-->

Watu 10 wauawa mashariki mwa DRC

Takriban watu 10 wanaripotiwa kuuawa Jumapili usiku wakati wa makabiliano kati ya wanajeshi na waasi, wanaoaminiwa kutoka nchini Uganda eneo lililo mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo. Raia 8 waliuawa kwa kupigwa risasi akiwemo mwanajeshi mmoja na mtu mwingine anayekisiwa kuwa muasi. Wanamgambo wa ADF kutoka nchini Uganda wanaoipinga serikali ya rais Yoweri Museveni wamekuwa wakiendesha harakati eneo hilo kwa miongo miwili. Serikali na Umoja wa Mataifa wamewalaumu ADF kwa misururu ya mashambulizi eneo hilo. Takriban raia 700 wameuawa kwa muda wa miaka miwili iliyopita kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu linalosema kuwa haijulikani ni nani amehusika na mauaji hayo.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments