-->

Video ya raia wa Uganda akiuwawa na polisi Marekani yatolewa

Polisi katika mji wa Marekani San Diego wametoa mkanda wa video ya mwanamme mweusi aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi siku ya jumanne.Video hiyo inaonyesha maafisa wawili wa polisi wakimkaribia Alfred Olango - mkimbizi kutoka Uganda - ambaye hakuwa amejihami, kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi katika mtaa wa El Cajon. Polisi wanasema kwamba mwanamme huyo alionyesha tabia potovu isiyoeleweka, japo mamake mzazi anasema alikuwa na matatizo ya kiakili na alifaa kupata usaidizi. Tukio hilo lilisababisha maaandamano makali katika eneo la El Cajon. Polisi huyo anaonekana akifyatua risasi mara nne, baada ya mwanamme huyo kuinua mikono yake hadi kwenye eneo la kifua, ishara ambayo polisi wanasema ilikuwa ya kujitayarisha kufyatua risasi. Video hiyo imetolewa baada ya siku tatu za maandamano makali , na katika mkesha wa siku ambayo familia ya mwanamme huyo iliitisha maandamano makubwa. Familia ya mwanamme huyo ilikuwa ikiwashinikiza polisi kutoa mkanda wa video wa tukio hilo. Mkuu wa polisi Jeff Davis anasema video hiyo imetolewa ili kutuliza ghadhabu ya umma.

Nemo enim ipsam voluptatem quia voluptas sit aspernatur aut odit aut fugit, sed quia consequuntur magni dolores eos qui ratione voluptatem sequi nesciunt.

Disqus Comments