-->

Viongozi wakuu wa chama cha Republican wanazidi kuondoa uungaji wao mkono kwa Donald Trump kwa matamshi yake ya kuwadhalilisha wanawake.

Miongoni mwa wanasiasa wa hivi punde zaidi ni pamoja na aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, na aliyegombea kiti cha urais nchini humo, Senator John McCain. Lakini Trump amesema kwamba hatajiondoa kutoka katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti hicho licha ya malalamishi kutoka kote duniani kutokana na matamshi yake ya kuudhi kuwahusu wanawake, aliyo-yatoa mwaka 2005. Zaidi ya wanasiasa 24 wa chama chake cha Republican, sasa wamesema hadharani kuwa hawamuungi mkono bilionea huyo na wanamtaka kumuachia mgombea mwenza Mike Pence nafasi ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani hapo mwezi Ujao. Miongoni mwa wanaolaani matamshi hayo ya Trump ni pamoja na mkewe Trump- Melania.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments