-->

nyumba ya maajabu [37-41]

NYUMBA YA MAAJABU: 37 Walipofika kwenye hiyo njia wakapanga kumuonyesha Siwema hiyo hoteli ila walishangaa ambavyo hawakuiona hiyo hoteli wala nini, “Sophy, ile hoteli si ilikuwa hapo au nimesahau?” “Mie nakumbuka vizuri ilikuwa hapo, imekuwaje tena jamani?” Siwema alipoangalia kwa makini eneo lile alishangaa pia na kuwauliza, “Mbona eneo lenyewe limeandikwa ni eneo la makaburi sasa hiyo hoteli iko wapi?” Na wao wakaangalia kwa makini sasa wakaona kibao kilichoandikwa kwa herufi kubwa ‘ENEO LA MAKABURI’ wakatazamana na kushangaa, na walipoangalia vizuri wakaona makaburi mengi tu yamejipanga. Ibra alimuuliza mkewe kwa hamaki, “Eneo la makaburi kivipi? Tumesahau au?” “Makubwa haya mume wangu” Siwema akawauliza jina la hiyo hoteli lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa na kumbukumbu ya jina, “Hivi tuliangalia jina kwani?” “Hatukuangalia bhana, mi nakumbuka tuliingia na kula kisha kuondoka” Siwema alivyoona wanajiuma uma tu akawaomba waondoke eneo hilo, “Tuondokeni hapa na tuendelee na safari yetu” Ibra akaondoa gari kisha safari yao ikaendelea, Siwema alianza kuongea kwa kuwapa ushauri hawa watu wawili, “Kwanza kabisa mnachotakiwa kufahamu ni kuwa Neema ni mtu wa aina gani? Je ni binadamu wa kawaida? Na kama ni binadamu wa kawaida aliwezaje kufanya yote yale? Ni binadamu gani anayeweza kufanya vile? Jiulizeni ili mpate majibu ila mkiendelea hivi mtakuwa mnakutana na maajabu kila siku, na mkiona mambo yamewafika shingoni kuna Sheikh fulani hivi huwa anafanya sana dua itabidi niwapeleke huko” “Mmmh dada na wewe umeanza sasa, umemaliza ya waganga unatuletea habari za Masheikh” “Kwani kuna ubaya gani? Linaloshindikana kwa mwanadamu basi ujue Mungu anaweza” “Ndio Mungu anaweza, ila kwanini twende kote huko kwani sie Mungu hatusikilizi?” “Uwiiiiii nyie watu ni wabishi sana sijui hata mmeumbwa vipi nyie halafu wote mmekutana akili zenu zinafanana, ila kuhusu waganga siwapeleki tena mlinitia aibu sana” “Hata hivyo hatuna uhitaji wa kwenda kwa waganga tena, tutakapomtua huyu mtoto basi tumemaliza kila kitu. Maswala ya kutupeleka kwa Masheikh sijui wachungaji halafu waanze kutuomba sadaka hatupo tayari kwakweli” “Aliyewaroga kafa maana angekuwa hai basi angewaonea huruma” Kimya kidogo kikatawa huku ile safari ikiendelea mpaka walipofika eneo la tukio. Ibra akasimamisha gari na kushuka kisha Siwema nae akashuka ambapo wakapanga kuwa wakazungumze kwanza na wahusika kisha ndio wampeleke mtoto, kwahiyo walimuacha mtoto na Sophia ndani ya gari. Walifika mapokezi na kupokelewa vizuri tu kisha kuwakuta wale wahudumu wa kituo ambapo waliongea nao kwa urefu kidogo ili wapokelewe huyo mtoto, “Ila kama na nyie mnauwezo mnaweza mkamlea tu huyo mtoto bila tatizo ila cha msingi tu ni kutoa taarifa polisi na kwenye ubalozi wako watambue hilo ili kama atatokea mtu yeyote kumdai mtoto huyo muwe na haki za kisheria kama mtoto wenu kabisa” “Sisi tungemlea dada ila majukumu ni mengi sana, hata hivyo tutakavyomuacha hapa sio kwamba tumemtelekeza hapana ila tutakuwa tunakuja mara kwa mara kumtembelea.” Basi huyu dada akawapa taratibu zote ambapo kuna fomu walijaza kisha akawaambia wampeleke huyo mtoto, wakainuka kwa lengo la kwenda kumchukua mtoto nje. Walipofika nje Ibra alishangaa kuona gari yake ikiwa imefunguliwa milango yote yani iko wazi, akapata hofu na kujiuliza kama mkewe anaweza kufanya vile kweli. Wakasogea karibu na kuangalia ndani ya gari ila hakuonekana Sophia wala yule mtoto, Ibra alimshtua Siwema “Dada, hivi unajua Sophia na mtoto hawapo humu?” “Hawapo kivipi? Si tumewaacha humo? Na je ni nani aliyefungua milango yote ya gari hivyo?” “Hata mimi nakosa jibu dada, ni nani anayeweza kufanya hivi kwenye gari yangu?” Wakajaribu kuangaza huku na huko ila hakuonekana Sophia wala yule mtoto na haikujulikana ni wapi wameelekea, “Makubwa haya dada” “Sio makubwa ila ni maajabu, inamaana wametekwa?” “Usiseme hivyo dada, kumbuka nampenda sana mke wangu Sophy” “Sasa tutaanzia wapi kumtafuta?” Wakaambizana wajaribu kuuliza watu wa hapo karibu ili kama kuna mtu amewaona awaambie, wakazunguka pale ila kila mtu waliyemuuliza aliwashangaa tu na kuwaambia kuwa hawajamuona huyo mdada aliyebeba mtoto, walizunguka sana na kuchoka mwishowe Siwema akatoa wazo kuwa waende kuripoti polisi ili kama Sophia ametekwa wajue ni wapi pa kuanzia. Wakakubaliana hivyo na kuingia kwenye gari wakielekea kwenye kituo cha polisi, walipokuwa wanakaribia kituoni hapo wazo likamjia Ibra kuwa wampigie simu Sophia, “Kheee halafu kweli, yani muda wote tumekazana kumsaka bila ya kumpigia simu duh! Hebu mpigie hapo shemeji” Ibra akachukua simu yake na kumpigia simu Sophia muda huo huo ambapo baada ya sekunde chache tu kuita simu ikapokelewa na ni Sophia ndiye aliyekuwa akizungumza kwenye simu ile, “Uko wapi Sophy?” “Nipo nyumbani, kwani vipi?” “Vipi? Hujui kwani jamani, si tumekuja wote huku kwa lengo la kumuacha huyo mtoto, kwanini umeondoka bila ya kunitaarifu?” “Ibra usinichanganye bhana yani usinichanganye kabisa, wewe mwenyewe utoe wazo la kurudi nyumbani halafu saizi unilaumu, usinichanganye tafadhali. Leo umenifurahisha usitake kuibadilisha furaha yangu tafadhali, rudi nyumbani na ulete hiyo mboga uliyosema” Kisha Sophia akakata simu, Ibra akamuangalia Siwema na kumwambia, “Unajua dada huyu Sophia ni mwehu sana, yani hata haelewi ni jinsi gani wenzie tumehangaika kumtafuta jamani. Eti yupo nyumbani, yani nimeshindwa kumuelewa kabisa akili zake sijui zikoje” “Nyie mnajuana wenyewe, yani hapa nimechoka balaa kwa ujinga wenu. Mtu nimeacha shughuli zangu ila mmeishia kunisumbua tu. Hebu nirudishe nyumbani kwangu mie” “Basi tupitie nyumbani kwangu kwanza ukamseme mdogo wako” “Weee Ibra tafadhali usinitie uchizi, mi nina akili zangu timamu kabisa. Hebu fikiria ni toka saa ngapi tunamtafuta huyo Sophia wako hadi jioni hii halafu unaniambiaje? Hebu nipeleke nyumbani mie, nyie mtajuana wenyewe na akili zenu mbovu hizo” Ibra hakubisha sana zaidi ya kugeuza gari yake na kuanza safari ya kumpeleka Siwema nyumani kwake. Walipofika nyumbani kwa Siwema ilikuwa jioni sana ila Siwema aliposhuka Ibra akamuomba maji ya kunywa kwahiyo Siwema akaenda ndani kwa lengo la kumletea maji hayo, wakati Ibra yupo pale nje akiwa amefungua mlango wa gari yake na kuangalia angalia mazingira ya pale huku akisubiri hayo maji akaja yule bibi ambaye aliwahi pia kukutana na Sophia. Ibra alimsalimia yule, bibi ila yule bibi kabla ya kuitikia akamwambia Ibra, “Nyumba yako ni nyumba ya maajabu” “Nyumba ya maajabu! Kivipi?” “Wewe unaiona nyumba yako kuwa sawa? Je wewe mwenyewe unajiona kuwa sawa? Hilo gari unalotembelea je unahisi lipo sawa?” “Sikuelewi, hebu nieleweshe” “Nyumba yako ni ya maajabu, nimewahi kukutana na mkeo nikamwambia maneno haya na ilikuwa mapema sana ila hakutaka kunielewa. Mkihitaji msaada njooni niwasaidie ila ile nyumba ni ya maajabu” “Sikuelewi bibi yani sikuelewi kabisaa” “Ngoja nikueleweshe sasa” Mara Siwema akatoka ndani akiwa na kikombe cha maji, na alipomuona yule bibi tu kama kawaida akaanza kufoka, “Hivi wewe kizee unataka nini nyumbani kwangu jamani! Si kila siku nakwambia sitaki kukuona wewe, tafadhali ondoka, nimesema ondoka tena sasa hivi” Ibra akamuangalia Siwema na kumwambia, “Tafadhali usimfukuze, yupo kuniambia maneno ya maana sana hapa” “Maneno ya maana atakuwa nayo huyo bibi? Hawezi kuwa na la maana hata moja, huyo bibi ni mchawi wa wachawi, mtaani kwake kashafukuzwa ndio anatanga tanga huku yani usimsikilize hata moja uatajuta zaidi ya unavyojuta sasa” Kisha Siwema akamuangalia tena huyu bibi na kumfokea, “Hivi bibi husikii jamani, si nimekwambia uondoke! Nenda zako bhana hakuna mwenye haja ya miushauri yako isiyo na maana” Yule bibi alitikisa kichwa kisha akaondoka zake kisha Siwema akakzana kumwambia Ibra kuhusu mabaya ya yule bibi ambayo yeye amesimuliwa na watu wengine. “Ila ushawahi kushuhudia?” “Kushuhudia kitu gani? Mi nishakwambia kwamba huyu bibi ni mchawi na nilimuonya Sophia hivi hivi, mwisho wa siku hadi leo akibeba mimba zinatoka unafikiri ni sababu ya nini?” “Mmmh usiniambie ni sababu ya huyu bibi?” “Ndio, hiyo ndio sababu. Alikutana nae pale kwenye mpera wakati Sophy anatafuta pera, mi nikamkataza kuongea na huyu bibi ila yeye akakazana kuongea nae na mwisho wa siku ameishia kupoteza mimba kila leo. Ni huyu bibi tu anayekula watoto wenu” Ibra alishangaa sana na kumfanya ashindwe kunywa hata yale maji kisha akamuaga Siwema, “Kheee hata maji umeghairi kunywa?” “Yani nimejisikia vibaya gafla dada, roho huwa ianiuma sana nikikumbuka watoto wangu. Ngoja tu akili yangu ikae sawa ila huyu bibi nitamkomesha” Ibra akaingia kwenye gari yake na kuondoka zake akielekea nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake kuna kitu cha tofauti alikiona na kilimshangaza sana huku akiangalia mara mbili mbili na kujiuliza, “Tuseme kuna mgeni amekuja au? Na kama kuna mgeni amekuja basi mgeni huyo ni nani?” Alikosa jibu ila ile gari ya pale uwani kwake ilimchanganya sana kwani ilikuwa ni gari mpya kabisa tena ya gharama, Ibra akaingia ndani akitegemea kumuona mgeni ila alishangaa kumuona mkewe akiwa mwenyewe pale sebleni, akamsalimia ila kabla Ibra hajauliza chochote kuhusu ile gari, akaulizwa swali na Sophia “Hiyo mboga uliyosema unaifata iko wapi?” “Mboga? Mboga gani tena?” “Halafu Ibra acha masikhara, sijui unafikiri tutapika nini usiku wa leo jamani” Ibra hakuta kubishana na mkewe kuhusu maswala ya mboga kwahiyo moja kwa moja akamuuliza kuhusu gari aliyoiona pale nje, “Na ile gari pale nje ni ya nani?” “Gari gani hiyo?” “Ile mpya” Sophia akacheka kwanza kisha kumjibu mumewe kwa kicheko, “Ila Ibra mara nyingine unatakaga kunichekesha tu. Ile gari si umeninunulia mwenyewe jamani!” “Nimekununulia! Saa ngapi nimekununulia wakati mimi uliniacha kule” “Weee Ibra wewe hebu kuwa makini basi yani kabisa unaniuliza kuhusu gari ulilonunua mwenyewe jamani! Hiyo gari si umeninunulia kama tulivyoongea kipindi kile kuwa nahitaji gari langu” “Sophy acha kunichanganya bhana hebu niambie ukweli” “Ukweli gani sasa zaidi ya huo?” “Hebu niambie ulipotoka pale kituoni ulielekea wapi?” “Si tuliondoka pamoja pale au umesahau?” Ikabidi Ibra aseme amesahau kwani kila alipomwambia mkewe kuwa hawakutoka wote mkewe alibisha kwahiyo akamwambia kuwa amesahau ili amwambie ilivyokuwa maana alikuwa akishangaa tu yote aliyokuwa akielezwa na mkewe, “Na kweli naona umepoteza uelekeo kwenye kichwa chako, ngoja nikueleze vizuri labda kumbukumbu zako zitarejea” Ibra akatulia tuli kumsikiliza mkewe, “Mimi nilibaki kwenye gari na mtoto, kisha wewe na Da’Siwema mkashuka kwenda ndani mule muda kidogo ukarudi na kuniambia kuwa umeona sio vyema tumuache mtoto mahali hapo sababu mazingira yake sio mazuri na malezi yao yanaonekana kuwa duni, kwahiyo ukasema turudi nyumbani. Nikakuuliza vipi Da’Siwema tunamuacha? Ukasema kuwa amesema tumuache tu kuna vitu anachunguza, halafu tukarudi wote hapa. Ukasema unaenda kuniletea zawadi, ukatoka na muda kidogo ukarudi na hiyo gari na kunikabidhi kila kitu kuhusu hiyo gari nikafurahi sana hapa ndio ukaniaga kuwa kuna mboga umeikumbuka sana unaenda kuinunua tule leo. Na ndio muda huu umerudi mume wangu eti unajifanya umesahau kila kitu loh!” “Yani Sophy hata nikikuelekeza huwezi kunielewa kwakweli hata sijui nikuelekezeje” Ibra aliinama akiwa na mawazo sana huku akijiuliza kuwa ni vitu vya aina gani hivyo maana alishindwa kabisa kumuelewa mke wake na kumfanya Sophia nae amshangae tu. Sophia alifikiria kitu na kuhisi kuwa huenda mume wake amevurugwa tu, kisha akainuka na kumuomba funguo ili akaangalie kwenye gari ambapo Ibra alimkabidhi funguo hiyo. Sophia alitoka nje na kwenda kufungua gari ambapo pembeni ya kiti cha dereva akaona mfuko mweusi kufungua akakuta mboga, akacheka na kusikitika kisha akasema. “Huyu mwanaume sijui amevurugwa na nini jamani, mboga si hii hapa kwenye mfuko halafu anasema hajaileta loh! Huyu mume wangu nae kashakuwa tatizo tayari” Akabeba ule mfuko na kuelekea nao ndani kisha akamwambia mume wake, “Ibra, mboga si hii hapa umeleta halafu unasema hujaleta” “Mboga gani Sophia? Hivi unajua kama unanichanganya tu” “Nakuchanganyaje? Si ulisema leo unahamu na pweza wewe! Na hawa hapa umeleta, tena umeweka na chachandu inanukiaje” Kisha Sophia akaingiza mkono kwenye mfuko ili kuchukua kipande aonje, Ibra akashtuka na kumkataza mke wake “Tafadhali Sophy usile, mimi sijui ilipotoka hiyo mboga. Sijainunua mimi” “Acha masikhara yako bhana” Sophia akaingiza kile kipande mdomoni na kuanza kukitafuna huku akisifia kuwa ni tamu sana, kwakweli Ibra alitamani kufanya kitu ila alishindwa kwani aliiona akili yake kama ikichanganyikiwa hivi. Mara gafla Yule mtoto akaanza kulia chumbani kwa nguvu kamavile kaangushwa, Sophia akakimbilia chumbani kwenda kumuona mtoto Yule kuwa kwanini analia vile. Sophia alipomuona Yule mtoto alishtuka na kupiga kelele za kumuita Ibra, “Ibra, Ibra njoo uone” Ibra alikwenda kwa haraka sana, naye alishtuka pia kwani Yule mtoto alikuwa akilia sana halafu macho yake badala ya kutoa machozi yalikuwa yakitoa damu. Itaendelea kama kawaida…….!!!!!! Toa maoni yako mdau, · NYUMBA YA MAAJABU: 38 Mara gafla Yule mtoto akaanza kulia chumbani kwa nguvu kamavile kaangushwa, Sophia akakimbilia chumbani kwenda kumuona mtoto Yule kuwa kwanini analia vile. Sophia alipomuona Yule mtoto alishtuka na kupiga kelele za kumuita Ibra, “Ibra, Ibra njoo uone” Ibra alikwenda kwa haraka sana, naye alishtuka pia kwani Yule mtoto alikuwa akilia sana halafu macho yake badala ya kutoa machozi yalikuwa yakitoa damu. Ibra alimuangalia mkewe huku amejawa na hofu zaidi, kisha akamuuliza “Tutafanyaje sasa?” “Inabidi mimi nikuulize wewe maana hata sijui tufanyeje” “Hebu kalete maji jikoni” Sophia akatoka na kuelekea jikoni, ila ule muda Sophia alipotoka na yale machozi yaliyokuwa yakimtoka Yule mtoto kama damu yalikata na kumfanya Ibra ashangae zaidi kisha kumwambia mkewe kwa sauti, “Basi usilete tena” Sophia akarudi tena chumbani na gafla Yule mtoto akaanza kutoka tena machozi ya damu, “Kheee huyu mtoto vipi wakati hiyo damu ilishakatika?” “Labda hataki kuniona” “Mara ngapi anakuona? Iweje leo?” Ibra akamuangalia vizuri mkewe akaona akizunguka tu na ule mfuko wake wa pweza, “Mbona unazunguka na huo mfuko jamani! Kauweke jikoni basi” Sophia akatoka tena, safari hii Yule mtoto aliacha kulia na waala zile damu hazikumtoka tena. Sophia aliporudi alishangaa kumuona Yule mtoto akicheza tu wala damu hazikuwepo tena “Kheee umemfanya nini hadi katulia hivi?” “Sijamfanya chochote ila hata mimi mwenyewe nimeshangaa huo utulivu wake mara baada ya wewe kupeleka ule mfuko jikoni” “Mmmh inamaana ule mfuko ndio tatizo?” “Inawezekana” Sophia hakukubaliana na hiyo hoja ya mumewe kwahiyo akataka kuhakikisha kama ni kweli, akaenda tena jikoni kuchukua ule mfuko na kuja nao chumbani. Gafla Yule mtoto alianza kulia kwa nguvu na macho yake kutoa machozi ya damu. Ikabidi Sophia atoke na ule mfuko tena na kuurudisha jikoni kisha akaenda tena chumbani, Ibra akamwambia mkewe “Umeamini sasa kuwa ule mfuko ndio tatizo?” “Mmmh yani nashindwa kuelewa ujue kuwa kuna mahusiano gani kati ya huyu mtoto na ule mfuko hadi atoe machozi ya damu” “Hata mimi bado sielewi” “Ngoja nikauchukue tena” “Acha bhana Sophy usiende kuuchukua” “Naenda kuuchukua, nataka kujua kisa na mkasa. Nataka kujua nini ni nini” Sophia akatoka tena pale na kuelekea jikoni kwa lengo la kuuchukua tena ule mfuko. Alipoingia jikoni alishangaa kuona ule mfuko hauonekani pale alipouweka, na kujiuliza kuwa huenda umeanguka ila kila alipoangalia hakuuona “Mmmh ni nani anayeweza kuuhamisha mfuko ule ilihali humu ndani tupo wawili tu na muda wote huu mume wangu yupo chumbani!” Sophia alijiuliza bila ya kupata jibu la aina yoyote ile na kumfanya abaki na maswali mengi kichwani mwake, akaamua kurudi chumbani alipo mumewe ambapo safari hii alimkuta amekaa kitandani “Hivi unaweza kuamini kuwa ule mfuko haupo tena” “Haupo tena kivipi?” “Pale nilipouacha sijaukuta, unajua ni maajabu haya” “Yani hayo ndio unaona maajabu ila swala la mumeo kuwa wawili hata hushangai” “Mume kuwa wawili kivipi wakati uko peke yako?” “Hivi wewe hata akili yako haijafunguka mpaka sasa kuwa uleyerudi nae mchana nyumbani hakuwa mimi” “Mmmh kama hakuwa wewe, sasa lile gari amenunua nani?” “Ndio ujitafakari hapo mke wangu ila hakuwa mimi” Sophia akanyamaza kwa muda na kuwa kama akitafakari kitu kisha akamuangalia mume wake na kumwambia, “Hivi unakumbuka kuna siku kabla ya kumuokota huyu mtoto tuliwahi kusikia sauti ya mtoto akilia kama huyu, unakumbuka?” “Nakumbuka ndio na inanifanya nihisi kuwa kunakitu tumefanyiwa ila tu hatujajuwa kuwa tumefanyiwa na nani” “Inamaana kwamba huyu mtoto alikuwepo ndani toka siku hiyo, je ni nani aliyemleta?” “Umenifanya nifikirie kitu mke wangu, nahisi ni Neema aliyemleta huyu mtoto na ni yeye aliyetuwekea kwenye buti la gari na kuandika ile barua yenye vitisho vikali” “Unahisi alikuwa na lengo gani?” “Nahisi hakufurahishwa na swala la kuondoka hapa kwahiyo akatuletea huyu mtoto ili atusumbue na tupate shida halafu tuwe na uhitaji wake wa kutusaidia ndiomana akafanya hivi” “Na kwakumkomesha hata tusimtafute wala nini, ni bora tuhangaike na huyu mtoto mdogo kuliko kuhangaika na Neema mtu mzima” Wakapanga muda huu wamtengenezee huyu mtoto maziwa kwani hawana kumbukumbu kuwa alikula muda gani mara ya mwisho, baada ya majadiliano yao hayo wakasahau kabisa kuhusu ule mfuko uliokuwa na pweza. Sophia aliandaa maziwa na yalipokuwa tayari akaenda nayo chumbani kwa lengo la kumnywesha yule mtoto ila kama kawaida yule mtoto aliyakataa yale maziwa, “Anakataa mume wangu tufanyaje sasa?” “Achana nae, nadhani huyu mtoto anataka kutusumbua tu kwahiyo hata asikuchanganye akili” Yule mtoto alikuwa akiwaangalia tu kwani muda huu hakulia wala nini, Sophia na mumewe wakapanga kwenda kuoga kwanza kisha wale chakula na kulala ila walipotoka kuoga tu walijikuta wakijilaza kitandani na kila mmoja kuwa hoi kabisa. Wakati wamelala Sophia akajiwa na ndoto na akaona kamavile kuna mtu mkubwa sana amekuja mbele yake, akamvua blauzi kisha akalalia kifua chake na kuanza kumnyonya maziwa alijikuta akihangaika sana kumtoa bila ya mafanikio na alipambana nae kwa muda mrefu sana. Alipokuja kushtuka alimuona yule mtoto akiwa juu ya kifua chake akinyonya ila Sophia hakuwa hata na nguvu za ziada za kuweza kumuondoa yule mtoto kifuani mwake kwani mikono yake ilikuwa ikitetemeka sana na kukosa nguvu kabisa kwahiyo hakuweza hata kujisogeza zaidi zaidi machozi yalikuwa yakimtoka kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kifuani na kwenye maziwa jinsi yalivyokuwa yakivutwa. Machozi yalimtoka sana Sophia kwani hata sauti ya kulia pia hakuwa nayo kabisa, kulipokucha Ibra naye aliamka na kumkuta mkewe akitoa machozi huku yule mtoto akiwa juu yake akiendelea kunyonya.Ibra akashikwa na hasira na kumsukuma yule mtoto pembeni ambapo aliangukia pembezoni mwa mke wake, “Hivi wewe ni mtoto kweli wewe? Unataka kuniulia mke wangu kwanini? Sijapata kuona mtoto firauni kama huyu” Ibra akamnyanyua yule mtoto na wala hakutaka kujiuliza mara mbili, moja kwa moja alimpeleka chumba ambacho Neema alikuwa akilala na kumfungia humo kisha yeye akarudi kumuhudumia mke wake kwani alikuwa karegea kabisa na nguvu ameishiwa. Ibra aliingia kumpikia mkewe uji kwanza na kumnywesha, alivyorudiwa na nguvu ndipo alipoenda kupika chakula kingine kisha alikaa na kuanza kula na mke wake huku akimpa pole sana, “Yani kale katoto ni kajinga sana, pole mke wangu” “Asante, nimeumia sana yani kifua chote kinaniuma” “Pole sana, ila nimemfungia kule kwa Neema, tukikaacha kule kwa siku tatu tu katakuwa kamekufa halafu tutaenda kukazika” “Kheee tutakazika wapi sasa mume wangu si watu watatuona!” “Hata usijali, kakifa tu tutavizia usiku tutakabeba kwenye gari na kwenda kukatupa baharini yani wala hatuhangaiki kukachimbia shimo. Katoto gani kale hata hakavutii, katoto kanafanya mambo kama mtu mzima mara katutolee machozi ya damu yani sina huruma nako tena. Sina mtoto ila sio kwa mtoto yule jamani simtaki kabisa na kama ukibeba mimba na kuzaa katoto kama hako nitakatupa pia” “Usiseme hivyo mume wangu jamani” “Lazima niseme hujui tu ni kiasi gani huyu mtoto ananikera mke wangu” Wakajitahidi pale kula na kumaliza kile chakula kisha Ibra akainuka na mkewe kwenda kuoga na baada ya hapo wakawa na nguvu za kuendelea na maongezi mengine sasa ambapo Sophia alimueleza mume wake kuhusu ndoto aliyoota na jinsi alivyoamka na kumkuta huyo mtoto akinyonya, “Mmmh unamaanisha kwamba huyu mtoto ni mtu mzima?” “Sijui ila kwajinsi nilivyoona kwenye ndoto ndio hivyo, na kwanini basi nishindwe jinsi ya kumtoa kifuani pangu?” “Ila Sophy tusiwekee wazo kuwa ni mtu mzima sababu naona kama itakuwa tatizo zaidi ila tuweke kama ni mtoto tu aliyekosewa kuzaliwa” Kisha Ibra akamwambia mke wake kuwa waangalie Tv ili kuondoa mawazo waliyokuwa nayo ambapo walifanya hivyo na kuiwasha kisha kuangalia, Muda kidogo wakapigiwa simu na mpigaji alikuwa ni Siwema ambapo Ibra alipokea simu ile na kuanza kumsikiliza baada ya salamu, “Basi bhana yule mbibi wa jana si amekuja leo” “Akasemaje?” “Eti kaniambia kuwa mkeo amenyonywa damu usiku, unajua yule bibi ananishangaza sana. Mtu ananyonywaje damu jamani” “Hebu nielezee vizuri dada” “Ila nimemtimua bhana, sema kaniambiaje eti mumtafute haraka sana iwezekanavyo awasaidie ila mimi naona hana msaada wowote yule zaidi ya kutaka kuwatesa tu. Kumbuka kuwa ndiye anayefanya mimba za mkeo zitoke.” Kisha akawaaga na kukata ile simu. Sophia akamuuliza mumewe kuhusu jambo lililokuwa likiongelewa na Siwema. Ibra alikuwa kimya kwa muda akitafakari kisha akaamua kumuelezea mke wake vile ambavyo yule bibi alimwambia jana na jinsi ambavyo Siwema alivyopiga simu na yale aliyoyasema akihusisha na ndoto ya mke wake pamoja na huyo mtoto wao wa ndani. “Nahisi kuchanganyikiwa mke wangu yani nachanganyikiwa kabisa” “Mmmh inamaana nimenyonywa damu kweli?” “Hebu kwanza niambie, je ni kweli ulikutana na yule bibi kipindi ukiwa na mimba ya kwanza ile?” “Ndio na akaniambia kuwa nyumba yetu ni ya maajabu ila Da’Siwema alisema nisimsikilize eti yule bibi ni mchawi” “Siwema kaniambia kuwa yule bibi ndiye anayefanya mimba zako zitoke, sasa mimi nadhani kuna ulazima wa kuonana na huyu bibi ili kujua ukweli ingawa Siwema anatukataza kufanya hivyo au wewe unaonaje?” “Hata mimi nilikuwa na wazo kama lako ila sikuweza kukushirikisha mwanzoni kwani Da’Siwema alishanionya kuwa yule bibi ni mchawi na mwisho wa siku ndio kama hivyo kila nikibeba mimba zinatoka kumbe chanzo ni huyo huyo bibi” “Usijali, tutapanga kwenda kuonana nae” Muda kidogo wakamsikia Yule mtoto akilia kwa nguvu sana, “Vipi tukamchukue?” “Hakuna kumchukua, tujivike moyo wa kikatili huyu mtoto tumkomeshe mke wangu” “Sasa tunawezaje kukaa hapa na makelele ya mtoto kiasi hiko? Tutaweza kulala usiku kweli?” “Kuhusu kulala usijali, leo tutaenda kulala hotelini halafu kesho tutarudi hapa kusikilizia najua hadi kesho kutwa atakuwa ameshakufa huyo mtoto” “Basi tuondoke sasa hivi” Wakaamua kwenda kujiandaa kwa lengo la kuondoka hapo nyumbani kwao, wakati wanatoka nje sauti ya kilio cha Yule mtoto ilianza kukatika taratibu na walipofika nje kabisa haikusikika tena na kuwafanya wahisi kuwa Yule mtoto amenyamaza, ila kwavile walishapanga safari hawakuweza kurudi tena ndani zaidi ya kupanda kwenye gari yao na kuondoka. Walikuwa wakitafuta hoteli nzuri ambayo itawawezesha kula na kulala kwa furaha zaidi, “Vipi umekumbuka kubeba pesa lakini leo?” “Nimekumbuka sana tena nimebeba za kutosha ili tusiumbuke kama siku ile” Safari iliendelea ila kilichowashangaza ni kuwa hawakuweza kufika eneo la hoteli waliyokuwa wanahitaji kwenda na yakapita masaa kama manne wakiwa njiani hadi giza nalo likaanza kuingia, “Inamaana umesahau njia mume wangu au ni nini?” “Sijasahau ila nilikuwa nahitaji leo twende hoteli kubwa sana hapa mjini ila cha kushangaza hatufiki, sasa tufanyeje?” “Tuingie hoteli yoyote tu mume wangu kuliko kutanga tanga hivi bila ya uelekeo maalum” Wakakubaliana kuingia hoteli watakayoiona inapendeza zaidi, ikawa kama bahati kwani mbele yao wakaona hoteli kubwa sana na kuwafanya waamue kuingia hapo. Ila hoteli hii ilikuwa na mandhari ambayo waliiona kwenye hoteli waliyoenda mara ya mwisho hadi kukutana na Neema ila hawakuiona tena siku waliyopita na Siwema. Walitafuta mahali na kukaa huku wakijiuliza kuwa mbona inafanana na hoteli ambayo waliwahi kwenda, muda kidogo alifika muhudumu wa ile hoteli na kuwauliza mahitaji yao ambapo waliagiza chakula kisha wakahitaji wapewe chumba ili hiko chakula wapelekewe humo chumbani. Yule muhudumu aliwapa maelekezo yote ambapo moja kwa moja walielekea kwenye chumba na kuambiwa kuwa bili zote watalipia asubuhi. Chakula kikaletwa na wakaanza kula, chakula hiki kilikuwa na ladha ile ile ya vyakula vilivyokuwa vikipikwa na Neema na kuwafanya wajiulize sana, “Sio hoteli hii kweli tuliyokuja siku ile?” “Nahisi ndio hii hii” “Huyu muhudumu akija kuchukua sahani tumuulize kuhusu Neema” Wakakubaliana hivyo ila ulipita muda bila ya Yule muhudumu kuja kuchukua sahani ingawa walipiga simu mapokezi kuwataarifu kuwa wamemaliza kula ila muhudumu hakuja kuchukua sahani na mwisho wa siku wakaamua kulala tu. Kulipokucha, Ibra ndio alikuwa wakwanza kuamka kwakweli alishtuka sana na kujiangalia kwa makini, yeye na mkewe walikuwa wamelala makaburini tena kila mmoja kaburi lake. Itaendelea kama kawaida………!!!!!!!!!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 39 Wakakubaliana hivyo ila ulipita muda bila ya Yule muhudumu kuja kuchukua sahani ingawa walipiga simu mapokezi kuwataarifu kuwa wamemaliza kula ila muhudumu hakuja kuchukua sahani na mwisho wa siku wakaamua kulala tu. Kulipokucha, Ibra ndio alikuwa wakwanza kuamka kwakweli alishtuka sana na kujiangalia kwa makini, yeye na mkewe walikuwa wamelala makaburini tena kila mmoja kaburi lake. Ibra aliinuka pale kwenye kaburi alilolala yeye huku akiwa amejawa hofu na uoga akasogea pale kwa mkewe akimuamsha kwa kutetemeka ambapo aliamka kwa kushtuka sana huku akijishangaa pia kuwa amelalaje kwenye kaburi, “Tusishangae mke wangu tuondoke” Sophia akainuka pia huku akiwa haamini kabisa na alijiona kama yupo ndotoni vile, wakatembea na kutoka eneo la nje la makaburi yao kisha walipoangalia pembezoni mwa barabara waliona gari yao ikiwa imepaki hapo, Ibra hakutaka kuhoji wala kujihoji akamshika mkewe mkono hadi kwenye lile gari ambapo alipofungua mlango ulifunguka na funguo ilikuwepo ndani ya gari. Ibra aliendesha gari lile hadi nyumbani kwao wakashuka na kuingia ndani, walikaa chini wakitazamana na kujikuta wakiulizana kilichotokea, “Hivi imekuwaje hadi tukalala makaburini jamani? Yani mimi ninavyoogopa makaburi uwiiiiiii sijui hata imekuwaje” “Hata mimi sielewi mke wangu, nakumbuka tu niliposhtuka nikajiona kaburini huku na wewe ukiwa kwenye kaburi la jirani” Wakajaribu kuvuta kumbukumbu kuwa ilikuwaje, na wakakumbuka kuwa mara ya mwisho walikuwa hotelini na walikula na kulala hapo ila walichokuja kushtuka ni pale walipokumbuka kuwa kwenye hoteli hiyo wamewahi kumuona Neema, “Na licha ya hivyo nakumbuka siku tunapita eneo lile na Da’Siwema tuliona makaburi na sio hoteli” Wakashtuka wote kwani wakakumbuka vizuri sasa na kuhisi kuwa huenda wamefanyiwa kiini macho na Neema. Gafla wakasikia mtu akichek na sauti ilikuwa ni ya Neema, wakashtuka sana ila walipotaka kugeuka ili kumuangalia mtu huyo walishangaa kuanguka kwenye kochi lao na kulala usingizi mzito sana. Ilikuwa ni usiku tayari na Ibra akashtuliwa na mlio wa simu yakeambapo aliamka kutoka usingizini na kupokea simu hiyo, mpigaji alikuwa ni mama wa Ibra ambapo Ibra alimsalimia mama yake kimang’amu ng’amu kisha kuendelea na maongezi mengine, “Inamaana ulikuwa umelala mwanangu, umechoka sana eeeh!” “Kidogo tu mama” “Haya sasa nisikilize kwa makini” “Nakusikiliza mama” “Hivi Ibra unamatatizo gani mwanangu? Kwanini huji kututembelea nyumbani? Kwanini hutaki kunijulia hali mama yako? Mbona umebadilika sana mwanangu?” “Nisamehe mama” “Nikusamehe kitu gani? Nilijua hili tatizo ni kwetu tu, nikapiga simu nyumbani kwao mke wako nao wanasema hawana mawasiliano yoyote na nyie, mmekuwa watu gani nyie mnaojitenga na ndugu jamani? Tuwaelewaje sasa?” “Dah mama sijui hata niseme nini jamani” “Najua huna cha kujitetea, hivi ni watu gani hamuwasiliani na ndugu wala nini. Nilienda kule mlipokuwa mnaishi naambiwa kuwa mlihama siku nyingi sana, sawa mlihama sio tatizo ila kwanini hamjatupa taarifa kuwa mlihama? Nasikia mnaishi maisha ya kifahari, hata kama mnaishi maisha ya kifahari ndio msahau familia zenu kweli? Kwani sisi tunashida na pesa zenu jamani! Mnahisi tutawaomba pesa, hapana kama mimi najitosheleza na shughuli zangu mwanangu jamani kwanini umekuwa hivyo? Sijakulea hivyo mimi” Ibra aliishia kuomba msamaha tu kwani hata kujitetea alishindwa na hakujua aanzie wapi kujitetea na aishie wapi kwahiyo akajikuta akiishia kuomba msamaha tu ila mama yake alilalamika sana na kuonyesha wazi hajafurahishwa na kitendo cha mwanae, kisha Yule mama akaaga na kukata ile simu. Ibra sasa aliweza kuitafakarisha akili yake kwani kiukweli ni kitambo sana hakwenda kutembelea ndugu zake na wala hakuwafahamisha ndugu zake mahali anapoishi kwa kipindi hiki. Akamuangalia mke wake na kumuamsha ambaye alionekana kuamka na uchovu sana, “Mama kanipigia simu bhana” “Mama!!” “Ndio mama” Kisha Ibra akamueleza mkewe vile walivyoambiwa na mzazi wao huyo, “Kheee ila mume wangu hivi ni kwanini hatujawaleta ndugu zetu hapa? Kwanini maana hata mama yangu hajui kama nilishawahi kupata mimba na zikatoka” “Ni kweli hawajui, hata mimi mwenyewe sijui ni kwanini hatujawaleta hapa. Usikute haya matatizo yote tunayoyapata ni kutokana na vinyongo walivyonavyo wazazi wetu” “Ni kweli kabiisa” Wakakubaliana waende kuoga kwanza kisha kupanga mikakati yao ya mambo mengine kwani ilionyesha wazi yanayowasibu ni mengi. Wakainuka pale na kuelekea chumbani ila walipofungua mlango wa chumbani ili waingie walipokelewa na moshi mkubwa sana na mzito uliowakumba machoni na kuwaangusha chini kisha kupoteza fahamu kabisa. Walikuja kushtuka pamoja na ilikuwa pamekucha tayari, kila mmoja alimuangalia mwenzie kisha kuanza kukumbuka kilichowatokea nyuma. Ibra akakumbuka kila kitu kisha akajinusa nguo zake, “Unajua mke wangu tumeanza kutoa harufu ya umarehemu, maana ni toka tulipozinduka jana kule makaburini hatujabadilisha hizi nguo hadi leo” Sophia nae akajinusa na kuanza kujiziba pua huku akisema, “Halafu kweli mume wangu mmmh, hebu twende tukaoge tubadili hizi nguo haraka” “Ila jana si ndio tumeshindwa kuingia huko chumbani Sophia?” “Sasa tutafanayaje? Na kwanini tushindwe kuingia chumbani ndani ya nyumba yetu wenyewe? Kwani kuna nini humu ndani?” “Hata mimi mwenyewe sielewi, ila inuka tukaoge maana lazima tubadili hizi nguo la sivyo itakuwa hatari maana najihisi tupo kama marehemu hapa” Wakainuka tena ila walipofungua mlango wa chumbani kwao ili waingie ule mlango ulikuwa mgumu na haukufunguka, Ibra akapata wazo kuwa wasing’ang’anize kufungua kwani wanaweza patwa na matatizo mengine ila Sophia nae akatoa wazo lake “Kwanini tusiende kuoga kwenye kile chumba alichokuwa analala Neema” “Weee Sophia hebu futa hayo maneno kabisa, hebu tutoke” Ibra akamvuta mkewe mkono hadi kwenye gari kisha wakatoka kabisa kwenye lile eneo la nyumba yao ambapo mkewe akamuuliza kuwa wanaenda wapi, “Mi naona twende kwa Siwema tukaoge huko kwake na akatununulie nguo mpya tuvae” “Mmh mume wangu huoni aibu? Yani tukaoge kwa da’Siwema!” “Hakuna cha aibu kwenye matatizo, twende tukaoge huko kisha tutajua cha kufanya baada ya yote” Wakiwa njiani huku wakiendelea na maongezi yao ile gari ya Ibra iligoma kutembea tena, Ibra akashuka na kuangalia kuwa gari yao ina tatizo gani ila hakuweza kubaini tatizo lolote lile, kisha Sophia nae akashuka na kumuuliza mumewe kuwa tatizo ni nini na Ibra akamuweka wazi kuwa gari haikuwa na tatizo lolote lile, “Sasa tutafanyaje?” “Hata sielewi Sophy, hii gari sijui imekumbwa na nini pia?” “Sasa turudi nyumbani au tufanyeje?” “Hapana tusirudi nyumbani tuendelee na safari tu” “Mmmh tunaendeleaje sasa na gari imegoma?” “Kwani daladala zimeisha Sophy? Ilimradi tumeamua kwenda kwa Siwema basi tusighairi hata iweje” “Na hii gari itakuwaje?” “tutaiacha tu hapa, tukitoka huko nitakuja kuicheki kuwa tatizo ni nini? Siwezi kufanya chochote wakati najisikia vibaya na hizi nguo nilizovaa naona mikosi tu” Sophia akawa anasua sua kuondoka eneo lile na kuiacha gari yao ila Ibra akamshika mkono na kumlazimisha kuwa waondoke. Hawakufika mbali sana ikapita daladala hata Ibra akashangaa, “Hii daladala vipi jamani mbona hii sio njia ya daladala?” “Labda inakimbia foleni, tuisimamishe tupande tu mume wangu” “Hapana Sophy nakosa imani na hiyo daladala” “Kheee na wewe Ibra jamani kwani hujawahi kuona daladala zinazochepuka jamani?” “Nimeziona nyingi tu ila hii sina imani nayo” “Acha zako bhana Ibra” Ile daladala nayo ikasimama na kuwafanya wapande kwavile ilikuwa haijajaa kwahiyo wakapata siti na kukaa, ila baada ya dakika chache wakapitiwa na usingizi yani walilala usingizi mzito sana na kuwafanya wasielewe kinachoendelea. Walipokuja kuzinduka ilikuwa ni jioni sana, waliangaliana “Inamaana tumekaa ndani ya hili gari muda wote jamani?” “Nashangaa kwakweli” Walipoangalia pembeni ndani ya lile gari wakaona jeneza na kuwafanya washtuke sana kwani wakati wanapanda hawakuona jeneza hilo, Ibra akainuka kwa uoga na kupiga kelele, “Mnatupeleka wapi jamaniii?” Mtu mmoja kwenye lile gari akamjibu Ibra, “Kwani nyie vipi? Hamjui kama tunasafirisha msiba” Ibra akashtuka zaidi kusikia eti wanasAfirisha msiba wale wakati mwanzoni waliona ni gari ya kawaida ya abiria, kwa jinsi walivyokuwa wakitetemeka ikabidi mtu mwingine kwenye lile gari awaulize “Kwani nyie mnaenda wapi?” Ibra alishikwa kama kigugumizi wakati akijielezea, “Tulifikiri ni gari ya abiria” “Poleni sana, sie tulihisi nyie ni wenzetu basi mnaweza kushuka sasa” Ile gari ikasimamishwa kisha Ibra na mkewe wakashuka huku wamegubikwa na uoga na hofu moyoni. Wakati wanaangaza macho yao kwenye lile eneo waliloshushwa lilikuwa ni eneo la makaburi, yani hapo hofu ikawatawala zaidi ya mwanzo, Sophia alimkumbatia mumewe kwa nguvu sana kwani alijihisi kamavile mwisho wao umefika huku uoga ukiwa umewajaana kuwafanya watetemeke. Ibra akajivika ujasiri wa kiume na kumshika mkewe vizuri huku wakianza kutoka kwenye eneo lile, kuna kaburi walipita na kusikia sauti ya mtu akicheka yani hapo uoga uliwajaa zaidi ya mwanzo na kuwafanya wahisi mwisho wao ndio umefika kabisa ila Ibra alijikaza tena kiume na kumshika mkewe vizuri huku wakitoka kwenye eneo hilo mpaka wakafanikiwa kuwa nje kabisa ya makaburi hayo na kuwa barabarani, “Tunaenda wapi sasa mume wangu?” “Sijui” “Tutafanyaje sasa? Hivi haya mambo ni kweli au naota jamani?” “Tusijadili hapa, inatakiwa tujue ni jinsi gani tunapona kutoka kwenye hali hii mke wangu” “Sasa turudi nyumbani au?” “Sielewi ila hamu ya kurudi nyumbani sina kabisa, nadhani tutafute uwezekano wa kwenda kwa Siwema kwa njia yoyote ile” “Basi tukodi gari twende mume wangu” Ikawa kama bahati kwani muda huo huo ilitokea gari ya kukodi na kupita mbele yao kisha kuwauliza kama wanaenda ambapo waliitikia na kupanda. Dereva wa lile gari alikuwa ni mwanaume wa makamo ambapo Ibra alimuuliza, “Umejuaje kama sisi ni wasafiri?” “Nimejua sababu mmekaa eneo langu la kazi na hata hivyo nafahamu hadi mnapoenda” Ibra na mkewe wakatazamana na kumuuliza, “Unafahamu tunapokwenda? Ni wapi kama wapafahamu?” “Mnakwenda kwa mtu mmoja anaitwa Siwema” Wakashtuka sana na kumuuliza tena, “Umejuaje?” “Nyie mmeshuka kwenye eneo langu kwahiyo mimi huwa najua kila kitu cha watu wanapozungumza kwenye eneo langu au karibia na eneo langu” “Wewe eneo lako ni lipi?” “Pale makaburini ndio eneo langu” “Yani gari yako huwa unapaki pale?” “Hapana ila ndio ninapoishi” Ibra na Sophia wakapatwa na uoga kwani eneo lile hawakuona nyumba ya aina yoyote ile, Ibra akauliza kwa hofu “Mbona pale hapana nyumba yoyote sasa wewe unaishi wapi?” “Pale kuna kaburi langu ndio naishi humo ni nyumba yangu ile japo manaona ni kaburi” Wakazidi kupatwa na uoga huku wakimuangalia Yule mtu kwa mashaka, ila Yule mtu akacheka kisha akawaambia “Unajua mimi nimekufa miaka mingi sana iliyopita, kila mtu akiniona huwa ananishangaa sana ila mimi naona kawaida. Kwani kufa ni jambo la ajabu sana kwenu?” Ibra na mkewe walizidi kutetemeka na kumuomba awashushe, “Niwashushe vipi wakati bado hamjafika?” Ibra na mkewe waliomba sana kushushwa, Yule mtu alicheka sana na kusimamisha gari ambapo walishuka na kuanza kukimbia hovyo hovyo, ikabidi Ibra amshike mkewe mkono kwani aliona wazi watapotezana na ilikuwa usiku sana ukizingatia na majanga yale watakimbiaje mmoja mmoja kwani walihisi yakiwakuta wakiwa mmoja mmoja watashindwa hata cha kufanya. Wakati wameshikana mikono Ibra aliangalia pembezoni mwa barabara na kuona ile gari yao walipoiacha kwamaana kwamba wamerudishwa sehemu waliyoacha gari, Ibra aliongozana na mkewe hadi kwenye gari yao na kupanda tena wakati wanaiendesha safari hii ilitembea vizuri tu na kuwafanya warudi nyumbani kwao huku wamegubikwa na uoga na hofu moyoni. Wakiwa wamekaa sebleni bila ya kuelewa hili wala lile la kufanya, gafla wakamsikia Yule mtoto akilia na kuwafanya washtuke sana kwani walishasahau kama kuna mtoto mule ndani na kabla hawajafanya chochote walishtukia Yule mtoto akiwa tayari pale sebleni. Itaendelea kama kawaida………..!!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 40 Wakati wameshikana mikono Ibra aliangalia pembezoni mwa barabara na kuona ile gari yao walipoiacha kwamaana kwamba wamerudishwa sehemu waliyoacha gari, Ibra aliongozana na mkewe hadi kwenye gari yao na kupanda tena wakati wanaiendesha safari hii ilitembea vizuri tu na kuwafanya warudi nyumbani kwao huku wamegubikwa na uoga na hofu moyoni. Wakiwa wamekaa sebleni bila ya kuelewa hili wala lile la kufanya, gafla wakamsikia Yule mtoto akilia na kuwafanya washtuke sana kwani walishasahau kama kuna mtoto mule ndani na kabla hawajafanya chochote walishtukia Yule mtoto akiwa tayari pale sebleni. Ibra na Sophia wakapata mshtuko uliowafanya wakumbatiana zaidi, yule mtoto akaanza kusema “Mama ninyonyeshe” Sophia hakuweza hata kujibu zaidi ya kutetemeka tu, kisha yule mtoto akasema tena “Kwa usalama wenu na wako mama ninyonyeshe” Gafla yule mtoto akatua mikononi mwa Sophia hata aliyembeba na kumuweka hakuonekana, yule mtoto alikuwa akimtazama Sophia ambaye alikuwa akitetemeka tu. Ibra naye alikuwa akishangaa kuwa yeye na mkewe wameachanishwa muda gani hadi yule mtoto kuwekwa kwenye mikono ya Sophia huku akidai kunyonyeshwa. Ibra kwa sauti ya kutetemeka akamuomba mkewe amnyonyeshe mtoto huyo ambapo Sophia hakupinga zaidi ya kutoa ziwa lake na kuanza kumnyonyesha. Yule mtoto alikuwa ananyonya kama ng’ombe vile yani alikuwa akinyonya ziwa hili na kuhamia lingine kwa wakati mmoja, Ibra na Sophia walibaki kumuangalia tu bila ya kufanya chochote. Sophia alijikuta akimnyonyesha yule mtoto hadi palipokucha na nguvu zote zilimuisha hakuweza kufanya kitu chochote kile ndipo Ibra alipoamua kwenda kumuandalia mkewe chakula kwani hakuwa na nguvu hata ya kuongea. Alipofika jikoni alishangaa kuona kuna sufuria kwenye jiko na jiko likiwa linawaka, akasogea na kufunua lile sufuria akaona ni nyama yani supu ndio inachemshwa pale na ilikuwa na harufu nzuri sana. Ibra hakutaka kuisumbua akili yake kwa kujiuliza kuwa nani amebandika zaidi ya kupakua ile supu kwenye bakuli kisha kwenda kumuwekea mkewe ili anywe, akarudi tena jikoni akakuta kuna chapati juu ya meza ya jiko ambapo alizichukua pia na kwenda kumuwekea mkewe. Zoezi alilokuwa nalo sasa ni kumtoa yule mtoto ili mkewe aweze kula na kurudisha nguvu, ila kabla hajamtoa alishangaa kumuona yule mtoto yupo pembezoni mwa kochi kanakwamba kuna mtu amemnyanyua na kumuweka pembeni. Ibra hakuhoji pia zaidi ya kumsogelea mkewe na kuanza kumnywesha ile supu na zile chapati. Baada ya kumaliza kula, Sophia alianza tena kurejewa na nguvu ila mwili wake ulikuwa umechoka sana. Kisha Ibra akainuka na mkewe hadi chumbani kwao ambapo walipofungua mlango ulifunguka tu kisha wakaingia na moja kwa moja wakaenda kuoga kwanza na kubadilisha zile nguo walizokuwa wamevaa. Walikaa kitandani kila mmoja akimuangalia mwenzie, Sophia akajikuta akimuuliza mume wake, “Hivi hii nyumba ulinunua Ibra au ulipewa bure?” ‘Hivi ni swali gani hilo unaniuliza Sophia mke wangu jamani?” “Unajua maisha yetu yalikuwa na amani sana, ni kweli tuliishi kiumasikini, tuliishi uswahilini lakini tulikuwa na amani sana. Tunachopata tunakula na kufurahi, usiku tunalala vizuri na kuamka vizuri. Sikuona kasoro yoyote kwenye maisha yetu ale zaidi ya umasikini wetu tu. Hivi kuna faida gani ya kuishi nyumba kubwa hivi na nzuri huku tukiteseka kiasi hiki? Hivi unahisi ni maisha ya kawaida haya mume wangu? Hivi uanahisi huyu mtoto ni wakawaida? Mtoto mdogo vile atawezaje kuongea? Nimekuuliza kwa uzuri tu mume wangu, hivi hii nyumba ulinunua au ulipewa bure?” “Unajua wazi Sophia kuwa hii nyumba niliinunua mke wangu ingawa pesa niliyonunulia hii nyumba haiendani na thamani ya nyumba ila mwenye nyumba aliniambia kuwa anahama hii nchi ndiomana kaamua kuuza vitu vyake kwahiyo sikuona vibaya kuinunua hii nyumba. Sasa unamaana gani kusema hayo au unataka tufanye kitu gani?” “Mimi naona ni bora turudi maisha yetu ya zamani hata kama watu watatucheka ila ni bora kuishi maisha yenye amani kuliko haya” Ibra alitulia kidogo akitafakari maisha ambayu alikuwa akiishi na mkewe zamani, ni kweli yalikuwa ni maisha ya kimasikini ila yaliyojaa amani sana. Akakumbuka na jinsi mama yake alivyopiga simu na kuwalalamikia kuwa kwanini hawaendi kuwatemmbelea. Ibra alijiuliza sana na kukosa jibu kwani zamani ilikuwa ni lazima wawatembelee wazazi wao na ndugu zao au hata kuwaulizia hali zao ila kwa kipindi hiki imekuwa tofauti kabisa hawajawahi hata kuwapeleka wazazi wao hapo kwenye nyumba yao. Ibra akamuangalia mkewe na kumuuliza pia, “Kwahiyo unataka tukapange tena?” “Bora tukapange tena, mimi nimechoka kwakweli” “Pole mke wangu, hata mimi nimechoka kwakweli ila hata sijui tuanzie wapi na tuishie wapi” “Usijiulize mume wangu, chukua hela tafuta dalali atutafutie chumba tukaishi sehemu nyingine tuondoke kabisa hapa” Ibra akakubaliana na mkewe kuhusu hilo swala, kisha akainuka na kwenda kabatini ili kuchukua pesa walizokuwa wamehifadhi. Alifungua kweli na kukuta pesa zimeongezeka zaidi akamuangalia mkewe na kumwambia “Hivi unajua kama pesa zimeongezeka kwenye kabati?” “Kheee zimeongezeka? Nani kaziongeza?” “Sijui kabisa” “Chukua hivyo hivyo mume wangu tukatafute nyumba sehemu nyingine” Ibra akachukua pesa za kutosha kisha akatoka na mkewe ambapo walikubaliana kuwa akamuache mkewe dukani kisha yeye akazunguke na dalali. Waliondoka pale nyumbani kwao na kuelekea dukani ambapo Ibra alimuacha mkewe hapo kisha yeye akaenda kumtafuta dalali ili amsaidie kutafuta nyumba. Sophia alikaa dukani huku akiwa na mawazo sana hata akatamani arudishe siku nyuma ili hata siku moja asiwe ameyaonja yale maisha ya kitajiri kwani yalimuweka kwenye wakati mgumu sana akakumbuka jinsi alivyokuwa akiwaota watoto wake na vile mimba zake zilivyokuwa zikitoka. “Ningekuwa na kimtoto changu saivi nacheza nae, utajiri gani huu mimba zangu zimetoka zote watoto wangu wamelia kwa uchungu nakazana kunyonyesha sijui majini uwiiiii mimi jamani eeeh Mungu nisaidie” Akawaza kidogo kweli na kujicheka huku akijisikitikia na kusema, “Kweli mtu ukiwa na shida ndio wakati wa kumkumbuka Mungu jamani, nisaidie Mungu” Muda kidogo akasogea Yule baba John na kumkuta Sophia hapo dukani kisha akamsalimia na kuanza kuzungumza nae, “Naona leo umeamua ubaki mwenyewe dukani shemeji” “Ndio, naboreka kukaa nyumani. Hata hivvyo tulikuwa na matatizo kidogo hapa karibuni” “Poleni sana ila nini tatizo tena shemeji? Ila Ibra ni msiri sana sababu huwa namuona siku zote hapa akiwa na furaha tu” “Mmh siku zote! Jana ulimuona?” “Ndio, tena jana alikuwepo hapa hadi jioni kabisa tuliondoka wote na kumuacha mwenyewe ila sikuzungumza nae” “Mmmh jamani, kwani siku hizi imekuwaje tena? Mbona sielewi elewi?” “Huelewi nini kwani?” “Ibra nilikuwa nae nyumbani jana kutwa yote sasa huku dukani alikuwa nani?” “Halafu wewe na mumeo sijui mna matatizo gani jamani, kwani mkikubali mlikuwa hapa kuna tatizo? Ngoja niachane na hayo sio kilichonileta, hivi shemeji ile mimba yako yak wanza kwanini ilitoka?” Sophia akamuangalia baba John bila ya kumjibu kwani aliona kamavile anataka kumkumbushia machungu yaliyopita tu. “Naomba tuachane na habari hizo shemeji tafadhari” Baba John akaamua kuondoka kisha Sophia nae akafunga duka na kuondoka huku akili yake ikimuelekeza kwenda kwa Siwema moja kwa moja. Sophia alifika nyumbani kwa Siwema na hakumkuta hivyobasi akaamua kukaa nje akimsubiria kuwa huenda hakwenda mbali sana, wakati amekaa pale akakumbuka ule mti wa mpera na kuinuka hadi kwenye ule mti akiangalia angalia, muda kidogo Yule bibi ambaye mara nyingi huwa anazunguka eneo lile alisogea pale alipokuwa Sophia na kumsalimia. Sophia akashtuka kisha na yeye akamsalimia tena Yule bibi, bibi akaitikia huku akisikitika na kusema, “Nakuhurumia sana mjukuu wangu, najua hapo ulipo unamawazo sana ila inatakiwa mfungue akili zenu kwanza ndio muweze kuelewa mbichi na mbivu. Siku ya kwanza nilipokutana na wewe nilikwambia kuwa nyumba yenu ni nyumba ya maajabu ila hukunielewa. Najua hukunielewa kwavile hukutaka tu kunielewa ila kuna viashiria tayari ulishaviona kwenye nyumba yako kuwa si nyumba ya kawaida ila hukutaka kuhoji kuhusu hilo” “Tafadhali bibi naomba unieleweshe maana nashindwa kuelewa kweli ingawa nipo kwenye wakati mgumu” “Ile nyumba ni kama jela kwani kuingia pale ni rahisi sana ila kutoka si rahisi kama mnavyofikiria” “Kivipi bibi?” “Si mumeo umemuagiza akatafute nyumba nyingine? Jibu atakalokuletea najua utaelewa ni jinsi gani ilivyongumu kutoka kwenye ile nyumba tofauti na kuingia” “Kheeee na umejuaje kama mume wangu ameenda kutafuta nyumba nyingine?” “Mimi huwa naona vitu vingi sana ingawa watu nikiwaeleza huniona kamavile mimi ni mchawi na huwa wanasema kwavile nimetengwa na familia yangu ila maono yangu haya ndio yaliyofanya nitengwe ila siwezi kuacha kusema kile ninachokiona kwani sipendi kuona mwingine akiteketea wakati najua suluhisho lake” Sophia akapumua kidogo kisha akamuuliza huyu bibi, “Sasa sisi tutawezaje kutoka kwenye ile nyumba? Maana kiukweli tunateseka sana” “Kabla ya kutoka pale inatakiwa akili zenu zifunguke kwanza, nyie mmefungwa kwenye akili zenu na msipokuwa makini mtateketea wote wewe na mumeo kisha mtaingia kwenye mkumbo wa kuwa viumbe vya ajabu” Sophia akashtuka kidogo kisha kuvuta pumzi na kumueleza huyu bibi kuwa pale alipo hata anaogopa kurudi nyumbani kwake, “Yani natamani hata nisirudi kabisa” “Ni bora urudi tu kuliko kurudishwa, yani rudi kwa hiyari yako mwenyewe kuliko urudishwe pale. Tatizo ni moja hapo ulipo huna pa kujificha maana harufu ya damu yako inajulikana sana” “Damu yangu tena?” “Ndio damu, kwani wewe unafikiri Yule mtoto unayemnyonyesha kila siku unamnyonyesha nini?” “Sijui, ninachojua mimi ni kuwa namnyonyesha maziwa” Bibi akasikitika kidogo kisha akamwambia, “Humnyonyeshi maziwa ila unamnyonyesha damu, maisha yako yapo kwenye hatari zaidi kuliko maisha ya mumeo” Sophia akaogopa sana vile alivyosikia kuwa huwa anamnyonyesha Yule mtoto damu na kusikia kuwa maisha yake yapo kwenye hatari zaidi, alihisi kupagawa kabisa kwa uoga. “Nitafanyaje sasa, bibi nisaidie tafadhali” “Nitakusaidia ila kwanza akili yenu irudi ndio itakuwa rahisi kuwasaidia” “Na akili yetu itarudije? Kwani haipo?” “Nyie mnajiona mpo sawa ila akili yenu haipo sawa hata vitendo mnavyovifanya si vya kufanywa na binadamu wa kawaida ila nyie mnafanya, mnaweza mkarudi nyumbani kwenu na kukuta chakula si wewe wala mumeo aliyepika ila mnapakua chakula hiko na kukila tena huku mnakisifia kuwa ni kitamu sana. Unafikiri hiyo ni akili ya kawaida? Huwa manadhani chakula hicho kimeshushwa kutoka mbinguni au ni kitu gani? Mmefungwa akili zenu, ndiomana nasema kuwasaidia nyie ni mpaka pale mtakapofunguka hizo akili” “Tusaidie basi akili zetu ziwe sawa, zirudi katika hali ya kawaida” “Nitawasaidia” Bibi alitoa dawa kama mzizi hivi kisha akamkabidhi Sophia na kumwambia, “Mkiwa mnarudi nyumbani kwenu wewe na mumeo, mkifika getini sema asante Mungu kisha muingie ndani. Baada ya hapo endeleeni na shughuli zenu zingine kama kawaida, ikifika saa mbili usiku nenda na mumeo sebleni kisha sema tena asante Mungu, chukua hiyo dawa ikate na uitafune halafu mpe na mumeo nae aitafune kisha………” Mara Siwema akatokea na akakunja sura sana baada ya kumuona Yule bibi, “Uwiii uwiiii uwiiii wewe bibi toka nyumbani kwangu, nimesema tokaaaaaa” “Jamani Da’Siwema usifanye hivyo huyu bibi anataka kutusaidia” “Asaidie nini mchawi mkubwa huyu, wewe bibi tokaaaa hivi hunisikiii eeeh” Yule bibi akainuka na kuondoka kwani hakuwa bibi wa malumbano, Sophia akataka kumfata Yule bibi ila Siwema akamvuta mkono na kurudi nae kwenye nyumba yake. Siwema alianza kumlalamikia Sophia, “Laiti ungejua huyu bibi anavyonikosesha usingizi wala usingethubutu kuzungumza nae nyumbani kwangu. Hana maana yoyote Yule bibi yani hafai kabisa” Muda kidogo Ibra nae akawasili pale kwa Siwema, Sophia akamtazama mumewe na kumuuliza “Kheeee umejuaje kama nipo huku?” “Nilivyokukosa dukani, moja kwa moja nikahisi kuwa umekuja huku tu” “Vipi umefanikiwa?” “Nifanikiwe wapi? Yani majanga tu” “Majanga gani tena?” Ibra akamvuta mkewe pembeni na kuanza kumueleza, “Yani huwezi amini kabisa, nyumbani pale si nimeondoka na hela! Basi nimemfata dalali kweli nyumba ipo ila kutoa hela sina sh kumi, nikabaki kujishangaa tu basi tafuta tafuta hamna hela yoyote ndio nikamwambia Yule dalali nije nae dukani, kufika pale na wewe umefunga haupo. Kwavile na mimi nina funguo za pale nikaamua kufungua ili niangalie pesa za mauzo nimpe kidogo za kumpooza lakini hapakuwa na pesa yoyote ile. Yule dalali akamaindi na kuondoka zake ndio nikapata wazo kuwa utakuwa huku. Vipi ulibeba pesa za pale dukani?” “Sijabeba hela yoyote ndio nakushangaa tu hapa ila kuna kitu nataka nikwambie” Ibra akamsikiliza kwa makini mkewe ambapo alimueleza kwa kifupi vile alivyoelezwa na Yule bibi, Siwema alipoona hawamalizi maongezi yao akawafata, “Ni maneno gani manayoongea kwa kunificha? Haya ondokeni nyumbani kwangu, nimesema ondokeni” Ibra akaongozana na mkewe na kwenda kwenye gari yao kisha kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao, ilikuwa ni jioni tayari. Walipofika getini Sophia akasema asante Mungu kama alivyoelekezwa na kuingia ndanui, walikuta nyumba iko shwari tu kisha wakaendelea na shuguli zao zingine ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia pesa kwenye kabati ambapo walizikuta zipo za kutosha tu. Ilipofika saa mbili usiku, kama walivyoambiwa wakaenda sebleni na kukaa kisha Sophia akachukua ile dawa na kutafuna halafu akampa mumewe nae atafune. Gafla wakashangaa kujikuta wapo ndani ya damu. Itaendelea kama kawaida………!!!!!!! Toa maoni yako mdau. NYUMBA YA MAAJABU: 41 Walipofika getini Sophia akasema asante Mungu kama alivyoelekezwa na kuingia ndanui, walikuta nyumba iko shwari tu kisha wakaendelea na shuguli zao zingine ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia pesa kwenye kabati ambapo walizikuta zipo za kutosha tu. Ilipofika saa mbili usiku, kama walivyoambiwa wakaenda sebleni na kukaa kisha Sophia akachukua ile dawa na kutafuna halafu akampa mumewe nae atafune. Gafla wakashangaa kujikuta wapo ndani ya damu. Hakuna aliyeweza kujielewa kwa wakati ule kwani kila mmoja alijiona wa tofauti, gafla ikawa kamavile wapo kwenye sinema kwani walikuwa wakiona matendo mbalimbali mbele yao mengine yalifanyika vyumbani, jikoni, na sebleni ila yote waliyaona na matendo mengine waliyaona ila watu hawakuwafahamu kabisa. Kwanza walimuona Neema akiwa na mwanaume ambaye hawakumtambua ni nani ila Neema na Yule mwanaume walionekana ni wapenzi na walifurahiana sana, gafla wakamuona kama Neema akiugulia sana hadi kufa kisha Yule mwanaume alionekana akisikitika sana. Kwa mbali wakaona makaburi kisha wakamuona Yule mwanaume amesimama mbali kabisa kisha ikanyesha mvua kubwa sana. Gafla wakaona Yule mwanaume akiishi ndani na mwanamke mwingine ambaye hakuwa Neema na wakaona Yule mwanamke akiwa na mtoto mdogo ila Yule mtoto alionekana kuwa wa ajabu sana na alitenda vitu vya ajabu, kuna muda waliona Yule mtoto akiingiliwa na kitu ambacho kilikuwa kikibadili akili ya Yule mtoto na kutenda mambo ya ajabu na wakati mwingine kile kitu kilitoka na kufanya Yule mtoto aendelee kuwa mtoto mdogo, gafla hawakuwaona tena hao watu kwenye nyumba hiyo ila wakamuona Yule mwanaume akiwa na mwanamke mwingine ambapo sura ya huyu mwanamke ilimkumbusha kitu Ibra ala gafla wakamuona Yule mwanaume nae akitapatapa hadi kufa. Muda huo huo wakajiona wao wakiwa wamekaa kwenye makochi na chini yao hapakuwa na damu tena, wakatazamana na kuulizana ili kutambua kama wako sawa kabisa, “Sophia unanisikia?” “Nakusikia Ibra?” “Je umeona nilichoona mimi?” “Nadhani wotw tulikuwa tunaona, je ni kitu gani umekihisi kwa haya tuliyoyaona?” “Kuna kitu kimenishtua” “Kitu gani?” “Yule mwanamke aliyeonekana mwishoni kabisa ndiye mwanamke aliyeniuzia hii nyumba” “Na je yuko wapi?” “Mimi sijui alipo kwani tulipouziana nyumba tu kila mtu alishika ustaarabu wake” “Nadhani huyo dada ni muhimu sana kumtafuta na ndiye atakayetusaidia” “Hata mimi nadhani hivyo hivyo na ndiomana Yule bibi alisema ufahamu wetu urudi kwanza.” “Na je unafikiria nini kuhusu Neema?” “Naogopa hata kumuongelea kwani nahisi kuwa alishakufa siku nyingi sana” Gafla kikasikika kicheko kisha Neema akatokea mbele yao huku akitabasamu, hakuna aliyeweza kustahimili na walijikuta wakianguka na kuzimia. Walipozinduka walijikuta wakiwa chumbani kwao, wamelala kitandani. Ibra akawa wa kwanza kumuuliza mkewe “Unajisikiaje?” “Sijisikii chochote ila tu nakumbuka tulimuona Neema na tukapoteza kumbukumbu sasa imekuwaje tumeletwa humu chumbani?” “Kwanza kabisa naomba tupungue kumuongelea huyo mtu halafu tupange cha kufanya maana kama mambo makubwa yashatupata tayari” Wakaamua kuamka pale kwani palionekana kuwa pamekucha kabisa kisha wakaenda kuoga na kujiandaa kwaajili ya kutoka. Wakati wanatoka wakakuta chai imeandaliwa mezani na vitafunio vizuri kabisa, “Mmh haya maajabu ya humu yamezidi jamani, haya chaia kapika nani?” “Tuachane na hayo mke wangu, hebu twende” Ibra akamuongoza mkewe hadi nje kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka zao, ila walipofika pale walipowahi kuona hoteli kubwa sana leo waliweza kuona makaburi yakiwa yamezunguka pale kwa uzuri kabisa, Sophia akamuuliza mumewe “Je inawezekana kaburi la Neema likawa maeneo haya?” “Sophy tafadhali tusimuongelee huyo mtu” “Tusimuongelee kivipi wakati ndiye anayesumbua maisha yetu? Neema ndiye kikwazo kwetu na ndiye kikwazo kwenye nyumba yetu” Ibra hakutaka kumsikiliza sana mkewe hivyobasi akaondoa gari na kuendelea na safari, sehemu ya kwanza waliyoenda ilikuwa ni dukani kwao ambapo walikuta mitaa ya pale imepooza sana kanakwamba hapakuwa na mtu yeyote kwenye eneo lile kabisa na kuwafanya hata waogope kufungua duka lao kisha wakarudi kwenye gari na kupanga tena kwenda kwa Siwema ili angalau wakaonane na Yule bibi. Waliingia kwenye gari huku wakiulizana, “Imekuwaje leo watu hawajafungua maduka?” “Hata sielewi kwanini hawajafungua ingawa haijawahi kutokea hata siku moja eti maduka yote yawe yamefungwa vile” “Labda kuna mgomo wa maduka” “Inawezekana ila sidhani kwani tungejua tu kama kuna mgomo” “Inawezekana hatujui kutokana na matatizo yetu maana mambo mengi yanatupita sana” Wakakubaliana hivyo kuwa inawezekana hawajui kutokana na mambo mengi yaliyowapata na kuwafanya washindwe kupata taarifa kwa muda. Walipofika nyumbani kwa Siwema napo palikuwa kimya sana kanakwamba Siwema hakuwepo kabisa, wakajaribu kugonga ila hakuna hata mtu aliyetoka kuwafungulia, “Inamaana Da’Siwema hayupo?” “Itakuwa hivyo maana kimya kimetanda sana” “Je tutawezaje kumpata tena Yule bibi?” “Huo ndio mtihani sasa hata sijui tutafanyaje” “Ila mimi nina wazo” “Wazo gani?” “Kwanini tusiende kwa Yule mganga wakwanza kabisa tuliyepelekwa na Da’Siwema! Maana nadhani kule tutapata taarifa nyingi zaidi” “Ila huyo mganga si ndiye aliyetuhakikishia kuwa Jane ni mchawi?” “Sasa kwani Jane si mchawi?” “Jane si mchawi, hivi mpaka sasa bado unaamini kuwa Jane alikuwa mchawi? Hizo zilikuwa ni mbinu tu za Yule kiumbe ili tusijue mabaya yake ila kiukweli Jane sio mchawi” “Mbona Yule mganga alituhakikishia sasa!” “Ndiomana nakosa imani nae kwani alituhakikishia kitu ambacho si cha kweli” “Hata kama, bado tunapaswa kwenda kuonana nae na tutajua mambo mengi. Kwanza hawezi kubeba akili zetu kwasasa kwani zimesharudi” Wakakubaliana pale kuwa waende kwa huyo mganga ambaye mwanzoni kabisa waliwahi kwenda pamoja na Siwema, wakaingia kwenye gari yao na kuanza safari ya kwenda kwa huyo mganga. Walifika kwa huyo mganga na ilikuwa ni sehemu ile ile waliyopelekwa na Siwema ila ulionyesha kubadilika vitu vingi sana kwani mambo mengi yalionekana kuwa tofauti kabisa na kuwashangaza, “Hivi ni hapa kweli?” “Ndio ni hapa hapa, mimi nakumbuka kabisa. Nakumbuka hadi eneo ambalo tuliwachinja wale nwanyama” Sophia akatazama kwa makini nay eye akakumbuka kabisa, wakasogea karibu na kilinge cha Yule mganga ila leo hapakuwa na watu kabisa tofauti na walivyokuja kipindi kile na kuwafanya wahisi kuwa huenda wateja wameanza kupungua kwa mganga huyo. Walisogea karibu na kuingia mule kilingeni ambapo walimkuta Yule mganga akiwa amejiinamia, wakamsalimia na kukaa ambapo kabla hawajaitikiwa salamu Yule mganga aliwauliza, “Mmekuja kufanya nini?” “Tunashida mzee” “Najua kama mnashida ila je ni shida gani?” “Nyumbani kwetu kuna matatizo, kuna kipindi tuliwahi kwenda pamoja na ulituambia kuwa Yule jirani yetu ndiye mchawi ila kumbe kilichokuwa kinatutesa kilikuwa ndani ya nyumba yetu” “Kwahiyo mmekuja kunizodoa kuwa niliwaambia uongo?” “hapana, hatuna nia ya kukuzodoa kabisa ila tunaamini bado unaweza kutusaidia kwa jambo hili” Yule mganga akatabasamu kisha akawaambia, “Hivi mnajijua kama mnanukia kifo?” “Tunanukia kifo kivipi?” “Ni nani mliyeweza kuzungumza nae leo zaidi ya mimi?” Ibra na mkewe wakatazamana kwa muda kwani kiukweli toka wametoka nyumbani kwao hakuna waliyeweza kuzungumza nae zaidi ya huyu mganga kwani kila sehemu waliyopita hawakuwakuta wenyeji wao, Ibra akamjibu huyu mzee “Hakuna mtu yeyote tuliyezungumza nae kwani kila mahali tulipopita hatukuwakuta watu ambao tunaweza kuzungumza nao” Huyu mzee akacheka tena na kuwaambia, “Hivi mnajua kwanini mmeweza kuongea na mimi? Mnajua kwanini mimi mmenikuta?” “Hatujui” “Basi jibu ni rahisi kabisa, mimi I marehemu” Ibra na Sophia walishtuka sana hata uoga nao ukaanza kuwaingia moyoni kwani hawakutegemea kitu kama hiki. Ibra akauliza kwa sauti ya kutetemeka, “Ma-ma-marehemu kivipi?” “Mimi ni marehemu, nilishakufaga siku nyingi sana na ndiomana mmeweza kuniona na kuzungumza na mimi” “Una-unamaanisha nini? Inamaana na sisi ni marehemu?” Huyu mzee akacheka tena na kuwaambia, “Nyie si marehemu ila mnakaribia kuwa marehemu, na kama hamuamini maneno yangu basi mtakapotoka hapa na kukutana na watu njiani jaribuni kuwaongelesha muone kama mtajibiwa yani hamtajibiwa na wala hawatawaona kwavile nyie mnanukia umarehemu” Uoga ukawazidi na kuwafanya watetemeke sana, kisha wakajikuta wakiomba msaada kwa huyu mzee ili awasaidie ila huyu mzee alikuwa akicheka tu na kuwauliza, “Nawasaidia vipi wakati mimi ni marehemu tayari? Labda msaada wangu niwafanye na nyie kuwa marehemu” Hapo wakashindwa kustahimili na kuinuka haraka kisha kutoka nje ya kile kilinge, walitazamana na kugubikwa na uoga kisha wakarudi kwenye gari na kuondoka eneo lile. Wakaamua kurudi tena kwa Siwema ila ilikuwa vile vile kama mwanzo yani hapakuwa na mtu wa aina yoyote ile, Ibra akapata wazo la kupiga simu ila kila aliyempigia hakumpata hewani kabisa na kumfanya uoga umzidie kisha wakarudi tena kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea popote na kila walipopita na kuona watu walijaribu kusimamisha gari na kuongelesha watu hao ila ilionekana kuwa hakuna aliyejali uwepo wao kwani hakuna aliyewajibu kabisa na kila waliyemwongelesha alionekana kuendelea na shughuli zake kanakwamba hajaongeleshwa kitu, “Inamaana hawatuoni au?” “Sijui” “Na je inamaana ndio tumekufa?” Sophia akamsogelea mumewe na kumkumbatia kisha akasema kwa uoga sana, “Naogopa kufa mume wangu” “Hata mimi naogopa ila wakati wetu ukifika tutakufa tu haiepukiki hiyo” “Sasa kwani ndio wakati wetu umefika? Kwanini jamani? Sijaweza hata kuwaaga ndugu zangu” Sophia alimkumbatia mumewe huku machozi yakimtoka, ila Ibra bado alijipa moyo, “Ila naamini tutakomboka tu mke wangu” “Hata sijui tutakombokaje, je ni nani atakayeweza kutusaidia? Inamaana Yule bibi ametupotosha zaidi” “Ila mke wangu wakati mwingine tunatakiwa kuwa na shukrani tusimlaumu moja kwa moja Yule bibi halafu pia kumbuka hukumsikiliza Yule bibi hadi mwisho labda kulikuwa na ujumbe mwingine ambao tulipaswa kufanya kwahiyo tusimlaumu moja kwa moja tujilaumu na sisi wenyewe kuwa kwanini hatukuwa makini kumsikiliza? Hata baada ya Siwema kukatisha kwanini tusingemtafuta siku ileile? Kwahiyo tusimlaumu moja kwa moja” Wakarudi tena kwenye gari na kuendelea na safari ambapo kwa wakati huo hawakuwa na uelekeo unaoeleweka kabisa kwani kila waliposimamisha na kuongea na watu hakuna jibu walilolipata. Walikaa kwenye gari na kujadiliana kuwa ni bora warudi nyumbani tu kuliko kuendelea kuhangaika hivyo. Wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao, wakakutana tena na yale makaburi ya mwanzo ambapo moja kwa moja Sophia aliuliza tena swali ambalo halikutofautiana sana na swali la mwanzo walipoyaona, “Inamaana kaburi la Neema nalo lipo hapo?” “Tusimuongelee huyo mtu tafadhali kwanini husikii mke wangu jamani?” “Nasikia vizuri ila huyu Neema anatutesa sana mume wangu, anatutesa kwenye nyumba yetu sana” Mara gafla wakasikia sauti ikitokea kiti cha nyuma kwenye gari yao, “Nawatesa mpaka kwenye gari lenu” Walipogeuka wakamuona Neema, uoga ukawajaa wakafungua milango ya gari na kuanza kukimbia, kwa bahati mbaya wakati wanakimbia likatokea gari na kumgonga Sophia kisha damu zikatapakaa eneo lile. Ibra alikuwa kama amepigwa na butwaa hivi kwani mwanzoni walikuwa hawaonekani ila gari imeweza kumgonga Sophia na muda huo huo watu wakajaaa kwenye eneo lile. Itaendelea kama kawaida……!!!!!! Toa maoni yako mdau.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments