra amsimulie kilichotokea ila Lazaro hakupendezewa kabisa, “Lakini Ibra nilikwambia jamani mke wangu asiende kwanza nyumbani kwako, nilikwambia afike pale kwenye biashara yako kwanza ili akupe ushauri wa kiroho kabla ya mambo yote” “Mi sijaona tatizo maana mkeo ni mwanamaombi kwahiyo nilimpeleka nyumbani akapambane na Yule mchawi” “Hatuendi hivyo ndugu yangu, yani sijui kama unaweza kunielewa wewe. Ile nyumba yako imetawaliwa na nguvu za giza” “Sio nyumba yangu, pale mbaya ni mtu mmoja tu wala sio nyumba yangu” “Na nyumba yako pia inatakiwa ifanyiwe maombi ya nguvu ila tatizo lako unapenda kukurupuka. Yani mke wangu kwakweli Mungu amsaidie apone, itabidi kesho nije na mchungaji hapa anisaidie maombi” “Haya, ila hapa wanaomponya ni madaktari na sio huyo mchungaji wako” Lazaro aliamua kuwa kimya tu kwani aliona mtu anaebishana nae atakuwa na matatizo ya ziada. Asubuhi na mapema Ibra aliamua kurudi nyumbani kwake ila alipofika kila atakachomsemesha mke wake alimkalia kimya tu na kumfanya Ibra agundue kuwa mkewe amemnunia kisha akaenda kuoga na kujiandaa halafu akatoka kuelekea tena hospitali kumuona mke wa Lazaro ila alikuta ameshatoka hivyo ikabidi aelekee nyumbani kwa Lazaro ambapo aliwakuta wakiwepo na watu kadhaa, kuna mmoja alionekana akiongea sana ila uongeaji wake ulikuwa ni wa kufundisha, “Mnajua kuna ajari zingine huwa zinapangwa na mapepo halafu zinatekelezwa na wanadamu ambao hawajui njama za mapepo hayo, kwahiyo ni muhimu sana kujikabidhi mbele za Mungu wakati wote.” “Ila mke wangu ni mwanamaombi mzuri sana sasa sijui kwanini imekuwa hivyo” “Usiulize kwanini ila tambua kwamba ni jaribu tu ambalo lipo kwaajili ya kupima imani yake ila Mungu atamsaidia na atapona kabisa” Ibra alikuwa akiwasikiliza tu, kisha akakatisha maongezi yao kwa kutaka kujua hali ya mgonjwa, “Lakini vipi maendeleo ya shemeji?” “Anaendelea vizuri ila tu amepumzika kwasasa” Yule mtu aliyekuwa akifundisha alimuangalia Ibra na kumwambia, “Kijana unaonekana kuwa na matatizo ila unamichanganyo mingi sana” “Hapana sina michanganyo yoyote” “Ila Ibra rafiki yangu mbona mbishi hivyo? Mara nyingine uwe unatulia ukisikiliza unachotaka kufundishwa” “Hata hivyo nina haraka sana nilipita tu mara moja kumuangalia shemeji” Kisha akainuka na kuwaaga, ambapo alienda moja kwa moja kwenye gari yake na kuanza kuondoka huku akijisemea, “Wanafikiri siwajui, anataka anihubirie pale siku nzima na mwisho wa siku aniombe sadaka. Mambo yangu yenyewe yamenishinda halafu nianze kutoatoa sadaka zisizokuwa na mpango! Mmh siwezi kabisa, wanaweza hao hao wakina Lazaro ndiomana hawaendelei” Ibra akaondoka zake na kwenda moja kwa moja kwenye biashara zake. Alipofika alimkuta rafiki yake baba John ambaye baada ya salamu alimuuliza kama alifanikisha na kumuuliza pia kuwa kwanini jana hakuonekana kwenye biashara, “Majanga ndugu yangu” “Majanga gani tena?” “Yani wee acha tu” “Au ulikosea masharti?” Ikabidi Ibra amsimulie vile ilivyokuwa, “Yani nimejitahidi kwa kila hali ili kufanikisha lile swala ila mwisho wa siku masharti yakanishinda” “Yani sharti jepesi kama lile ukashindwa duh!! Mbona mi na mke wangu tuliweza yani tuliishi ndani siku tatu bila ya kuongea chochote hebu fikiria yani tulikuwa tunafanya tendo la ndoa siku zote hizo tatu bila ya kuzungumza na hatimaye tukampata mtoto wetu John yani wewe siku moja tu umeshindwa dah!” “Mkeo ni muelewa baba John sio kama mke wangu mimi, sijui Yule mganga atanielewa?” “Yani katika vitu ambavyo Yule mganga hapendi ni kukosea masharti, kwakweli nakuhurumia sana na sijui kama atakuelewa” Ibra alijikuta akikata tama kabisa ila mwenzie alimwambia kuwa asikate tama na wataenda kujaribu tena kesho yake kama atawaelewa. Sophia alikuwa amekaa ndani na Neema huku akimwambia, “Yani yule mwanaume nitamnunia hadi ashike adabu yake” “Ndio vizuri hivyo, unatakiwa kuwa ngangari sio kila siku usumbuliwe na mapenzi kwenye kichwa chako yani kama ulivyompenda yeye basi unaouwezo wa kumpenda mwingine vilevile tena na zaidi” “Mmh ila sijui kama naweza kumpenda mwingine kama ninavyompenda Ibra maana Ibra nampenda sana, unajua nimemvumilia sana hadi leo nipo nae sababu ya uvumilivu wangu hata namshangaa ananilipa kwa kunisaliti dah!” “Dada, mwanaume si mama yako wala baba yako kusema akuhurumie eti asikusaliti, asilimia kubwa ya wanaume akipata vijihela kidogo tu basi ni shida na tatizo. Pole sana ila utampata mwingine tu” “Ila mi ningependa ajirekebishe” “Ili ajirekebishe unatakiwa kuwa na mwinginme, halafu cha muhimu ni kuendelee kumnunia ili umshikishe adabu” Sophia akakubaliana na Neema kwani aliona ndio njia pekee ya kumkomesha mume wake. Jioni Ibra aliwasili nyumbani kwake na kuwakuta Sophia na Neema pale sebleni kisha akamsalimia mke wake ila alikuwa kimya tu na kumfanya aelekee chumbani huku akijiuliza kuwa mkewe ana tatizo gani, alijiuliza sana bila ya kupata jibu. Muda wa kulala ulipofika, moja kwa moja Sophia aliingia chumbani na kujilaza ambapo Ibra alianza kujiongelesha tena, “Hivi Sophia utaendelea kuninunia hivi mpaka lini? Ujue sikuelewi mke wangu halafu unaniumiza sana kwani sijui kosa langu hadi uninunie hivyo” Sophia alikuwa kimya tu huku akibedua bedua midomo yake na kujilaza vizuri, kwakweli Ibra hakuwa na la kufanya na kuamua nay eye kulala. Kulipokucha, asubuhi na mapema Ibra aliamka na kujiandaa kwenda kwenye shughuli zake ila kabla hajaondoka kama kawaida yake alimuamsha mkewe kwa lengo la kumuaga. “Za kuamka mke wangu, mi natoka naenda kwenye shughuli zangu” Hakujibiwa pia ila alimsogelea mkewe na kumbusu kwenye paji la uso kisha akaondoka zake. Sophia nae akaamka na kuelekea sebleni huku akijiongelesha, “Hata sijui kwanini nimeliachia jinga lile linibusu kwenye paji la uso kunitia nuksi tu” Neema akaanza kucheka, “Mbona unacheka hivyo?” “Nimefurahi tu, na Yule usipokuwa makini atakutia nuksi kweli” “Sijui ni nani anaemshauri ujinga mume wangu” “Kheee kumbe hujui! Ni rafiki yake Lazaro, Yule kijana ni mjinga sana halafu ubaya zaidi ni mchawi” “Kheee kumbe ni mchawi?” “Ndio, tena anamuonea wivu sana kaka ila yeye hajui tu. Siku akigundua atajilaumu sana kuwa nae pamoja” “Sasa nifanye nini?” “Ngoja nitakufundisha kitu, yani watagombana na hawatapatana tena” “Dah nitafurahi sana” Neema akatabasamu tu kwa muda huo. Ibra akaenda kwenye shughuli zake kisha moja kwa moja akamfata baba John ambaye walipanga kuwa siku hiyo wataenda tena kwa Yule mganga, “Tutaenda saa ngapi ndugu yangu?” “Subiri subiri kwenye mida ya saa sita na nusu hivi tutaenda maana saizi atakuwa na wateja wengi sana” Wakakubaliana kuwa wataondoka mida hiyo kisha kila mmoja kuendelea na shughuli zake kwa muda huo. Mida ilipofika Ibra alienda tena kumkumbusha baba John ambapo wakaianza safari ya kwenda kwa Yule mganga, walipokuwa njiani Ibra akapokea ujumbe kwenye simu yake ambao ulimshtua sana hadi baba John naye akamuuliza kuwa tatizo ni nini, “Hebu soma na wewe” Ibra alimpa baba John ile simu na kusoma pia ule ujumbe, “Mmh inawezekana kweli shemeji akawa na mwanaume mwingine?” “Kama sio kweli, imekuwaje huyu aliyeandika kusema kuwa amemuona hotelini na huyo mwanaume mida hii? Pengine ndiomana ananinunia ndani” “Duh! Ila mimi siamini, kwavile ameandika jina la hoteli na chumba walichopo kwanini tusiende kuwafumania” “Hilo ni wazo zuri sana, kwakweli mimi nitaua mtu jamani, mke anauma sana hivi wanajua nimemuhudumia vipi mke wangu mpaka kawa vile? Roho inaniuma sana” Baba John alimpooza pale kisha wakageuza gari na kuelekea kwenye hiyo hoteli. Walifika kwenye hoteli ile na palikuwa kimya sana, moja kwa moja wakaenda kwenye chumba walichoelekezwa na kugonga ambapo aliyefungua alikuwa Sophia na alipoona ni mumewe moja kwa moja akaenda kukumbatia Lazaro, kwakweli Ibra alishikwa na hasira za ajabu akawasogelea na kumsukuma mkewe ambaye alianguka chini kisha akampiga ngumi nzito Lazaro na kumfanya aanguke pia halafu akaenda pale chini na kuzidi kumshindilia ngumi za usoni, ikabidi baba John awaamulie ambapo Ibra kwa hasira alimshika mkewe mkono na kutoka naye kwenye hoteli ile. Baba John alimuangalia Lazaro huku akisikitika, “Kwanini umemfanyia hivi rafiki yako? Kweli kabisa Lazaro wewe ni wa kumsaliti Ibra kweli?” “Kwakweli mpaka muda huu nashangaa tu yani hata sielewi, mnanipa lawama za bure jamani” Lazaro alikuwa akitokwa na damu tu, ikabidi baba John amsaidie na kuanza kumkokota ili kumpeleka hospitali. Ibra alifika na mkewe nyumbani huku akiwa amefura kwa hasira, na kuingia na Sophia ndani huku akifoka, “Yani Sophia umeninunia kumbe unanisaliati, kwakweli siwezi kuvumilia hili” Akamnasa kibao Sophia kilichompeleka hadi chini na kuwa kimya kabisa, Neema akamsogelea na kumwambia “Hivi unawezaje kumpiga mwanamke kiasi hiko?” “Na wewe usiniongeleshe, nisije nikakupiga bure” Neema akacheka na kumwambia, “Yani kunipiga mimi sahau tena sahau kabisa” Kisha akampulizia kitu usoni ambapo Ibra alianguka chini na kupoteza fahamu. Ibra na Sophia walipozinduka walijikuta wamelala kitandani tena wakiwa wamekumbatiana. Itaendelea kama kawaida…………..!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 26 Akaamua kumnyanyua, ila alipomnyanyua tu alishangaa damu zikimtoka Sophia kama maji, yani hapo Ibra alichanganyikiwa kupita maelezo ya kawaida na kutoka nje na mke wake. Wakati anapita sebleni alimkuta Neema amekaa huku akicheka sana ila Ibra bado aliendelea na msimamo wake wa kutokuongea chochote ila wakati anatoka akajikwaa mlangoni na kufanya yeye na mkewe waanguke chini. Kwakweli kile kitendo cha kujikwaa na kuanguka kilimpa maumivu sana Ibra na kumfanya augulie kwa muda kidogo kisha kuinuka na kumuingiza mkewe kwenye gari akielekea nae hospitali. Walipofika hospitali walipokelewa ila kwavile Sophia hakuwa na ufahamu wowote ikabidi daktari azungumze na Ibra ili ajue nini chanzo, “Vipi wewe ni bubu?” Ibra aliangua kilio kwakweli kwani alijiona wazi zoezi likimshinda, “Una matatizo gani wewe? Una kichaa au? Una mahusiano gani na mgonjwa na ugonjwa wake umeanza vipi? Sema basi ili tumuhudumie mgonjwa au la tutampoteza huyu” Ibra alijikuta akiongea kwa huzuni sana, “Kwani wale wagonjwa wanaoletwa na mabubu mnawahudumiaje?” “Mabubu huwa wanafanya vitendo na wanaeleweka sasa wewe unatulilia halafu sisi tutafanye, haya sasa elezea matatizo ya mgonjwa” “Hata sijui kwakweli ameanza gafla tu” Daktari akamuhoji hoji pale Ibra kisha akaandika maelezo na kuendelea kumshughulikia mgonjwa, kwakweli Ibra aliwaza sana; “Amakweli ng’ombe wa masikini hazai yani kujitahidi kote kule na sharti nililopewa na mganga mwishowe yamenishinda dah!” Ibra aliumia sana rohoni na kukosa raha kabisa ila ndio hivyo ilishatokea. Ibra aliitwa na daktari na kuelezwa kuwa Sophia alikuwa na mimba ila hiyo mimba imetoka. “Ila dokta unajua siku si nyingi tulikuwa hospitali mke wangu mimba yake ilitoka sasa kumbe alishapata nyingine tayari nayo imetoka dah!!” “Usishangae sana, mwanamke ambaye mimba imetoka au kuharibika mara nyingi kizazi chake kinakuwa wazi sana na kinakuwa tayari kubeba mimba nyingine kwa wakati wowote ule. Mimba ya mkeo imetoka ila ilikuwa changa sana yani haikuwa hata na wiki ila ndio hivyo imetoka. Kwasababu alishawahi kupatwa na matatizo ya hivi ndiomana ameumwa sana. Pole sana ndugu yangu kwa kuipoteza hii mimba” “Ila sababu ni nini dokta hadi mimba ya mke wangu kutoka?” “Sababu huwa ni nyingi ila nadhani alianguka, maana mimba ikiwa changa namna hii inakuwa bado haijajishikilia vizuri” Ibra aliishia kusikitika tu huku akijiuliza kuwa huenda pale walivyojikwaaa na kuanguka ndio kumesababisha yote yale ila alijiuliza kuwa mbona mkewe alianza kutokwa damu kabla ya kuanguka pale na kukosa jibu la moja kwa moja. Karibia na alfajiri Sophia alizinduka na kuitiwa mumewe ambapo alipewa taarifa za kutoka kwa mimba yake, kwakweli Sophia alijikuta akilia sana na kumuuliza Ibra kuwa kwanini imekuwa vile. “Ni mkosi gani huu mume wangu jamani, ni kitu gani hiki? Kwanini sisi jamani? Wiki mbili zilizopitz tulikuwa hapa hospitali mimba yangu kubwa ilikuwa imetoka halafu leo mimba yangu change ni nini hiki jamani?” “Pole sana mke wangu, kwakweli hata mimi sina majibu kabisa naishia kuchanganyikiwa tu Sophia” “Halafu imekuwaje hadi nimeumwa hivi jamani!” Sophia akakumbuka mara ya mwisho kuwa alikuwa akimuigizia tu mumewe kuwa anaumwa sasa ameshangaa kiasi cha kuigiza hadi kuja kulazwa hospitali vile, “Mke wangu ilikuwa gafla tu yani ulianza kulalamika tumbo” “Ila sikuwa serious wala nini, nilikuwa natania tu” “Ulikuwa unatania kivipi?” “Nilikuwa nakutania ili uongee, sasa nashangaanimeumwa kweli” “Nani aliyekutuma unitanie ugonjwa?” “Neema alisema tufanye hivyo” Ibra akawa kimya kwa muda kisha akamwambia mkewe, “Yani wewe ni bure kabisa, wewe ni bure bure bure. Umeona sasa faida ya ujinga wako? Huwa hakuna masikhara kwenye mambo ya ugonjwa. Ngoja tukirudi nyumbani nikuelezee vizuri ujinga wako” Sophia akasononeka na kuwa kimya kwani hakupendezewa jinsi mumewe alivyomwambia kuwa ni mjinga. Walisubiri hadi daktari alipowapa ruhusa ya kurudi nyumbani na kuanza safari ya kurudi sasa. Walipofika nyumbani kama kawaida walimkuta Neema akiwa amekaa sebleni, ila alipowaona tu aliwakaribisha vizuri sana. “Karibuni jamani, karibuni sana” Ibra hakujibu hata ile karibu ya Neema kwani alijua wazi jinsi ilivyo ya kinafki, Neema alimuangalia Sophia na kumpa pole “Pole sana dada” “Asante, yani hata sijui nina mkosi gani jamani” Ibra aliwaacha pale sebleni kisha akaenda chumbani kujiandaa na kuondoka zake huku akiwa hana furaha kabisa. Sophia alibaki na Neema kisha akamuuliza, “Hivi Neema, mimi na wewe si tulipanga kuwa nimuongopee Ibra naumwa ili aongee sasa imekuwaje jamani?” “Kheeee unaniuliza mimi!! Nitajuaje sasa? Yani mimi mwenyewe nimebaki kushangaa tu, kwani ilikuwaje maana tulipanga uigize hata nikashangaa Ibra akikutoa chumbani mbio mbio kuwa unaumwa sana” “Yani hata sielewi, nilikuwa namuigizia Ibra kuwa tumbo linaniuma sana, wakati najikunja kunja kiuongo uongo sijui ikawaje eti nikazimia pale chini. Unajua nimekuja kushtuka niko hospitali na ninaambiwa kuwa mimba yangu imetoka jamani, kwanini mimi jamani kwanini?” “Pole sana dada, ila mbaya ni mumeo sababu alianguka na wewe hapo mlangoni nadhani ndio amesababisha mimba yako itoke. Kwanza kilichokuwa kinamfanya asiongee ni nini?” “Hata sielewi jamani huyu mwanaume ana matatizo gani” “Ila usijali dada utapata tu mimba nyinginme” Sophia alisononeka tu pale kisha akainuka na kuelekea chumbani kupumzika, ila leo Neema hakumwambia habari ya chakula wala nini. Akili ya Ibra haikuwa sawa kabisa, alipotoka nyumbani kwake aliwaza kuwa aelekee wapi ili akapooze mawazo kidogo, kwanza akaamua kwenda hotelini ambapo aliagiza kinywaji na kunywa ili kupoteza mawazo ila wapi mawazo yalizidi kumtawala na kumuumiza, akaamua ampigie rafiki yake Lazaro ili kumuomba ushauri ambapo Lazaro alivyopokea tu akaanza kumlaumu. “Nasikia jana ukaenda kwa mganga wa kienyeji, ila rafiki yangu mbona unapenda kujichanganya jamani?” “Kujichanganya vipi wakati nina matatizo?” “Sasa mimi si nilikwambia usubiri mke wangu aje akupe maneno ya kiroho, sasa kwa kujichanganya hivyo tutafika kweli na nyumba yako ile ilivyonzito?” “Aaah Lazaro na wewe unanichanganya tu, huyo mkeo si umwambie aje tu nyumbani?” “Pale nyumbani kwako hapafai kwasasa Ibra, inatakiwa azungumze na wewe kwanza kabla ya kuja nyumbani kwako” “Hebu nipe niongee nae” “Hayupo na atachelewa kurudi kidogo leo, ila kuwa makini sana Ibra na maamuzi yako” Kisha Ibra akakata simu na kuona kamavile pale hotelini hapamfai tena kwahiyo akaamua kuondoka. Moja kwa moja Ibra alielekea ufukweni ambapo alikaa kwenye michanga huku akiwaza sana, “Hivi nitawezaje kumtoa Yule mtu kwenye nyumba yangu jamani? Nitawezaje mimi? Yani mtihani wangu ulikuwa unafika mwisho lakini mke wangu ndio kauharibu sababu ya kupandikizwa ujinga na Neema jamani! Yani Sophy hata ameshindwa kutumia akili na kuanza kuniigizia ugonjwa hadi mwisho wa siku kaumwa kweli. Yule mwanamke hana akili kabisa sijui hata amekuwaje jamani” Ibra alikuwa na mawazo sana ila kuna mtu alimshika began a kumshtua kutoka kwenye yale mawazo aliyokuwa nayo, Ibra akageuka na kumkuta ni shemeji yake Tausi. “Kheee Tausi!!” “Ndio shemeji, kumbe na nyie mnakujaga huku ufukweni? Dada yuko wapi?” “Yupo nyumbani, tena kuna kipindi tulitaka kuja kukuchukua ili ukaishi na sisi” “Waongo nyie shemeji hata hamkuwa na hilo lengo, hivi ni watu gani nyie hatuwasiliani wala hatujui mnaendeleaje yani mama analalamika kweli utafikiri mnaishi mkoa mwingine” “Dah!! Nisamehe sana shemeji yangu yani nisamehe bure hata sijui kwanini hatujawasiliana” “Haya, ngoja mi niende nimekuja na wenzangu wale pale” Tausi akaondoka na kumuacha Ibra akiwa mwenyewe na mawazo yake huku akipata swali jipya kichwani, “Ila ni kwanini hatuwatembelei ndugu zetu? Na kwanini wao hawatutembelei? Kuna nini hapa katikati jamani? Si mimi wala Sophia anaemkumbusha mwenzie kuhusu ndugu, ni kwanini?” Ibra aliwaza bila ya kupata jibu la moja kwa moja kwani alikuwa akijishangaa tu kuwa ni kitu gani kinawazuia kutembelea ndugu zao. Ibra akiwa pale ufukweni akakumbuka kuwa kuna siku aliwahi kujadiliana na mke wake kuhusu kumchukua huyo mdogo wa mkewe kwa lengo la kuwasaidia ila akashangaa kuwa lile wazo liliyeyukia wapi, kisha gafla likamjia wazo la Yule mtoto ambaye walikuwa wanamuona njiani kuwa aliishia wapi ila hakutaka kufikiria zaidi kisha akarudi kwenye gari lake kwa lengo la kuondoka. Alipofungua mlango wa gari akashangaa kwenye kile kiti cha dereva akiwa amekaa Yule mtoto aliyemfikiria muda mfupi uliopita, kwakweli Ibra alikuwa kapatwa na mshtuko wa hali ya juu na kujikuta akipiga kelele kisha kuanza kukimbia. Ibra alikimbia sana ila kwa bahati nzuri alikutana na mtu anayemfahamu njiani na alipomuangalia vizuri akagundua kuwa ni mke wa Lazaro na akaona ile ni nafasi ya pekee kwa yeye kwenda na mke wa Lazaro nyumbani kwake ili labda aweze kushuhudia kinachoendelea kwenye nyumba ile. “Shemeji afadhali nimekuona, naomba unisaidie tafadhali nisaidie” “Nikusaidie nini? Kwani umepatwa na nini shemeji na mbona ni usiku tayari?” “Nina matatizo shemeji hata gari yangu nimeiacha huko ufukweni tafadhali nisindikize nikalifate” “Kwani una nini jamani maana si kwa kuchanganyikiwa huko” “Nisaidie tafadhali, naomba twende wote” Kwakweli huyu mke wa Lazaro alijikuta akiingiwa na huruma kwani Ibra alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha akaanza kuongozana nae hadi huko ufukweni kufata gari. “Kheee kumbe mbali hivi yani hadi nimechoka, unajua Lazaro anajua nipo nkiani narudi nyumbani!” “Pole sana shemeji yangu ila mimi nina matatizo kwakweli” Walifika sehemu ambayo Ibra aliliacha gari yake na kulikuta palepale kisha Ibra akamuomba mke wa Lazaro alifungue ambapo alipolifungua hapakuwa na kitu chochote cha kustaajabisha. Kisha Ibra akamuomba aongozane nae hadi nyumbani kwake, “Ngoja nimpigie simu Lazaro kwanza ili asiwe na mashaka” Alipopiga simu ya Lazaro haikupatikana. “Mmmh kwakweli shemeji sitaweza kuongozana na wewe, acha kwanza niende nyumbani” Ibra aliamua kumuomba sana shemeji yake kwani alijiona kuwa peke yake hatoweza kuendesha lile gari kurudi nyumbani, alimuomba sana na kufanya mke wa Lazaro akubali kuongozana nae. Walipokaribia kufika Ibra alienda na ile gari moja kwa moja gereji na kuamua kuliacha hapo kwani hakutaka kwenda kuliweka nyumbani kwa siku hiyo. Kisha akamwambia mke wa Lazaro aongozane nae tu hadi kwake kwani hapakuwa mbali sana, “Tena itakuwa vyema ukamfahamu na mke wangu” “Sawa, ila mida nayo inakwenda sana, unajua huwa sipendi kwenda safari nisizozipanga ila twende tu kwavile una matatizo” Ibra akafurahi na kuongozana nae. Sophia wakati amelala akajiwa na ndoto ambayo ilimuonyesha watoto wawili kisha mmoja akaondoka ila alimkimbilia bila kumpata halafu pale alibakia mmoja ambapo alipojaribu kumfata alijikuta tu akishtuka, moja kwa moja akaangalia masaa ambayo yalikuwa yameenda sana na kumfanya aende sebleni ambapo alikuwepo Neema tu. Sophia alizidi kuangalia mida kwani masaa yalienda ila Ibra hakurudi, Sophia akamuuliza Neema “Hivi unafikiri huyu Ibra atakuwa na matatizo gani siku hizi?” “Nahisi atakuwa na mwanamke mwingine” “Mmh Neema hata mimi nimehisi hivyo, hivi inawezekana vipi kwa mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa mkewe akijua kuwa mke wangu ana matatizo kwasasa halafu aondoke na kuchelewa kurudi hivi?” “Pole sana dada ila nahisi Ibra atakuwa na mwanamke tu maana ni kawaida ya wanaume kubadilika pindi wapatapo wanawake wengine” Sophia akajikuta akijiwa na wivu kiasi huku muda nao ukiiendelea mbele na kumfanya azidi kuumia kichwa, “Yani mpaka saa nne hii hajarudi jamani, lazima Ibra ananisaliti tu.” Sophia alivimba kwa hasira na kisha akasema anaenda kumngoja getini ili amuone vizuri anavyokuja. Sophia akiwa pale getini gafla akamuona Ibra akija akiwa ameongozana na mwanamke, kwakweli Sophia hakufikiria mara mbili kwani alijikuta akijawa na hasira na moja kwa moja akaenda kumsukuma Yule mwanamke ambaye alianguka vibaya sana. Itaendelea kama kawaida. Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 27 Sophia akiwa pale getini gafla akamuona Ibra akija akiwa ameongozana na mwanamke, kwakweli Sophia hakufikiria mara mbili kwani alijikuta akijawa na hasira na moja kwa moja akaenda kumsukuma Yule mwanamke ambaye alianguka vibaya sana. Kwakweli Ibra hakuwa na la kusema zaidi ya kumkimbilia Yule mwanamke pale chini na kumshikilia huku akimlaumu mke wake, “Jamani Sophia ndio umefanya nini sasa jamani?” “Nimefanya nini? Hebu niondolee huyo Malaya wako upesi” “Utajutia kwa hiki ulichokifanya, njoo ukae nae hapa nikafate usafiri tumpeleke hospitali” Sophia akacheka kile kicheko cha hasira na kumwambia mumewe, “Yani unapoenda kutafuta huo usafiri mbebe na huyo kinyago wako uondoke nae la sivyo utakuta nimeshammaliza kitambo sana” Kwakweli Ibra hakuweza kuelewa kwa haraka kilichompata mke wake kwa muda huo mpaka kuwa hivyo, Ibra aliamua kumnyanyua mke wa Lazaro na kumweka begani kwani alikuwa akichuruzika damu ukizingatia aliangukia kwenye jiwe. Ibra akainuka na kuanza kuondoka na Yule mwanamke ila akamsikia mke wake akisema, “Na upotelee huko huko na huyo mwanamke shwaini wewe” Kisha Sophia akarudi ndani ila alipokaa akaanza kulia kwa hasira huku wivu ukiwa umemjaa kwani aliona ndio kampa ruhusa kabisa mumewe ya kufanya vile alivyofanya, alilia kwa uchungu sana ambapo Neema alimsogelea na kuanza kumbembeleza, “Yani Ibra Ibra kwanini amenifanyia hivi jamani!! Mtu kama amekuchoka si akwambie tu, bora nirudi kwetu maana sijauwa mimi jamani siwezi kuvumilia haya mateso” “Nyamaza dada, mbona haya sio mateso hata kidogo. Hivi unawajua wanaume watesaji wewe? Kwanza kwa kifupi tu nikwambie dada yangu usipende sana kumuamini mwanaume yani utajuta maisha yako yote. Mwanaume hatakiwi kuaminiwa dada yangu, madhara yake ndio hayo unalia hadi unachanganyikiwa. Tatizo lako umempenda sana ila usingempenda wala usingeumia hivyo ila mimi nitakusaidia” “Utanisaidiaje sasa Neema jamani? Sijaweza kuamini kabisa kama Ibra anaweza kunisaliti jamani kwajinsi tunavyopendana” “Sio kwa jinsi mnavyopendana ni kwajinsi unavyompenda yani nikikupa siri ya mumeo kwa hakika hutaweza kuamini. Mumeo hajatulia kabisa ni tofauti na unavyomfikiria, mimi mwenyewe amewahi kunitongoza ila kulinda heshima yenu nikamkataa kwahiyo usimuamini sana. Sasa ili kufanya moyo wako usiumie sana unatakiwa kuwa na mwanaume mwingine dada” Sophia alikaa kimya bila ya kujibu chochote kisha akainuka na kuelekea chumbani kwake ambako alienda kulia vizuri sasa sababu alikuwa mwenyewe. Ibra alifika na mke wa Lazaro hospitali ambapo alipokelewa na madaktari na kuanza kupewa matibabu, kwakweli Ibra hakuweza kuondoka kwani yeye ndio chanzo cha kila kitu. Kwahiyo alichokifanya ni kuchukua simu yake na kumpigia Lazaro ambaye kwa muda ule alipatikana hewani. Baada ya muda mfupi Lazaro aliwasili pale hospitali na kutaka kumuona mke wake ambapo aliambiwa kuwa asubiri kwanza. “Hivi kwani imekuwaje Ibra?” Ikabidi Ibra amsimulie kilichotokea ila Lazaro hakupendezewa kabisa, “Lakini Ibra nilikwambia jamani mke wangu asiende kwanza nyumbani kwako, nilikwambia afike pale kwenye biashara yako kwanza ili akupe ushauri wa kiroho kabla ya mambo yote” “Mi sijaona tatizo maana mkeo ni mwanamaombi kwahiyo nilimpeleka nyumbani akapambane na Yule mchawi” “Hatuendi hivyo ndugu yangu, yani sijui kama unaweza kunielewa wewe. Ile nyumba yako imetawaliwa na nguvu za giza” “Sio nyumba yangu, pale mbaya ni mtu mmoja tu wala sio nyumba yangu” “Na nyumba yako pia inatakiwa ifanyiwe maombi ya nguvu ila tatizo lako unapenda kukurupuka. Yani mke wangu kwakweli Mungu amsaidie apone, itabidi kesho nije na mchungaji hapa anisaidie maombi” “Haya, ila hapa wanaomponya ni madaktari na sio huyo mchungaji wako” Lazaro aliamua kuwa kimya tu kwani aliona mtu anaebishana nae atakuwa na matatizo ya ziada. Asubuhi na mapema Ibra aliamua kurudi nyumbani kwake ila alipofika kila atakachomsemesha mke wake alimkalia kimya tu na kumfanya Ibra agundue kuwa mkewe amemnunia kisha akaenda kuoga na kujiandaa halafu akatoka kuelekea tena hospitali kumuona mke wa Lazaro ila alikuta ameshatoka hivyo ikabidi aelekee nyumbani kwa Lazaro ambapo aliwakuta wakiwepo na watu kadhaa, kuna mmoja alionekana akiongea sana ila uongeaji wake ulikuwa ni wa kufundisha, “Mnajua kuna ajari zingine huwa zinapangwa na mapepo halafu zinatekelezwa na wanadamu ambao hawajui njama za mapepo hayo, kwahiyo ni muhimu sana kujikabidhi mbele za Mungu wakati wote.” “Ila mke wangu ni mwanamaombi mzuri sana sasa sijui kwanini imekuwa hivyo” “Usiulize kwanini ila tambua kwamba ni jaribu tu ambalo lipo kwaajili ya kupima imani yake ila Mungu atamsaidia na atapona kabisa” Ibra alikuwa akiwasikiliza tu, kisha akakatisha maongezi yao kwa kutaka kujua hali ya mgonjwa, “Lakini vipi maendeleo ya shemeji?” “Anaendelea vizuri ila tu amepumzika kwasasa” Yule mtu aliyekuwa akifundisha alimuangalia Ibra na kumwambia, “Kijana unaonekana kuwa na matatizo ila unamichanganyo mingi sana” “Hapana sina michanganyo yoyote” “Ila Ibra rafiki yangu mbona mbishi hivyo? Mara nyingine uwe unatulia ukisikiliza unachotaka kufundishwa” “Hata hivyo nina haraka sana nilipita tu mara moja kumuangalia shemeji” Kisha akainuka na kuwaaga, ambapo alienda moja kwa moja kwenye gari yake na kuanza kuondoka huku akijisemea, “Wanafikiri siwajui, anataka anihubirie pale siku nzima na mwisho wa siku aniombe sadaka. Mambo yangu yenyewe yamenishinda halafu nianze kutoatoa sadaka zisizokuwa na mpango! Mmh siwezi kabisa, wanaweza hao hao wakina Lazaro ndiomana hawaendelei” Ibra akaondoka zake na kwenda moja kwa moja kwenye biashara zake. Alipofika alimkuta rafiki yake baba John ambaye baada ya salamu alimuuliza kama alifanikisha na kumuuliza pia kuwa kwanini jana hakuonekana kwenye biashara, “Majanga ndugu yangu” “Majanga gani tena?” “Yani wee acha tu” “Au ulikosea masharti?” Ikabidi Ibra amsimulie vile ilivyokuwa, “Yani nimejitahidi kwa kila hali ili kufanikisha lile swala ila mwisho wa siku masharti yakanishinda” “Yani sharti jepesi kama lile ukashindwa duh!! Mbona mi na mke wangu tuliweza yani tuliishi ndani siku tatu bila ya kuongea chochote hebu fikiria yani tulikuwa tunafanya tendo la ndoa siku zote hizo tatu bila ya kuzungumza na hatimaye tukampata mtoto wetu John yani wewe siku moja tu umeshindwa dah!” “Mkeo ni muelewa baba John sio kama mke wangu mimi, sijui Yule mganga atanielewa?” “Yani katika vitu ambavyo Yule mganga hapendi ni kukosea masharti, kwakweli nakuhurumia sana na sijui kama atakuelewa” Ibra alijikuta akikata tama kabisa ila mwenzie alimwambia kuwa asikate tama na wataenda kujaribu tena kesho yake kama atawaelewa. Sophia alikuwa amekaa ndani na Neema huku akimwambia, “Yani yule mwanaume nitamnunia hadi ashike adabu yake” “Ndio vizuri hivyo, unatakiwa kuwa ngangari sio kila siku usumbuliwe na mapenzi kwenye kichwa chako yani kama ulivyompenda yeye basi unaouwezo wa kumpenda mwingine vilevile tena na zaidi” “Mmh ila sijui kama naweza kumpenda mwingine kama ninavyompenda Ibra maana Ibra nampenda sana, unajua nimemvumilia sana hadi leo nipo nae sababu ya uvumilivu wangu hata namshangaa ananilipa kwa kunisaliti dah!” “Dada, mwanaume si mama yako wala baba yako kusema akuhurumie eti asikusaliti, asilimia kubwa ya wanaume akipata vijihela kidogo tu basi ni shida na tatizo. Pole sana ila utampata mwingine tu” “Ila mi ningependa ajirekebishe” “Ili ajirekebishe unatakiwa kuwa na mwinginme, halafu cha muhimu ni kuendelee kumnunia ili umshikishe adabu” Sophia akakubaliana na Neema kwani aliona ndio njia pekee ya kumkomesha mume wake. Jioni Ibra aliwasili nyumbani kwake na kuwakuta Sophia na Neema pale sebleni kisha akamsalimia mke wake ila alikuwa kimya tu na kumfanya aelekee chumbani huku akijiuliza kuwa mkewe ana tatizo gani, alijiuliza sana bila ya kupata jibu. Muda wa kulala ulipofika, moja kwa moja Sophia aliingia chumbani na kujilaza ambapo Ibra alianza kujiongelesha tena, “Hivi Sophia utaendelea kuninunia hivi mpaka lini? Ujue sikuelewi mke wangu halafu unaniumiza sana kwani sijui kosa langu hadi uninunie hivyo” Sophia alikuwa kimya tu huku akibedua bedua midomo yake na kujilaza vizuri, kwakweli Ibra hakuwa na la kufanya na kuamua nay eye kulala. Kulipokucha, asubuhi na mapema Ibra aliamka na kujiandaa kwenda kwenye shughuli zake ila kabla hajaondoka kama kawaida yake alimuamsha mkewe kwa lengo la kumuaga. “Za kuamka mke wangu, mi natoka naenda kwenye shughuli zangu” Hakujibiwa pia ila alimsogelea mkewe na kumbusu kwenye paji la uso kisha akaondoka zake. Sophia nae akaamka na kuelekea sebleni huku akijiongelesha, “Hata sijui kwanini nimeliachia jinga lile linibusu kwenye paji la uso kunitia nuksi tu” Neema akaanza kucheka, “Mbona unacheka hivyo?” “Nimefurahi tu, na Yule usipokuwa makini atakutia nuksi kweli” “Sijui ni nani anaemshauri ujinga mume wangu” “Kheee kumbe hujui! Ni rafiki yake Lazaro, Yule kijana ni mjinga sana halafu ubaya zaidi ni mchawi” “Kheee kumbe ni mchawi?” “Ndio, tena anamuonea wivu sana kaka ila yeye hajui tu. Siku akigundua atajilaumu sana kuwa nae pamoja” “Sasa nifanye nini?” “Ngoja nitakufundisha kitu, yani watagombana na hawatapatana tena” “Dah nitafurahi sana” Neema akatabasamu tu kwa muda huo. Ibra akaenda kwenye shughuli zake kisha moja kwa moja akamfata baba John ambaye walipanga kuwa siku hiyo wataenda tena kwa Yule mganga, “Tutaenda saa ngapi ndugu yangu?” “Subiri subiri kwenye mida ya saa sita na nusu hivi tutaenda maana saizi atakuwa na wateja wengi sana” Wakakubaliana kuwa wataondoka mida hiyo kisha kila mmoja kuendelea na shughuli zake kwa muda huo. Mida ilipofika Ibra alienda tena kumkumbusha baba John ambapo wakaianza safari ya kwenda kwa Yule mganga, walipokuwa njiani Ibra akapokea ujumbe kwenye simu yake ambao ulimshtua sana hadi baba John naye akamuuliza kuwa tatizo ni nini, “Hebu soma na wewe” Ibra alimpa baba John ile simu na kusoma pia ule ujumbe, “Mmh inawezekana kweli shemeji akawa na mwanaume mwingine?” “Kama sio kweli, imekuwaje huyu aliyeandika kusema kuwa amemuona hotelini na huyo mwanaume mida hii? Pengine ndiomana ananinunia ndani” “Duh! Ila mimi siamini, kwavile ameandika jina la hoteli na chumba walichopo kwanini tusiende kuwafumania” “Hilo ni wazo zuri sana, kwakweli mimi nitaua mtu jamani, mke anauma sana hivi wanajua nimemuhudumia vipi mke wangu mpaka kawa vile? Roho inaniuma sana” Baba John alimpooza pale kisha wakageuza gari na kuelekea kwenye hiyo hoteli. Walifika kwenye hoteli ile na palikuwa kimya sana, moja kwa moja wakaenda kwenye chumba walichoelekezwa na kugonga ambapo aliyefungua alikuwa Sophia na alipoona ni mumewe moja kwa moja akaenda kukumbatia Lazaro, kwakweli Ibra alishikwa na hasira za ajabu akawasogelea na kumsukuma mkewe ambaye alianguka chini kisha akampiga ngumi nzito Lazaro na kumfanya aanguke pia halafu akaenda pale chini na kuzidi kumshindilia ngumi za usoni, ikabidi baba John awaamulie ambapo Ibra kwa hasira alimshika mkewe mkono na kutoka naye kwenye hoteli ile. Baba John alimuangalia Lazaro huku akisikitika, “Kwanini umemfanyia hivi rafiki yako? Kweli kabisa Lazaro wewe ni wa kumsaliti Ibra kweli?” “Kwakweli mpaka muda huu nashangaa tu yani hata sielewi, mnanipa lawama za bure jamani” Lazaro alikuwa akitokwa na damu tu, ikabidi baba John amsaidie na kuanza kumkokota ili kumpeleka hospitali. Ibra alifika na mkewe nyumbani huku akiwa amefura kwa hasira, na kuingia na Sophia ndani huku akifoka, “Yani Sophia umeninunia kumbe unanisaliati, kwakweli siwezi kuvumilia hili” Akamnasa kibao Sophia kilichompeleka hadi chini na kuwa kimya kabisa, Neema akamsogelea na kumwambia “Hivi unawezaje kumpiga mwanamke kiasi hiko?” “Na wewe usiniongeleshe, nisije nikakupiga bure” Neema akacheka na kumwambia, “Yani kunipiga mimi sahau tena sahau kabisa” Kisha akampulizia kitu usoni ambapo Ibra alianguka chini na kupoteza fahamu. Ibra na Sophia walipozinduka walijikuta wamelala kitandani tena wakiwa wamekumbatiana. Itaendelea kama kawaida…………..!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 28 Neema akacheka na kumwambia, “Yani kunipiga mimi sahau tena sahau kabisa” Kisha akampulizia kitu usoni ambapo Ibra alianguka chini na kupoteza fahamu. Ibra na Sophia walipozinduka walijikuta wamelala kitandani tena wakiwa wamekumbatiana. Walishtuka sana ila walipojiangalia vizuri ndio walikuwa wametoka kumalizia tendo la ndoa, kila mmoja alishtuka na kumwangalia mwenzie kwa hasira, huku kila mmoja akihisi kuwa kuna mchezo ambao amefanyiwa na mwenzie. Ibra alikurupuka na kwenda kuoga haraka haraka kisha hakumuaga hata mkewe akaondoka zake, kisha Sophia nae aliamka na kwenda kuoga halafu akaenda sebleni kukaa na Neema “Huyu mwanaume mpuuzi sana, kwahiyo baada ya yale mambo ya jana akaamua amalizane kwa kulala na mimi bila kutaka, ni mwehu sana Yule” “Ila dada naomba nikupongeze maana najua jana ulicheza vizuri sana ule mchezo, kwa hakika wale wawili hawatopatana tena” “Na nilivyoweza kulilaghai lile lilazaro yani halijaamini macho yake, si nililiambia kuwa nina matatizo aje pale hotelini halafu niakaliambia lije chumbani yani pale pale nikajifunga khanga basi Ibra alipogonga tu nikaenda kumfungulia na kurudi haraka kwenda kumkumbatia Yule Lazaro. Yani kadundwa jana khatari, hata kama na mimi nimepigwa ila Yule Lazaro ndio kapigwa zaidi” “Amakweli umemkomesha” “Yani na nilivyojua kumuigizia basi, muda ule kaingia chumbani tu anashangaa kuwa shemeji ni nini nikamwambia subiri kwanza basi nikaingia chooni na kujifunga khanga yani nimetoka muda wanagonga mlango moja kwa moja nimeenda kufungua basi Lazaro kabakia kutoa mimacho, hapo ndio nikamkimbilia na kumkumbatia weee Ibra kampiga jamani sijui kama amepona ile pua yake Yule Lazaro” Wakacheka sana huku wakipongezana kwa kile kitendo, “Yani hao hawataongea tena, halafu leo akirudi jifanye kumuomba msamaha mwambie kuwa rafiki yake ndio alikulaghai ila wewe hukutaka kumsaliti kabisa” “Hakuna tatizo juu ya hilo, bora wasiongee tu kwanza Lazaro mwenyewe mchawi yani bora kabisa wasiongee kamwe na mume wangu” “Hapo sasa ndio umekuwa mwanamke ngangari, inuka ukale chakula tayari” Sophia aliinuka kwa tabasamu na kuelekea mezani ambapo alikuta Neema amemuandalia chakula anachokipenda sana. Ibra alikuwa na mawazo sana huku akiwa na hasira za kutosha dhidi ya rafiki yake, hata kwenye biashara zake hakwenda ila moja kwa moja alienda kwa Siwema kupata ushauri. Alimkuta na kukaribishwa, “Mmmh nahisi huko si salama, nini tatizo tena Ibra jamani?” “Yani dada kwakweli ni matatizo makubwa sana yani huwezi amini rafiki yangu mpendwa kanisaliti kwa mke wangu” “Kivipi mbona sikuelewi?” Ikabidi Ibra amsimulie ilivyokuwa yani jinsi alivyowafumania hotelini. “Mmmh mbona inakuwa ngumu kukuamini jamani, yani Sophia anaweza kufanya hivyo kweli?” “Ndio amefanya hivyo dada, kwakweli nimeumia sana” “Mimi nina mashaka na huyo rafiki yako, huenda alimuwekea madawa mkeo sababu Sophia hawezi kufanya hivyo kwajinsi anavyokupenda. Yani aache kukusaliti kipindi kile mnalalia godoro kama mbavu za mbwa kwenye nyumba inayovuja aje akusaliti leo kwenye mjengo jamani!” “Ila hata mimi nina mashaka na yule rafiki yangu maana yeye alinikataza kuwa nisiende na mkewe nyumbani kwangu labda alihisi tabia zangu ni kama zake kumbe mimi sina mambo hayo. Kwakweli ameniumiza sana halafu anajidai ni mlokole” “Kheeee mdogo wangu kumbe hujui kama walokole ni wanafki! Kwanza ukikutana na mtu yeyote anayejifanya kashika dini sana ujue ni mnafki, kuna kibibi flani kinazungukaga zumgukaga hapa yani kale kabibi kanajulikana mtaa mzima kuwa ni kachawi ila kanajifanya kanasoma Kuran hatari yani washika dini wote ni wanafki. Sophia alishawahi kuonana nae na kuzungumza nae yani ilibaki kidogo tu atekwe na maneno ya Yule bibi kwahiyo ndugu yangu usiwaamini kabisa hao washika dini ndiomana mimi huwa najiendea zangu kwa waganga kujikinga” “Unafikiri nina hamu nao dada yani sina hamu nao kabisa kabisa, kumbe ni msaliti Yule, ila Sophia nae kaniudhi sana” Siwema akafanyakazi ya kumtetea Sophia pale ili Ibra asimchukie mke wake, “Cha kukushauri mdogo wangu usimchukie mkeo, endelea kumpenda zaidi ila kaa mbali na huyo rafiki yako sio mtu mzuri” “Nimejifunza dada na wala sitawasiliana nae tena” Kidogo moyo wa Ibra ulipata nafuu kwasasa kwani pale mwanzo alikuwa na maumivu makali sana ukizingatia mkewe alikuwa anamuamini na rafiki yake pia alikuwa anamuamini, ila maneno ya Siwema yalimpa imani kiasi ya kusonga mbele. Akamuaga pale na kuondoka zake. Sophia alipomaliza kula na shughuli zake zingine alirudi na kukaa na Neema huku wakiongea mawili matatu, “Ila mumeo anakaribia kurudi dada, kwahiyo cha kukushauri naomba nenda chumbani ili akukute huko halafu utajifanhya unajutia sana kilichotokea mwambie hata kula umeshindwa halafu msingizie yote Lazaro” “Mmmh nimsimuliaje sasa akitaka kujua kwa undani?” “Ngoja nikufundishe” Neema akamuelekeza Sophia cha kumwambia mumewe, kisha Sophia akainuka na kuelekea chumbani. Muda kidogo Ibra nae akawasili na kumkuta Neema pale sebleni “Dada yako yuko wapi?” “Yupo chumbani yani hajatoka kabisa leo hata chakula nimemuita kuja kula lakini hajaja kula” Ibra akajikuta akiingiwa na roho ya huruma na kuelekea chumbani alipokuwa mke wake, alimkuta amekaa huku amejiinamia kitandani. Ibra akamsogelea mkewe ambapo Sophia alipiga magoti na kuanza kulia huku akimuomba msamaha, “Tafadhali nisamehe mume wangu, halikuwa kusudio langu kabisa” “Usijali, ila mimi nitakusamehe iwapo utaniambia ukweli. Nieleze ilikuwaje?” “Sikiliza mume wangu, rafiki yako Lazaro amekuwa akinisumbua kwa kipindi kirefu sana yani toka umekuja nae hapa nyumbani kazi yake imekuwa ni kunitumia meseji za kijinga tu ila mimi huwa nafuta sababu sikutaka mgombane kwaajili yangu. Sasa jana hata sikujua kama ingetokea vile, nimetulia zangu hapa nyumbani kanipigia simu kuwa niende kwenye ile hoteli eti kuna maombi kwavile mimi naona maisha yangu na huku kutoka toka kwa m,imba kamavile kuna tatizo ikabidi niende huku nikijua kuwa kuna watu wengi. Kufika pale nikamkuta nje ananisubiri, akaseme nimfuate nami nikafanya hivyo. Sasa si ndio nikashangaa akanipeleka chumbani na kunitishia nilale nae na nisipolala nae ataniua” “Kheeee kwahiyo ulilala nae?” “Nisamehe mume wangu, Lazaro alinitolea kisu tafadhari nisamehe” Ibra alijishika kichwa huku akiwa amejawa na uchungu sana kwani maumivu yalimzidi kusikia kuwa alilala nae. “Yani Lazaro ni mbwa mbwa mbwa, yani wakunifanyia mimi hivi!! Na nitamkomesha yani nitamkomesha Lazaro mimi haiwezekani anichezee akili kiasi hiki” “Nisamehe mume wangu tafadhali yani hata kula nashindwa kwa hiki kilichotokea” “Usijali mke wangu ila nimeumia sana” Kisha Ibra akamuomba mkewe kuwa waende kula, naye akafanya hivyo. Usiku ulipoingia, Ibra aliinuka na mkewe na kwenda kulala ila bado Ibra alikuwa na mawazo sana kiasi kwamba hata usingizi kumpata ilikuwa kwa mbinde ingawa Sophia yeye alilala muda ule ule. Wakati yuko macho Ibra aliona kitu kwenye ukuta na kumfanya ashtuke sana kwani ukuta wa chumbani kwao ulikuwa kama unafuka moshi, kwakweli Ibra hakuelewa na kadri alivyozidi kuangalia ndivyo moshi nao ulivyozidi, mara gafla akasikia sauti za vicheko zikitokea kwenye kuta zake na kumfanya Ibra ashikwe na uoga huku akitetemeka gafla akabanwa na mkojo kiasi kwamba akahisi kama anataka kujikojolea, kwakweli hapo hapo ndipo alipoamua kumuamsha mkewe kwa nguvu zote, “Sophia, Sophia, wee Sophy amka bhana” Sophia aliamka huku macho yake yakionekana kuwa mazito sana kwa usingizi aliokuwa nao, na wakati uleule hapakusikika tena sauti za vicheko na wala ule moshi haukuonekana tena. “Nini tatizo mume wangu?” “Mkojo umenibana sana” “Kheee sasa unataka nikusindikize chooni au?” Ibra akaamua kuinuka huku akipepesa macho yake huku na kule, Sophia akapiga mikono huku akisikitika na kusema, “Una matatizo wewe” Ila kile kitendo cha Sophia kupiga mikono yake kilimshtua sana Ibra ukizingatia tayari alikuwa ametawaliwa na hofu kwahiyo akashtuka sana nusura azimie, Sophia alimshangaa sana mume wake na kumwambia “Kheee Ibra na wewe jamani mara nyingine unachekesha tu, sasa kilichokushtua hapo ni nini? Mwanaume gani unakuwa muoga hivyo jamani? Hebu nenda huko chooni mi silali nakusubiri utoke usije kujikojolea hapa bure” Sophia aliongea hayo huku akicheka ila hakujua hofu ambayo imemuingia Ibra kwa wakati ule, ikabidi Ibra ajikaze hadi chooni ambako aliingia na kuacha mlango wazi kisha kujisaidia fasta fasta ila alipogeuka ili atoke alikuta ule mlango umefungwa na kumfanya atetemeke kiasi kisha akasikia sauti ya mtu akicheka kwakweli Ibra alipiga kelee mule chooni “Nisaidieni, nisaidieni” Kisha Sopphia akafungua ule mlango, “Jamani mume wangu una matatizo gani?” Ibra alitoka mule chooni fasta huku akiwa anatetemeka na kutikisa kichwa, Sophia akamsogelea mume wake na kumpa pole kisha akamkumbatia na kumuomba walale, Ibra hakubisha kwani alikuwa ametawaliwa na uoga kwahiyo akalala huku akiwa amekumbatiwa na mkewe. Kulipokucha kama kawaida Ibra alikuwa ameamka ila leo alikuwa amechelewa kiasi tofauti na siku zingine ila akajitayarisha hivyo hivyo na kuondoka pale nyumbani, alipofika njiani akajiwa na wazo la kwenda kumtembelea Jane kwani alihisi kichwa chake kusongwa na mawazo kwahiyo moja kwa moja akaenda kwakina Jane na kumkuta Jane akiwa nje ambapo alimuomba pembeni na kuzungumza nae, “Kwakweli mdogo wangu mimi nina matatizo sana” “Mengine tena au yaleyale?” “Yale yale na mengine yameibuka, unajua dada yako alinisaliti kwa rafiki yangu mpendwa” “Mmh uliwafumania au umeambiwa?” “Bora hata ningeambiwa isingeniuma ila nimewafumania kwa macho yangu” “Pole sana kaka, ila muombe Mungu akupe faraja na amani” “Halafu pia mpaka leo Yule mwenyekiti hajaja tena nyumbani kwangu, kuna matatizo mengi sana yalitokea hapo katikati ndiomana nikawa kimya mdogo wangu” “Mmh! Naomba nikuulize kitu kaka yangu” “Uliza tu” “Hivi wewe dini gani?” “Kwanini umeuliza hivyo?” “Sijawahi hata siku moja kukusikia unaenda kanisani wala msikitini, hivi ni dini gani wewe maana ungepata msaada wa kiroho ungesaidiwa kwa urahisi” “Achana na hayo mambo ya dini, kuna njia nyingi tu za mimi kuweza kusaidiwa kuliko kung’ang’ania hizo dini. Kwanza hao wachungaji na mashekhe wote wanapenda pesa kitu kidogo utasikia sadaka kwahiyo mimi na mke wangu tuliamua kuachana na mambo ya dini. Siku moja nitakusimulia kisa chetu cha kuachana na hayo mambo ya dini nadhani uatanielewa kwa urahisi” “Hata kama huwaamini hao viongozi wa dini ila na Mungu je humuamini? Unajua sote tumeumbwa na Mungu, tunatakiwa kuamini matendo yake” “Mungu namuamini ndio lakini kwanini kaniacha nisumbuke hivi tena kwenye nyumbna yangu mwenyewe?” “Kheee wewe unakosea kusema hivyo” “Kwakweli Jane naona leo huna msaada, au kama unayaamini sana hayo maombi yako njoo nyumbani uombe Yule Neema aondoke pale nimemaliza” Ibra akamuaga Jane na kuondoka na kumuacha Jane akisikitika sana. Ibra alikaa kwenye gari yake na kutafakari kidogo, kisha akaondoa lile gari ila alipofika mahali alisimama na kuanza kujisemea, “Ngoja tu nikampange baba John niende nae kwa Yule mtaalamu, yani watu wengine sijui vipi wanafikiri kuna mtu duniani asiyemuamini Mungu jamani? Basi kujifanya wenyewe ndio watakatifu dunia nzima, kile kijane nacho kimeanza kunikera sasa.Tunaamini ndio Mungu yupo lakini kwanini hawa wachawi wananitesa hasa huyu Neema jamani kwanini ananitesa hivi yani natamani nimnyongelee mbali” Akasikia sauti ikisema, “Thubutuuu” Kugeuka nyuma akamuona Neema amekaa kwenye siti ya nyuma ndani ya gari lake. Itaendelea kama kawaida……………..!!!!!!! Toa maoni yako mdau NYUMBA YA MAAJABU: 29 Ibra alikaa kwenye gari yake na kutafakari kidogo, kisha akaondoa lile gari ila alipofika mahali alisimama na kuanza kujisemea, “Ngoja tu nikampange baba John niende nae kwa Yule mtaalamu, yani watu wengine sijui vipi wanafikiri kuna mtu duniani asiyemuamini Mungu jamani? Basi kujifanya wenyewe ndio watakatifu dunia nzima, kile kijane nacho kimeanza kunikera sasa.Tunaamini ndio Mungu yupo lakini kwanini hawa wachawi wananitesa hasa huyu Neema jamani kwanini ananitesa hivi yani natamani nimnyongelee mbali” Akasikia sauti ikisema, “Thubutuuu” Kugeuka nyuma akamuona Neema amekaa kwenye siti ya nyuma ndani ya gari lake. Ibra akaanza kutetemeka na kushikwa na uoga kitu kilichomfanya ashindwe kuendesha gari vizuri, mwishowe akagonga mti na kupoteza fahamu. Watu walioishuhudia ajari ile walienda kuisogelea gari kwa lengo la kujua kama ni mzima au amekufa, eneo lile lilikuwa na vibaka ambao walianza kwanza kumsachi Ibra kabla ya kumpatia huduma, kwa bahati Lazaro nae alitokea eneo lile na aliposogea akaona ni rafiki yake hivyo aliomba msaada zaidi na kumkimbiza hiospitali ambako walipokelewa na Ibra kuanza kupewa huduma. Lazaro aliwaza sana juu ya kumpigia simu mke wa Ibra na kumtaarifu ila kila alipokumbuka lile tukio alishikwa na hofu ila hakuwa na jinsi zaidi ya kumpigia simu, “Hallow, Lazaro anaongea hapa” Sophia nae kusikia ni Lazaro akaanza kuwa na kigugumizi kwani alijua wazi kuwa Lazaro angemsema kwa kile alichomtendea ila Lazaro aligundua hilo mapema na kuanza kumueleza tatizo la mume wake, “Sikia shemeji, huku Ibra amepata ajali na tupo hospitali” Ndio hapo Sophia aliposhtuka na kuuliza kwa makini kuwa ni hospitali gani ili aende, Lazaro akampa maelekezo yote ya hospitali ilipo. Sophia alijiandaa haraka haraka kwaajili ya kutoka, alipofika sebleni alimkuta Neema na akaulizwa swali, “Unaenda wapi?” “Nasikia Ibra amepata ajali yupo hospitali kalazwa nataka kwenda kumuona” “Ndio ulitaka kutoka bila kuaga?” “Hapana Neema ningetokaje bila kuaga? Umeniwahi tu” “Haya nenda ila kuwa makini sana” “Haya nashukuru” “Mpe pole eeh” Neema aliyasema maneno hayo huku akicheka na kumfanya Sophia ajiulize maswali kuwa Neema anacheka kitu gani ila hakutaka kumuhoji sana na kuondoka zake. Wakati Sophia akiwa stendi kusubiri daladala ili awahi hospitali akakutana na Jane pale stendi ambapo Jane alimsalimia bila ya kinyongo ila mwanzoni Sophia alinyamaza kimya kanakwamba hakusikia ile salamu ya Jane, ikabidi Jane amwambie tena “Jamani dada nakusalimia!” “Kheee kwani lazima kuitikia salamu?” “Ila dada kwanini unakuwa na kinyongo hivyo na mimi? Kwanini usiwe kama mumeo? Huwa anakuja mara nyingi kuomba ushauri, hata leo alikuja pia” “Aaah kumbe alikuja kwenu ndiomana mume wangu kapata ajali jamani” “Kheee kapata ajali wapi hapo na sasa hivi yuko wapi?” “Nikwambie ili ukammalizie, tena ukome kufatilia maisha yangu Jane” “Hapana dada hata sina lengo la kufatilia maisha yako ila nimekuuliza kwasababu hapa namsubiri mchungaji wetu sasa nikawaza kuwa akifika twende nae hata akamfanyie maombi” “Jifanyieni maombi nyie na umasikini wenu, yani ile nyumba yetu inawapa jamba jamba sana nyie ndiomana mnamtamani mume wangu tena mtukome” Kisha lilikuja daladala na Sophy akapanda na kuondoka zake huku akiwa amemuacha Jane akisikitika tu. Sophia alifika hospitali na kumkuta Lazaro nje kisha akasalimiana nae kwa aibu, Lazaro akatikisa kichwa tu, “Kwakweli pepo aliyekuingia shemeji unatakiwa uombe sana” “Nani mwenye pepo sasa? Hebu nionyeshe wodi aliyolazwa mume wangu maana nyie wenyewe ndio mliosababisha ajali yake” Lazaro hakutaka kubishana na huyu shemejiye hivyo akaongozana nae hadi wodini alipolazwa Ibra ambaye walimkuta ameshazinduka tayari, ila alipowaona alionyesha kuchukizwa sana. Lazaro alimsogelea na kumpa pole, “Sidhani kama pole yako ni ya muhimu kwangu, tafadhali kafanye mambo mengine tu. Kwanza daktari ameshaniruhusu, twende nyumbani Sophia” “Mmh Ibra umeruhusiwa saa ngapi?” “Kwahiyo ulitaka leo nilale hospitali ili ukamfaidi mke wangu” “Hivi nyie watu kwani mnamatatizo gani? Ibra nimekukuta umepata ajali nikakusaidia kukuleta hapa, halafu mimi sina mahusiano yoyote na mkeo” “Umetumwa unisaidie au ni kiherehere chako tu!” Ibra aliinuka pale kitandani na kumshika mkono mkewe na kuondoka, yani Lazaro alikuwa akishangaa tu kwani hakuwaelewa kabisa watu hawa. Kisha na yeye Lazaro akaamua kutoka tu pale hospitali na kuondoka zake huku akizidi kusikitika. Sophia na mumewe walipotoka nje ya hospitali, gari ya Ibra ilikuwa pale nje wakaingia na kupanda ambapo njiani Sophia alimuhoji mumewe, “Si niliambiwa umepata ajali, sasa ni ajali gani mbona gari lipo zima kabisa?” “Kwanza hata sikumbuki kama nilipata ajali kweli, nadhani hizi ni njama za lazaro” “Sio Lazaro peke yake na Jane mume wangu” “Naye anahusika kwani?” “Ndio si ulionana nae kabla hujapata ajali” “Umejuaje kama nilionana nae?” “Nilikutana nae njiani akaniambia eti akataka tuje wote hospitali yani mnimemshushulia mbali maana nadhani nia yake ni kuja kukumaliza kabisa” “Aaah yule Jane achana nae mke wangu” “Ila wewe hukomi maana nakukataza kila siku kuwa usiende kwakina Jane ila unaenda tu” Gafla wakaanza kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia na kuwafanya wote washtuke na kuangaliana, “Mmh mtoto! Hiyo sauti itakuwa inatokea wapi Ibra?” “Hata mimi mwenyewe nashangaa” Waliisikilizia kwa muda kisha ile sauti ikapotea na kuwafanya waendelee na safari yao ila hawakuongea chochote cha zaidi hadi walipofika kwao na kuingia ndani ambapo kama kawaida walimkuta Neema akiwa pale sebleni na aliwakaribisha vizuri mezani ambapo walienda kula kisha kwenda kupumzika kwani kila mmoja alijihisi uchovu sana. Ibra alishtuka usiku sana na kujikuta akikaa na kuanza kuwaza, yale matukio yaliyompata mchana yote aliyakumbuka hadi jinsi alivyogonga ule mti, “Sasa mbona gari yangu imepona wakati niligonga mti! Na ni nani aliyeniletea gari yangu hadi nje ya hospitali? Kama Lazaro ndiye aliyenisaidia je alinisaidia kupeleka gari langu kwa fundi au ni kitu gani? Na mbona funguo za gari nilikuwa nazo kwenye mfuko wa suruali?” Ibra alijiuliza maswali mfululizo bila ya jibu lolote la maswali yake na kumfanya awe na mashaka zaidi, aliendelea kujiuliza, “Hivi na Neema nae alipanda saa ngapi ndani ya gari langu? Hapana jamani huyu Neema ni mchawi na ndiye aliyesababisha mimi nipate ajali, basi kwa mauchawi yake saa hizi atakuwa sebleni akiangalia video ngoja niende nikamuulize maswali yangu, nijivike moyo wa kiume tu” Ibra aliinuka leo huku akiwa hasna uoga hata kidogo kwani alionekana kabisa kudhamiria kwenda kuzungumza na Neema. Ibra alipofika sebleni kama kawaida alimkuta Neema akiangalia video, kisha Ibra akakaa na kumtazama Neema halafu akamuuliza “Hivi Neema, wewe ni binadamu wa aina gani?” “Aliyekwambia mimi ni binadamu ni nani?” “Kwahiyo wewe si binadamu?” Neema akacheka huku macho yake yakitoa damu na kumfanya Ibra atetemeke kiasi na kuuliza kwa sauti ya kutetemeka, “Ina-ina-inamaana Neema wewe sio binadamu?” Gafla Ibra akaanguka pale sebleni na kupoteza fahamu. Kulipokucha Sophia aliamka na kumuangalia mumewe bila ya kumuona pembeni yake moja kwa moja akahisi kuwa huenda Ibra amewahi kwenye shughuli zake, “Kheee ndio bila hata ya kuniaga jamani?” Sophia akajisikia vibaya kiasi kisha akaamka na kuelekea sebleni ila alishtuka sana kumuona mumewe yupo chini na akiwa hana fahamu kabisa, akajikuta akipiga kelele za kumuita Neema ambapo Neema alifika na kusimama huku akimuangalia Sophia, “Ona Neema, muone mume wangu sijui amepatwa na nini? Nisaidie tumpeleke chumbani” “Muache hapo hapo ataamka mwenyewe” “Jamani Neema!” “Mwache tu, mumeo siku hizi kaanza ulevi na hiyo ndio faida ya ulevi yani kila mahali unaona ni kitanda” “Jamani! Huo ulevi kaanza lini, mbona jana nilirudi nae na hadi nikaenda kulala nae?” “Nenda kaangalie jikoni machupa ya pombe ya mume wako, aliamka usiku na kuanza kufakamia mapombe mwishowe karudi na kulala hapo chini” “Jamani mume wangu dah!” Sophia akainuka na kuelekea jikoni ambako aliona chupa za pombe nyingi sana na kushangaa kuwa mumewe alizinunua muda gani, kisha akarudi tena sebleni na kumwambia Neema, “Hata sijui alizinunua muda gani wakati nimerudi nae vizuri hapa” “Nadhani zilikuwa ndani ya gari kwani alitoka kwanza kwenda kuzichukua” “Dah! Hata hivyo si vizuri akalala hapa, naomba unisaidie tumpeleke chumbani” “Nimekwambia muache hapo hapo ajifunze adabu” “Jamani Neema mbona unakuwa na roho mbaya hivyo, ngoja nimkokote mwenyewe” Sophia akawa anajaribu kumsukuma mumewe ila alishindwa kwani Ibra alikuwa ni mzito sana yani kama jiwe kubwa hivi kwa uzito aliokuwa nao na kumfamnya Sophia ashindwe kumbeba, “Neema ungenisaidia tu, Ibra kawa mzito sana” “Unafikiri atakuwa mwepesi wakati hapo yupo kama maiti” “Neema usiseme hivyo mume wangu sio maiti” “Usinichekeshe na wewe, kuna binadamu ambaye hatokuwa maiti?” “Hata kama, ila muda wake bado wa kuwa hivyo” Sophia akaenda chumbani na kuchukua mto kisha akamletea mumewe na kuinua kichwa chake na kukiweka kwenye mto. “Unampenda sana eeeh! Vizuri sana” Kisha Neema akapiga kama makofi na kurudi kukaa sebleni akiangalia video kama kawaida. Sophia alikaa pembeni ya mume wake kwa wakati huo, muda kidogo simu yake ikaanza kuita akaichukua na kuangalia mpigaji alikuwa ni Siwema kisha Sophia akapokea simu ile, “Hallow Da’ Siwema” “Huko salama kabisa Sophy?” “Kwanini dada?” “Nimeota vibaya” “Umeotaje dada?” “Samahani lakini ila nimeota Ibra amekufa” Sophia akashtuka sana huku moyo ukimuenda mbio na kumuangalia mumewe pale chini, kisha akainama na kumsikilizia mapigo ya moyo ambapo akasikia yakifanya kazi na kumfanya apumue kiasi. “Da-da-dada ndoto mbaya hizo, hata hivyo Ibra ana hali mbaya sana hapa” “Kwani ana tatizo gani?” “Sijui dada eti alilewe na kuzinduka hazinduki” “Kheee ngoja nije” Kisha Siwema akakata simu, na kumfanya Sophia azidi kumuangalia mumewe ila akasikia sauti kutoka kwa Neema ikimwambia. “Kama unampenda huyo mumeo basi mzuie huyo Siwema wako asije” “Kwanini sasa wakati wewe umekataa kunisaidia? Bora aje yeye anisaidie” “Narudia tena na tena kama unampenda huyo mumeo mzuie huyo Siwema wako asije” “Mbona sikuelewi Neema?” “Unanielewa vizuri ila unajifanya kichwa maji, nakwambia hivi kama unampenda huyo mumeo mzuie huyo Siwema wako asije” “Jamani kwani Da’ Siwema ana tatizo gani akija ni ndugu yetu yule na tunashirikiana nae kwenye mambo mbalimbali na anakuja tu kunisaidia” “Unajifanya kiburi si ndio?” “Mbona umebadilika hivyo Neema unajua sikuelewi” “Sasa ole wako huyo Siwema aje” Sophia alishindwa kabisa kumuelewa Neema anamaanisha nini au anataka nini, ikabidi achukue tu simu yake na kumpigia Siwema ili amwambie kuwa asiende tena, “Weee unaniambia nisije kivipi? Nipo kwenye daladala tayari tena nakuja na mtaalamu kabisa kwani siamini kama Ibra anaumwa kawaida kwa jinsi ulivyosema atakuwa amerogwa tu” “Ila ameshapona tayari” “Weee Sophy usinifanye mimi mtoto, amepona tayari huku sauti yako inatetemeka hivyo? Nipe niongee nae” “Hapana hajapona ila usije tu” “Hebu niondolee ujinga mie, ndio tupo njiani tunakuja” Siwema akakata tena ile simu na kumfanya Sophia ashikwe na uoga kwani alijihisi kama atagombana na Neema kwa wakati huo ila hakuwa na jinsi kwani alishindwa kumzuia Siwema kuwa asiende. Muda kidogo mlango ukagongwa na kumfanya Sophia ainuke na kwenda kufungua, Neema alimuangalia tu Sophia kwa jicho lenye mwanga ang’avu na kumfanya kidogo Sophia atetemeke na kufungua ule mlango kwa haraka. Aliingia Siwema akiwa ameambatana na mbabu mmoja. Moja kwa moja Siwema alimuuliza Sophy mahali alipo huyo Ibra. “Yuko wapi sasa mgonjwa?” “Amelala pale chini” Huku Sophia akimuangalia Neema kwa mashaka kidogo ila gafla Neema hakuonekana tena pale sebleni na kumfanya Sophia ashtuke, halafu wakasogea eneo ambalo Ibra alikuwa amelala naye hakuwepo pia yani ulibaki ule mto tu katika eneo lile. Itaendelea kama kawaida…… NYUMBA YA MAAJABU: 30 Huku Sophia akimuangalia Neema kwa mashaka kidogo ila gafla Neema hakuonekana tena pale sebleni na kumfanya Sophia ashtuke, halafu wakasogea eneo ambalo Ibra alikuwa amelala naye hakuwepo pia yani ulibaki ule mto tu katika eneo lile. Sophia akashangaa sana, ambapo Siwema alimuuliza kwa mshangao pia, “Huyo Ibra yuko wapi sasa?” “Alikuwepo hapa hata mimi nashangaa kuwa ameenda wapi tena” “Kheee basi maajabu haya loh!” Siwema alimuangalia yule babu na kumuuliza, “Umeelewa hapa babu na tutafanyaje?” Huyu babu akakohoa kidogo kisha akawaambia, “Kuna mchezo tumefanyiwa hapa” Sophia na Siwema wakatazamana, kisha wakamuuliza yule mzee kuwa ni kitu gani. Yule mzee alimtazama Sophia na kumuuliza chumba chao cha kulala ambapo Sophia alimuonyesha kwa mkono kisha yule mzee akawahitaji waelekee humo. Walipoingia mule ndani tu walimkuta Ibra akiwa amelala kitandani yani alionekana kuwa amelala usingizi wa kawaida kabisa na hakuwa na hofu yoyote. Yule babu akamwambia Sophia amuamshe Ibra ambapo alifanya hivyo nae Ibra akaamka na kukaa kitandani huku akishangaa kuwa Siwema na yule babu asiyemjua wameingia kufanya nini chumbani kwao, kisha yule babu akaanza kumueleza Ibra, “Usitushangae, tumekuja kwa lengo la kukusaidia na kukuokoa” Ibra akajaribu kuvuta kumbukumbu kidogo na kujikuta akikumbuka kila kitu kilichomtokea kabla ya kupoteza fahamu kisha akasema, “Neema ni mchawi sio mtu mzuri kabisa, tafadhali tusaidieni tuweze kumtoa Neema humu ndani” Yule babu akamwambia Ibra, “Usijali hiyo ni kazi nyepesi sana yani kwahakika utafurahia wala huyo kiumbe hatokusumbua tena niamini mimi, nishafanya kazi za namna hii nyingi sana” Siwema nae akauliza, “Kwahiyo mbaya hapa ni huyo Neema?” Ibra akadakia na kumjibu Siwema, “Ndio, huyo Neema ni mbaya sana yani hafai hata kidogo” “Msijali nitamtokomeza” Kisha huyu mzee akawaambia waelekee sebleni ili awafundishe ya kufanya. Walifika sebleni na kukaa ambapo huyu mzee alianza kuwaeleza, “Unajua wewe kijana una mazindiko mengi sana na ndiomana unaweza ukafanyiwa vitu na kuvikumbuka vyote, ila wewe mwanadada huna zindiko lolote yani wewe ni mweupe kabisa ndiomana kila unachofanyiwa unasahau halafu ni rahisi sana kurubuniwa. Mumeo anapohitaji mkomboke wewe unarubuniwa na kuzuia ile kukomboka sababu wewe ni rahisi sana kutumiwa na kiumbe mbaya” “Kheee sasa tufanyaje?” “Mi nitawasaidia, kwanza kabisa itatakiwa mkeo huyu afanyiwe tambiko tena tambiko la nguvu kisha tutafanya kafara ili huyu kiumbe asiwasumbue tena” “Sasa akirudi itakuwaje?” “Hawezi akarudi na hatakama akirudi hatokuwa na nguvu kama za awali kwahiyo nyie mtulie tu sikilizeni porojo zake huku tunammaliza kabisa” “Dah nashukuru sana babu, hilo tambiko mke wangu utamfanyia lini?” “Keshokutwa itakuwa ni Jumanne na ndio siku nzuri sana nitafanya tambiko pamoja na kafara kisha kila kitu kitakuwa sawa” Ibra na Sophia walimshukuru sana kwani waliona kamavile wamepata mkombozi wao, “Kwahiyo hiyo Jumanne tuje huko nyumbani kwako?” “Ndio, Siwema hapa atawaleta yani tutaifanya hii shughuli na hamtasumbuka tena” “Jamani hata sijui nikulipe nini mzee wangu?” “Usijali kijana” Kisha yule mzee alitoa vitu kama unga unga na kuwaambia Ibra na Sophia waulambe ambapo walifanya hivyo, halafu akawaaga na kuamua kuinuka wote kwenda kuwasindikiza yule mzee pamoja na Siwema huku wakimshukuru Siwema njia nzima kwa kuwaletea mkombozi wao. Ibra na Sophia waliwaacha yule babu na Siwema wakiwa wamepanda daladala kisha wao kuanza kurudi huku Ibra akiongea kwa furaha, “Nilijua tu kuna watu wanaweza kazi bhana, ona sasa babu wa watu hana hata shida yani Neema na kiburi chake kwisha kabisa” “Kumbe Neema ni mtu mbaya eeh” “Tena ni mbaya sana yani wewe amefunika akili zako hadi huwa huuoni ubaya wake kumbe hujawahi kufanyiwa tambiko” “Mmmh mama yetu na mambo ya matambiko yupo nayo mbalimbali” “Amewakosesha kinga sasa watoto wake ndiomana huwa hukumbuki chochote yani unafanywa kama boya” “Jamani Ibra umeanza sasa kunitukana, yule babu si amesema Jumanne atanifanyia tambiko basi ndio itakuwa mwisho wa uboya wangu” Mbele kidogo wakakutana na Jane ambaye aliwasalimia na ni Ibra tu aliyeitikia ile salamu ya Jane, kisha Jane akamuuliza, “Kwanza pole maana nilisikia kuwa ulipata ajali, na pia nikuulize je lile swala lenu mshapata ufumbuzi?” “Tumeshapata ndio” “Safi kama umeamua kumrudia Mungu, itakuwa ni vyema kama utaruhusu watu wa Mungu waje pale kwaajili ya maombi” “Hivi wewe hunaga mengine ya kuongea? Kuna mganga anatusaidia” “Mmh ila kumbuka amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu” Sophia akamsonya Jane na kumwambia, “Umelaaniwa mwenyewe, mwanga mkubwa wewe” Kisha Sophia akamshika mkono mumewe na kuendelea nae mmbele na kumwambia, “Sijui kwanini hatukumueleza yule babu kuhusu hili shetani lijane yani silipendi khatari” “Basi punguza hasira mke wangu ilimradi tumeanza na hili la Neema basi la kuhusu Jane lisikupe shida tutamshughulikia tu.” Sophia akatabasamu halafu yeye na mumewe wakaendelea zao kurudi nyumbani kwao. Walipofika nyumbani wakafungua mlango na kuingia ndani ila leo haikuwa kama inavyokuwaga kwani hawakumkuta Neema pale sebleni na kuwafanya wafurahi na wazidi kumuamini yule mganga, wakatazamana na kuambizana “Kheee huyu babu tungemfahamu zamani ingekuwa raha sana yani Neema na kilanga chake kwisha kabisa” Ibra akatabasamu na kumwambia mkewe, “Naona sasa akili imeanza kukukaa sawa mke wangu jamani, yani yule Neema alikuwa hafai kabisa. Haya kaandae chakula tule sasa” “Twende tukasaidiane kuandaa basi” “Umeanza uvivu wako sasa, kwani kuandaa chakula kuna kazi gani jamani hebu usiwe hivyo mke wangu” “Nilishazoea Neema anatuandaliaga” “Uvivu wako huo ndio ukatuingiza kwenye janga la Neema, mpaka sasa tunajutia tu. Bora hata tumepata mkombozi” “Basi ndio utaongea hapo hadi panakucha ngoja nikapike hiko chakula sasa” Sophia akaelekea jikoni kupika, ambapo alipika wali, nyama na mchicha kisha kutayarisha mezani ili wale. “Yani chakula kimechukua muda wote huo jamani?” “Jamani mume wangu hebu acha gubu basi, unafikiri mimi ni mashine kusema naweza kupika dakika mbili nimemaliza? Mimi ni binadamu” “Mbona Neema alikuwa anapika fasta fasta?” “Wewe mwenyewe ulishakiri kuwa Neema alikuwa mchawi sasa utamfananisha na mimi binadamu wa kawaida?” “Mbona na Jane alipika fasta fasta?” “Kheeee wewe mwanaume mbona una gubu jamani, huyo Jane na Neema wanatofauti gani? Wote wachawi wale” “Aaah usijali mke wangu, ila mboga hizi zilikuwepo ndani kwani maana sijakuona ukitoka kwenda kununua?” “Jana alizinunua Neema ndio zipo kwenye friji” Wakaanza kula ila Ibra alikuwa anakula huku akiguna tu, “Mbona waguna hivyo?” “Sitaki kusema tena usije kuona nakuonea bure” “Kitu gani hicho jamani si uniambie tu” “Kiukweli Sophia chakula ni kibaya mke wangu yani hakinogi hata kidogo” “Unajua hata mimi nakishangaa hiki chakula jamani wakati nimekipika vizuri kabisa, yani hakinogi hapa nakula tu kwavile nimepika mwenyewe” “Nilijua mwenyewe ndio najilazimisha kula kumbe hadi uliyepika unajilazimisha kula?” Sophia akaonekana kusononeka kidogo na kumfanya Ibra ambembeleze kwani hakupendezewa na kumuona mkewe akiwa amesononeka. Walipomaliza kula walishauriana kwenda kulala ambapo kwa pamoja wakaenda chumbani na walipolala tu wakapitiwa na usingizi kabisa, walikuja kushtuka usiku wa manane ambapo aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Ibra ambapo alichukua simu yake na kuangalia mida akaona kuwa ni saa nane usiku ila gafla akasikia kuna watu wanazungumza sebleni na kumfanya ashtuke kasha kumuamsha mke wake ili nae asikie kinachoendelea, vile vile Sophia nae akasikia sauti za watu wakizungumza sebleni. “Mmmh tumevamiwa mume wangu au?” “Hata mimi nashangaa, ni wakina nani hao wanaozungumza huko sebleni?” “Maajabu haya Ibra” “Hebu twende tukashuhudie” “Mi naogopa kwakweli, yani naogopa kabisa hata sijui” “Usiogope bhana, tunatakiwa kujua ni nini kinaendelea” “Mfano tukiwakuta watu wa ajabu tutafanyaje?” “Kwani unaamini juu ya mambo yoyote ya ajabu mke wangu?” “Hapana siamini” “Basi twende tukaangalie” Wakainuka kwa uoga na kuanza kwenda sebleni ili kushuhudia kuwa ni kitu gani kinaendelea, walipofungua malango na kuangaza sebleni hawakuona mtu yeyote na wala zile sauti hawakuzisikia tena na kuwafanya watazamane bila ya majibu yoyote kisha kurudi tena chumbani na kushauriana kulala tu, ambapo walipojilaza tu na usingizi ukawachukua tena hapo hapo. Kulipokucha Sophia alishtuka akiwa anathema sana na kumfanya mumewe amuulize kuwa tatizo ni nini, “Nimeota ndoto ya ajabu sana” “Ndoto gani hiyo?” “Eti ule muda tuliokuwa tunakula kile hakikuwa chakula” “Kheee kilikuwa kitu gani sasa?” “Eti yalikuwa ni mavi ya mbuzi” “Aaarrghhh jamani mambo gani haya? Mavi tena? Yani tumekula mavi?” “Ila ni ndoto tu mume wangu” Wakainuka pale kitandani na kuelekea jikoni ambapo walifunuka jungu la chakula wakashangaa kuona ni mavi ya mbuzi yamejaa kwenye sofuria. “Aaaarrghh jamani tumelishwa uchafu ptuuu ptuuu jamani nasikia hadi kichefuchefu” “Sophia ila mimi nilikwambia kuwa chakula hakikuwa cha kawaida” “Sasa mimi ningefanyaje mume wangu jamani? Sikupenda tule uchafu pia yani hapa najisikia kichefuchefu khatari. Mi leo sipiki kwakweli” “Hata ukipika unadhani nani atakula? Labda ule mwenyewe kwakweli mimi siwezi” “Unaonaje tukienda kwa dada Siwema tukapotezee muda huko leo” “Hapana, twende tukapotezee muda kwenye biashara yangu humu ndani tutarudi kulala tu” Wakakubaliana hivyo kisha kwenda kujiandaa na kutoka ambapo moja kwa moja walienda kwenye biashara ya Ibra ila kuna jambo lilimstaajabisha kidogo Ibra kwani kwenye duka lake hakununua mzigo mpya kwa muda mrefu ila alishangaa kuona duka limejaa sana, “Kheeee yani kila siku unalalamika umeishiwa kumbe pesa umewekeza humu” “Unajua hata mimi mwenyewe nashangaa kuwa imekuwaje tena maana mzigo uliisha kabisa” “Basi maajabu haya” “Ila maajabu kama haya ndio mazuri mke wangu sio yale ya kula mavi ya mbuzi” “Mmh usinikumbushe ule uchafu. Ila hata hivyo tunatakiwa kuchunguza mume wangu maana haya maajabu yamezidi jamani ya kununuliwa bidhaa duh!” Siku hiyo walikaa hapo dukani na vitu vilinunulika sana na kuwafanya waingize pesa nyingi na kuchekelea, hadi muda wanafunga duka bado wateja waliendelea kumiminika yani walifunga duka sababu tu muda ulikuwa umeenda tayari. Walipofika nyumbani walikuwa na furaha sana huku wakisifia kuhusu hiyo siku, “Yani mke wangu ikiwezekana basi kila siku tuwe tunaenda wote dukani maana haya mauzo si mchezo” “Nina baraka mimi mume wangu” “Nimeamini kweli una baraka” Wakatabasamu ila kwavile walishakula huko huko hawakuona sababu ya kula tena na kuamua kuoga na kulala huku wakiwaza kuwa kesho wawahi kwa Yule babu. “Halafu mume wangu nimekumbuka kitu” “Ni kitu gani hicho?” “Nahisi Yule babu ndio katuletea baraka zote hizi” “Halafu kweli, dah nitamuandalia zawadi kubwa sana baada ya haya mambo kuisha kabisa” Kisha wakalala na siku hiyo hakuna jambo lolote lililowatisha kwani walilala vizuri kabisa hadi kunakucha. Asubuhi na mapema waliamka na kujiandaa kisha wakatoka na kuelekea kwa Siwema ambako naye walimkuta ameshajiandaa, hawakupoteza muda na kuanza kuelekea kwa Yule babu. Walipofika walishangaa sana kuona kuna umati mkubwa wa watu wakahisi huenda ni kwavile mganga, wakashuka kwenye gari na kusogea karibu ila walishangaa kila mmoja akiongea la kwake walipoulizia vizuri wakagundua kuwa Yule babu alikuwa amekufa. “Kheee amaekufa? Haiwezekani jamani haiwezekani” “Haiwezekani kivipi? Mzee ametutoka bhana tena gafla tu” Ibra alihisi kunyong’onyea gafla na kukosa nguvu kisha akamuomba mkewe waondoke kwani alijihisi kamavile anaota. Sophia na Ibra waliondoka eneo lile huku wakiwa na mawazo hata kumsahau Siwema ambaye walienda nae pale, walirudi nyumbani kwao moja kwa moja na kuingia ndani, walikaa sebleni wakiwa wamejawa na mawazo wakasikia sauti ya mtu akicheka kugeuka wakamuona Neema akicheka. Itaendelea kama kawaida……!!!!!!!!!

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments