-->

Chombo cha anga za juu cha Ulaya kutua Mars

Chombo cha anga za juu cha Ulaya Schiaparelli kimefanikiwa kujitenga na "chombo mama" angani na kwa sasa kinaelekea kwenye sayari ya Mars. Chombo hicho kinatarajiwa kujaribu kutua kwenye sayari hiyo Jumatano. Chombo hicho cha uzani wa kilo 577 kilifanikiwa kujitenganisha na chombo mama Jumapili saa 14:42 GMT (saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki). Chombo hicho kitakuwa na muda wa chini ya dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita 21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua salama kwenye sayari hiyo. Schiaparelli ni kifaa cha kufanyia majaribio teknolojia, na lengo kuu ni kudhihirisha uwezo wa Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) kutua katika sayari hiyo. Jaribio la awali la shirika hilo kutua katika sayari hiyo lilifanyika mwaka 2003, kwa kutumia Chombo hicho kilifanikiwa kutua salama lakini kikashindwa kufungua mitambo yake ya kawi ya jua vyema na hivyo mawasiliano yakakatika. Chombo hicho kikifanikiwa kutua salama, kitatumiwa kufanya uchunguzi kwenye sayari hiyo.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments