Muigizaji wa Nigeria aomba radhi kwa kukumbatiwa
Muigizaji mashuhuri, aliyepigwa marufuku katika sekta ya uigizaji ya Hausa kutokanana 'utovu wa nidhamu' ameomba radhi.
Kuonekana kwa Rahama Sadau akikumbatiwa katika kanda ya video ya mwanamuziki mashuhuri wa Nigeria Classiq kumewauadhi baadhi ya watu.
Bi Sadau ameomba radhi kwa aliowaudhi, lakini amesema 'hakufanya makosa'.
Filamu za Hausa ni maarufu sana kaskazini mwa Nigeria kuliko na idadi kubwa ya waislamu ambako ni mwiko kwa wanaume na wanawake kushikana mikono hadharani.
Sekta hiyo , inayojulikana kama Kannywood, imeshutumiwa na viongozi wahafidhina wa kidini kwa kuharibu maadili ya watu.Muungano wa filamu Motion Pictures Practitioners nchini Nigeria ulimpiga marufuku muigizaji huyo katika filamu za Kannywood, ukisema kuwa kuonekana kwake katika video hiyo kunakwenda kinyume na maadili ya sekta hiyo ya uigizaji.
Uliongeza kuwa unatumai kuwa marufuku hiyo itakuwa funzo kwa waigizaji wengine wanaotarajiwa kuwa 'vioo vya jamii'.
Bi Sadau anasema yeye ndio wa kulaumiwa kwa kilichotokea lakini amelalamika kuwa katika kazi yake, hana budi "kuwagusa watu pasi kuwana dhamira mbaya ".
Lakini amewahakikishia watu kuwa atakuwana nidhamu zaidi akiongeza kuwa: "nina mipaka ambayo siwezi kuthubuti kuyavuka."
Image copyright Finesse Entertainment Muigizaji nyota huyo wa Kannywood alionekana katikavideo ya wimbo wa Classiq kwa jina 'I Love You'.
Classiq anaonekana kulemazwa kwa mapenzi na mchuuzi wa mboga sokoni amabye ni Bi Sadau.
Mwanzo anamkataa na anamfukuza lakini mwishowe anamkubali.
Wanashikana mikono na kukumbatiana kidogo, jambo ambalo ni kawaida katika filamu za matifa ya magharibi.
Lakini kwa wengi kaskazini mwa Nigeria wameona kwamba amevuka mpaka na Classiq katika video hiyo, anasema mwandishi wa BBC kutoka Abuja.
Disqus Comments