Bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani ajiuzulu
Bingwa wa ndodi katika uzani mzito duniani Tyson Fury anasema kuwa amejiuzulu kutoka kwa ndondi katika ujumbe uliochapishwa katika mtandao wa Twitter.
Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28,alijiondoa katika pigano la marudiao dhidi ya raia wa Ukrain Wladmir Klitschko,lililopangwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na maswala ya kiafya.
Fury ambaye anamiliki mataji ya WBA na WBO anakabiliwa na kesi mnamo mwezi Novemba inayohusisha madai ya utumiaji wa sawa za kusisimua misuli.
''Ndondi ni kitu kibaya zaidi nilichoshiriki'',ilisema Twitter yake akiongezea: ''Mimi ndio bingwa ,na aliyestaafu''
Fury alitarajiwa kupata kitita kikubwa tangu alipojiunga na ndondi wakati wa pigano lake la pili dhidi ya Klitschko katika uwanja wa Manchester mwezi huu.
Aliahirisha pigano la marudio dhidi ya raia huyo wa Ukrain ,ambalo lilipangwa kufanyika mnamo mwezi Julai baada ya kupata jereha la kifundo cha mguu wakati wa mazoezi.
Amepewa siku 10 na shirikisho la ndondi duniani WBO kutoa maelezo na kuahirishwa ka pigano hilo la marudio kwa mara ya pili.
Disqus Comments