-->

Ubabe wa China walazimu Japan kurusha ndege zake

Japan imesema kuwa ilirusha ndege zake hewani siku ya Jumapili baada ya ndege nane za China kupaa kati ya visiwa vya vyake. Ndege hizo zinaozodaiwa kuwa zile za kurusha mabomu,kufanya uchunguzi pamoja na ndege ya kivita ,zilipaa juu ya Miyako,kati ya Okinawa na Miyakojima. China imesema kuwa takriban ndege 40 zilihusika katika kile inachokitaja kuwa zoezi la kawaida. Ndege hizo hazikupita katika anga ya Japan,lakini hatua hiyo inaonekana kuwa maonyesho ya ubabe ya China.
Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Japan kusema itashiriki katika zoezi la pamoja na wanamaji wa Marekani katika bahari ya kusini mwa China. Msemaji mkuu wa Japan amesema kuwa taifa hilo linachunguza hatua hizo za China kwa karibu.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments