-->

Polisi yamsaka mshukiwa wa ugaidi Ujerumani

Polisi katika mji wa mashariki wa Chemnitz nchini Ujerumani wanamsaka kijana wa Kisyria mwenye umri wa miaka 22 ambae anatuhumiwa kupanga njama za shambulizi la bomu. Maafisa wanasema wamekamata vitu vyenye uwezo mkubwa wa kutengeneza viripuzi katika makazi yake baada ya kupata taarifa kutoka kwa taasisi ya upelelezi wa ndani ya Ujerumani. Wameanzisha msako mkali wa mtuhumiwa, aliyetambuliwa kama jina la Jaber A., na wanawashikilia watu watatu ambao inaaminika kuwa ni washirika wake. Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa mtuhumiwa ana mahusiano na kundi la kigaidi, linalojiita Dola la Kiislamu, na kwamba alikuwa anapanga kushambulia uwanja wa ndege wa Ujerumani. Msemaji wa Polisi Tom Bernhardt amesema kiripuzi kilichopatikana katika chumba chake mjini Chemintz ni sawa na kilichotumika katika mashambulizi ya Paris na Brussels.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments