-->

Hofu Marekani kutokana na kimbunga Matthew

Gavana wa jimbo la Florida nchini Marekani, Rick Scott ameonya kuwa uharibifu utakaotokea utakuwa mkubwa sana ikiwa kimbunga Matthew kitapiga jimbo hilo. Bw Scott ametoa wito kwa wakazi wa jimbo hilo kujiandaa kuhama makwao zoezi ambalo ndilo litakalokuwa kubwa zaidi katika historia ya jimbo hilo. Msongamano mkubwa wa magari na watu umetokea katika barabara huku watu wakihamia maeneo ya bara. Wakazi katika jimbo la Carolina Kusini pia wametakiwa kuhama maeneo yaliyo hatarini. Gavana Nikki Haley amesema watu 250,000 watahamishwa kutoka maeneo ya pwani. Rais wa Marekani Barack Obama amesema kimbunga hicho kinaweza kuwa hatari sana na kuwataka wakazi wa eneo hilo kufuata ushauri unaotolewa na mamlaka. Kwa Picha: Kimbunga Matthew Shule zimefungwa na wagonjwa wametolewa katika baadhi ya hospitali. Kimbunga kikubwa cha mwisho kukumba jimbo la Florida kilikuwa ni Katrina miaka 10 iliyopita.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments