-->

Wanajeshi wa Iraq wapambana na IS ndani ya Mosul

Wanajeshi wa Iraq wanapambana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS ndani kabisa ya mji wa Mosul, na kuwaongezea shinikizo wanamgambo hao wenye itikadi kali ambao hawana njia nyingine za kutoroka na badala yake kuwaacha raia waliokwama kujikuta katikati ya mapigano. Wanajeshi wa Iraq walichukua udhibiti wa maeneo zaidi mashariki mwa Mosul, wakilenga kuendeleza kasi ya kujaribu kupambana na wapiganaji hao katika juhudi za kuuokomboa mji huo ambao ndio ngome ya mwisho ya IS nchini Iraq. Katika siku za karibuni, wanajeshi wa Iraq wamekata barabara muhimu inayotoka Mosul hadi mpaka wa magharibi wa Syria, ambako IS bado inadhibiti mji wa Raqa. Kwingineko, mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari umewauwa karibu watu 80, wengi wao mahujaji waliokuwa wakirejea kutoka mji mtakatifu wa kishia wa Karbala. Gari hilo lilipuka katika kituo cha petroli ambako mabasi yaliyokuwa yamewabeba mahujaji hao yalikuwa yameegeshwa. Maafisa wa usalama wanasema kulikuwa na karibu mabaso saba katika kituo hicho cha petroli.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments