-->

Watoa pesa benki wakihofia ghasia Gabon

Milolongo mirefu imeshuhudiwa kwenye benki na vituo vya kutoa pesa, kwenye mji mkuu wa Gabon Libreville wakati wanajaribu kutoa pesa, wakihofia kuwa mzozo wa kisiasa uliopo unaweza kuzua ghasia nchini humo. Watu wengine walielezea ghadhabu yao kuwa hawangeweza kutoa pesa zao kwenye benki. "Benki tena hazitaki kutoa pesa, kwa sababu zinaelewa hali sio nzuri na uchumi uko hatarini," alisema mwalimu mmoja. Baadhi ya maduka mjini Libreville yanaishiwa na bidhaa huku familia nyingi nazo zikiishiwa bidhaa muhimu.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments