-->

Mji wa kale wa zaidi ya miaka 5,000 wagunduliwa Misri

.
Wanaajiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 5,000 iliyopita. Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa. Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos. Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011
Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na mawe. Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa. Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji makuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments